Nakumbuka baadhi ya majina ya walimu waliyopewa na wanafunzi kama ifuatavyo:
1. Solar system - mwalimu wa geograph form 1 au 2 alifundisha solar system akapatiwa jina hapohapo
2. Bambabay - mwalimu wa commerce form 3 alikua akielezea transport system,akaitaja bambabay ndio ikawa jina lake.
3.magazijuto - mwalimu wa hisabati darasa la saba alifundisha magazijuto na yeye ndio ikawa jina lake la utani au aka
4. Chonya of chilimwa - mwalimu wa kiswahili secondary alisoma habari za chonya of chilomwa akawa ndio jina lake
tupeni majina zaidi
Huu wimbo, ulikua na neno kama 'chukuru-chukuru-chu' halafu wanaitikia 'baasuba' unasikia tena 'okaye' basubabasuba-mwalimu wa english tulimfuma kona anacheza wimbo mmoja hivi wa kikongo uliokuwa na kikorombwezo basubaaaa
Kale kajamaa kalikotokea Bismarck Sec au mwingine?Mkwele alikua mkuu islamiya sec school mwz akiitwa hivo kutokana na kumfanana sana mkwele wa mizengwe kwa kila kitu
Umefika hadi sekondari unaandika hovyo mamna hii. Habari nzima hamna nukta umejaza mikato tuu.Kuna ticha tulikuwa tunafundisha naye shule x alikuwa wa history, sasa yeye alikuwa anafundisha topic ya African resistance kidato cha tatu,kwenye kipengere cha Nama and Herero resistance,basi watoto wakawa wanamwita Mwalimu Herero,nikiwa mgeni shuleni pale nikiwa na three months ,sijui hili wala lile ,na huyo ticha alikuwa mshikaji wangu sana,basi akaja mwanafunzi tukiwa na walimu wengine anataka kuchukua chaki ,basi akaulizwa na moja ya walimu nani kakuagiza chaki ,mtoto akijibu mwl Herero,duh likawa jina geni kwa walimu,bahati mbaya hata mtoto mwenyewe alikuwa hajui jina sahihi la mwalimu,akabidi amuelezee kwa phiscal appearance ndo tukamuelewa,staff mzima ilibaki kucheka tu
Sent using Jamii Forums mobile app
Ndio walimu wetu hao!Umefika hadi sekondari unaandika hovyo mamna hii. Habari nzima hamna nukta umejaza mikato tuu.
Halafu ni kipengele sio Kipengere.
Ni physical sio Phiscal.
Umechezea ada ya baba yako.