Tukumbuke Zamani: Historia ya Taifa letu katika picha

Tukumbuke Zamani: Historia ya Taifa letu katika picha

Mwalimu,

Je kunauwezekano kuwa kuvuruga kwa maendeleo kiduchu tuliyokuwa nayo yalitokana na woga wa nchi zilizoendelea kuwa tukiachiwa huru tukajitutumua kwa udhaifu wa uchumi wetu lakini tukiwa na msimamo, tungekuwa mfano wa kuigwa na hivyo kuvunja nguvu za kuwa Taifa tegemezi?

Je Mwinyi, Mkapa na hata Kikwete sasa hivi wamepumbazwa kabisa kwa nyimbo nzuri za globalization na free market economy bila kujua athari zake kwa uchanga wa Taifa kama letu ambalo bado halijawa na Wananchi wazawa wenye uwezo wa kuzalisha na kumiliki misingi na njia za uchumi?

Reverend,

Nadhani kuwa hiyo pointi yako niliyowekea rangi ndiyo sahihi kabisa. Ukiangalia ile ripoti ya CIA ya mwaka 1965 niliyoweka kwenye thread nyingine inaonyesha wazi kuwa jamaa hawa hakupenda kabisa mambo yote yaliyokuwa yakifanywa na Nyerere; kwa hiyo jambo la kwanza walilolenga ni kubomoa kila jambo lilioachwa na Nyerere, na kwa bahati mbaya waliwapata vibaraka wa kutumia kukamilisha lengo lao. Kikwete ameongeza chumvi kwenye donda lilioachwa na Mkapa na Mwinyi. I still believe that SAS could have repaired all the mess created by Mkapa and Mwinyi. Hebu sikiliza ujumbe ulioko kwenye kibao hiki hapa.
 
Mwalimu,

Shukrani sana kwa wimbo huo, umenikumbusha mbali sana.

Ukisikiliza ule wimbo wa "mimi msafiri" unasema;

Mimi msafiri nipo njiani,
Sijui lini nitafika,
Naulizia watu kule ninapokwenda,
Waniambia ni ni mbali,
kutwa kucha nipo njiani

mwili umechoka maungo yamelegea,
kweli nimejitahidi mpaka nifike kule ninakokwenda
...Mungu aniangazie mwanga...

Njoo kwenye wimbo wa Marquis, nasema sina ndugu,

Nasema sina ndugu, wakuweza kunisaidia,
Nikifa leo na kesho maiti yangu ni bure
yatatupwa kama mbwa na kuyasahau pale pale

Nikizisikiliza na kuziimba hizi nyimbo, najiuliza ni falsafa ya namna gani tuliyokuwa tumejijengea. Sichukulii kama nafsi yangu kama binadamu, bali kama Taifa tukiimba nyimbo hizi.

Franklin Boukaka alipoimba Le Bucheron na Les Immortels ilikuwa ni kuhusu African struggle! same struggle continues today na ndio maana nauliza Tanzania inasema sina ndugu wa kuweza nisaidia na kuwa badi ni msafiri njiani sijui lini tutafika!
 
Najua hapa tunaongelea Tanzania lakini naomba niwape sauti ya Franklin Boukaka!

http://www.youtube.com/watch?v=wKvwxqv8Ot4&feature=related

http://www.youtube.com/watch?v=o1ERQ0LQawI


Asante sana kwa nyimbo hizi. In fact, huo wimbo wa pili ni kati ya nyimbo ambazo huzikosi kwenye gari yangu. La ajabu ni kuwa siku zote nilikuwa naamini kuwa ni wimbo wa Dr. Nico. Inaelekea kuwa nilichelewa sana kwani jina la Franklin halikuwapo kabisa kwenye orodha ya wanamziki wa kikongo ninaofahamu.

