Tukubali tukatae, CHADEMA haikuzichanga vema karata zake wakati wa kushughulikia usaliti wa Wabunge 19

Tukubali tukatae, CHADEMA haikuzichanga vema karata zake wakati wa kushughulikia usaliti wa Wabunge 19

Tukubali ama tukatae, ukweli ni kwamba, CHADEMA haikuliangalia suala hili la kina Mdee na wenzake Kwa umakini kama chama

Hoja ya kina Mdee ni kwamba! waliapa kulitumikia Taifa kama wabunge wa kuteuliwa kwa sababu ipo barua iliyotoka Kwao CHADEMA yenye Baraka zote ya wao kufanya hivyo!

Ndugu zangu ni kwamba!

Pesa ni Adui wa haki, na kiukweli linapokuja swala la pesa, wenye kubaki salama ni wachache Sana na huenda hata tuliomo humu tusipone,

Tukumbuke, CCM Kwa sasa ni taasisi ambayo kiuchumi iko vizuri kuliko Wakati wowote, na kama kweli inatumia pesa zake kuvunja vunja nguvu za wapinzani wake, maana yake vyama pinzani havihitaji kukurupuka kwenye uamzi wake kushughurikia wale wanaodaiwa wanahongwa na CCM

Katika suala ambalo limehusisha wabunge wanawake kutoka Chama cha CHADEMA na namna ambavyo limeshughulikiwa, kuna dosari, na dosari hizi ndizo zitakazoifanya CCM iendelee kutumia fimbo hiyo kuviua Vyama pinzani hasa Vyama vinavyoibukia kupata umaarufu Kwa sababu ya kushindwa namna nzuri ya kudili na mienendo na Tuhuma hizo kutoka CCM

Ikumbukwe pia kwamba, zimekuwepo tu tuhuma za kuituhumu CCM kuwa inanunua watu!! Kina Tomaso tunaka uthibitisho wa Hilo

Ndiyo, Inawezekana kweli kina Mdee wamekula shere na CCM ili kuhujumu nguvu ya Chama Chao, na kama Hilo limefanyika, ndipo unaiona nguvu ya fedha inavyoweza kuangamiza hata taasisi imara kabisa, na tukumbe kipindi cha nyuma, Pesa hiyohiyo iliweza kununua Chama chote cha Chadema kupitia mgombea mmoja wa Uraisi aliyevumaga sana enzi hizo

Na kama CHADEMA wanataka Chama Chao kipone, basi kinatakiwa kudili na Mbinu hizi mbovu kutoka CCM ili kuweza kukinusuru Chama Chao, ni kudili na kila Aina ya michezo mibovu inayosababisha mvurugano kwa Chama Chao! Ile saini inayodaiwa ni ya katibu mkuu chama, ndio ingelikuwa ni Jambo la kuanza nalo ndipo kina Mdee wafuate!!

Mf. Mdee na wenzake, wanasema, wao wamepewa Baraka zote za kushiriki Bunge Kupitia ofsi ya KM Chadema,

CHADEMA isingedili moja Kwa moja na kina Mdee, badala yake ingedili na huo mfumo uliosababisha kina Mdee waape bungeni!! Yaani wafuatilie Kwanza hiyo saini inayohusishwa Kutokea kwenye ofs za CHADEMA kwamba ilitokea wapi na nani anahusika.

Naamini ingebainika, na kama ingebainika, moja Kwa moja inahusisha Chama cha CCM, CCM tungeidharau watu wengi sana na endapo wangelikumbatia Kwa namna yoyote Ile, wao CCM lingewaletea matatizo makubwa ya kuaminika Kwa wananchi kuhusu swala la kushughurikia Rushwa nchini.

Kilicho fanyika Kwa CHADEMA sasa, ni kujaribu kufunika kidonda Kwa bandage bila dawa yake, bado kina Mdee wengine wataendelea kupigwa pesa humo ndani ya CHADEMA na kuendelea kufukuzwa, Zifedhehesheni Kwanza njia mbovu mnazozituhumu Kutokea CCM.

CHADEMA tujitahidi Sana kudili na mifumo na ujanja ujanja wa CCM kutaka kuuwa Vyama vya Upinzani nchini, na endapo tutakuwa tunadili na tunodhani ni wasaliti tu wa chama, pengine huo mchezo Usiwe na kikomo, Ukiniuliza kwamba kwamba, ni Nani anayeweza kukwepa pesa za CCM zikitumwa hapo chadema, nitakwambia, Ni Lissu pekee ambaye anaweza kuzikwepa angalau Kwa 70% lakini wengine wote, hakuna atakwepa pesa hizo.

