kazi nzuri wakuu......Mimi naomba kama anaweza kujua majina ya hawa vijana walioshika hilo bakuli ambalo mwalimu anachanganya mchanga huo na bado wako hai?mbona sijawahi kusikia wakikumbukwa.......pia hao akina mama kushoto ni akina nani na huyo mzee kushoto anaepiga makofi......
FMES,
..Hussein Tindwa hakuwa mshambuliaji.
..nadhani Hussein Tindwa ndiye mrithi wa Omar Chogo.
..halafu Mohamed Bakari "Tall" alikuja kumrithi Tindwa[r.i.p].
..Baada ya Omar Mahadhi alifuata Athumani Mambosasa.
..sina uhakika kama Moses Mkandawile alicheza kabla au baada ya Iddi Pazi.
..nina uhakika Iddi Pazi hakucheza na Mohamed Kajole. Pazi amecheza miaka ya kina Raphael Paul, Mussa Kiwelu, na Lila Shomari.
..Halafu Willy Mwaijibe,Abdalah Mwinyimkuu, na Ezekiel Greyson "juju man," walicheza miaka ipi?
1. Kama ninakumbuka vizuri ni kwamba Yanga ilichukua wachezaji wawili toka Mlimani, nao ni Leodgar Tenga, na Edward Hizza, wote walikuwa benchi kwa sababu Tenga, alikuwa akimsaidia Hassan Gobbos, Hizza hakuweza hata kucheza mechi kubwa,
However, Yanga wakiwa wanajitayarisha kwa safari ya Brazil, Tenga na Hizza, waliitwa kwenye timu ya Mlimani, ili kuiwakilisha kwenye michezo ya Vyuo Vikuu iliyokuwa inafanyika Mexico, hivyo wote wawili wakashindwa kwenda Brazil na Yanga,
2. kwa sababu ninakumbuka vizuri sana kwamba baada tu ya mechi ya Nyamagana, ambapo Sunday na Sembuli waliifunga Simba, timu hizi ziilirudiana tena kwenye Uwanja Wa Tartan wa Zanzibar, kwenye finali ya Kombe la Ubingwa wa East and Central Afrika, ambako kwa mara nyingine tena Yanga waliishinda Simba kwa magoli mawili kwa moja, yaliyofungwa na wale wale Sunday Manara na Sembuli na this time Tenga alikuwemo ndani ya ile mechi upande wa Yanga, mechi mabayo kwa mara ya kwanza katika historia ya michezo bongo ilichezwa usiku.
Kipindi kati ya cha mechi ya Nyamagana na Zanzibar, kilikuwa ni kifupi sana kwamba Tenga ndio alijiunga na kuweza kucheza mechi kubwa namna ile, lakini I colud be wrong pia.
3. Wachezaji waliojiunga na Yanga kutokea Morogoro, baada ya kombe la Taifa, kwenye ngwe ya kwanza alikuwa ni Sembuli peke yake,
Ngwe iliyofuatia walikuwa ni kipa Patric Nyaga, Juma shaabani, Jella Mtagwa, na Juma Matokeo, Muhaji Mukhi, naamini alitokea timu ya mkoa wa Kigoma kama Makumbi Juma.
Ngwe ya mwisho ya wachezaji wa Morogoro kuingia Yanga, ilimalizwa na Ahmed Jongo na Omar Hussein. Otherwise, wakuu heshima mbele kwa historia na marekebisho, nia na madhumuni ni kuelimishana.
Hawa jamaa walicheza just at time Wanyama pori walipotuliza Jangwani 6-0 1976
Mwalimu,
Mambosasa na Mahadhi walipokezana hata baada ya Mahadhi kuanza kuachia ngazi.
Mkandawire na Pazi walipokezana pamoja na Nemes (Khadija Kopa).
Yanga nayokumbuka ni ile ya Bernard Madale, kisha akaja Dunia Adonis, kisha kuja nafikiri Hamisi Kinye. Kama sikosei, hata Steven Nemes alidakia Yanga kwa muda mfupi na alipomrithi Pazi, ndipo tulipoanza kumuita Khadija Kopa.
Pondamali alikuja mrithi Kinye, kisha akaja yule kipa kutoka Pamba, i am not sure kama alikuwa ni Lubigisa, but a cycle ya makipa wazuri walikuja Yanga huku Mwameja akishikilia usukani Simba kwa muda (possibly the longest Simba GK)
Je mwamkumbuka Paul Ssali wa KCC na Uganda Cranes?
Mkuu uko sawa-
1. Willy Mwaijibe - alikuwepo Mwanza, lakini akielekea ukingoni kwa sababu hata Chitete alikuwepo Nyamgana lakini ndio waliokuwa wakielkea mwishoni mwa career zao.
Ni kweli Idd Pazi "Father" Alikuwa hajaingia hapa ananikumbusha mbali sana huyu mkulu, ambaye niliwahi kucheza naye mpira utotoni, na mpaka leo ni jirani yangu kule Kinyerezi, maana huyu alikuwa kile kitu kinaitwa multi-talented, originally alikuwa mshambuliaji akitumia mguu wa kushoto nilicheza naye timu moja ya mabaharia Jangwani ya Muungano Sports Club,
Baadaye nilicheza naye tena kwenye timu ya kiwanda cha nguo cha Sungura-Tex, ambako mara kwa mara tulikuwa tukipambana na Kurugenzi ya Kisarawe timu ya Ezekieli Greyson "Jujuman", kabla hajachukuliwa na Simba. Nilipoamua seriously ku-stick na ubaharia, Idd Pazi na wachezaji wengine niliocheza nao pale kama Hamzuruni, na Makobe, wao walienda Nyota ya Mtwara, baadaye Idd alichukuliwa na Simba, Hamzuruni alichukuliwa na Yanga, Makobe naye alikuja Ummangani kwenye Meli.