Asante sana kwa nyimbo hizi; inaelekea alikuwa mwana mapinduzi kweli kweli
 
hili jina tanzania,lina utata,kuna muhindi alihojiwa na gazeti la guardian la uingereza,about two yers ago,akidai yeye ndio ali coin hilo jina,this indian alihaidiwa zawadi,lakini hakupewa,katika government circles wanadai ni nyerere ndio alianzisha hilo jina.kinachojulikana ni kwamba tender ya kuchagua jina kweli ilitolewa na zawadi kuhaidiwa

Nilisoma mahali hii story ilikuwa ndefu tu, na kulikuwa na picha yake na certificate aliyopewa kama mshindi katika kubuni jina. nadhani anaitwa Ahmadi, Mohammed Iqbal (more soon)
 
Nilisoma mahali hii story ilikuwa ndefu tu, na kulikuwa na picha yake na certificate aliyopewa kama mshindi katika kubuni jina. nadhani anaitwa Ahmadi, Mohammed Iqbal (more soon)

Hata mimi niliwahi kusoma story hiyo lakini nimeshindwa kuweka comment kwa vile sikumbuki niliisoma wapi. Alisema kuwa alichukua herufi tatu za TAN kutoka jina Tanganyika, na herufi nyingine tatu za ZAN Kutoka jina Zanzibar, halafu akamilizia na herufi mbili IA za jina lake. Inawezekana alikuwa akiitwa Iqbal Ahmed, au jina lolote linalohusiana na herufi za IA; na nakumbuka alisema kuwa anaishi Uingereza sasa hivi.
 
Iddi Pengo Mogadishu 1942.jpg
Iddi Abdallah Pengo 1942 Mogadishu

Kati watanzania waliopigana katika jeshi la Kings African Rifles. Hawa walito mchango mkubwa sana katika vuguvugu la uhuru wa nchi yetu

_43038573_iddi203.jpg
Idd Pengo 2007.

Lakini yupo pia Ally Skyes aliye pigana Burma
_43038571_ally-sykes203.jpg

Huyu anamchango mkubwa sana katika historia ya Tanzania. He is the one who "... personally came up with the name of TANU and the party emblem of the Green (peace) and Black (the Africans) and this was while still in Burma" Ilichukua takribani miaka 16 mpaka TANU alipoanzishwa rasmi na yeye kupata kadi namba 2. Alikuwa ni baba yake aliyeanzisha TAA mwaka 1929.

Sykes na Kikwete.JPG
Mzee Ally Sykes ni aliye kushoto mwa Raisi Kikwete

Historia ya uhuru wetu inaanzia haswa kwa hawa wazee waliopigana katika vita ya pili ya dunia. Kuna haja ya kuchukua historia zao mapema na kuziweka sawa. Wengi wao waliobaki wako in thier late 70's and above.
 
Wakuu heshima mbele, naomba kuuliza nini uasilia wa jina Tanzania? Je lilitokana na majina ya Tanganyika na Zanzibar? Kama ndio ni nani aliyelicoin hilo jina? Walikuwa ni viongozi wa nchi hizo mbili, chama,kamati maalum au kuna mtu binafsi alilitunga?

Je kulikuwa na options zingine (kwa mfano Tanzibar) ndo hili la Tanzania likachaguliwa?

Inawezekana hili swali likawa la kipuuzi kwa wazee waliobobea kwenye historia ya nchi yetu, naomba mnivumilie maana hii kitu sikumbuki kuambiwa katika somo la historia nikiwa shule ya msingi nakupitia thread hii gafla limenijia kichwani...........

hili jina tanzania,lina utata,kuna muhindi alihojiwa na gazeti la guardian la uingereza,about two yers ago,akidai yeye ndio ali coin hilo jina,this indian alihaidiwa zawadi,lakini hakupewa,katika government circles wanadai ni nyerere ndio alianzisha hilo jina.kinachojulikana ni kwamba tender ya kuchagua jina kweli ilitolewa na zawadi kuhaidiwa


Gazeti lenyewe ni The Independent (Tuesday, 12 June 2007). The story runned under the title "Mohammed: How this popular name tells story of changing nation" Mmoja wa wahojiwa ndie "Mohhamed Iqbal Dar" ambaye katika hayo mahojiano anasema ndiye aliye ipa Tanzania Jina lake.
Here is the print..
"Mohamed Iqbal Dar, 62, Radio and TV Engineer, Birmingham
I was born in Tanzania. I named the country, actually. There was a competition to change the names of Tanganyika and Zanzibar. I was a student and I picked the letters from the two words.

