Tukumbuke Zamani: Historia ya Taifa letu katika picha

Tukumbuke Zamani: Historia ya Taifa letu katika picha

Hamisi Musa, maarufu kama Nyau, alikuwa jambazi ambaye alikuwa katika kundi la majambazi 15 kama sikosei ambao walitoroka Ukonga. Majambazi hawa walikuwa ni hatari sanana Nyau alikuwa akisifika kwa ushirikina na kudaiwa kuwa alikuwa akigeuka kuwa paka,na ndio kisa cha kuitwa Nyau.

Tukirudi kwenye kesi ya uhaini, kulikuwa na Hatibu Ghandi maarufu kama Hatty McGhee, Pius Lugangira maarufu kama Father Tom,, Caption Cris Kadego, Metusela Kamando, Ramadhani Otto (mkwe mwenza Kitwana Kondo), Bayona, Zacharia Hans Pope na nduguye, Banyikwa, na wenginewe ambao siwakumbuki.

Kwenye msanga huu wa uhaini ambao jamaa waliwakilishwa na Hussen Muccadam na nafikri Murtaza Lakham (huyu alipotea ghafla baada ya hiyo kesi na kutokomea), kulikuwa na wafanyabiashara kadhaa waliowekwa ndani. Nakumbuka wazee wakihindi fulani ambao walikuwa wafanyabiashara maarufu, Mzee Rajani, Abdul Haji na wenginewe waliwekwa jela kwa muda wa kutosha.

Sawa sawa mkuu tena kwa 100%.
 
Cooper Motors na Tanganyika Motors ndio walokuwa na kibali enzi hizo cha kuingiza magari(?)
magari ya enzi hizo ni kama Ford Escort, Cortina, Zephyr, mini Cooper classic, Vw beetle...etc hakukuwa na 2nd hand Cars toka Japan/Dubai!!!
...magari ya heshima enzi hizo, mfano Vauxhal Viva...

View attachment 2193

...Enzi hizo, Zulli Rhemtulla, na Bert Shackland walikuwa "wanatuburudisha na vumbi" kwenye East African Safari rally, japo (kama kawaida yao) kuna kipindi serikali ilipiga marufuku rally kupitia Tanzania...
View attachment 2194

Peugeot 504, "nguruwe",... mabaharia waliyaingiza kwa mbwembwe magari haya. Nakumbuka hata Balozi Opanga alikuwa nalo lake moja la nguvu!

Mwenye Coopers MotorsAbdul Haji ndiye aliwekwa ndani wakati wa kesi ya uhaini 1981. Kulikuwa na Colt Motors ambayo ilikuwa ya Rajpar.

Hilo guruwe uliloliona hapo chini ni la wale jamaa pale Moshi mjini kina Khambaita ambao ni wafanyabiashara wakubwa.
 
FMES,

Umenikumbusha mbali sana na wimbo wa Kiki, "mimi msafiri niko njiani" je unao ule origino?

Natafuta original songs za OSS, Marquiz, Makassy, Juwata, Mlimani, Kyauri Voice na nyingine na si remake za siku hizi zinazofanana na Ndombolo!
 
son-of-alaska said:
1985,9 people given life imprisonment for attempted coup plot,hawa walikuwa akina nani? na sasa hivi wako wapi?

..kesi ya uhaini iliamuliwa na Jaji Kiongozi Nassoro Mzavas[r.i.p].

..kulikuwa na vifungo tofauti, lakini cha juu kabisa ilikuwa maisha. pia wapo washitakiwa walioachiwa huru.

..kesi ile ilitusisimua sana tuliokuwa tukiifuatilia. upande wa utetezi ulikuwa na mawakili machachari sana kama Murtaza Lakha, Hussein Muccadam, Tarimo,...

..nadhani wengi tulikuwa tunastaajabu jinsi mawakili hao walivyokuwa wakiwahoji mashahidi wa serikali. kwetu sisi ilionekana kama wanaihoji serikali yenyewe!! kwangu mimi ilikuwa ni kitendo cha ajabu kwelikweli.

..upande wa mashtaka nao ulikuwa haujachacha. nadhani mwendesha mashtaka mkuu alikuwa William Sekule, akisaidiwa na wengine kama Mwanyika[ ag wa sasa].

..kwa mtizamo wangu upande wa mashtaka ukiongozwa na William Sekule made very strong closing arguments na hilo lilisaidia ktk kushinda kesi.

..washitakiwa ninaowakumbuka ni: Thomas Lugakingira, Hatibu Gandhi/Hatty McGhee, Suleiman Kamando, Badru Rwechungura Kajaja, Deutrich Mbogoro, vijana wawili wa familia ya Hans Pope. wengine walikuwa Banyikwa[if not mistaken walikuwa mtu na mkewe], na Ngaiza.

..Hans Pope alikuwa ni afisa wa Polisi ambaye alitekwa nyara na majeshi ya Amini na kuuwawa Uganda. mwili wake nadhani ulipatikana baada ya majeshi yetu kuingia Uganda. vijana wake ndiyo hao walioshtakiwa kwa uhaini.

..washitakiwa wa Uhaini waliachiwa huru wakati Raisi Mwinyi anaondoka madarakani.


son-of-alaska said:
nilisikia one uncle tom,alitoroka gerezani kwa kutumia presidential motorcade,

..Uncle Tom Lugakingira, pamoja na Hatibu Gandhi, walitoroka toka rumande[ukonga au keko]. walitorokea Kenya, na nadhani walipitia mpaka wa horohoro[sina uhakika].

..Uncle Tom alikuwa na pesa hivyo moja kwa moja akakimbilia UK. Hatibu Gandhi aliendelea kuzubaa Kenya, akaja kuwa exchanged na wahaini[ochuka,...] wa Kenya waliotorokea Tanzania.

..ni kipindi hicho hicho Moi alipinduliwa na askari wa jeshi la anga. kiongozi wao alikuwa ni Mjaluo. tuliofuatilia redio kenya tulijuwa it was over for Moi, lakini baadaye tukasikia tangazo toka kwa Maj.Gen.Joseph Mulinge kwamba jaribio limezimwa.

son-of-alaska said:
alaafu nikasikia,katika hawa kulikuwa na commando,ambaye aliuwawa baada ya gunfight kubwa mitaa ya kinondoni.

..Commandoo aliyeuawa alikuwa akijulikana kama Mussa Tamimu. maofisa usalama walijaribu kumkamata maeneo ya mwananyamala lakini akawaponyoka. baadaye walimkimbiza akarukia pickup iliyobeba bia na kuanza kuwarushia maofisa usalama. baada ya hapo alipigwa risasi na kufariki.


NB:

..FMES amemchanganya Cpt.Tamimu na jambazi sugu aliyekuwa akiijulikana kwa nickname Nyau. jina lake lilikuwa Hamisi .... "nyau."

..Nyau pamoja na majambazi wenzake 19 walitoroka gerezani Ukonga. sina uhakika walitoroka vipi. serikali ilifanya shake up kubwa sana Magereza ambapo Mkuu wao alipoteza kazi.

..baada ya hapo vitendo vya ujambazi na hali ya wasiwasi ilitawala jiji zima la DSM na vitongoji vyake. road blocks zilikuwepo kila mahali, na msako mkubwa ulifanyika.

..ujambazi ulitokana na matokeo ya vita vya Kagera. maisha yalikuwa magumu sana, na kulikuwa na askari wengi, haswa mgambo, waliorudi nyumbani na kuwa-released toka jeshini.
 
Commandoo aliyeuawa alikuwa akijulikana kama Mussa Tamimu. maofisa usalama walijaribu kumkamata maeneo ya mwananyamala lakini akawaponyoka. baadaye walimkimbiza akarukia pickup iliyobeba bia na kuanza kuwarushia maofisa usalama. baada ya hapo alipigwa risasi na kufariki.

Sahihi kabisa aliitwa Capt Tamim aliuawa pale maeneo ya Kinondoni na watu wa usalama, kuna nyepesi nyepesi kuwa aliendesha operation alikuwa Mabere Marando ( not sure abt this )
 
Wakuu heshima mbele, naomba kuuliza nini uasilia wa jina Tanzania? Je lilitokana na majina ya Tanganyika na Zanzibar? Kama ndio ni nani aliyelicoin hilo jina? Walikuwa ni viongozi wa nchi hizo mbili, chama,kamati maalum au kuna mtu binafsi alilitunga?

Je kulikuwa na options zingine (kwa mfano Tanzibar) ndo hili la Tanzania likachaguliwa?

Inawezekana hili swali likawa la kipuuzi kwa wazee waliobobea kwenye historia ya nchi yetu, naomba mnivumilie maana hii kitu sikumbuki kuambiwa katika somo la historia nikiwa shule ya msingi nakupitia thread hii gafla limenijia kichwani...........
 
many thanks members,hizi contribution humu,are just priceless.nina swali lingine,kuna wakati hapo miaka ya nyuma tulikua tunaambiwa kwamba security wise tanzania was second to none,eti you could hardly do anything bila serikali kujua.was this true au ilikuwa ni propaganda ya serikali,to instill fear kwa wananchi ili to have them in check.
 
hili jina tanzania,lina utata,kuna muhindi alihojiwa na gazeti la guardian la uingereza,about two yers ago,akidai yeye ndio ali coin hilo jina,this indian alihaidiwa zawadi,lakini hakupewa,katika government circles wanadai ni nyerere ndio alianzisha hilo jina.kinachojulikana ni kwamba tender ya kuchagua jina kweli ilitolewa na zawadi kuhaidiwa
 
Hii kitu imenitatiza, kwa wanaojua ukweli wa hili naombeni mtuelimishe wengine.

D.12 Short-term domestic travel is not restricted, and there are no entry controls whatsoever for Zanzibar-born Tanzanians onto the mainland. Zanzibaris may travel to live and work freely on the mainland, subject to the same laws that apply to mainlanders, and there is no requirement for mainlanders to show identification to travel to Zanzibar. Mainlanders are allowed to work in the islands but not allowed to own land there. Zanzibaris own property, work and run businesses on the mainland. The "Kazi Nguvu" laws, which date back to the colonial period, and the Human Resources Development Act 1983 were intended to prevent migration to the cities from agricultural areas, and to support the 'Ujamaa' (community) policies of Nyerere to resist urbanisation. They stipulate that persons who are unemployed must return to their home region. These laws are however practically never used, with the exception of removing professional beggars from city streets. Tanzanian citizens can return to Tanzania without difficulty.
 
From 1977 to 1979, Amin titled himself as "His Excellency, President for Life, Field Marshal Al Hadji Doctor[2] Idi Amin Dada, VC,[3] DSO, MC, Lord of All the Beasts of the Earth and Fishes of the Seas and Conqueror of the British Empire in Africa in General and Uganda in Particular

To put it correctly, it was : His Excellency President for Life, Field Marshall Al Hadji Doctor Idi Amin Dada, Lord of All the Beasts of the Earth and Fishes of the Sea, and Conqueror of the British Empire in Africa in General and Uganda in Particular, Distinguished Service Order of the Military Cross, Victoria Cross and Professor of Geography.
 
...enzi hizo, kuangalia sinema bubu, nje ya uzio wa ukuta wa Drive inn Cinema, (sasa hivi ubalozi wa marekani!!!), enzi hizo movie ya "saturday nite fever" foleni ya magari kuingia drive inn ilianzia 9mchana!, vipi na ile sinema ya wakenya, "mlevi"... 😀
View attachment 2190

...enzi hizo "jumapili kama leo" majumba ya cinema yanayofurika watu ni Empire, ikifuatiwa na Empress, New Chox, Odeon,... Bruce Lee na fists of fury zake...


Hivi kweli biashara ya sinema hapo Dar bado iko active tena? Nadhani eneo lote la Drive Inn lilichukuliwa na ubalozi wa marekani, na Empress waligeukia biashara ya kubadilisha hela za kigeni (Bureau De Change). Thieta hizo nyingine nadhani zilijifia kifo cha mende tangu ukodishaji wa kanda za video uanze. Nadhani biashara hiyo itaweza kufufuka tena iwapo tu zitajengwa thieta za kisasa zaidi na kufungua mtandao mzuri wa kupata sinema mpya mpya kabla hazijawekwa kwenye DVD.
 
many thanks members,hizi contribution humu,are just priceless.nina swali lingine,kuna wakati hapo miaka ya nyuma tulikua tunaambiwa kwamba security wise tanzania was second to none,eti you could hardly do anything bila serikali kujua.was this true au ilikuwa ni propaganda ya serikali,to instill fear kwa wananchi ili to have them in check.


