Tukumbuke Zamani: Historia ya Taifa letu katika picha

Tukumbuke Zamani: Historia ya Taifa letu katika picha

NA FEMILI YAKE ...HAKUNA AMBACHO MZAZI ANAWEZA KUMPA MWANAYE ZAIDI YA ELIMU
jk.jpg
 
WOLD CUP 1994...hivi POKI ndio alizamia huko USA?

attachment.php
 

Attachments

  • liky.jpg
    liky.jpg
    30.4 KB · Views: 359
BIASHARA YA KWENDA UCHI HAIKUANZA JANA WA LEO NA AKINA NDOLANGA...ILIKUWEPO TANGU ENZI HIZO

missy1.jpg
 
MPAKA ZENJI MAMBO HAYA YALIKUWEPO

attachment.php
 

Attachments

  • missy39.jpg
    missy39.jpg
    89.5 KB · Views: 1,291
HOW CAN WE FFORGET MAREHEMU SISTER SHENAZ ...cheki domo hilo...

attachment.php
 

Attachments

  • shenaz.jpg
    shenaz.jpg
    60.1 KB · Views: 1,473
mara baada ya mapinduzi zanzibar,karume alitoa order,mtu yoyote anayetaka kuoa binti wa kiasia anaruhusiwa hata kwa nguvu (amri ilitoka kwa sababu ya ta bia ya wahindi kujitengatenga) what happened next dunia nzima ili condemn,indian woman rather then get forced into marriage wengine wali commit sucide,hata thabit kombo alipata muhindi.waziri mkuu wa india sikumbuki kama ni gandhi au nehru alimuomba nyerere aingilie kati,to the atonishment of the world,nyerere did not utter a word
 
mara baada ya mapinduzi zanzibar,karume alitoa order,mtu yoyote anayetaka kuoa binti wa kiasia anaruhusiwa hata kwa nguvu (amri ilitoka kwa sababu ya ta bia ya wahindi kujitengatenga) what happened next dunia nzima ili condemn,indian woman rather then get forced into marriage wengine wali commit sucide,hata thabit kombo alipata muhindi.waziri mkuu wa india sikumbuki kama ni gandhi au nehru alimuomba nyerere aingilie kati,to the atonishment of the world,nyerere did not utter a word

whats your point?
 
Game theory,my point is as a result of a directive from karume,asian women were forcefully married to africans against their wishes,rather then go ahead,some commited sucide.the indian government asked nyerere to intervene in this sad turn of events.nyerere kept mum,perhaps for fear of a backlash from karume- zanzibar was condemned worldwide
 
Burudani na muzik wa Dansi;

View attachment 2321
Mbaraka Mwinshehe Mwaruka, nani kama yeye East Africa...? R.I.P

View attachment 2322
Hemed Maneti, "Chiriku"...R.I.P! Huyu enzi hizo alikuwa anaongoza troop la Wana pambamoto moto kweli kweli!... Maskini Vijana Jazz, TOT wakaja kuwapiku kwenye ulaji wa uhamasishaji! CCM bwana, arrgghh!


View attachment 2323
...wana Sikinde Ngoma ya ukae enzi hizo na Leyland lao, palikuwa 'hapatoshi' hawa jamaa na wana Masantula Ngoma ya Mpwita chini ya Guitar lenye nyuzi dazeni la Ndala Kasheba na King Kikii..
 
...thread imekuwa ndefu, kumradhi kama picha hii ilishatundikwa hapo awali...Mzee wetu naye alikuwa 'championi' wa bao...

attachment.php
 
attachment.php

...asilimia kubwa ya wasomi wa Tanganyika enzi hizo walipitia Tabora Boys, na Tabora Girls... i.e Spika Sitta na Mkewe, Mzee Bob Makani, mama Migiro etc

attachment.php

...halafu wakaendelea na degree zao za kwanza Makerere University, kabla ya kutawanyika huko na huko duniani kuongeza ujuzi, na wengine wanaendelea kulitumikia taifa mpaka leo...