I came to the UK in 1962 to study. It was easy to get used to Britain. There is a bit of racism, but I cope well. I love this country. I was educated here and I'm proud to be British. People are very civilised here.

My name is great. The Holy Book was revealed to the Prophet Muhammad, so most people prefer to have his name. We follow his footsteps and most parents want to name their children after him.

I have two brothers and they are both named after the Prophet, too. It's not confusing: we call each other by the middle name. The name is easy to remember. It is spelt differently from the Prophet because that is the way it is on my birth certificate. But it's the same thing. I'm proud of it."


Ingawa story ilikuwa kuhusu jina Mohhamed anajitambulisha kama mshindi wa shindano la kutafuta jina Tanzania. (Bado natafuta certificate yenyewe)
 
asante sana mzeeba,i think story niliyosoma mimi was not this one,i cleary remember it was some serious piece of investigative journalism,which left you in no doubt that,mdai wa jina la tanzania,was telling the truth
 
"Mohamed Iqbal Dar, 62, Radio and TV Engineer, Birmingham
I was born in Tanzania. I named the country, actually. There was a competition to change the names of Tanganyika and Zanzibar. I was a student and I picked the letters from the two words.

Heshima mbele mkuu, ahsante kwa kipande hiki cha historia.
 
Hivi kweli biashara ya sinema hapo Dar bado iko active tena? Nadhani eneo lote la Drive Inn lilichukuliwa na ubalozi wa marekani, na Empress waligeukia biashara ya kubadilisha hela za kigeni (Bureau De Change). Thieta hizo nyingine nadhani zilijifia kifo cha mende tangu ukodishaji wa kanda za video uanze. Nadhani biashara hiyo itaweza kufufuka tena iwapo tu zitajengwa thieta za kisasa zaidi na kufungua mtandao mzuri wa kupata sinema mpya mpya kabla hazijawekwa kwenye DVD.

Mzee kweli umeondoka siku nyingi sana huku na pia unawezekana hupewi updates za huku.
Movie theaters ziko mbili Dar mpya na Arusha pia.Za Dar,moja iko Mwenge ambayo inaonyesha movie za kihindi tu(kuna theaters 3 au 4 hapo),then kuna nyingine Mlimani City,karibu na chuo kikuu,kuna shopping mall mpya pale.Hao wana theaters kama tatu hivi...huko ni movies za kizungu tu.

http://www.africa-beat.com/films.aspx
 
asante sana mzeeba,i think story niliyosoma mimi was not this one,i cleary remember it was some serious piece of investigative journalism,which left you in no doubt that,mdai wa jina la tanzania,was telling the truth

Nakubaliana na wewe kabisa kuhusu hili. Nakumbuka story ili run katika matoleo mawili ya gazeti (Mwanachi???). Jamaa alikuwa amekuja Tanzania kwenye harusi ya ndugu yake (how we remember the wrong things!!!). Habari yenyewe ilielezea na majina mengine yaliyoshika nafasi ta pili na ya tatu. Certificate alisema anayo UK. Anybody who know this guy or a guy who knows a guy, ili walau tupate hio certificate kama ukumbusho hapa.
 
..kesi ya uhaini iliamuliwa na Jaji Kiongozi Nassoro Mzavas[r.i.p].

..kulikuwa na vifungo tofauti, lakini cha juu kabisa ilikuwa maisha. pia wapo washitakiwa walioachiwa huru.

..kesi ile ilitusisimua sana tuliokuwa tukiifuatilia. upande wa utetezi ulikuwa na mawakili machachari sana kama Murtaza Lakha, Hussein Muccadam, Tarimo,...

..nadhani wengi tulikuwa tunastaajabu jinsi mawakili hao walivyokuwa wakiwahoji mashahidi wa serikali. kwetu sisi ilionekana kama wanaihoji serikali yenyewe!! kwangu mimi ilikuwa ni kitendo cha ajabu kwelikweli.

..upande wa mashtaka nao ulikuwa haujachacha. nadhani mwendesha mashtaka mkuu alikuwa William Sekule, akisaidiwa na wengine kama Mwanyika[ ag wa sasa].

..kwa mtizamo wangu upande wa mashtaka ukiongozwa na William Sekule made very strong closing arguments na hilo lilisaidia ktk kushinda kesi.