Binafsi, ninaamini kuwa haya maneno yalikuwa na ukweli ndani yake ila kunaweza kuwa na debate of how much percentage ya huu ukweli, kwa sababu kama ingekua ni kweli 100%, basi ile Mutiny ingezimwa kabla haijaanza, Karume asingeuwawa kinyama namna ile, suprise ya Idd Amin kutushambulia Bukoba, mpango wa mapinduzi wa kina Ngaiza usingefikia kwenye matured stage, na Lugakingira asingetoroka kwenye max jela kama Ukonga, Osama asingetulambisha mabomu kwenye ubalozi wa US Dar, Kasusura asingechota zile dola Millioni mbili pale Airport kama mchezo.

However, binafsi niliwahi kufika baadhi ya nchi tulkizokuwa tunafanana nazo kitikadi za siasa kama China, Russia, Hungary, Bulgaria, na Yugoslavia kabla hazijavunjika. Ukweli ni kwamba hizi nchi kama sisi zilikuwa na system ya kuwa-turn wananchi against each other, na that is exactly kilichokuwa kikifanyika kwetu, nchi ilikuwa tight economically, wananchi hatukuwa very active socially, kwa hiyo ilikuwa rahisi kwa uwt kutu-monitor wachache tuliokuwa active, hasa kwa kuwatumia wajumbe wa nyumba kumi kumi, madreva wa tax, waalimu wa level mbali mbali nationally, ma-bar maids, wahudumu wa guest house, wananchi oppressed siku zote ni lazima watafute njia flani socially kuweza ku-realese their frustrations, ambazo huwa hawaelewi chanzo chake ni nini? nani? au wapi?

Nchi za majuu, utakuta wananchi wakitumia sana drugs, na kuuana bila sababu, bongo wananchi wengi tulianza kuwa walevi na sex addiction, na ni huku kwenye ma-bar na sehemu za starehe ndiko uwt walitega sana watu wao, wake kwa waume, as the results mipango mingi ya uhaini na the rest of the story kama wizi wa mali za serikali na rushwa, ilikuwa ikibainika kwa urahisi sana kwenye hizi areas, na that usalama wetu ukaonekana kuwa very sophisticated, lakini ukweli ni kwamba kwa maoni yangu hii ilikuwa kweli only kwa local ishus, lakini ishus ambazo zilikuwa zinawahusisha at least one individual kutoka nje ya nchi, kwa kweli ninaamini kuwa the record is clear kuwa we were not that good, na mpaka leo bado tuko nyuma sana ndio maana hata uchunguzi Richimonduli, na na zingine zimetupa shida sana kuupata ukweli wake.

Kwa maoni yangu ni Labda we were good kulinganisha na nchi zingine za ki-Afrika, na hasa za majirani zetu wa karibu.
 
FMES,

Umenikumbusha mbali sana na wimbo wa Kiki, "mimi msafiri niko njiani" je unao ule origino?

Natafuta original songs za OSS, Marquiz, Makassy, Juwata, Mlimani, Kyauri Voice na nyingine na si remake za siku hizi zinazofanana na Ndombolo!

Rev,

Heshima mbele mkuu, nilikuwa na tabia ya kwenda pale Uhindini, yaanikati kati ya mitaa ya Mnazi Mmoja ambako miaka miwili iliyopita kulikuwa na duka maalum la TFC, walikuwa wakiuza tapes zote za zamani zilizokuwa zikichezwa na Radio Tanzania sijui kama bado wapo mpaka leo,

Sasa nilinunua tapes nyingi sana, kwa ajili maktaba yangu ya muziki na I took a time na kuzihamisha into CDs, kwa hiyo ninazo most of them, hasa za Marquis, Makassy, Sikinde, Safari Trippers, Afro 70, Ndala Kasheba, Urafiki Jazz, Msondo Ngoma, na the rest.

Anyways, later on tunaweza kuwasiliana kwa pembeni nione namna ya kukusaidia sina noma, kwa sababu siku zote huwa ninazitoa bure kwa wananchi wengi tu, ingawa pia I am working on kufungua internent Cafe na Studio ya Muziki, kwenye jengo ambalo hivi karibuni nilifungua Bar in patnership na ndugu yangu mmoja pale Dodoma, nina mpango wa kuiendeleza hii historia ya muzki wa taifa letu kwa muda mrefu sana to come.
 
Banyikwa, na wenginewe ambao siwakumbuki.[/B]
.

Nakumbuka Banyikwa aliwekwa rumamnde yeye na mkewe mpaka walipokuja kuachiwa huru baada ya kuonekana hawana hatia. Inasemekana vikao vingi vya hii timu vilifanyikia nyumbani kwao maeneo ya drive-inn flats enzi hizo.
 
