Tukumbuke Zamani: Historia ya Taifa letu katika picha

Tukumbuke Zamani: Historia ya Taifa letu katika picha

Man!! This is absolutely awesome!!

...naaaam , historia hiyo. Jambo jingine linalonikera ni Zanzibari, hata Tanzania bara ya leo, bado kuna kasumba ya kusema fulani sio MTANZANIA, ...ni Mmalawi etc! Kumbe maskini ya mungu mababu na mabibi zao walikuja pwani ya Unguja wakiwa watumwa.

I remember the fate ya mwanamama machachari wa CCM Zbar, sijui Modline Costico au..., (jina limenitoka)...

Hata Mzee Abeid Aman Karume naye ishasemekana sana kwamba ana uasilia wa Malawi, japo alizaliwa Mwera. Tukiendelea kuchunguzana Uasilia tutajikuta wengi Tanganyika au Unguja sio asili yetu.

BTW, kabla ya 1964, sote tulikuwa sio WATANZANIA 😀
 
...
...
oscar kambona said:

i braved the storm and for two painful days was left alone to deal with the soldiers. I was virtually in control of affairs then, and if i had political ambitions other than serving under him, i would easily have replaced the president who had by then become a fugitive. These are contrete examples to prove to prove my loyalty to tanzania and africa.

...

...
 
Originally Posted by oscar kambona

i braved the storm and for two painful days was left alone to deal with the soldiers. I was virtually in control of affairs then, and if i had political ambitions other than serving under him, i would easily have replaced the president who had by then become a fugitive. These are contrete examples to prove to prove my loyalty to tanzania and africa.

Wakuu unajua huyu mkuu ananichanganya sana sometimes, I mean kuna wakati ninaamini ninamuelewa lakini tena anakuja kunifanya nione simuelewi, Kambona is something man!
 
Hivi kwanini tulikuwa tunafunga safari kwenda Airport kuangalia ndege zikipaa na kutua? Yaani mgeni akija kutoka bara mojawapo ya maeneo ya kumpeleka ilikuwa Airport.!!
 
Mwanakijiji,
Tumetoka mbali. Hiyo tabia ya kwenda airport niliendelea nayo hadi hapa Marekani mpaka walipozidisha parking fees.
 
nakumbuka nimewahi kusikia kwamba ndege imewahi aanguka salender bridge.vilevile nimewahi soma kwamba ndani ya crater ya kilimanjaro mountain kuna mabaki ya ndege iliyoanguka .someone please enlighten us
 
Mbuga ya wanyama ya selous is named after captain fredrick selous,british explorer,officer,hunter and conservationist,famous for his exploits in africa.his adventures inspired Sir Rider to create the fictional ALLAN QUATERMAN character.died in combat during 1st world war and was buried in the selous game reseve
 
FMES,
Hapana. Mwalimu asili yake si Malawi. Ni Burundi.

Hii aliisema Mtikila wakati anajitahidi kujitafutia "soko" la kisiasa. Sidhani kama ina ukweli wowote.Wazanaki hawana dalili yoyote kuhusiana na makabila yaliyoko Burundi.
 
Kumbukumbu zangu siyo nzuri sana lakini wimbo huu wa Niliruka ukuta ulipigwa kati ya mwaka 1974 na 1975 wakati ambapo vijana Vijana Jazz walikuwa wakutumia mtindo wa Kokakoka. Vile vile Kamata Sukuma ulikuwa wimbo mmojawapo uliotolewa kipindi kile kile pamoja na Niliruka ukuta. Kama niko off, tafadhali niwieni radhi.

Najua kuwa Maneti alikuwa mfipa wa Sumbawanga aliyekulia Tanga; ila nadhani alitokea Morogoro ambako ama alikuwa akipiga na Cuban Marimba au Morogoro Jazz au TK Lumpompo ndipo akajiunga na Vijana Jazz. Kuingia kwake Vijana jazz kuliibadilisha kabisa bendi ile kimapigo na kumwondoa John Ondoro aliyekuwa akiingoza bendi hiyo na aliyepiga wimbo uliokuwa maarufu sana kukaribisha kipindi cha wagonjwa kule RTD.