..washitakiwa ninaowakumbuka ni: Thomas Lugakingira, Hatibu Gandhi/Hatty McGhee, Suleiman Kamando, Badru Rwechungura Kajaja, Deutrich Mbogoro, vijana wawili wa familia ya Hans Pope. wengine walikuwa Banyikwa[if not mistaken walikuwa mtu na mkewe], na Ngaiza.

..Hans Pope alikuwa ni afisa wa Polisi ambaye alitekwa nyara na majeshi ya Amini na kuuwawa Uganda. mwili wake nadhani ulipatikana baada ya majeshi yetu kuingia Uganda. vijana wake ndiyo hao walioshtakiwa kwa uhaini.

..washitakiwa wa Uhaini waliachiwa huru wakati Raisi Mwinyi anaondoka madarakani.




..Uncle Tom Lugakingira, pamoja na Hatibu Gandhi, walitoroka toka rumande[ukonga au keko]. walitorokea Kenya, na nadhani walipitia mpaka wa horohoro[sina uhakika].

..Uncle Tom alikuwa na pesa hivyo moja kwa moja akakimbilia UK. Hatibu Gandhi aliendelea kuzubaa Kenya, akaja kuwa exchanged na wahaini[ochuka,...] wa Kenya waliotorokea Tanzania.

..ni kipindi hicho hicho Moi alipinduliwa na askari wa jeshi la anga. kiongozi wao alikuwa ni Mjaluo. tuliofuatilia redio kenya tulijuwa it was over for Moi, lakini baadaye tukasikia tangazo toka kwa Maj.Gen.Joseph Mulinge kwamba jaribio limezimwa.



..Commandoo aliyeuawa alikuwa akijulikana kama Mussa Tamimu. maofisa usalama walijaribu kumkamata maeneo ya mwananyamala lakini akawaponyoka. baadaye walimkimbiza akarukia pickup iliyobeba bia na kuanza kuwarushia maofisa usalama. baada ya hapo alipigwa risasi na kufariki.
NB:

..FMES amemchanganya Cpt.Tamimu na jambazi sugu aliyekuwa akiijulikana kwa nickname Nyau. jina lake lilikuwa Hamisi .... "nyau."

..Nyau pamoja na majambazi wenzake 19 walitoroka gerezani Ukonga. sina uhakika walitoroka vipi. serikali ilifanya shake up kubwa sana Magereza ambapo Mkuu wao alipoteza kazi.

..baada ya hapo vitendo vya ujambazi na hali ya wasiwasi ilitawala jiji zima la DSM na vitongoji vyake. road blocks zilikuwepo kila mahali, na msako mkubwa ulifanyika.

..ujambazi ulitokana na matokeo ya vita vya Kagera. maisha yalikuwa magumu sana, na kulikuwa na askari wengi, haswa mgambo, waliorudi nyumbani na kuwa-released toka jeshini.


Mkuu, pongezi. nilichelewa kuchangia kwa sababu nilikuwa natafuta hili jina lilikuwa limenitoka akilini kidogo. Huyu ndio aliwapelekesha jamaa pale mitaa ya Kinondoni wakati wanajaribu kumkamata. Ilikuwa ni 'Picha' worth the 'Bourne' trilogy!
 
kichuguu,FMES,babaDesi,Jasusi,Rev.Kishoka,mzeeba,.....

..vipi kuhusu wimbo wa taifa? hivi ulitungwa na nani?
 
Hata mimi niliwahi kusoma story hiyo lakini nimeshindwa kuweka comment kwa vile sikumbuki niliisoma wapi. Alisema kuwa alichukua herufi tatu za TAN kutoka jina Tanganyika, na herufi nyingine tatu za ZAN Kutoka jina Zanzibar, halafu akamilizia na herufi mbili IA za jina lake. Inawezekana alikuwa akiitwa Iqbal Ahmed, au jina lolote linalohusiana na herufi za IA; na nakumbuka alisema kuwa anaishi Uingereza sasa hivi.


