Tukumbuke Zamani: Historia ya Taifa letu katika picha


Reverend,

Nadhani kuwa hiyo pointi yako niliyowekea rangi ndiyo sahihi kabisa. Ukiangalia ile ripoti ya CIA ya mwaka 1965 niliyoweka kwenye thread nyingine inaonyesha wazi kuwa jamaa hawa hakupenda kabisa mambo yote yaliyokuwa yakifanywa na Nyerere; kwa hiyo jambo la kwanza walilolenga ni kubomoa kila jambo lilioachwa na Nyerere, na kwa bahati mbaya waliwapata vibaraka wa kutumia kukamilisha lengo lao. Kikwete ameongeza chumvi kwenye donda lilioachwa na Mkapa na Mwinyi. I still believe that SAS could have repaired all the mess created by Mkapa and Mwinyi. Hebu sikiliza ujumbe ulioko kwenye kibao hiki hapa.
 
Mwalimu,

Shukrani sana kwa wimbo huo, umenikumbusha mbali sana.

Ukisikiliza ule wimbo wa "mimi msafiri" unasema;

Mimi msafiri nipo njiani,
Sijui lini nitafika,
Naulizia watu kule ninapokwenda,
Waniambia ni ni mbali,
kutwa kucha nipo njiani

mwili umechoka maungo yamelegea,
kweli nimejitahidi mpaka nifike kule ninakokwenda
...Mungu aniangazie mwanga...

Njoo kwenye wimbo wa Marquis, nasema sina ndugu,

Nasema sina ndugu, wakuweza kunisaidia,
Nikifa leo na kesho maiti yangu ni bure
yatatupwa kama mbwa na kuyasahau pale pale

Nikizisikiliza na kuziimba hizi nyimbo, najiuliza ni falsafa ya namna gani tuliyokuwa tumejijengea. Sichukulii kama nafsi yangu kama binadamu, bali kama Taifa tukiimba nyimbo hizi.

Franklin Boukaka alipoimba Le Bucheron na Les Immortels ilikuwa ni kuhusu African struggle! same struggle continues today na ndio maana nauliza Tanzania inasema sina ndugu wa kuweza nisaidia na kuwa badi ni msafiri njiani sijui lini tutafika!
 
Najua hapa tunaongelea Tanzania lakini naomba niwape sauti ya Franklin Boukaka!

http://www.youtube.com/watch?v=wKvwxqv8Ot4&feature=related

http://www.youtube.com/watch?v=o1ERQ0LQawI


Asante sana kwa nyimbo hizi. In fact, huo wimbo wa pili ni kati ya nyimbo ambazo huzikosi kwenye gari yangu. La ajabu ni kuwa siku zote nilikuwa naamini kuwa ni wimbo wa Dr. Nico. Inaelekea kuwa nilichelewa sana kwani jina la Franklin halikuwapo kabisa kwenye orodha ya wanamziki wa kikongo ninaofahamu.

Asante sana kwa nyimbo hizi; inaelekea alikuwa mwana mapinduzi kweli kweli
 

Nilisoma mahali hii story ilikuwa ndefu tu, na kulikuwa na picha yake na certificate aliyopewa kama mshindi katika kubuni jina. nadhani anaitwa Ahmadi, Mohammed Iqbal (more soon)
 
Nilisoma mahali hii story ilikuwa ndefu tu, na kulikuwa na picha yake na certificate aliyopewa kama mshindi katika kubuni jina. nadhani anaitwa Ahmadi, Mohammed Iqbal (more soon)

Hata mimi niliwahi kusoma story hiyo lakini nimeshindwa kuweka comment kwa vile sikumbuki niliisoma wapi. Alisema kuwa alichukua herufi tatu za TAN kutoka jina Tanganyika, na herufi nyingine tatu za ZAN Kutoka jina Zanzibar, halafu akamilizia na herufi mbili IA za jina lake. Inawezekana alikuwa akiitwa Iqbal Ahmed, au jina lolote linalohusiana na herufi za IA; na nakumbuka alisema kuwa anaishi Uingereza sasa hivi.
 

