Tukumbuke Zamani: Historia ya Taifa letu katika picha

Tukumbuke Zamani: Historia ya Taifa letu katika picha

Starehe na Burudani;

View attachment 2378

...Yvonne Chaka Chaka naye alikuja kututumbuiza miaka ile na vibao vyake, kama ..."am in love with a Dj", nk, na huyo jamaa alikuwa 'mbabe kweli kweli' (utadhani willy Isangura!) Kwenye Club moja maarufu mjini Dar, ambayo mmiliki wake sasa ni Mwenyekiti wa Chama kikuu cha Upinzani Bara.
 
mchongoma unanikosha vibaya na posts zako ....!
 
Starehe na Burudani;

View attachment 2378

...Yvonne Chaka Chaka naye alikuja kututumbuiza miaka ile na vibao vyake, kama ..."am in love with a Dj", nk, na huyo jamaa alikuwa 'mbabe kweli kweli' (utadhani willy Isangura!) Kwenye Club moja maarufu mjini Dar, ambayo mmiliki wake sasa ni Mwenyekiti wa Chama kikuu cha Upinzani Bara.

Huyo jamaa alikuwa anaitwa Wandiba na ni marehemu sasa hivi.Kweli alikuwa mbabe sana.
 
Mchongoma hapo umeniacha hoi mkuu, ubarikiwe tu huyu mshikaji aliyesimama na Chaka Chaka, ni Mkulu Wandiba (RIP) enzi za Mbowe RSVP DISCO Club, DJ Jerry Koto, Kali Kali na Seydou, duh mkuu this is wasup kwa kweli maana jamaa enzi hizo kama hujalip kiingilio pale mlangoni usingeweza kuingia bro, mzee wa Musoma huyo saafi sana.

Halafu picha ya Chifu Kikanga,

Unajua kuna one thing kwenye picha, ni jinsi wananchi walivyokuwa na furaha ingawa maisha yao kwa standard za sasa tunaweza kuita maisha duni, lakini wanaonekana kuwa walikuwa wameridhika kabisa na maisha, as opposed na pciha za siku hizi ambazo unaona wananchi wana wasi wasi sana.

Mkuu Mchongoma ubarikiwe maana mchango wako kwenye hii thread na hasa Kichuguu, Idacon, Joka Kuu, Lamba, na wenginineo ni baabu kubwa sana, mbarikiwe tu.
 
pale mbowe disco,kulikuwa na dj mmoja i think gerald,wanasema alikuwa hajui kusoma,eti yeye akiipapasa sahani ya santuri na vidole vyake,ameshajua nyimbo gani.hii mutu ilikuwa inapanga ngoma hatari. wakuu,eti nini asili ya jina la hospitali ya muhimbili ?
 
pale mbowe disco,kulikuwa na dj mmoja i think gerald,wanasema alikuwa hajui kusoma,eti yeye akiipapasa sahani ya santuri na vidole vyake,ameshajua nyimbo gani.hii mutu ilikuwa inapanga ngoma hatari. wakuu,eti nini asili ya jina la hospitali ya muhimbili ?

...soko la ajira enzi hizo, akili kumkichwe!, hata RAY ABDUL (R.I.P) alikuwa anakula kwa domo lake, ila hiyo ya Jerry Kotto kupapasa nyuzi bin nyuzi 😀...imetiwa chumvi maazee, the guy was just gifted!

Kuna mwingine aliajiriwa na huyu mheshimiwa wa siku hizi kuokota chupa pale, muda si muda (huenda kutokana na makelele ya kila siku ya beats mbali mbali) siku alipoachiwa Deck mambo aliyoyafanya siku hiyo hakuna aliyebaki kitini, and the rest is History!...


View attachment 2384

Ocean Rd Hosp, built in 1897, ...birth records zetu wengine tulozaliwa hapo huenda mafaili yeshaliwa na panya ama yamegeuka Vumbi!!!
 