Kuna Story nilipata kuisoma kwenye miaka ya mwanzo ya 80' kwenye gazeti la Africa Now ambapo ilielezwa kuwa miongoni mwa majina ya mwisho ambayo yalipigiwa kura ilikuwa ni pamoja na Tangibar[/I]
 
Na ukweli ni kwamba hata viongozi wetu wa sasa wa juu wanalijua sana hili, wanachofanya sasa ni wana-count tu the time, kwamba lini wananchi tutaamuka kabisaa, so far wanajua kuwa bado tumelala na itachukua muda kidogo, lakini pole pole tunaanza kuamka, ingawa bado sana,

Hotuba ya juzi ya Kikwete, iliyonikatisha tamaa sana, ukiiangalia kwa makini the side ya political saikolojia yake na impact yake kwetu wananchi, utagundua kuwa hawa viongozi wetu wana-benki kwenye ujinga wetu wananchi.

I think it's good sometimes to call a spade a spade. And thanks mkuu Marshall kwa hii post, maana kuwa wengi humu hawapendi kabisa wanaposikia neno kuwa "bado wabongo wamelala usingizi." .
 
Binafsi, ninaamini kuwa haya maneno yalikuwa na ukweli ndani yake ila kunaweza kuwa na debate of how much percentage ya huu ukweli, kwa sababu kama ingekua ni kweli 100%, basi ile Mutiny ingezimwa kabla haijaanza, Karume asingeuwawa kinyama namna ile, suprise ya Idd Amin kutushambulia Bukoba, mpango wa mapinduzi wa kina Ngaiza usingefikia kwenye matured stage, na Lugakingira asingetoroka kwenye max jela kama Ukonga...

Wakuu, nani anafahamu [kiundani] kuhusu uhaini wa aliyewahi kuwa the first Chief of Defence Forces, General Mrisho Sam Hagai Sarakikya...? Niliwahi kusimuliwa zamani kuwa huyu jamaa alipanga kuipindua nchi/ua Nyerere enzi hizo[Lugalo], na kwamba mtu pekee aliyeokoa hayo mapinduzi alikuwa ni General David Musuguri. Je, ni kweli? Aliye na picha ya Sarakikya, please, do me a favor, tuwekee hiyo pic hapa...
 
Wakuu, nani anafahamu [kiundani] kuhusu uhaini wa aliyewahi kuwa the first Chief of Defence Forces, General Mrisho Sam Hagai Sarakikya...? Niliwahi kusimuliwa zamani kuwa huyu jamaa alipanga kuipindua nchi/ua Nyerere enzi hizo[Lugalo], na kwamba mtu pekee aliyeokoa hayo mapinduzi alikuwa ni General David Musuguri. Je, ni kweli? Aliye na picha ya Sarakikya, please, do me a favor, tuwekee hiyo pic hapa...

Gustanza,
Ninachofahamu mimi, kwa mujibu wa sources zilizokuwa karibu na Mwalimu wakati huo, ni kwamba njama za Sarakikya hazikugunduliwa na Musuguri, bali maafisa wa usalama wa taifa. Mwalimu aliarifiwa na akamwita Sarakikya nyumbani kwake pale Msasani. Alimwonyesha kile kiti alichokuwa amekikalia na kumwambia kuwa kama anataka hicho kiti basi awaombe raia wa Tanzania waliomkabidhi Mwalimu na si kutumia njama zitakazoleta umwagaji damu nchini. Baaada ya hapo Sarakikya aliondolewa jeshini na kupewa kazi ya ubalozi nchi ya nje.
 
Jasusi said:
Ninachofahamu mimi, kwa mujibu wa sources zilizokuwa karibu na Mwalimu wakati huo, ni kwamba njama za Sarakikya hazikugunduliwa na Musuguri, bali maafisa wa usalama wa taifa. Mwalimu aliarifiwa na akamwita Sarakikya nyumbani kwake pale Msasani. Alimwonyesha kile kiti alichokuwa amekikalia na kumwambia kuwa kama anataka hicho kiti basi awaombe raia wa Tanzania waliomkabidhi Mwalimu na si kutumia njama zitakazoleta umwagaji damu nchini. Baaada ya hapo Sarakikya aliondolewa jeshini na kupewa kazi ya ubalozi nchi ya nje.

Jasusi,

..I thought Sarakikya alipoondolewa jeshini aliteuliwa kuwa Waziri wa Michezo....??

