1.
kabla ya kujiunga na Simba Ezekiel Greyson 'Jujuman' alijinga kwanza na Yanga mwishoni mwa mwaka 1975 akiwa miongoni mwa wachezaji wenye umri mdogo wa timu hiyo. Ni Yanga ndio waliompa jina la Jujuman wakifananisha uchezaji wake na upigaji gitaa la Rithim wa mzaire Vata Mombassa 'Jujuman' wa Orch Lipua Lipua iliyokuwa ikitamba miaka hiyo na mipigo ya kavasha.
1. Ni kweli mkuu Ezekiel Greyson, akiwa Kurugenzi ya Kisarawe, alichaguliwa kuichezea timu ya mkoa wa Pwani kwenye Taifa Cup,ambako alinga'ara sana na kuchukuliwa na Yanga,
2. Huko nako alisifika sana na kuitwa "Jujuman", lakini akajitoa na kuingia Simba baada ya kushawishiwa sana na wa nyumbani mwenzake, aliyekuwa katibu wa Simba, Mkulu David Ngonya.
2.
Alikuwemo kwenye kikosi cha Yanga kilichotunguliwa 6-0 na Mnyama akiwa na akina Yanga Bwanga, Benard Madale, Boniface Makomole,Selemani Jongo, Ayoub Shabaan, Mwinda Ramadhani na wengineo. mwishoni mwa mwaka huo 1977 ndio akajiunga na Simba.
1. Baada ya mechi na Enugu Rangers, ilidaiwa kuwa Kitwana "Popat" Manara, alihongwa hela na Wa-Nigeria, ili asifunge kabisaa, na hasa alipokosa goli la wazi dakika za mwisho ndipo hiyo theory ikathibitishwa,
2. Yanga ikapata viongozi wapya kina Mohamed Misanga na David Mwambungu, ambao walidhani kuwa Le` Grande Mangara Tabu Mangara, aliyekuwa Supreme Leader wa Yanga then, ndiye aliyekuwa chanzo cha kina Kitwana kutokuwa na nidhamu, inasemekana hawa walikuwa wametumwa na baadhi ya viongozi wakuu wa serikali waliokuwa wapenzi wa Yanga, kwenda Yanga kurekebisha mambo hasa ya nidhamu,
3. Lakini wakagonga mwamba pale wachezaji, ambao wengi walikuwa Royal kwa Mangara, walipokataa kukubali sheria zao mpya, viongozi hao wakaamua kutumia ubabe kwa kuwapa conditions mpya wachezaji hao na wasipokubali watakuwa wamejifukuza wenyewe kwenye team, Wachezaji wakagoma na ndipo ikaundwa Pan Afrika (Panya), na wengine wakajiunga na timu ya kampuni ya Sigara, lakini huko mbele ya safari wote walijiunga na Pan.
a. Baadhi ya wachezaji hao walioenda Pan moja kwa moja, ni pamoja na Jella Mtagwa, Juma Matokeo, Juma Shaaban, Sunday Manara, Kitwana Manara, Patric Nyaga, Maulid Dilunga, Omar Kapera, James Mwalusako, na wengineo.
b. Walioenda Sigara ni pamoja na Juma Pondamali, Hussein Mkweche, Jafari Abdulrahaman, Rashid Idd "Chama", Adolf Rishad, Mohamed Yahaya "Tostao", Kassim Manara, na Gordian Mapango, chini ya kocha Saaban Marijan.
c. Lakini baadaye wote walijiunga na Pan, ingawa Sunday na Kassim, walienda Holland kucheza pro-ball, baadaye pia Nico Njohole naye aliondoka, huku kina Haidari Abeid, Bakari Tall, Jummane Masuminti, Ahmed Amasha, Isihaka Kaungu, Aluu Ally, nao wakazamia Uarabuni kucheza Pro.
d. Shaaban Katwila, George "Best" Kulagwa, Isaack Mwakatika, wakahamia Burundi kucheza Pro pia, kwenye timu ya soka ya rais wa huko Bagaza, kwa jina Intele au (International)