Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 17,048
- 22,790
Mkuu Jasusi,
Heshima mbele sana, nimewahi kuongea na mkulu mmoja aliyehudhuruia hicho kikako OAU, kule Adis ambako Nkurumah alikuwa amepania sana kuanzisha huo muungano wa Afrika na jinsi alivyokuwa akumuona Mwalimu kama ni tatizo katika hiyo ndoto yake ya kuwa rais wa kwanza wa huo muungano,
Nkurumah alifanya mambo mengi ya aibu sana kwenye hicho kikao, akijaribu kummshusha hadi Mwalimu, lakini Mwalimu hakuonyesha kuwa na wasi wasi naye wala kugombea hiyo power kama Nkurumah alivyofikiri, mkulu aliniambia kuwa katika hiyo kiu ya power Nkurumah alisafiri sana kuonana na Wareno, watawala wa Then Mozambique, katika kutafuta njia za kuiua EAA,
Anyways, ninakushukuru sana mkuu kwa kuweka habari hii sawa, kwa kweli tunakula elimu nzito sana hapa.
Hilo la Nkurumah kupinga alichokiita "Balkanization of Africa" na kutaka Africa nzima iungane kuunda United States of Africa ni la kweli na limekuwa documented sawasawa, na Nyerere aliwahi kuliongelea mara nyingi sana katika hotuba zake. Vile vile ile tamaa yake ya kutaka kuwa George Washington wa United States of Africa linajulikana sana ingawa hilo halikuwa documented nadhani ili kumtunzia heshima. Nilikuwa sifahamu kuwa ndiye alikwamisha juhudi za Nyerere za kuchelewesha uhuru wa Tanganyika kuwasubiri ndugu zetu wa Kenya na Uganda kusdi tuunde Shirikisho la Afrika ya Mashariki, na nawashukuru sana FMES na Jasusi kwa kulileta. Nilichopinga hapo nyuma ni hii EAC ambayo iliundwa mwaka 1967 baada ya yeye kuwa alishafukuzwa huko kwao.
Hata mimi nimewahi kusimuliwa kuwa wakati wa mkutano wa kuundwa kwa OAU mwaka 1963 kule Ethiopia, baadaye Nkrumah alimwomba Nyerere samahani baada ya kugundua kuwa katika mkutano ule , Nyerere aliokena kuwa more intellectual na alionekana kusikilizwa zaidi na viongozi wengine wengi hasa Mfalme Haile Selassie, ambaye alikuwa anaheshimiwa na viongozi wote wakati huo, na Gamal Abdul Nasser.
Charter ya OAU iliyosainiwa na viongozi hao siku hiyo ni hii hapa, kwa wale ambao walikuwa hawajaiona: