Nakubaliana nawe Kichuguu. Maneti alitokea TK Lumpopo ya Juma Kilaza mwaka 1973 mwishoni na kujiunga na Vijana Jazz na mtindo wake wa kwanza kabisa ulikuwa ni Koka Koka na nyimbo za mwanzo kabisa alizotoa na Vijana Jazz mwaka 1974 ilikuwa ni pamoja na huo 'Kuruka UKuta' (sio ile maana ya vijana wa siku hizi!), Regina, 'Sabina' ambayo walikopi mngurumo wa gita la Solo kutoka wimbo mmoja wa TP OK Jazz, Salima na nyinginezo, Baada ya hapo akaja na mtindo wa Kamata Sukuma ambao kwanza ulikuwa wimbo halafu ukawa mtindo ambao hata hivyo haukudumu sana kwa sababu wazee wa Tanu hawakuyapenda sana hayo maneno, akaibuka na TakaTuka kisha Pambamoto na Pambamoto awamu ya pili. Nawasilisha.
Mkuu Babadesi,
Heshima mbele, mengi umepatia sana na ni ukweli mtupu, isipokuwa ni kwamba:-
1. Maneti alipoingia Vijana Jazz, mtindo wake wa kwanza ulikuwa ni wa "Kamata Sukuma", solo zima la hii album ambayo aliirekodi Nairobi, alilipiga Hamza Kalala "Komandoo" akiwaiga Orch. Sosoliso ya Zaire. Album hii ilikuwa na nyimbo zifuatazo:-
- 1. Kamata Sukuma, 2. Magdalena, 3. Dada Sabina, 4. Nimeruka ukuta, 5. Salima, 6. Viva Frelimo.
2. Waliporudi kama ulivyosema wazee wa Chama hawakuridhika kabisa na mwenendo mzima wa bendi, kwamba waliiona ikianza kukiuka maadili ya chama, kwa hiyo wakamuamuru Maneti, abadili ile style, Maneti akabuni mtindo mpya wa "Koka Koka ni Balaa" , again wakatoa album mpya yenye nyimbo kama:-
- 1. Pili, 2. Operesheni Maduka, 3. Belibe, 4. Kalulu dibweze djigolo djangu, 5. Masido, 6. CCM.
3. Sasa wakaletewa vyombo vipya vya kisasa, Maneti akaibuka na mtindo mpya wa "Heka Heka" na vibao kama:-
1. Lela, 2. Ngoma, 3. Heka Heka Huyo Anapata, 4. Weekend, 5. Mwisho wa Mwezi. 6. Mozambique (Wembe ni ule ule)
4. This time Maneti akaja na extension ya Heka Heka, akaiita Heka Heka Takatuka, na Pambamoto na nyimbo kama:-
1. Maria, 2. Bujumbura, 3. Chiku, 4. Shoga,
Ndipo Mkulu Maneti sasa akatangulia kwenye haki, na kumuachia Eddy Sheggy aliyekuja na mtindo wa Sagarumba, ulikuwa mwisho wangu wa kuwafuatilia, maana sikuelewa kabisa walichoanza kupiga, lakini otherwise Babadesi, maneno yako yote ni sawa kabisa na kwa kumbu kumbu tu ni kwamba hivi vibao vyote ninavyo kwenye maktaba yangu.