Duh! ukweli lazima niukubali kwenye hili ES kula tano mwanangu. Regardless madongo mepesi mepesi ambayo huwa nakupiga lakini hiyo si sababu ya kukataa pale unapo fanya vitu vyako

duh
 
Si vibaya pia kuona hali ilivyo sasa ili kujenga uwiano baina zama zile na hizi

Hapa ni Coco beach ambayo karibu itanunuliwa na "wawekezaji" kutoka kutoka Ras al Khaimah

170077-coco-beach-dar-es-salaam-tan.jpg


Siku hizi children amusement bongo kama majuu, hapa ni ni mtaa jirani na ninapoishi na familia yangu slipway

170100-the-slipway--family-friendly.jpg



Bila kusahau "terminal one" yetu

39069-small-airport-in-dar-dar-es-s.jpg


Tazara nayo during heydays

174442-dar-es-salaam-tazara-station.jpg
 
...eti nini asili ya jina la hospitali ya muhimbili ?

...Wazaramo watatusaidia, ila 'nadhani' kabla ya kuitwa Muhimbili, ilikuwa inajulikana kwa jina la Princess Margaret Hospital, katika wodi zake tatu mashuhuri, KIBASILA, MWAISELA, SEWA HAJI, huyu ndiye Bwana SEWA HAJI-PAROO ( 1851-1897), aliyejitolea kujenga zahanati kusaidia watanganyika na wazanzibari...R.I.P, mchango wako kwa watanganyika na waunguja uhidimiwe.

View attachment 2385
 
Mwanakijiji,
Tumetoka mbali. Hiyo tabia ya kwenda airport niliendelea nayo hadi hapa Marekani mpaka walipozidisha parking fees.
Hata mimi nashindwa kuelewa hako katabia kametoka wapi.....kinawagusa wengi!!
 
Nchi zilizo Mstari wa Mbele katika Ukombozi wa Nchi za Kusini mwa Afrika.... Pichani chini ni mojawapo wa Viongozi waliopata kunufaika na nafasi ya Tanzania katika front line states...

337225955_e1e3bde712.jpg
 
mchongoma said:
Kiongozi lazima awe na VISION, awe mtekelezaji na msimamizi wa maendeleo ya wananchi wake! ...bahati mbaya viongozi wetu 'wengi' wa kiafrika (mpaka leo hii) wanaukosefu wa hiyo kitu!...

...hebu angalia (mfano) Chief Kikanga na wananchi wake wa BUKUMBI miaka ya 1900's, halafu linganisha na Unguja ya miaka ya 1800's kwa ushahidi wa picha, kisha uniambie hiyo picha inakupa sura gani?

mchongoma,

..Ikulu,reli,skuli,etc etc wakati wa utawala wa Sultani yalikuwa ni maendeleo ambayo wananchi/watumwa hawakuwa na faida nayo.

..of course, Sultani alikuwa na exposure na ujuzi wa kiufundi kuliko huyo Chief wa Bukumbi uliyetuletea picha yake. but that wasnt my point to begin with. nilichokipinga mimi ni ile hali ya unyama/utumwa iliyotumika ktk kuleta "maendeleo" wakati wa utawala wa Sultani.


mchongoma said:
...juu ya ubaya wote wa Utawala wa kisultani na kikoloni, Miundombinu na mengineo yote walohenyeshwa mababu zetu kuijenga, leo hii tunakula matunda yake na hata kuringia.

Angalia, Kuanzia Ikulu zetu ya Dar es salaam na ya Unguja zilijengwa na Mkoloni/Sultani, halafu angalia wakajenga Hospitali zetu kubwa Tanzania, Muhimbili, V.I Lenin a.k.a Mnazi mmoja, nk...

...miaka 44 tangu 'mapinduzi matukufu' ya kumng'oa Sultani, umeme bado 'kimeo' unguja na Pemba? aaaahh aibu!!!

Ukweli ukidhihiri uongo hujitenga!

mchongoma,

..ninavyoelewa mimi serikali zetu za uhuru zimejenga miundombinu mingi, na kutoa huduma kwa jamii, kuliko wakati wa wakati wa mkoloni na huyo "sultani mtukufu."

..matatizo yapo, na kila mtu anaelewa, lakini hiyo haiwezi kunifanya hata siku moja niote na kutamani kuishi chini ya Utawala wa Sultani wa Zanzibar kama wengine mnavyojaribu kuchombeza hapa.
 