Nakubaliana nawe Kichuguu. Maneti alitokea TK Lumpopo ya Juma Kilaza mwaka 1973 mwishoni na kujiunga na Vijana Jazz na mtindo wake wa kwanza kabisa ulikuwa ni Koka Koka na nyimbo za mwanzo kabisa alizotoa na Vijana Jazz mwaka 1974 ilikuwa ni pamoja na huo 'Kuruka UKuta' (sio ile maana ya vijana wa siku hizi!), Regina, 'Sabina' ambayo walikopi mngurumo wa gita la Solo kutoka wimbo mmoja wa TP OK Jazz, Salima na nyinginezo, Baada ya hapo akaja na mtindo wa Kamata Sukuma ambao kwanza ulikuwa wimbo halafu ukawa mtindo ambao hata hivyo haukudumu sana kwa sababu wazee wa Tanu hawakuyapenda sana hayo maneno, akaibuka na TakaTuka kisha Pambamoto na Pambamoto awamu ya pili. Nawasilisha.
 
Wana JF napenda kuchukua fursa hii kueleza jinsi nilivyofuraishwa na mpaka hata machozi yananilenga kwa jinsi navyoona mambo mazuri na ya muhimu mno yanayoendelea katika thread hii...vitu kama hivi ndivyo vinavyovipa Forum yetu hii ya jamii heshima kubwa mno ndani ya jamii.... ni kweli huwezi kujua unakokwenda kama huna ufahamu wa ulikotoka, ni vizuri uelewe ulitokea wapi ili ujifunze makosa yaliyofanyika huko nyuma usije ukayarudia uko unakokwenda au yale mazuri yaliyofanyika uko nyuma uyachukue na yakusaidie uko unakokwenda, hiyo iko wazi kabisa....... tunatumia mda mwingi sana humu ndani na effort kubwa sana kujadili mambo makubwa na kupiga kelele juu ya utawala wetu wa sasa jinsi unavyokwenda.lakini sio siri ni watu wengi sana tulikua hatuna picha halisi ya mambo mengi mazuri yaliyokuwepo huko nyuma na hata mengine mabaya...... laiti tungalijua nafikiri moto wake ungalikua ni zaidi ya sasa..maana hizi picha zina tia uchungu mno ukiziangalia na kuona kua miundo mbinu mingi na vitu vingii vizuri vimepotea mikononi mwa viongozi wachache waliokua na tamaa na uroho..au kuwa na uelewa mdogo.....sio siri kwa mfano ile picha ya lile basi la usafiri wa zamani..UDA- Kumbakumba'' imenisikitisha mno hata machozi yakanilenga......... yako wapi hayo mazuri???????mbona viongozi wetu wametutesa namna hii?? nambona watanzania bado tunaendelea kuwa ng'ang'ania????????

Ningependa kuona sasa kampeni za uchaguzi au kampeni zozote za uhamasishaji ziwe zinaendana na kuonyesha picha za zamani...naona wananchi watapata uchungu..na hamasa zaidi....nahisi watanzania wengi hawazifahamu picha hizi na historia yao na nchi yao kwa ujumla,...wengi ni mashabiki wa siasa na hawaijui nchi yao vizuri...laiti wangalijua wasingalifanya haya wanayoyafanya sasa ya kushabikia siasa........kwa staili ya Picha nafikiri wengi watafahamu kua wanachofanya ni makosa makubwa..na wote tutajenga nchi hii bila kuoneana aibu yeyote na kuifanya nchi yetu iwe na neema kama ilivyokua hapo zamani...

Shukurani nyingi ziende kwa Icadon, Kichuguu,Mchongoma,GAme Theory, son of alasaka, jasusi,na wengine wengi waliochangia hapa na bila kumsahau aliyeileta post hii humu...Mkuu FMES mungu akubariki sana, nafikiri hujajua tu ni jinsi gani ulivyoleta,unavyoleta na utakavyoleta imapact kubwa katika hili...la muhimu ni kujipanga tu vizuri,...ila it's a very good idea.. Keep it up man.!
 
nakumbuka nimewahi kusikia kwamba ndege imewahi aanguka salender bridge.vilevile nimewahi soma kwamba ndani ya crater ya kilimanjaro mountain kuna mabaki ya ndege iliyoanguka .someone please enlighten us



yeah that was childhood stories ..watoto wa siku hizi hawadanganyiki kama zamani...

..teh..like "mdogo wako tumemnunua hospitali...."..hadi darasa la nne unaamini hivo..hadi uje usome sayansi ya class v......
 
kama utumwa uliisha kwenye 1900 ......jee wale wanaosema sultani alipinduliwa zanzibar ili kuondoka mateso kwa watumwa/watu weusi humaanisha nini?
 