Iddi Abdallah Pengo 1942 Mogadishu

Kati watanzania waliopigana katika jeshi la Kings African Rifles. Hawa walito mchango mkubwa sana katika vuguvugu la uhuru wa nchi yetu


Idd Pengo 2007.

Lakini yupo pia Ally Skyes aliye pigana Burma


Huyu anamchango mkubwa sana katika historia ya Tanzania. He is the one who "... personally came up with the name of TANU and the party emblem of the Green (peace) and Black (the Africans) and this was while still in Burma" Ilichukua takribani miaka 16 mpaka TANU alipoanzishwa rasmi na yeye kupata kadi namba 2. Alikuwa ni baba yake aliyeanzisha TAA mwaka 1929.


Mzee Ally Sykes ni aliye kushoto mwa Raisi Kikwete

Historia ya uhuru wetu inaanzia haswa kwa hawa wazee waliopigana katika vita ya pili ya dunia. Kuna haja ya kuchukua historia zao mapema na kuziweka sawa. Wengi wao waliobaki wako in thier late 70's and above.
 



Gazeti lenyewe ni The Independent (Tuesday, 12 June 2007). The story runned under the title "Mohammed: How this popular name tells story of changing nation" Mmoja wa wahojiwa ndie "Mohhamed Iqbal Dar" ambaye katika hayo mahojiano anasema ndiye aliye ipa Tanzania Jina lake.
Here is the print..
"Mohamed Iqbal Dar, 62, Radio and TV Engineer, Birmingham
I was born in Tanzania. I named the country, actually. There was a competition to change the names of Tanganyika and Zanzibar. I was a student and I picked the letters from the two words.

I came to the UK in 1962 to study. It was easy to get used to Britain. There is a bit of racism, but I cope well. I love this country. I was educated here and I'm proud to be British. People are very civilised here.

My name is great. The Holy Book was revealed to the Prophet Muhammad, so most people prefer to have his name. We follow his footsteps and most parents want to name their children after him.

I have two brothers and they are both named after the Prophet, too. It's not confusing: we call each other by the middle name. The name is easy to remember. It is spelt differently from the Prophet because that is the way it is on my birth certificate. But it's the same thing. I'm proud of it."


Ingawa story ilikuwa kuhusu jina Mohhamed anajitambulisha kama mshindi wa shindano la kutafuta jina Tanzania. (Bado natafuta certificate yenyewe)
 
asante sana mzeeba,i think story niliyosoma mimi was not this one,i cleary remember it was some serious piece of investigative journalism,which left you in no doubt that,mdai wa jina la tanzania,was telling the truth
 
"Mohamed Iqbal Dar, 62, Radio and TV Engineer, Birmingham
I was born in Tanzania. I named the country, actually. There was a competition to change the names of Tanganyika and Zanzibar. I was a student and I picked the letters from the two words.

Heshima mbele mkuu, ahsante kwa kipande hiki cha historia.
 

Mzee kweli umeondoka siku nyingi sana huku na pia unawezekana hupewi updates za huku.
Movie theaters ziko mbili Dar mpya na Arusha pia.Za Dar,moja iko Mwenge ambayo inaonyesha movie za kihindi tu(kuna theaters 3 au 4 hapo),then kuna nyingine Mlimani City,karibu na chuo kikuu,kuna shopping mall mpya pale.Hao wana theaters kama tatu hivi...huko ni movies za kizungu tu.

http://www.africa-beat.com/films.aspx
 
asante sana mzeeba,i think story niliyosoma mimi was not this one,i cleary remember it was some serious piece of investigative journalism,which left you in no doubt that,mdai wa jina la tanzania,was telling the truth

Nakubaliana na wewe kabisa kuhusu hili. Nakumbuka story ili run katika matoleo mawili ya gazeti (Mwanachi???). Jamaa alikuwa amekuja Tanzania kwenye harusi ya ndugu yake (how we remember the wrong things!!!). Habari yenyewe ilielezea na majina mengine yaliyoshika nafasi ta pili na ya tatu. Certificate alisema anayo UK. Anybody who know this guy or a guy who knows a guy, ili walau tupate hio certificate kama ukumbusho hapa.
 


