Tukumbuke Zamani: Historia ya Taifa letu katika picha

Tukumbuke Zamani: Historia ya Taifa letu katika picha

.DJ Mc hope[makop]....CAVE DISCO TQ -arusha...........or arusha by nite ..late 70"s To early 90"s [RIP]

KURUGENZI JAZZ BAND....msimbe and bonzo...

nyerere alikuwa bomba sana enzi zake tulikuwa na band kila mkoa zikiburudisha....tulikuwa na ligi za ushindani[tena bila wadhamini ]..kila mkoa......timu za mashirika....arusha na moshi...

KILTEX
MOULBADOW-karatu
mbuni...
AICC
NDOVU
USHIRIKA -MOSHI
CCP
TPC
AFRICAN SPORT[WANA KIMANU MANU]
COASTAL UNION

DODOMA....

KURUGENZI
CDA
MTO - SINGIDA

ZIWA..

RTC KAGERA
RTC - SHINYANGA
RTC MWANZA-----DANNY MUHOJA...
PAMBA - WAANA KAWEKAMO...
RTC KIGOMA
RELI KIGOMA...

DUU jamani unaweza kulia.....hatukuwa na pesa lakini tulikuwa tunapata entertainment..........
 
Nchi zilizo Mstari wa Mbele katika Ukombozi wa Nchi za Kusini mwa Afrika.... Pichani chini ni mojawapo wa Viongozi waliopata kunufaika na nafasi ya Tanzania katika front line states...

Mkuu Kibunango,

Heshima mbele sana, hapo nimewaona Sam Nujoma(SWAPO-Namibia), Samora Machel (Frelimo-Mozambique), Kaunda (ex-Rais Zambia), na Mugabe (ZANU-PF Zimbabwe).

Wallahi enzi hizi wananchi tulikuwa hatulazimishwi na viongozi kwenda Airport kuwapokea hawa viongozi, yaani it was so good a history in the making kwamba hakuna aliyetaka kuikosa kuiona ikitengenezwa na Mwalimu.

Ahsante sana Mkuu Kibunango.
 
MAJI MAJI-SONGEA...wappi shafie bora..
KATAVI RANGERS - RUKWA
LIPULI-IRINGA
MECCO-MBEYA
TUKUYU STARS...wapi KAKA..
UFUNDI-MBEYA[PRISONS?]
TRM-MUHEZA[now TANROADS]
MWADUI - SHINYANGA
BANDARI-MTWARA
LINDI[?]
RELI-MORO..wapi JUMA LIMONGA 'stop engine"..WAPI ..dr madundo mtambo...
TUMBAKU
MSETO....

dar WAPI...

PILSNER...
KILIMANJARO HOTEL..wapi nico kiondo,maliro...
..BOOM ...RIP...amir ali bamchawi..mlezi wa wana...,mzee wa pilau mbuzi..mtaalamu wa mvua..simba dume..
FARU DUME..
SIGARA..
WAZO..
........................
 
field marshall,dj kalikali ni marehemu,baadaye akaibuka mdogo wake katika fani ya reggae kwa jina kalikawe naye vilevile ni marehemu.
jamani humu ukumbini inabidi tuseparate the man from the boys.NAULIZA je kuna member yoyote humu kacheza disco sansui lililokuwa seaview.
 
Wakuu naomba kutoa ombi kidogo, kwa wananchi wote ni kwamba so far tunakosa kuwa na picha za historia ya Vyama vya upinzani Tanzania kwenye hii thread, kwa hiyo tunawaomba kwa yeyote mwenye anything kuhusiana na historia ya upinzani nchini, tumwagieni wakuu ili tuchambue,

Natanguliza Shukrani.
 
.DJ Mc hope[makop]....CAVE DISCO TQ -arusha...........or arusha by nite ..late 70"s To early 90"s [RIP]

KURUGENZI JAZZ BAND....msimbe and bonzo...

nyerere alikuwa bomba sana enzi zake tulikuwa na band kila mkoa zikiburudisha....tulikuwa na ligi za ushindani[tena bila wadhamini ]..kila mkoa......timu za mashirika....arusha na moshi...

KILTEX
MOULBADOW-karatu
mbuni...
AICC
NDOVU
USHIRIKA -MOSHI
CCP
TPC
AFRICAN SPORT[WANA KIMANU MANU]
COASTAL UNION

DODOMA....

KURUGENZI
CDA
MTO - SINGIDA

ZIWA..