Picha zimekwisha?

attachment.php


attachment.php
 

Attachments

  • polydor_label.jpg
    polydor_label.jpg
    11.6 KB · Views: 366
  • philips_jamhuri.jpg
    philips_jamhuri.jpg
    16.7 KB · Views: 363
Duh,

Mada hii baaabu kubwa sanaaaa yaani Jamii Forums inabidi kujiweka sawa na kuanzisha kumbukumbu hizi kisha kuzikabidhi Makumbusho!...FMES mkuu wangu hongera sana kwa kutoa hoja hiii...
........
Ni wapi tulikwenda mrama...

Wakati tukiendelea kujadili historia yetu ni vema kujadili wapi tulikosea kama anavyo uliza Mkandara
 
The "Kazi Nguvu" laws, which date back to the colonial period, and the Human Resources Development Act 1983 were intended to prevent migration to the cities from agricultural areas, and to support the 'Ujamaa' (community) policies of Nyerere to resist urbanisation. They stipulate that persons who are unemployed must return to their home region. These laws are however practically never used, with the exception of removing professional beggars from city streets. Tanzanian citizens can return to Tanzania without difficulty.

Mkuu Icadon,

Heshima mbele, niliwahi kuziona hizi operation mbili kwa wakati tofauti,

1. Niliwahi kuona kwa macho yangu uhamishaji wa wanachi kwenda kwenye vijiji, nikiwa likizo kijijini mwishoni mwa 69 na mwanzoni mwa 70s, operation ambayo ilkuwa ikifanywa kwa kutumia malori ya aina ya J-fong, kutoka China, na pia malori haya yalikuwa yakitumika kuleta maji kwa wananchi kwa jina la ma-Boza ya maji, haya yalikuwa yakija kijijini wananchi wanajipanga nyuma yake na ku-share maji kwenye ndoo na madebe, au yalikuwa yakiweka maji kwenye visima maalum kwa vijiji vilivyokuwa na visima.

- The outcome ya hii operation, kisiasa kuna maoni mengi sana tofauti, kuna ambao wanadhani ilikuwa a nightmare na kuna wanaodhani ilikuwa a success, lakini siku zote hutumika kama the litmus test ya mafanikio na the downside ya utawala wa Mwalimu.

- Again, binafsi sikuwa a political fan of Mwalimu, lakini bado ninampa heshima kwa sababu angalau he stood for something, au alikuwa ana vision of something, ingawa nilikuwa mdogo sana kujua uzuri na ubaya wake, lakini haiwezi kuwa a brainer kujua kuwa here the government was at work tena for wananchi, na ninakubaliana kabisa na wale wanaosema kuwa huenda tatizo lilikuwa kwenye watekelezaji na wafuatiliaji, lakini judjing from what nilichokiona then na kinachoendelea sasa kwenye serikali yetu, I would rather have a serikali inayojaribu na kushindwa kuliko serikali isyoeleweka exactly inasimamia nini?

- Na ni lazima niwe mkweli, kuwa ninaamini kuwa pamoja na all the downside za ile operation, bado ilitusaidia sana kwenye taifa, na location of ID kwa sababu leo huwezi kumtafuta mwananchi yoyote Tanzania, ukashindwa kujua jina la tarafa au kijiji anachotoka.

2. Pia mkuu niliwahi briefly kuliona zoezi la "Nguvu kazi" likifanyika Dar, under uongozi wa RC Mhaville, ambalo liliambatana sana na zoezi la wahujumu uchumi under Sokoine (RIP), na hili zoezi lilipelekea kutengenezwa kwa Filamu maarufu ya "Fimbo Ya Mnyonge" na Yomba Yomba, ambayo ilimuudhi sana Mwalimu, kwenye Premier yake kwa sababu ya act moja ndani yake ambayo ilisababisha kuharibiwa kwa shamba kubwa la mahindi, kule Iringa, Mwalimu hakusubiri hata iiishe aliondoka pale pale.

- Hili zoezi najua for a fact kuwa halikufanikiwa kabisaa kwa 100%, na ninakumbuka mataifa mpaka ya nje kama Germany, wakisema kuwa iwapo lingefanikiwa basi wangewachukua the architects wake bongo, wakawasaidie nao nchini kwao, kulitatua hili tatizo la wananchi kuhamia mijini kutafuta maisha bora zaidi ya kule vjijini au miji midogo.