Mkuu, pongezi. nilichelewa kuchangia kwa sababu nilikuwa natafuta hili jina lilikuwa limenitoka akilini kidogo. Huyu ndio aliwapelekesha jamaa pale mitaa ya Kinondoni wakati wanajaribu kumkamata. Ilikuwa ni 'Picha' worth the 'Bourne' trilogy!
 
kichuguu,FMES,babaDesi,Jasusi,Rev.Kishoka,mzeeba,.....

..vipi kuhusu wimbo wa taifa? hivi ulitungwa na nani?
 


Kuna Story nilipata kuisoma kwenye miaka ya mwanzo ya 80' kwenye gazeti la Africa Now ambapo ilielezwa kuwa miongoni mwa majina ya mwisho ambayo yalipigiwa kura ilikuwa ni pamoja na Tangibar[/I]
 

I think it's good sometimes to call a spade a spade. And thanks mkuu Marshall kwa hii post, maana kuwa wengi humu hawapendi kabisa wanaposikia neno kuwa "bado wabongo wamelala usingizi." .
 

Wakuu, nani anafahamu [kiundani] kuhusu uhaini wa aliyewahi kuwa the first Chief of Defence Forces, General Mrisho Sam Hagai Sarakikya...? Niliwahi kusimuliwa zamani kuwa huyu jamaa alipanga kuipindua nchi/ua Nyerere enzi hizo[Lugalo], na kwamba mtu pekee aliyeokoa hayo mapinduzi alikuwa ni General David Musuguri. Je, ni kweli? Aliye na picha ya Sarakikya, please, do me a favor, tuwekee hiyo pic hapa...
 

Gustanza,
Ninachofahamu mimi, kwa mujibu wa sources zilizokuwa karibu na Mwalimu wakati huo, ni kwamba njama za Sarakikya hazikugunduliwa na Musuguri, bali maafisa wa usalama wa taifa. Mwalimu aliarifiwa na akamwita Sarakikya nyumbani kwake pale Msasani. Alimwonyesha kile kiti alichokuwa amekikalia na kumwambia kuwa kama anataka hicho kiti basi awaombe raia wa Tanzania waliomkabidhi Mwalimu na si kutumia njama zitakazoleta umwagaji damu nchini. Baaada ya hapo Sarakikya aliondolewa jeshini na kupewa kazi ya ubalozi nchi ya nje.
 

Jasusi,

..I thought Sarakikya alipoondolewa jeshini aliteuliwa kuwa Waziri wa Michezo....??

..halafu Major Kavana alipotelea wapi? najua ni utamaduni wa CDF kuondoka na Chief of Staff wake, lakini sijui Kavana alipelekwa wapi baada ya kutoka jeshini.

..Kavana alikuwa ni kati ya maofisa wa Jeshi wasomi. he graduated with a Physics degree frm London Univ. wakati huo ukisoma science Makerere ulikuwa unahitimu na degree ya London Univ.

..kuna kipindi maofisa vijana wasomi waliondolewa toka jeshini na kupelekwa kwenye mashirika ya umma. je walihusika na jaribio hilo la Sarakikya?

..hivi Mwalimu alitaka kupinduliwa mara ngapi? maana kuna tetesi nyingine nilisikia kuhusu Mwalimu kuwa na mazungumzo na majenerali[musuguri,kiwelu,mayunga,..] kama aliyokuwa nayo na Sarakikya, lakini hayo yalifanyika Monduli.
 
kichuguu,FMES,babaDesi,Jasusi,Rev.Kishoka,mzeeba,.....

..vipi kuhusu wimbo wa taifa? hivi ulitungwa na nani?

Nakumbuka kuambiwa na mwalimu mmoja wa Mziki kuwa wimbo wa Taifa ulitungwa na Nyerere mwenyewe. Aliweka maneno ya kiswahili kwenye melody ya Nkosi Sikeleli IAfrika uliotungwa na mwalimu mmoja wa kizulu Enoch Sontonga mwaka 1887. Ni wimbo maarufu sana unaotumia kama wimbo wa Taifa na nchi nyingi kusini mwa Afrika. Hebu soma hapa:

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…