RTC KAGERA
RTC - SHINYANGA
RTC MWANZA-----DANNY MUHOJA...
PAMBA - WAANA KAWEKAMO...
RTC KIGOMA
RELI KIGOMA...

DUU jamani unaweza kulia.....hatukuwa na pesa lakini tulikuwa tunapata entertainment..........

Sawa Sawa Mkulu PM,

1. Tulikuwa na shida lakini masikini jeuri, ni kweli nilisahau hawa Kurugenzi Jazz ya Arusha, ambao nusu yake walimeguka na kuondoka na Simba Wa Nyika, kuhamia Nairobi, Lazaro Bonzo aliyekuwa the right hand man wa Mbaraka Mwinshehe naye baadaye alihamia Nairobi na kuanzisha bendi ya Orc. Lombe Lombe,

2. Kwenye michezo ya Mashirika ya Umma ilikuwa balaa maana huko ndio ulikuwa unawakuta wachezaji wote wakubwa wakicheza kwenye viwanja vya bure, yaani bila kulipa kwenye michuano ya awali, umeisahau Tumbaku ya Morogoro ikiwa na meneja wao aliyewahi kuwa RC wa Morogoro Mzee Lyanda, ambaye alitishia kuwa atamuweka ndani kiongozi yoyote wa Yanga au Simba atakayejaribu kunyemelea wachezaji wa Tumbaku, wakati akiwa RC Mwalimu akam-demote na kumpa u-meneja wa Pamba hapo hapo Morogoro ili aongoze vizuri mpira.

- Halafu kulikuwa na mashindano ya Sekondari Umiseta, duh ile ilikuwa baabu kubwa, maana ni kutoka kwenye hii michezo tuliweza kupata wachezaji kama Nico Njohole, Rahim Lumelezi, Jella Mtagwa, George Kulagwa, Patric Rugaimukamu na wengineo.

Ahsante mkuu.
 
mchongoma,

..Ikulu,reli,skuli,etc etc wakati wa utawala wa Sultani yalikuwa ni maendeleo ambayo wananchi/watumwa hawakuwa na faida nayo.

..of course, Sultani alikuwa na exposure na ujuzi wa kiufundi kuliko huyo Chief wa Bukumbi uliyetuletea picha yake. but that wasnt my point to begin with. nilichokipinga mimi ni ile hali ya unyama/utumwa iliyotumika ktk kuleta "maendeleo" wakati wa utawala wa Sultani.




mchongoma,

..ninavyoelewa mimi serikali zetu za uhuru zimejenga miundombinu mingi, na kutoa huduma kwa jamii, kuliko wakati wa wakati wa mkoloni na huyo "sultani mtukufu."

..matatizo yapo, na kila mtu anaelewa, lakini hiyo haiwezi kunifanya hata siku moja niote na kutamani kuishi chini ya Utawala wa Sultani wa Zanzibar kama wengine mnavyojaribu kuchombeza hapa.

...WHAAAAAT???

Anyway!, ..."Ukubwa jaa", 🙂

...tunaendelea na mapicha, siku hizi ukivaa kama kina Makochela au Braza masouuuuud masoud, utaonekana "mluga luga!"......


View attachment 2387
 
Mzee Fd ES,
Umesahau akina Ibrahim Kiswabi, Ahmed Amasha, Ibrahim Marekano, Daudi Salum aka Kaburu, Mwalusako, Abdalah Mtemi, Said George n.k.,toka timu ya Kamiseta Tabora, hawa ilikuwa chachu kubwa saana fainali ya Umiseta Iringa, nafikiri ilikuwa 76, Tabora ilipokutana na Dar ambayo ilikuwa na safu uliyoitaja hapo. Wakati huo Tabora ilikuwa ilikuwa inavifaa kwelikwli
 
Mkuu Babadesi,

Heshima mbele, mengi umepatia sana na ni ukweli mtupu, isipokuwa ni kwamba:-

1. Maneti alipoingia Vijana Jazz, mtindo wake wa kwanza ulikuwa ni wa "Kamata Sukuma", solo zima la hii album ambayo aliirekodi Nairobi, alilipiga Hamza Kalala "Komandoo" akiwaiga Orch. Sosoliso ya Zaire. Album hii ilikuwa na nyimbo zifuatazo:-

- 1. Kamata Sukuma, 2. Magdalena, 3. Dada Sabina, 4. Nimeruka ukuta, 5. Salima, 6. Viva Frelimo.