Hivi kwanini tulikuwa tunafunga safari kwenda Airport kuangalia ndege zikipaa na kutua? Yaani mgeni akija kutoka bara mojawapo ya maeneo ya kumpeleka ilikuwa Airport.!!

Kwikwikwiiiiiii.....Ndivyo Tulivyo!!!

Wengine tulikuwa tunaenda pale posta ya zamani kuangalia meli......
 
nyani,posta ya zamani kwenda kuangalia meli labda wewe,sisi tulikuwa tunafunga pale kuhunt videnish
 
pale mbowe disco,kulikuwa na dj mmoja i think gerald,wanasema alikuwa hajui kusoma,eti yeye akiipapasa sahani ya santuri na vidole vyake,ameshajua nyimbo gani.hii mutu ilikuwa inapanga ngoma hatari. wakuu,eti nini asili ya jina la hospitali ya muhimbili ?

1. Unajua Tanzania, pamoja na siasa zetu enzi zile, lakini bado tulikuwa na nafasi ya ku-socialize hasa kwenye ma-Disco na muziki wa Dance, kwenye hili ni lazima tuwe fair kuwa Mwalimu hakuwa na tatizo kabisaa.

2. Ni kweli kwamba ex- DJ Gerard, au kama alivyokuwa akifahamika kwa jina la "Jerry Kotto", alitokea kuwa mmoja wa the best DJs mjini Dar, na ni kweli kwamba alikuwa na matatizo ya kusoma, lakini Jerry alikuwa na tabia moja nayo ni akipata Album au Tape hukaa chini na kuisikiliza mwanzo mpaka mwisho, akisikia ngoma anayoamini kuwa ni safi basi husimamisha na kuweka alama kwanza kwenye Tape/Album na pia kwenye namba ya ile song, sasa akingia kupiga Disco huzikumbuka nyimbo zote zilipo na ni zipi, tena bila ya tatizo.

3. Kwa kadri ninavyokumbuka tumewahi kuwa na Ma-DJ waliokuwa waburudishaji na wakali, kwa sababu pamoja na kwamba wao yaani ma-DJ walikuwa sio wapigaji hasa wa zile nyimbo, lakini siku zote mchele ni ule ule, ila mapishi ndio hubadili matokeo, hata ma-DJ nao ilikuwa ni hivyo hivyo, kwa kweli ningeomba kuwakumbuka tena kwa nafasi zao, wale wote yaani ma-DJ waliowahi kutuburudisha mjini Dar kama ninavyowakumbuka na pia msaada unakubalika iwapo kuna niliowasahau au kuwaweka kwenye nafasi wasizofaa:-

1. DJ Justin Kusaga - Clouds (Morogoro).
2. DJ Kali Kali (Kalikawe) - YMCA/Mbowe.
3. DJ Ebbo Night Woo Jack! (Bob Rich Mazula) - Msasani Beach.
4. DJ Chris Phaby "The Lover" - Mbowe/Margott.
5. DJ Choggy Sly (Choggo Salum) & DJ JPP (John Peter Pantalakis) - Msasani Beach/Rungwe Beach
6. DJ Roma Pop Juice (RIP) - Mwanayamala.
7. DJ Jerry Kotto (Gerard) - Mbowe RSVP Club.
8. DJ Nigger Jay - YMCA.
9. DJ DC Washington (RIP) - Rungwe Beach.
10. DJ Lucas
11. DJ Tito Jackosn (Tito Kalumanga) - Rungwe Beach.
12. DJ John Bure
13. DJ Joe Kusaga (Joseph Kusaga) & DJ Stewart (Sterwart Chiduo) - Clouds.
14. DJ Kim (Kim) - Rungwe Beach.
15. DJ Kessy (Kessi) - Blue Sky Disco.
16. DJ Eddy - Magomeni.
17. DJ Super Deo (Deo) - YMCA/Margott.

