Tukumbuke kisa hiki cha msanii Noorah na Fiesta

N'gwanantugwa

JF-Expert Member
Joined
Apr 25, 2015
Posts
347
Reaction score
345
NOORAH Kitandani…..FIESTA Uwanjani!!

Japo muda kidogo umepita tangu utokee huu mkasa lakini sio mbaya tukikumbushana hii kitu. Jinale halisi ni Haji Nurah Ngarama almaarufu kama ‘Noorah’ au Baba Stylz.

Mwaka 2005 Noorah mwanachemba Squad alipata bahati ya kushiriki kwenye tamasha la Fiesta. Sasa akiwa katika hiyo Tour ya Fiesta alipata ajali mbaya sana,angalau kwa kipindi hicho ajali haikutangazwa sana kama kulivyotangazwa kufana kwa show hizo.

Noorah alipata ajali akiwa kazini. Baada ya kwenda hospital daktari akasema hatakiwi tena sio tu kufanya show bali hata kufanya kazi yoyote ngumu. Hapo ndipo mtihani kwa MwanaChemba huyu ulipoanzia.

Noorah akaona hapana, sasa ntaishije aisee? Akaamua kujivuta hadi muhimbili kwa uchunguzi zaidi ndipo ndipo ilipogundulika kuwa ajali ile imesababisha sehemu ya fuvu la kichwa chake kupata ufa.

Daktari wa hospitali ya Taifa Muhimbili akashauri kwamba sio tu kutofanya kazi ngumu bali mgonjwa huyo anatakiwa apumzike kabisa. Hakuwa na namna Noorah akapumzika na kuwa baba wa nyumbani.

Noorah akapumzika lakini show za Fiesta ziliendelea na zingalipo zinaendelea mpaka leo, kwao yaliyotokea kwa Noorah ni kama ajali kazini tu. Hapo kwenye ajali kazini ndipo hasa kwenye mzizi wa matatizo. Kwanini ajali kazini kwa wasanii hazina bima? Mikataba karibia yote ya wasanii haizungumzii wasanii watafidiwaje wakipata ajali ya kupelekea ulemavu/ugonjwa/kufariki wakiwa kazini. Mikataba mingi haitambui show kama nazo ni kazi iwe ya muda mfupi au mrefu. Kuburudisha kunachukuliwa juu juu tu.

Katika wimbo NSSF Mbeleni wimbo unaopatikana katika mixtape za Anti Virus, Mapacha walizungumzia hii kitu. Nini mustakabali wa msanii katika maisha yake ya baadae? Hii sio kwa Noorah tu bali wengi wanakutana na changamoto kama hizi wakiwa kwenye mikataba ya kazi.

Noorah alikaa nyumbani mpaka alipoona sasa inatosha,akaamka na kwenda shule pale IFM na baadae akarejea tena kwenye muziki ingawaje haikuwa kama zile zama akiwa katika ubora wake.
Na Iddy Mwanaharam
 
SIKUMBUKI KAMA AJALI YA NOORAH ILIKUWA NA UHUSIANO NA FIESTA

NOORAH hakupata ajali akiwa kazini alipata ajali akiwa na demu wake (sandra)

nakumbuka gari ilikuwa rav 4 huyo demu wa noorah alikuwa anasoma uganda (Kenya ndio sahihi nimesahihishwa) na alikuja tanzania bila kwao kujua

lengo lilikuwa kumuona bwana ake akiperfom sasa baada ya noorah kumaliza show yake wakawa wanarudi wote wamelewa na wako speed ulitokea ubishani

maana noorah alikuwa anataka kumrudisha yule demu kwao(oysterbay) na yule demu hataki kurudi kwao maana nyumban kwao walikuwa wanajua yupo shule Kenya

katika mabishano huku gari ikiwa speed yule demu aliisukuma gear kwenye parking

kama ujuavyo gari za zaman hazikuwa na sensor za kutema gear ya packin gari inapokuwa speed kali basi ilifanya tairi zote nne kufunga ghafla na gari ilibingirita mara nane

noorah hakufunga mkanda alitupwa nje ya gari na akapata ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu alikuwa anamkumbuka huyo demu tu...

na siyo kwamba alijipeleka hospital noorah alitoka eneo la ajali akiwa hajitambui kabisa alikuja kupata fahamu akiwa hospital

alikaa sana muhimbili hadi alipokuja kupona na kuendelea na mziki pamoja na masomo (IFM)

hawa jamaa fiesta wana mapungufu yao ila sometimes mnazidisha kuwaonea
 
Hii habari ungeweka source ya uhakika ingekuwa vizuri kwani naiona kama inaelea.
 
Hii ndio inaeleweka sasa
 
Aiseeeee Jamaa alikuwa anakula MADEMU wa OYSTERBAY 😳😳😳😳.
 

Wewe sasa ndo umeeleweka, sijui tukupe hati milki ya huu uzi maana umeonyesha ilivyokuwa na hali ilivyo sasa
 
Hili liko kwenye uwezo wa msanii mwenyewe. Kimsingi mtu unapoingia mkataba wowote ni juu yako wewe kuhakikisha una manufaa kwako. Hivyo wasanii wanatakiwa kusisitiza kuwekewa kipengele cha bima kwenye mikataba yao. Kama wanaona ni shida kukubaliwa basi wajiwekee wenyewe. Katika fani zote nadhani sanaa ndiyo yenye watu wanaopenda kulalamika lalamika hata kwa mambo wanayoweza kuyatatua wenyewe. Imefikia stage msanii akiugua anataka atibiwe kwa gharama ya serikali tena nje ya nchi wakati wakiwa wazima hawaishi kutanua.
 
Jamaa kachanganya madesa wewe ndo umeongea ukweli
 
asante mzee muanzisha thread atakuwa kwa sasa anachungulia tu, hili ndio tatizo la kuwa na data kidogo
 
Jimmie Gatsby, nadhani Sandra alikuwa anasoma Kenya na sio Uganda.

Lakini pia kwenye hiyo ajali, Sandra alivunjika mguu na meno au jino la mbele kutoka.

Mzee wake alikasirika sana na ile issue. Mara ya mwisho kumuona Sandra wakati anapona ni mbezi beach kwenye mgorofa, mawazo yangu yote nilijua hapo ndiyo kwao na sio oysterbay.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…