2. Waliporudi kama ulivyosema wazee wa Chama hawakuridhika kabisa na mwenendo mzima wa bendi, kwamba waliiona ikianza kukiuka maadili ya chama, kwa hiyo wakamuamuru Maneti, abadili ile style, Maneti akabuni mtindo mpya wa "Koka Koka ni Balaa" , again wakatoa album mpya yenye nyimbo kama:-

- 1. Pili, 2. Operesheni Maduka, 3. Belibe, 4. Kalulu dibweze djigolo djangu, 5. Masido, 6. CCM.

3. Sasa wakaletewa vyombo vipya vya kisasa, Maneti akaibuka na mtindo mpya wa "Heka Heka" na vibao kama:-

1. Lela, 2. Ngoma, 3. Heka Heka Huyo Anapata, 4. Weekend, 5. Mwisho wa Mwezi. 6. Mozambique (Wembe ni ule ule)

4. This time Maneti akaja na extension ya Heka Heka, akaiita Heka Heka Takatuka, na Pambamoto na nyimbo kama:-

1. Maria, 2. Bujumbura, 3. Chiku, 4. Shoga,

Ndipo Mkulu Maneti sasa akatangulia kwenye haki, na kumuachia Eddy Sheggy aliyekuja na mtindo wa Sagarumba, ulikuwa mwisho wangu wa kuwafuatilia, maana sikuelewa kabisa walichoanza kupiga, lakini otherwise Babadesi, maneno yako yote ni sawa kabisa na kwa kumbu kumbu tu ni kwamba hivi vibao vyote ninavyo kwenye maktaba yangu.

Mzee FMES,

Najua una rekodi kubwa sana ya mambo ya wakati huo, ila nakuomba tena upitie kumbukumbu zako vizuri na kwa makini. Ukweli ni kuwa mtindo alioanza nao Marehemu Maneti pale Vijana Jazz ulikuwa ni Koka Koka. Wimbo wa Kamata Sukuma ulitolewa kipindi kimoja na Niliruka Ukuta, na ulipigwa pia katika mtindo wa Koka Koka, ila kutokana na umaarufu ulioambatana na wimbo ule wa Kamata Sukuma, Maneti akapromote wimbo wa "Kamata Sukuma" kuwa mtindo uliorithi Koka Koka mwaka 1976 hivi, na ulidumu muda mfupi sana kabla hajaanzisha Heka Heka. Kumbukumbu yangu kuhusu wimbo wa "Niliruka Ukuta" ambamo sauti ya Marehemu Maneti ilikuwa haitofautiani na ile ya Marahemu Mbaraka inakuja vizuri sana. Vile vile chini ya mtindo wa Koka Koka, Maneti alipiga wimbo wa "Zuhura Ninaondoka" ambao binafsi nilikuwa nauhusisha sana na mpenzi wangu wa wakati huo Marehemu Zuhura (RIP). Nilikuwa nina T-Shirt moja ya Sunflag iliyokuwa na picha ya kichwa cha tembo kifuani; mgongoni nikaandika pale maneno matatu kwa style ya aina yake: maneno hayo yalikuwa ni Masika, Sokomoko na Koka Koka, ambayo ilikuwa mitindo ya muziki niliyokuwa naizimia sana wakati ule. Marafiki zangu wa wakati huo wa ujingani wakisoma post hii watakumbuka sana ninayosema. Wakati Maneti anatoa wimbo wa "Niliruka Ukuta," Mbaraka naye alitoa wimbo wa "Mshenga" ambapo Marijani naye alikuwa ametoa wimbo uliokuwa unasema "Wapangaji mnawaacha watoto wenu wanavunjavunja milango na madirisha ndani ya nyumba yangu, hivyo ni afadhali muondoke kwani mnaleta sokomoko ndani ya nyumba yangu": jina halisi la wimbo huu silikumbuki tena. Nyimbo hizi zilikuwa kiboko sana wakati huo ndiyo maana kwangu mimi muziki ukawa ni Masika, Koka Koka na Sokomoko.


Kuna watu wengine wanaweza pia kuthibitisha hili. Hebu soma hapa:

Vijana Jazz isiachiwe ife

Ibrahim Mkamba Februari 6, 2008



VIJANA Jazz au Vijana Orchestre, vyovyote utakavyoiita, iko taaban na imelazwa kwenye wodi ya wagonjwa mahututi ingawa ukiiangalia inaonekana kuwa na afya njema.