-Again, bado hiii ilikuwa ni serikali iliyokuwa inasimamia something kwa hiyo ni politically correct kutoa heshima na salute kwa viongozi waliohusika, kwa sababu there is a political record hapo, as opposed na serikali ya sasa.
 
Wakati tukiendelea kujadili historia yetu ni vema kujadili wapi tulikosea kama anavyo uliza Mkandara

Mimi ninadhani kuwa kosa letu la kwanza na kubwa kuliko yote ni pale tulipoanza kujenga imani kuwa Nyerere alikuwa amekosea kwa kila jambo alilofanya. Kama serikali ya Mwinyi ingeanza kwa kutambua kuwa mengi ya yaliyofanywa na Nyerere yalikuwa ni sahihi na yalistahili kuimarishwa ila yale machache aliyoshindwa kuhusu usimamizi wa uchumi ndiyo yafanyiwe marekebisho, nadhani tungekuwa katika nafasi nzuri sana. Mwinyi alianza kwa kupangua kila jambo alilofanya Nyerere, na hivyo kupanda mbegu za tamaa za mali miongoni mwa viongozi wa serikali, na Mkapa alipofika, akakuta zile mbegu za tamaa zilizopandwa na Mwinyi zimeshakomaa ndipo ufisadi ukapanda chati exponentially, na nchi iakosa mwelekeo kabisa.
 
Wakati tukiendelea kujadili historia yetu ni vema kujadili wapi tulikosea kama anavyo uliza Mkandara

Mkuu Kibunango,

Heshima mbele sana, siamini kwamba kwenye hii thread tunaweza kuwa na a clear answer on that, kwa sababu kuna wanaomini kuwa hatuja enda mrama so far, na kuna tunaoamini kuwa tuko mrama tayari na toka siku nyigni sana zilizopita,

Labda ninaweza kusema kuwa, hii topic bado inaendelea kwa hiyo labda historia inayotolewa hapa, inaweza kumsaidia mwananchi kujumlisha na kutoa kuwa ni wapi tulianzia kwenda au kutokwenda, mrama.

My personal experience, kwa brief tu ni kwamba matatizo yakitaifa kiuchumi, yalikuwepo siku zote lakini yalikuwa yanavumilika, lakini maisha yalikuwa safi na yalianza kubadilika kwenye miaka ya mwanzoni mwa 80s, hasa betweeen 1981-1984, ndipo kwa mara ya kwanza yakaanza kuwa hayavumiliki tena na hasa utawala wa awamu ya pili ulipoanza tu,

Lakini ninaamini hii ni ishu nzito sana by itself, inahitaji independent thread kujadilika kwa kirefu na mapana.
 
Mimi ninadhani kuwa kosa letu la kwanza na kubwa kuliko yote ni pale tulipoanza kujenga imani kuwa Nyerere alikuwa amekosea kwa kila jambo alilofanya. Kama serikali ya Mwinyi ingeanza kwa kutambua kuwa mengi ya yaliyofanywa na Nyerere yalikuwa ni sahihi na yalistahili kuimarishwa ila yale machache aliyoshindwa kuhusu usimamizi wa uchumi ndiyo yafanyiwe marekebisho, nadhani tungekuwa katika nafasi nzuri sana. Mwinyi alianza kwa kupangua kila jambo alilofanya Nyerere, na hivyo kupanda mbegu za tamaa za mali miongoni mwa viongozi wa serikali, na Mkapa alipofika, akakuta zile mbegu za tamaa zilizopandwa na Mwinyi zimeshakomaa ndipo ufisadi ukapanda chati exponentially, na nchi iakosa mwelekeo kabisa.

Mwalimu,

Je kunauwezekano kuwa kuvuruga kwa maendeleo kiduchu tuliyokuwa nayo yalitokana na woga wa nchi zilizoendelea kuwa tukiachiwa huru tukajitutumua kwa udhaifu wa uchumi wetu lakini tukiwa na msimamo, tungekuwa mfano wa kuigwa na hivyo kuvunja nguvu za kuwa Taifa tegemezi?

Je Mwinyi, Mkapa na hata Kikwete sasa hivi wamepumbazwa kabisa kwa nyimbo nzuri za globalization na free market economy bila kujua athari zake kwa uchanga wa Taifa kama letu ambalo bado halijawa na Wananchi wazawa wenye uwezo wa kuzalisha na kumiliki misingi na njia za uchumi?
 
Back
Top Bottom