Sasa hivi Idd ambaye ninawasiliana naye mara kwa mara, yupo Thailand ambako ni mfanya biashara mkubwa sana. wadogo zake Idd yaani Omar na Muhidini, nao pia waliwahi kuchezea Simba na Yanga, lakini hawakuwa na talent kama ya kaka yao Idd, the guy was just phenominal ninakumbuka kuna wakati wa mechi zetu za utotoni timu za adui zilikuwa zikimkataa kabisa kushiriki kwa sababu akiwa mdogo sana tayari alikuwa akichukuliwa kucheza timu za watu wazima, kwa hiyo maadui walidai kuwa asiruhusiwe kushiriki, off course sasa it sound like a joke, lakini I wish ungewepo uone how serious hii ishu ilikuwa.
2. Abdallah Mwinyimkuu "Carlos" na Ezekiel Greyson "Jujuman", hawa walikuwemo katika miaka ya kati kati ya 70s, kwa sababu nakumbuka sana ile mechi ya Simba na AS Vita ya Zaire, pale Uwanja wa Taifa, hawa wawili walikuwemo na kwenye lists ya zamani aliyekuwemo siku ile alikuwa ni Kibadeni,
Maana hizi zilikuwa enzi za kina Daudi Salum "Bruce Lee", unakumbuka Simba walikuwa na huyu mchezaji aliyetokea Tabora?
Rev. Kishoka, hapo pa Hamis Kinye umemsahau kipa aliyepata kuwa miongoni mwa makipa wazuri Yanga iliyowahi kuwa nao ambaye alikuwa akishindana na Hamisi Kinye...Joseph Fungo!!
IDDY PAZI NDIYE GOLKIPA ALIYEMRITHI OMAR MAHADHI BIN JABIRI WAKATI MAMBO SASA NDIYE ALIYEIPELEKA SIMBA NUSU FAINALI,
TINDWA NI KWELI ALIMRITHI CHOGO NA BAADA KUFA KWA TINDWA NDIPO MOHAMED BAKARY TALL ALIPORITHI MIKOBA AKIWA NA BRUCE LEE DAUD SALUM,
BAADA YA PAZI KUTIMKIA ELHILAL SUDAN 82-3 NDIPO MOSSES MKANDAWILE ALIPOBEBA JUKUMU HILO MPAKA 87
NI SIMBA PIA ILIYOBAHATIKA KUMPATA KIJANA WA KINDAMBA OCD DEO NJOHOLE(mungu mlaani Abbasy Gulamali kwa kumharibia maisha kijana huyu kwa kumlaghai), Mmenikumbusha mbali wakuu maana hayo muyasemayo ni utoto wangu primary hasa, mzee akiwa na ile 277 ya mbao wacha kabisa, It was more than fantastic,comrades,Thank you very much
kabla ya kujiunga na Simba Ezekiel Greyson 'Jujuman' alijinga kwanza na Yanga mwishoni mwa mwaka 1975 akiwa miongoni mwa wachezaji wenye umri mdogo wa timu hiyo. Ni Yanga ndio waliompa jina la Jujuman wakifananisha uchezaji wake na upigaji gitaa la Rithim wa mzaire Vata Mombassa 'Jujuman' wa Orch Lipua Lipua iliyokuwa ikitamba miaka hiyo na mipigo ya kavasha.
Alikuwemo kwenye kikosi cha Yanga kilichotunguliwa 6-0 na Mnyama akiwa na akina Yanga Bwanga, Benard Madale, Boniface Makomole,Selemani Jongo, Ayoub Shabaan, Mwinda Ramadhani na wengineo. mwishoni mwa mwaka huo 1977 ndio akajiunga na Simba.
Kasi ya picha imepungua!!!
1.
Katika hiki kipindi Simba iliwahi kuwa na mabeki kama Omar Choggo/Aloo Mwitu/Isihaka Mwitu/Athumani Juma/Mohamed Bakari "Tall"/Nico Njohole/Daudi Salum/Shabaan Baraza/Kajole Machela/Malota Soma/Raphael Paul, au?
Mkuu FMES na wote,
Shukurani sana kwa kutukumbusha historia hii ya kabumbu ... nasikitika kuwapa taarifa kwamba kwamba Nico Njohole ni mgonjwa sana .. yuko Uingereza. Nitawapa taarifa zaidi kadri hali yake itakavyokuwa inaendelea.
Kasi ya picha imepungua!!!
Shukurani sana kwa kutukumbusha historia hii ya kabumbu ... nasikitika kuwapa taarifa kwamba kwamba Nico Njohole ni mgonjwa sana .. yuko Uingereza. Nitawapa taarifa zaidi kadri hali yake itakavyokuwa inaendelea.
..huyo askari mwenye miwani ndiye nani? je aliyemuua Karume ni mmoja kati ya walinzi wake?