Hii aliisema Mtikila wakati anajitahidi kujitafutia "soko" la kisiasa. Sidhani kama ina ukweli wowote.Wazanaki hawana dalili yoyote kuhusiana na makabila yaliyoko Burundi.
Wildcard,
Believe me, I know it is true. Nimemsikia Mwalimu mwenyewe kwa masikio yangu( in a light moment) akizungumza na Mkanzabe kuhusu walikotokea.
Na kule Mara hawakuitwa Waza-naki for nothing.
 
kama utumwa uliisha kwenye 1900 ......jee wale wanaosema sultani alipinduliwa zanzibar ili kuondoka mateso kwa watumwa/watu weusi humaanisha nini?

Gaijin,
Jibu lako rahisi sana. Wakati wa utawala wa Sultani ubaguzi dhidi ya Waafrika wa rangi nyeusi uliendelea Zanzibar. Kuna sehemu za mji weusi walikuwa hawatakiwi kuonekana baada ya jua kutua. Umesahau ya ubwana na utwana?
 
gaijin said:
kama utumwa uliisha kwenye 1900 ......jee wale wanaosema sultani alipinduliwa zanzibar ili kuondoka mateso kwa watumwa/watu weusi humaanisha nini?

gaijin,

..tatizo lilikuwa WAKOLONI, yaani Waingereza na Waarabu, kubadilishana nafasi/madaraka wakati wa "UHURU" wa mwaka 1963.

..Muingereza alipaswa kukabidhi MAMLAKA kwa MTU MWEUSI na siyo serikali ya Kiarabu iliyoendelea kumsujudia Sultani.

..Waingereza kwa kushirikiana na Waarabu waliunda mfumo wa Uchaguzi ambapo serikali iliundwa na chama kilichopata majimbo mengi badala ya kile kilichoshinda kura nyingi.

..Mfumo niliouelezea hapo juu hutumika ktk nchi ambazo hujaribu kuzuia kile kinachoitwa the tyranny of the majority. lakini kwa Zanzibar the minority Arab and their surrogates walikuwa ndiyo tyrranies wenyewe.

..kulifanyika chaguzi karibu tatu na zote zililalamikiwa kwa kasoro mbalimbali. kila mara ASP walikuwa wakishiriki wakitegemea watakuja kushinda kwa wingi wa majimbo. naamini mwisho wake walikata tamaa kwamba kutokana mfumo wa uchaguzi, na kuwepo kwa vyama vibaraka vya Kiarabu, kulikuwa hakuna uwezekano wa serikali kuundwa na Chama cha mtu mweusi.

..tatizo lingine lilojitokeza ni nafasi na hadhi ya Sultani ktk mfumo wa Utawala wa Zanzibar.

..ni kweli kabisa biashara ya Utumwa ilipigwa marufuku miaka ya 1900. lakini naamini kwa Zanzibar ingekuwa muafaka zaidi kama Utawala wa Sultani nao ungepigwa marufuku kwa kushiriki ktk jinai ile.

..sasa utaona kwamba pamoja na biashara ya Utumwa kusitishwa in the 1900's, status quo iliyotokana na mfumo ule bado iliendelea kuwepo, na Mwafrika aliendelea kuwa mtwana/mtu baki ktk ardhi yake mwenyewe.

NB:

..kuna wengine wamekuwa wakidai kwamba Sultani alijenga reli,bandari, na kuleta maendeleo ya kila aina Zanzibar. ukweli utabaki kwamba maendeleo yote hayo yalitokana na JASHO na DAMU ya Waafrika wa Zanzibar.
 
mchonga na nanihii eeeee aga khan
8200357l.jpg
 
Nakubaliana nawe Kichuguu. Maneti alitokea TK Lumpopo ya Juma Kilaza mwaka 1973 mwishoni na kujiunga na Vijana Jazz na mtindo wake wa kwanza kabisa ulikuwa ni Koka Koka na nyimbo za mwanzo kabisa alizotoa na Vijana Jazz mwaka 1974 ilikuwa ni pamoja na huo 'Kuruka UKuta' (sio ile maana ya vijana wa siku hizi!), Regina, 'Sabina' ambayo walikopi mngurumo wa gita la Solo kutoka wimbo mmoja wa TP OK Jazz, Salima na nyinginezo, Baada ya hapo akaja na mtindo wa Kamata Sukuma ambao kwanza ulikuwa wimbo halafu ukawa mtindo ambao hata hivyo haukudumu sana kwa sababu wazee wa Tanu hawakuyapenda sana hayo maneno, akaibuka na TakaTuka kisha Pambamoto na Pambamoto awamu ya pili. Nawasilisha.