 
1.
Mbaraka Mwinshehe Mwaruka, nani kama yeye East Africa...? R.I.P

Mkuu Mchongoma,

Wewe ni kuweka historia hata kama tukirudia, hapo naona ni Mzee mwenyewe Zole Zole, akiwa na Morogoro Jazz wana "Sululu Saka Saka", nafikiri unakumbuka ile ngoma yake ya "Dawa ya moto ni....." kabla hajajitoa na kuunda bendi yake mpya ya Super Volcano wana "Masika Zole Zole",

Wakati huu ndio Mulogolo ulikuwa ni mji hasa kasoro bahali tu, maana Mbaraka na kiongozi wa Cuban Marimba, aliyechukua ukanda baada ya kifo cha Salum Adallah, bwana Juma Kilaza mzee wa "Subi...Subi...Subiani...Nyonya" ulikuwa mwaka 1973 ndio hasa wote walikuwa kileleni mwa vipaji vyao, nakumbuka enzi hizo watu wazima wakisaifir kwenda huko kila weekend, kula mziki Mungu awalaze pema wote wawili magwiji wa muziki Morogoro, unajua siku hizi Morogoro sio ile ya zamani tena hata kwa mpira tena sio kama enzi za kombe la taifa la kina:-

Hussein Ngulungu, Shiwa Lyambiko, Adam Sabu, Adam Sakuru, Gibbson Sembuli, Aluu Ali, Jella Mtagwa, Abdallah Husein, Omar Hussein, Zamoyoni Mogella, Malota Soma, Ahmed Jongo, Charles Boniface "Mkwasa", Mwinyimkuu Carlos, Juma Shaabani, na Omar Choggo "Choggo Mluya", na Boi Wickens, Mnyepe, Vincent Mkude.

Kwa kweli zilikuwa ni enzi hasa, kama huwezi kwenda uwanja wa Karume, basi ni kuwasikiliza, Mshindo Mkeyenge, Abdul Masudi "Jaws", au Tido Mhando kwenye Radio Tanzania wakikuletea live kutoka Karume Stadium.


2.
Hemed Maneti, "Chiriku"...R.I.P! Huyu enzi hizo alikuwa anaongoza troop la Wana pambamoto moto kweli kweli!... Maskini Vijana Jazz, TOT wakaja kuwapiku kwenye ulaji wa uhamasishaji! CCM bwana, arrgghh!

1. Mungu amuweke mahali pema, Mkulu Hemed "Chiriku" Maneti mzee wa Sumbawanga, ninamkumbuka enzi za mwanzoni mwa 70s, alipojiunga rasmi na Vijana Jazz yaani bendi ya Vijana wa Tanu Youth League na baadaye ndio wakawa Vijana wa CCM,

2. Yeye ndiye aliyeibadilisha kabisa bendi hii, Maneti alikuwa ni mpenzi mkubwa sana wa bendi maarufu wakati ule kule Zaire ya Orch. Sosoliso, chini ya Matididi Mabele Mwana Kitoko, na kina Loko Masengo,

- Akawafundisha Vijana kupiga mtindo unaofanana sana na hao wa-Zaire, akishirikiana na kina Hamza Kalala "Komandoo", Bure Musa, Mwinyipembe na Mafumu Bilali, alianzisha mtindo wa "Kamata Sukuma" na wimbo wake maarufu wa "Nimeruka Ukuta", baadaye akabadili na mtindo wake mpya wa "Koka Koka ni Balaa" na wimbo wake maarufu wa "Operesheni Maduka", ndipo akaja na mtindo mpya tena this time akiwa vyombo vipya kabisa vya aina ya Rangers, akaja na "Heka Heka Takatuka" na wimbo wa "Maria" na "Bujumbura",

- akafikia mahali akaamini kuwa amekuwa babu kubwa, kuna safari moja akawadindia UV-CCM, akitaka kusaifiri kwa ndege na kukaa hoteli kubwa, enzi hizo UV-CCM kweli chini ya Mwenyekiti wake Liundi, ndio kwanza alikuwa amemaliza kuukimbiza mwenge, akampa masaa 72 kuomba radhi au awe amejifukuza mwenyewe kuanzia bendi mpaka unachama, hakukuwa na sababu ya kusubiri kikao, maji mazito Maneti akaomba msamaha na kumaua kugombea ubunge wa Sumbawanga.