Kataeni ubaya unaotengenezwa na CCM na kuushughurikia Kisha kuanika na kutilia mashaka juu ya kile CCM wanawaaminisha wananchi na Dunia kuwa wanashughurikia na kaikomesha Rushwa, mkidhibiti Hilo mtakiponya Chama chenu na Vyama vingine vya upinzani, la sivyo zitaendelea kuwa ni tuhuma tu zisizo na msingi wowote na mtaendelea kutimua wanachama wengine wengi tu hapo kama kweli CCM inacheza mchezo huo.
Ni muhimu kujenga taifa la watu wamoja na wanaoaminiana.
Vyama vya siasa ni vikundi vidogo tu vinavyotafuta kuchaguliwa kuongoza taifa kwa mujibu wa katiba.
Kushabikia kuvunjwa kwa sheria na katiba kwa sababu ya uanachama wako ni kukosa uzalendo.
Uzalendo ni kuunganisha wananchi kwa kufuata katiba, sheria, kanuni na haki.
 
Wananchi kuunganishwa ni rahisi Sana,Ila Kwa hivi Vyama vinavyoisaka Ikulu ndio chanzo cha kuparaganisha jamii, Kwa sababu havitakaa vipatane
 
Wananchi kuunganishwa ni rahisi Sana,Ila Kwa hivi Vyama vinavyoisaka Ikulu ndio chanzo cha kuparaganisha jamii, Kwa sababu havitakaa vipatane
Chama chochote cha siasa kina lengo la kushika madaraka.
Kusaka ikulu ndiyo lengo lenyewe la kuanzisha mfumo wa vyama vingi.
Adui mkubwa wa taifa ni watumishi wa uma na taasisi zinazotakiwa kusimamia mfumo wa vyama vingi kuonesha upendeleo wa wazi.
Hali hii husababishwa na ujinga ambao huzalisha kutojiamini na mwisho fikra za kipuuzi za kwamba upinzani ni uadui.
Mimi ni mwana CCM ninayependa ushindani wa kutumia akili na tuoneshe haki na ustaarabu vimetendeka kwa mustakabali mwema wa taifa.
We have to be smart. Ubabe na matumizi ya nguvu umepitwa na wakati. Siku hizi wanatumika smiling killers.
 
Itajulikana tu, Nani ni Nani?

Tuliwaambia hamkuelewa, Chama kikiwa kimebebwa na mtu na sio watu, matokeo yake ndio haya
kama KORONA ilivyoshikiliwa na MEKO wenu nanyi mnaburuzwa mnakubali KORONA hakuna TANZANIA jifanyeni hamjui
 
Chama chochote cha siasa kina lengo la kushika madaraka.
Kusaka ikulu ndiyo lengo lenyewe la kuanzisha mfumo wa vyama vingi.
Adui mkubwa wa taifa ni watumishi wa uma na taasisi zinazotakiwa kusimamia mfumo wa vyama vingi kuonesha upendeleo wa wazi.
Hali hii husababishwa na ujinga ambao huzalisha kutojiamini na mwisho fikra za kipuuzi za kwamba upinzani ni uadui.
Mimi ni mwana CCM ninayependa ushindani wa kutumia akili na tuoneshe haki na ustaarabu vimetendeka kwa mustakabali mwema wa taifa.
We have to be smart. Ubabe na matumizi ya nguvu umepitwa na wakati. Siku hizi wanatumika smiling killers.
Kwa nini unadhani kwamba, Vyama vinatakiwa vitendewe haki?

Kama mtazamo wako huo unadhani ndio sahihi, bado tunasafari ndefu Sana kama taifa
 
Mmojammoja wanajiunga CCM. Na CCM ndiyo imeimaliza Chadema kwa kuwapata visu vyao. Chama Kubwa na akili Kubwa.
 
Hii kesi imeshakwisha kitambo sana kwa kuwa CCM imepora mamlaka ya Serikali, Bunge, Mahakama na Msajiri wa Vyama. Tugange yajayo tu maana 2025 sio mbali sana.

Kwa trend ya sasa ambapo wapenda mageuzi na wapinzani "wanalialia tu" kwenye social media bila kuwa na solution inayoeleweka, CCM na Serikali yake watafanya waliyoyafanya October 2020 bila woga wowote maana wanajua watu watasusa na maisha yataenda.

Mwisho wa siku inabaki case ya "if you can't fight them, join them". Sintoshangaa sana kusikia kwamba baadhi ya viongozi ndani ya CHADEMA walishiriki kwa njia moja ama nyingine kusaidia wale wamama kuingia Bungeni.
 
Umenifikisha Sana mkuu
 
Back
Top Bottom