Mkuu Babadesi,

Heshima mbele, mengi umepatia sana na ni ukweli mtupu, isipokuwa ni kwamba:-

1. Maneti alipoingia Vijana Jazz, mtindo wake wa kwanza ulikuwa ni wa "Kamata Sukuma", solo zima la hii album ambayo aliirekodi Nairobi, alilipiga Hamza Kalala "Komandoo" akiwaiga Orch. Sosoliso ya Zaire. Album hii ilikuwa na nyimbo zifuatazo:-

- 1. Kamata Sukuma, 2. Magdalena, 3. Dada Sabina, 4. Nimeruka ukuta, 5. Salima, 6. Viva Frelimo.

2. Waliporudi kama ulivyosema wazee wa Chama hawakuridhika kabisa na mwenendo mzima wa bendi, kwamba waliiona ikianza kukiuka maadili ya chama, kwa hiyo wakamuamuru Maneti, abadili ile style, Maneti akabuni mtindo mpya wa "Koka Koka ni Balaa" , again wakatoa album mpya yenye nyimbo kama:-

- 1. Pili, 2. Operesheni Maduka, 3. Belibe, 4. Kalulu dibweze djigolo djangu, 5. Masido, 6. CCM.

3. Sasa wakaletewa vyombo vipya vya kisasa, Maneti akaibuka na mtindo mpya wa "Heka Heka" na vibao kama:-

1. Lela, 2. Ngoma, 3. Heka Heka Huyo Anapata, 4. Weekend, 5. Mwisho wa Mwezi. 6. Mozambique (Wembe ni ule ule)

4. This time Maneti akaja na extension ya Heka Heka, akaiita Heka Heka Takatuka, na Pambamoto na nyimbo kama:-

1. Maria, 2. Bujumbura, 3. Chiku, 4. Shoga,

Ndipo Mkulu Maneti sasa akatangulia kwenye haki, na kumuachia Eddy Sheggy aliyekuja na mtindo wa Sagarumba, ulikuwa mwisho wangu wa kuwafuatilia, maana sikuelewa kabisa walichoanza kupiga, lakini otherwise Babadesi, maneno yako yote ni sawa kabisa na kwa kumbu kumbu tu ni kwamba hivi vibao vyote ninavyo kwenye maktaba yangu.
 
Mkuu Wakunyuti,

Heshima mbele mkuu, maneno yako mazito sana yamenitoa machozi, hii thread huwa ninaingalia yote mwanzo mpaka mwisho, angalau mara moja kila siku, imetulia wala haina mikwaruzo picha zinajisema zenyewe hata bila maelezo ahsante kwa baraka na ninaomba zikurudie na wewe pia maana kuweza tu kuyaona uliyoyasema kuhusu hii thread sio bahati mbaya, na kama nilivyoahidi ni kwamba huu ni mwanzo tu bado picha zitawekwa sana na historia zaidi kwa wananchi wote kuelimika na kuelimishana, ahsante mkuu na ubarikiwe:-


Quote:- Wakunyuti

1. Wana JF napenda kuchukua fursa hii kueleza jinsi nilivyofuraishwa na mpaka hata machozi yananilenga kwa jinsi navyoona mambo mazuri na ya muhimu mno yanayoendelea katika thread hii

2. ...vitu kama hivi ndivyo vinavyovipa Forum yetu hii ya jamii heshima kubwa mno ndani ya jamii.... ni kweli huwezi kujua unakokwenda kama huna ufahamu wa ulikotoka, ni vizuri uelewe ulitokea wapi ili ujifunze makosa yaliyofanyika huko nyuma usije ukayarudia uko unakokwenda au yale mazuri yaliyofanyika uko nyuma uyachukue na yakusaidie uko unakokwenda,

3. hiyo iko wazi kabisa....... tunatumia mda mwingi sana humu ndani na effort kubwa sana kujadili mambo makubwa na kupiga kelele juu ya utawala wetu wa sasa jinsi unavyokwenda.

4. lakini sio siri ni watu wengi sana tulikua hatuna picha halisi ya mambo mengi mazuri yaliyokuwepo huko nyuma na hata mengine mabaya...... laiti tungalijua nafikiri moto wake ungalikua ni zaidi ya sasa..

