Mgagaa na Upwa
JF-Expert Member
- Sep 30, 2013
- 13,481
- 28,116
Mwalimu Wajad a.k.a mdudu wa jitegemee huyu jamaa alikuwa noma
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nakumbuka baadhi ya majina ya walimu waliyopewa na wanafunzi kama ifuatavyo:
1. Solar system - mwalimu wa geograph form 1 au 2 alifundisha solar system akapatiwa jina hapohapo
2. Bambabay - mwalimu wa commerce form 3 alikua akielezea transport system,akaitaja bambabay ndio ikawa jina lake.
3.magazijuto - mwalimu wa hisabati darasa la saba alifundisha magazijuto na yeye ndio ikawa jina lake la utani au aka
4. Chonya of chilimwa - mwalimu wa kiswahili secondary alisoma habari za chonya of chilomwa akawa ndio jina lake
tupeni majina zaidi
Enzi hizo nipo NJOSS kuna Mwl. tulikuwa tunamwita RAMBO ni marehemu sasa. Toka naingia form one hadi form four sijawahi muona akicheka wala kutabasamu. RIP Mwl. Rambo
Umenikumbusha mbali Rambo. pia tulikuwa na mkuu wa shule Mwanyigu sisi tulikuwa tukimwita Kichuma kutokana na staili yake ya kuchapa viboko kwa kichuma mboga. Pia Njoss alikuwepo mwalimu Tyson.
Nakumbuka baadhi ya majina ya walimu waliyopewa na wanafunzi kama ifuatavyo:
1. Solar system - mwalimu wa geograph form 1 au 2 alifundisha solar system akapatiwa jina hapohapo
2. Bambabay - mwalimu wa commerce form 3 alikua akielezea transport system,akaitaja bambabay ndio ikawa jina lake.
3.magazijuto - mwalimu wa hisabati darasa la saba alifundisha magazijuto na yeye ndio ikawa jina lake la utani au aka
4. Chonya of chilimwa - mwalimu wa kiswahili secondary alisoma habari za chonya of chilomwa akawa ndio jina lake
tupeni majina zaidi
Von soden= mwalimu wangu wa history la sita (topic ya scramble for and partition of africa)
Diki short form ya DICTATOR= rector wangu secondary alikuwa mkali dunia nzima
Perfomerr= Mwalimu wangu na manual work cordinator, huyu jamaa alikuwa kama john cena ulingoni
Maya= mwalimu wangu wa commerce na book keeping; alikuwa mtu mzima but she behaved like a teenager
Lawino= mwalimu wangu wa literature aligombana na mumewe zikachapwa kavu kavu shuleni tena baada ya parade ya saa tisa.
Babu= ni kawaida kwa walimu wazee
Mandible= mwalimu wangu wa biology form three alikuwa na mdomo mpana balaa
Kenge= huyu ticha alikuwa mkali halafu ana sura ka jiwe
Nyerere= mwalimu wangu wa siasa la tano, mwaka mzima alifundisha juu ya azimio la Arusha
kipipa= alikuwa mwalimu wangu wa kiingereza la nne, alikuwa binti na kiherehere usiombe ukutwe na kosa halafu upelekwe ofisini na ye awepo alikuwa na umbo la mviringo mwili mzima ka mpira.
Kimbilio= huyu alikuwa maza angu si mnajua alikuwa ticha wa primari? alikuwa mpole na alipenda kuwatetea madenti!
Faru huyu aliitwa Mwl Byarugaba, alikuwa akitokea kule BK kwa kina iwe, alikuwa ka faru, uwe na kosa huna ukikutana naye unakula kwenzi (nyundo). Alipenda sana kunywa "pingu" hata aubuhi alikuwa nzwi!
Kuni= huyu mama nadhani hakuwa na bajeti ya mkaa manake kila ijumaa alituagiza kuni!
Jamani tumetoka mbali!
Umenikumbusha mbali Rambo. pia tulikuwa na mkuu wa shule Mwanyigu sisi tulikuwa tukimwita Kichuma kutokana na staili yake ya kuchapa viboko kwa kichuma mboga. Pia Njoss alikuwepo mwalimu Tyson.
Halafu haya majina wkt mwingine husababisha hadi mwanafunzi unakuwa humfahamu mwalimu jina lake halisi...Kila anayekuuliza unamtajia jina hili hujui jina la mwalimu la kweli..
ISNT IT, mwl wa kemia f2 alikuwa kila baada ya sentens anasema isnt it ndo likawa jina lake.
NTAKULIMA, Alikuwa akikukuta na kosa anakuambia ntakulima bakora.
KISIKIO. Sikio lake moja lilikuwa kama limekatwa
aha haaa,umenikumbusha mbali,cjui yupo wapi huyu mzee cku hizi,aliwahi kunityt,kisa nimeingia dini darasa la wahindi,palikuwa hapatoshi,alichukua madaftari yangu akakaa nayo karibu siku nzima!daaah