- Mambo yalikuwa yameanza kumyoonyookea na ilikuwa ni clear kuwa yuko njiani kuwa mbunge, akaugua ghafla na kutangulia mbele ya haki, binafsi nilikuwa ninamzimia sana tena sana, na nilikuwa mwenyeji sana pale Vijana Social Hall Mwananyamala siku za Jumapili mchana, maana Vijana Jazz walikuwa permanent pale, hakuwa ameoa lakini alikuwa ana mtoto na Air Hostess mmoja saafi sana,

Long live Maneti, mpaka leo ninazo collections ya record zake zote kuanzia alipoanza na Vijana Jazz mpaka alipoacha, ninazimia sana hasa na kibao chake kimoja cha "Amba Baharia", Mungu amuweke mahalii pema Mkulu Maneti.


3.
...wana Sikinde Ngoma ya ukae enzi hizo na Leyland lao, palikuwa 'hapatoshi' hawa jamaa na wana Masantula Ngoma ya Mpwita chini ya Guitar lenye nyuzi dazeni la Ndala Kasheba na King Kikii..

Hapo kwenye picha nafikiri walikuwa ndio kwanza wanaanza, maana namuona Hamis Uvuruge, Jerry Nashon " Sauti Ya Dudumizi", Hamisi Kumbakisa, Mwanyiro "Internent", Bushoke, Cosmas Chidumule, King Enock, na Abeli Baltazari waliokuwa ndio kwanza wametoka Dar International "Super Bomboka" ya Mkulu Marijani Rajabu "Mwana Manyema". Siwaoni Mkulu Gurumo na Hassan "Stereo" Bitchuka, ambao walijiunga baadaye toka Msondo Ngoma, wazee wa Amana Ilala, na Sauti Ya Zege Shabaan Dede kutoka Bima Lee.

Sikinde ni moja ya bendi zilizoshiriki sana kwenye kuubadilisha muziki wetu wa bongo na kuwa wa kisasa sana, hasa kutokana na safari zao za mara kwa mara nje ya nchi ambako walikuwa wakirekodi sana miziki yao, leo hata maduka makubwa ya muziki huko majuu utazikuta CD zao, siku hizi wapo bado lakini sio kama enzi zile,

pia mashindano yao makubwa na bendi ya Msondo Ngoma, yamewapunguza sana nguvu kwa sababu Msondo siku zote ina washabiki wengi sana wa asili na wapigaji makini sana, yaani kina Mabere, Lusungu, Mkulu Zahoro Bangwe mtoto wa nyumban, na mtoto Jumbe, George Bush Mnyali na mzee masharubu Ali Rashid, ni nguzo nzito sana za bendi hiyo, lakini kifo cha hivi karibuni cha Mkulu TX Moshi William, ambaye originally alianzia bendi ya Police Jazz, kimeipunguza sana nguvu bendi hii, ingawa majuzi imefanikiwa kumpata mtoto wa TX Moshi William (RIP) ambaye naye yuko kwenye safu ya uimbaji, lakini bado wanapwaya kidogo! Lakini ninazimia nao sana maana huko ndio unakuta mtu anacheza na kivuli chake usiku kucha mpaka muziki uishe!

ahsante Mkuu Mchongoma na hizi picha, maana ni kumbu kumbu kubwa sana ya tulikotoka
!
 
View attachment 2325
...asilimia kubwa ya wasomi wa Tanganyika enzi hizo walipitia Tabora Boys, na Tabora Girls... i.e Spika Sitta na Mkewe, Mzee Bob Makani, mama Migiro etc

View attachment 2326
...halafu wakaendelea na degree zao za kwanza Makerere University, kabla ya kutawanyijka huko na huko duniani kuongeza ujuzi, na wengine wanaendelea kulitumikia taifa mpaka leo...