5. maana hizi picha zina tia uchungu mno ukiziangalia na kuona kua miundo mbinu mingi na vitu vingii vizuri vimepotea mikononi mwa viongozi wachache waliokua na tamaa na uroho..au kuwa na uelewa mdogo.....

6. sio siri kwa mfano ile picha ya lile basi la usafiri wa zamani..UDA- Kumbakumba'' imenisikitisha mno hata machozi yakanilenga......... yako wapi hayo mazuri???????mbona viongozi wetu wametutesa namna hii?? nambona watanzania bado tunaendelea kuwa ng'ang'ania????????

7. Ningependa kuona sasa kampeni za uchaguzi au kampeni zozote za uhamasishaji ziwe zinaendana na kuonyesha picha za zamani...naona wananchi watapata uchungu..na hamasa zaidi....

8. nahisi watanzania wengi hawazifahamu picha hizi na historia yao na nchi yao kwa ujumla,...wengi ni mashabiki wa siasa na hawaijui nchi yao vizuri...laiti wangalijua wasingalifanya haya wanayoyafanya sasa ya kushabikia siasa........

9. kwa staili ya Picha nafikiri wengi watafahamu kua wanachofanya ni makosa makubwa..na wote tutajenga nchi hii bila kuoneana aibu yeyote na kuifanya nchi yetu iwe na neema kama ilivyokua hapo zamani...

Shukurani nyingi ziende kwa Icadon, Kichuguu,Mchongoma,GAme Theory, son of alasaka, jasusi,na wengine wengi waliochangia hapa na bila kumsahau aliyeileta post hii humu...Mkuu FMES mungu akubariki sana, nafikiri hujajua tu ni jinsi gani ulivyoleta,unavyoleta na utakavyoleta imapact kubwa katika hili...la muhimu ni kujipanga tu vizuri,...ila it's a very good idea.. Keep it up man.!
 
NB:

..kuna wengine wamekuwa wakidai kwamba Sultani alijenga reli,bandari, na kuleta maendeleo ya kila aina Zanzibar. ukweli utabaki kwamba maendeleo yote hayo yalitokana na JASHO na DAMU ya Waafrika wa Zanzibar.


Swadakta!!!

Kiongozi lazima awe na VISION, awe mtekelezaji na msimamizi wa maendeleo ya wananchi wake! ...bahati mbaya viongozi wetu 'wengi' wa kiafrika (mpaka leo hii) wanaukosefu wa hiyo kitu!...

...hebu angalia (mfano) Chief Kikanga na wananchi wake wa BUKUMBI miaka ya 1900's, halafu linganisha na Unguja ya miaka ya 1800's kwa ushahidi wa picha, kisha uniambie hiyo picha inakupa sura gani?


View attachment 2374

View attachment 2375

...kisha soma kipande cha nukuu ya Mkuu FMES kutoka kwa Jasusi, maneno mazito haya!

Mkuu Kichuguu, heshima mbele hii nimeikuta mahali under mkulu Jasusi, imetulia sana:-

Tanzania Election 95: 29 August 1995

Ndugu zangu wote katika ,URAIS NA HATIMA YA TAIFA

Nadhani rais wa nchi iwayo yoyote lazima awe na zaidi ya sifa za "mshona viraka." Lazima aweze kusanifu na kushona mavazi wanayoyataka wateja wake. Yaani, lazima aweze kubainisha walimpigia kura, abainishe matakwa yao na abuni siasa na mikakati ya kutekeleza siasa hiyo. Kisha aitekeleze siasa hiyo kwa ari na uwezo wake wote.

...juu ya ubaya wote wa Utawala wa kisultani na kikoloni, Miundombinu na mengineo yote walohenyeshwa mababu zetu kuijenga, leo hii tunakula matunda yake na hata kuringia.

Angalia, Kuanzia Ikulu zetu ya Dar es salaam na ya Unguja zilijengwa na Mkoloni/Sultani, halafu angalia wakajenga Hospitali zetu kubwa Tanzania, Muhimbili, V.I Lenin a.k.a Mnazi mmoja, nk...

...miaka 44 tangu 'mapinduzi matukufu' ya kumng'oa Sultani, umeme bado 'kimeo' unguja na Pemba? aaaahh aibu!!!

Ukweli ukidhihiri uongo hujitenga!
 
Back
Top Bottom