N'gwanantugwa
JF-Expert Member
- Apr 25, 2015
- 347
- 345
NOORAH Kitandani…..FIESTA Uwanjani!!
Japo muda kidogo umepita tangu utokee huu mkasa lakini sio mbaya tukikumbushana hii kitu. Jinale halisi ni Haji Nurah Ngarama almaarufu kama ‘Noorah’ au Baba Stylz.
Mwaka 2005 Noorah mwanachemba Squad alipata bahati ya kushiriki kwenye tamasha la Fiesta. Sasa akiwa katika hiyo Tour ya Fiesta alipata ajali mbaya sana,angalau kwa kipindi hicho ajali haikutangazwa sana kama kulivyotangazwa kufana kwa show hizo.
Noorah alipata ajali akiwa kazini. Baada ya kwenda hospital daktari akasema hatakiwi tena sio tu kufanya show bali hata kufanya kazi yoyote ngumu. Hapo ndipo mtihani kwa MwanaChemba huyu ulipoanzia.
Noorah akaona hapana, sasa ntaishije aisee? Akaamua kujivuta hadi muhimbili kwa uchunguzi zaidi ndipo ndipo ilipogundulika kuwa ajali ile imesababisha sehemu ya fuvu la kichwa chake kupata ufa.
Daktari wa hospitali ya Taifa Muhimbili akashauri kwamba sio tu kutofanya kazi ngumu bali mgonjwa huyo anatakiwa apumzike kabisa. Hakuwa na namna Noorah akapumzika na kuwa baba wa nyumbani.
Noorah akapumzika lakini show za Fiesta ziliendelea na zingalipo zinaendelea mpaka leo, kwao yaliyotokea kwa Noorah ni kama ajali kazini tu. Hapo kwenye ajali kazini ndipo hasa kwenye mzizi wa matatizo. Kwanini ajali kazini kwa wasanii hazina bima? Mikataba karibia yote ya wasanii haizungumzii wasanii watafidiwaje wakipata ajali ya kupelekea ulemavu/ugonjwa/kufariki wakiwa kazini. Mikataba mingi haitambui show kama nazo ni kazi iwe ya muda mfupi au mrefu. Kuburudisha kunachukuliwa juu juu tu.
Katika wimbo NSSF Mbeleni wimbo unaopatikana katika mixtape za Anti Virus, Mapacha walizungumzia hii kitu. Nini mustakabali wa msanii katika maisha yake ya baadae? Hii sio kwa Noorah tu bali wengi wanakutana na changamoto kama hizi wakiwa kwenye mikataba ya kazi.
Noorah alikaa nyumbani mpaka alipoona sasa inatosha,akaamka na kwenda shule pale IFM na baadae akarejea tena kwenye muziki ingawaje haikuwa kama zile zama akiwa katika ubora wake.
Na Iddy Mwanaharam