Duh!!, mkuu wangu Mchongoma, tafadhali sana kwenye listi yako ongezea na Kichuguu. Hilo jengo la mawe (Government School) nilikaa kwa miaka minne kabnla ya kuhamia Sina. Niliwahi kuwa na study room kule Muhimbili na Zombie. Vile vile nilikuwa mwanachama sana wa Snake's House, na mara kwa mara tulikuwa tunakwenda Orchard.!!! Hata hivyo wakati wa enzi zetu kulikuwa Gatundu iliyokuwa inatesa sana. Nawakumbuka sana akina Charles Kileo (RIP), Leonard Msaki (Uduli), General Christopher Gimonge (wakati huo Luteni, alikuwa akitamba kuwa anatembea na masignature ya rais, na hakuna aliyejuwa kuwa jamaa huyu atakuja kuwa General siku moja), Col Anatoly Tarimo (Wakati huo Luteni) na wengineo wengi tu.

Wewe wacha tu; usikumbushe hiyo TS au Berlin
 
Akawafundisha Vijana kupiga mtindo unaofanana sana na hao wa-Zaire, akishirikiana na kina Hamza Kalala "Komandoo", Bure Musa, Mwinyipembe na Mafumu Bilali, alianzisha mtindo wa "Kamata Sukuma" na wimbo wake maarufu wa "Nimeruka Ukuta", baadaye akabadili na mtindo wake mpya wa "Koka Koka ni Balaa" na wimbo wake maarufu wa "Operesheni Maduka", ndipo akaja na mtindo mpya tena this time akiwa vyombo vipya kabisa vya aina ya Rangers, akaja na "Heka Heka Takatuka" na wimbo wa "Maria" na "Bujumbura",

Kumbukumbu zangu siyo nzuri sana lakini wimbo huu wa Niliruka ukuta ulipigwa kati ya mwaka 1974 na 1975 wakati ambapo vijana Vijana Jazz walikuwa wakutumia mtindo wa Kokakoka. Vile vile Kamata Sukuma ulikuwa wimbo mmojawapo uliotolewa kipindi kile kile pamoja na Niliruka ukuta. Kama niko off, tafadhali niwieni radhi.

Najua kuwa Maneti alikuwa mfipa wa Sumbawanga aliyekulia Tanga; ila nadhani alitokea Morogoro ambako ama alikuwa akipiga na Cuban Marimba au Morogoro Jazz au TK Lumpompo ndipo akajiunga na Vijana Jazz. Kuingia kwake Vijana jazz kuliibadilisha kabisa bendi ile kimapigo na kumwondoa John Ondoro aliyekuwa akiingoza bendi hiyo na aliyepiga wimbo uliokuwa maarufu sana kukaribisha kipindi cha wagonjwa kule RTD.
 
Nyerere hakuwa na Bifu na Mtu


Baada ya ile kesi ya uhaini iliyovuma mwanzoni mwa miaka ya sabini ambapo baadhi ya washikaji wake kama Oscar Kambona, Bibi Titi Mohamedi, na Kamaliza kuonekana na hatia ambayo pamoja na mambo mengine walikuwa na njama za kumwua Nyerere, Nyerere huyo huyo alitangaza kuwa Kambona alikuwa ni royal member wa TANU na alikuwa huru kurudi nyumbani siku yoyote akitaka, na vile vile baada ya muda mfupi tu wa Titi kukaa jela, Nyerere alitumia madaraka yake kisheria kumtoa huko mahala. Je ni kweli Nyerere alikuwa anawachukia wapinzani wake kama wengi tunavyoamini?

Hapa Nyerere amekumbatiana na Titi mwaka 1984 baada ya kumtoa jela siku nyingi sana; ni kama vile hakukuwa na kesi ya uhaini kabisa baina yao.


attachment.php
 

Attachments

  • nyererenatiti.jpg
    nyererenatiti.jpg
    59.8 KB · Views: 1,201
Back
Top Bottom