..halafu Major Kavana alipotelea wapi? najua ni utamaduni wa CDF kuondoka na Chief of Staff wake, lakini sijui Kavana alipelekwa wapi baada ya kutoka jeshini.

..Kavana alikuwa ni kati ya maofisa wa Jeshi wasomi. he graduated with a Physics degree frm London Univ. wakati huo ukisoma science Makerere ulikuwa unahitimu na degree ya London Univ.

..kuna kipindi maofisa vijana wasomi waliondolewa toka jeshini na kupelekwa kwenye mashirika ya umma. je walihusika na jaribio hilo la Sarakikya?

..hivi Mwalimu alitaka kupinduliwa mara ngapi? maana kuna tetesi nyingine nilisikia kuhusu Mwalimu kuwa na mazungumzo na majenerali[musuguri,kiwelu,mayunga,..] kama aliyokuwa nayo na Sarakikya, lakini hayo yalifanyika Monduli.
 
kichuguu,FMES,babaDesi,Jasusi,Rev.Kishoka,mzeeba,.....

..vipi kuhusu wimbo wa taifa? hivi ulitungwa na nani?

Nakumbuka kuambiwa na mwalimu mmoja wa Mziki kuwa wimbo wa Taifa ulitungwa na Nyerere mwenyewe. Aliweka maneno ya kiswahili kwenye melody ya Nkosi Sikeleli IAfrika uliotungwa na mwalimu mmoja wa kizulu Enoch Sontonga mwaka 1887. Ni wimbo maarufu sana unaotumia kama wimbo wa Taifa na nchi nyingi kusini mwa Afrika. Hebu soma hapa:

"Nkosi Sikelel' iAfrika" ("God Bless Africa" in Xhosa), is part of the joint national anthem of South Africa. It was originally composed as a hymn in 1897 by Enoch Sontonga, a teacher at a Methodist mission school in Johannesburg, South Africa. For decades during the apartheid regime it was considered by many to be the unofficial national anthem of South Africa, representing the suffering of the oppressed. In 1994 after the fall of apartheid, the new State President of South Africa Nelson Mandela declared that both Nkosi Sikelel' iAfrika and the previous national anthem, Die Stem (The Call of South Africa) would be national anthems. While the inclusion of Nkosi Sikelel' iAfrika rejoiced in the newfound freedom of many South Africans, the fact that Die Stem was also kept as an anthem even after the fall of apartheid, signified to all that the new government under Mr Mandela respected all races and cultures and that an all-inclusive new era was dawning upon South Africa. In 1996, a shortened, combined version of the two anthems was released as the new South African National Anthem under the constitution of South Africa.

The hymn is also the national anthem of both Tanzania and Zambia, and was formerly the anthem of Zimbabwe and Namibia. Outside of Africa, the hymn is perhaps best known as the long-time (since 1925) anthem of the African National Congress (ANC), as a result of the global anti-Apartheid movement of the 1970s and 1980s, when it was regularly sung at meetings and other events. It became part of South Africa's national anthem in 1994, following the ANC's victory in the country's first multi-racial elections.

The words of the first stanza were originally written in Xhosa as a hymn. In 1927 seven additional Xhosa stanzas were added by the poet Samuel Mqhayi. Solomon Plaatje, one of South Africa's greatest writers and a founding member of the ANC, was the first to have the song recorded. This was in London in 1923. A Sotho version was published in 1942 by Moses Mphahlele. Rev. John L. Dube's Ohlange Zulu Choir popularised the hymn at concerts in Johannesburg, and it became a popular church hymn that was also adopted as the anthem at political meetings. It has also been recorded by Paul Simon and Miriam Makeba, Ladysmith Black Mambazo, [1], Boom Shaka, Oliver Mtukudzi (the Shona version that was once the anthem of Zimbabwe) and the Mahotella Queens.

Boom Shaka, a prominent South African kwaito group, performed the anthem in kwaito style, a popular South African genre influenced by hip-hop. The interpretation was controversial, and viewed by some as a commercial subversion of the anthem; Boom Shaka counter that their version represents liberation and introduces the song to younger listeners, [2], [3].
 
Back
Top Bottom