Tukubali tumezidiwa tujifunze kutoka Kenya

Tukubali tumezidiwa tujifunze kutoka Kenya

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
9,780
Reaction score
15,488
Tukubali tumeziwa tujifunze kutoka Kenya. Badala ya kuweka ushindani usio na sababu na majirani zetu na ndugu zetu wa Kenya kama taifa tungenufaika kwa kujifunza mazuri na kuacha mabaya badala ya kijidanganya kwamba tumewazidi. kuna mambo machache ya kujifunza

1. Katiba Mpya: Kenya pamoja na ukabila wao na makundi walikaa chini kama nchi na kutengeneza katiba kwa faida ya nchi na sio Chama au watu fulani. Kizuri katiba yao ilitengenezwa na watu ambao ni wataalamu na walijaribu sana kupunguza siasa kwenye mchakato badala yake wakaunda kundi la kitaalamu ndiyo limesaidia kwenye katiba. Hatutaweza kupata katiba kama litaongozwa na makundi ya wakada wa vyama hiyo katiba haitakubaliwa na bunge hili la kitapeli mbele ya wananchi halliwezi kukubaliwa kwenye katiba.

2. Tujilulize ni kwanini kwenye kila list mbaya za huko USA na Ulaya Kenya hawapo. Tanzania imewekwa kwenye list za kuzuiwa kupata viza za uhamiaji USA Kenya hawapo> Sisi badala ya kujiuliza tunatafuta visingizio kila siku

3. Uchumi sio idadi ya watu na maeneo. Kenya wana watu wachache zaidi, nchi ndogo zaidi, rasilimali ndogo zaidi lakini wana uchumi mkubwa kuliko sisi. Hiyo si bahati mbaya ni kwasababu ya katiba nzuri, mifumo bora ya nchi na mahakama na elimu bora.

4. Ni gharama kuendesha nchi bila kujua lugha ya kiingereza. Tunaweza kuwa na Lugha zaidi ya moja na English ifundishwe kuanzia elimu ya msingi.

5. Tanzania ni wazi sasa hatuna Amani zaidi ye wenzetu tuko chungu kimoja. Bila HAKI hakuna Amani

Haya ni mambo ambayo tunaweza kujifunza kwa wenzetu.
 
Sioni la kujifunza kwa haya yote uliyoandika.

Kenya na Tanganyika hakuna wa kumfunza mwenzake zote nchi takataka zisizo jielewa.
 
Kenya ni vibaraka wa mabeberu hawana maliasili za maana kama yureniamu🐼
 
Tunaongozwa na wajinga, ni ndoto kupata katiba mpya ya haki chini ya hii serikali, wanaiba uchaguzi, wanateka, wanaua etc unategemea watatupa katiba ya haki mezani,kwa sasa ni kupambana kuwatoa kwanza
 
Kenya ni vibaraka wa mabeberu hawana maliasili za maana kama yureniamu🐼

Vibaraka maana yake ni nini ? wewe unajuaje kama sisi sio vibaraka? Kwani wanaoiba chaguzi ni kwa faida ya watanzania au vibaraka wao. ?

Je waarabu ambao sisi ni vibara wao sio mabeberu?
 
Back
Top Bottom