4. Kwa upande wa muziki wa Dance, pia tilkuwa na bendi za wazawa na wageni, hasa kutoka Zaire na wao pia kulingana na nafasi zao kimuziki as I remmember, na time pia lakini pia msaaada unakubalika:-

1. End of The 60s:-

1. Orch. Morogoro Jazz - Mbaraka Mwinshehe (RIP).
2. Orch. Cuban Marimba - Salum Abdallah (RIP).
3. Orch. Nova Success - Baba Gaston (Nairobi).
4. Orch. Nuta Jazz - Muhidini Gurumo (Ilala - Msondo Ngoma).
5. Orch. Tabora Jazz - Wema Abdalalh/Shem Karenga (Tabora).
6. Orch. Western Jazz - Wema Abdallah (Sikukuu street Kariakoo, Dar).
7. Orch. Dar Jazz - Dar.
8. Orch. Unyanyembe Jazz - (Nyanyembe Tabora.)
9. Orch. Kilwa Jazz - Ahmed Kipande/Juma Mrisho (Kilwa).
10. Orch. Police Jazz - Dar.
11. Orch. Atomic Jazz - John Kijiko (Tanga).
12. Orch. Kilombero Jazz - (Kiwanda cha Sukari Kilombero).
13. Orch. Butiama Jazz - Ifakara.
14. Orch. Boma Liwanza - (Zaire/DSM).
15. Orch. Banangenge - Fataki Masumbuko Ya Dunia (Zaire/DSM).

2. In the 70s. to 80s:-

1. Orch. Super Volcano - Mbaraka Mwinshehe (Morogoro).
2. Orch. TK Lumpopo - Juma kilaza (Morogoro).
3. Orch. Afro 70 - Patric Balisidya (DSM).
4. Orch. Urafiki Jazz - Juma Mrisho (DSM).
5. Orch. Nuta Jazz - Muhidini Gurumo (DSM).
6. Orch. Marquiz du Zaire - Chinyama chiyanzi (Zaire/DSM).
7. Orch. Vijana Jazz - Andoro/Maneti (DSM).
8. Orch. Safari Trippers - Marijani Rajabu (DSM).
9. Orch. Mwenge Jazz - George Mpupua (JWTZ- DSM).
10. Orch. JKT Kimbunga - Mzee Zakaria (DSM).
11. Orch. Kimuli muli - Zahiri Zoro (JKT Mafinga/DSM)
12. Orch. Simba Wa Nyika - Wilson & George Peter (Arusha/Nairobi).
14. Orch. Dar International - Abel Baltazari/Marijani Rajabu (DSM).
15. Orch. Police Jazz - Moshi William (DSM).
16. Orch. BarKeys - George Mhando (DSM).
17. Orch. Sola TV - (Temeke - DSM).
18. Orch. Makassy - Mzee Makassy (Zaire/DSM)
19. Orch. Nkashama Nkoi - Ndala Kasheba (RIP) (Zaire/DSM).
20. Orch. Matimila - Remmy Ongalla (Songea/DSM).
21. Orch. Sunburst - Kassim Magati (DSM).
22. Orch. Tanzanite - Nembo (DSM).
23. Orch. Toma Toma - Thomas (DSM).
24. Orch. Mpakani Kyauri Voice - Mzee Khatibu Itei Tei (DSM).
25. Orch. Mlimani Park - Abel Baltazari/Gurumo (DSM).
26. Orch. Doble O - King Kiki (Zaire/DSM).
27. Orch Safari Sound - Mbombo wa Mbombo-Ka/King Kiki/Ndala Kasheba (Zaire/DSM).
28. Orch. Mk Group - Kossongo Mpinda/shem Karenga (DSM).

Huenda kuna niliowaacha, lakini ninaamini kuwa ma-DJ tulionao sasa na bendi za muziki, ni kuanzia in 90s hadi leo ni almost wale wale na bendi ni zile zile ingawa cha kusikitisha sana ni kwamba kama ni bendi zilizopo leo labda hazizidi nne, zingine zote zilikufa kifo cha mende, lakini ni vyema kukumbuka kuwa katika enzi zile za 70s, 80, na mwanzoni mwa 90s pamoja na msiha kuwa magumu kidogo siku zote tulikuwa na burudani kabambe ambazo some of us zilitusaidia sana kuendelea kuyakabili maisha, knowing kwamba kuna weeek end kwenda kula mangoma na kuku za kibongo bongo.

Heshima Mbele Wakuu.
 
Back
Top Bottom