Ndiyo, inaonekana ina afya njema kutokana na mseto wa wanamuziki mahiri ilio nao wanaojumuisha watu wazima wenye uwezo mkubwa wa aina ya muziki wa kiutu uzima na vijana walio mahiri katika midundo ya ujana ujana.

Penye mseto kama huo ni lazima patoke vitu vikali vya kuwafurahisha watu wazima na vijana lakini mbona mambo hayaendi?

Bendi hii haipaswi kufa kwani ni mali ya vijana na ni alama ya harakati za vijana wa Tanzania za kujenga nchi yao. Ilianzishwa mwaka 1974 katikati ya vuguvugu la kuwahamasisha vijana wajibu wao wa kujenga nchi na kujiandaa kupokea uongozi wa nchi kutoka kwa wazee.

Kiongozi wa kwanza wa bendi hii kwa muda mfupi alikuwa John Ondolo, mwanamuziki Mtanzania aliyeishi Kenya kwa miaka mingi na kujipatia umaarufu mkubwa katika fani ya muziki nchini humo bila wengi kujua kuwa alikuwa Mtanzania, wakiamini alikuwa Mkenya hadi aliporudi nyumbani mwaka 1971.

Muda mfupi baadaye, marehemu Hemed Maneti Ulaya alipokea mikoba ya uongozi wa bendi hiyo kutoka kwa John Ondolo. Maneti alikuwa ametokea Morogoro kwenye bendi ya TK Lumpopo ya Marehemu Juma Kilaza.

Kimuziki, marehemu Maneti aliibuliwa, kuinuliwa na kulelewa na marehemu Kilaza. Sauti yake inasikika sana kwenye nyimbo za "Maisha Ya Sasa", "Esther Chaguo Langu"," Inanyonya Subusubi" na nyingine za TK Lumpopo.



Marehemu Maneti alipochukua uongozi wa bendi ya Vijana Jazz alianza nao na mtindo wa Kokakoka. Vibao maarufu vya mwanzo mwanzo vya bendi hiyo vilikuwa "Nimeruka Ukuta" uliofahamika na wengi, "Sabina" na Magdalena". Kwenye wimbo wa Sabina alimuomba mpenzi wake Sabina arudi kwani siku nyingi zilikuwa zimepita tangu aondoke na kwenye wimbo "Magdalena" alikuwa analalamika kuzuiwa na wazazi wake kumuoa Magdalena kwa sababu alikuwa na ulemavu wa jicho wakati yeye alikuwa akimpenda sana.

Pamoja na nyimbo hizo, nyimbo nyingine za mwanzo mwanzo za bendi hiyo zilikuwa, "Zuhura Naondoka", "Kamata Sukuma" waliotumia kujitaja majina, "Salima", "Nimeruka Ukuta Namba Mbili" na "Magdalena Namba Mbili" ambamo Maneti alifurahi baada ya wazazi wake kukubali amuoe Magdalena.



Kama ilivyoelezwa awali, bendi hii ilikuwa na majukumu rasmi katika kuwapo kwake. Hii inathibitishwa na aina ya nyimbo ilizowahi kutunga. Hebu angalia mifano hii: Kwanza bendi hii ni bendi pekee nchini kuwahi kutunga wimbo usio na lugha ya mafumbo wala utata wa kukemea rushwa, Huu ni ule wimbo uliorekodiwa RTD mwaka 1976 ambapo mpwa ameenda kumuomba mjomba wake nauli ya kurudi kijijini akawe mjamaa kamili baada ya kukosa ajira mjini kutokana na kuombwa rushwa ndipo aajiriwe.

Katika wimbo huo, kuna mahali marehemu Maneti aliimba,"nitapata wapi pesa ya kumpa ikiwa na mimi natafuta kazi, tabia kama hii lazima ikomeshwe"

Pili,ni bendi hii pekee ndiyo iliyojitokeza na kuunga mkono wito wa chama tawala (Chama cha TANU wakati huo wa mfumo wa chama kimoja) uliotolewa mwanzoni mwa mwaka 1976 wa kuanzishwa kwa maduka ya ushirika.

Waliimba hivyo katika wimbo wa "Operesheni Maduka" waliourekodi pamoja na huo wa Rushwa. Nyimbo nyingine katika toleo hilo zilikuwa "Masido", "Uhuru wa Mapenzi" na nyingine.

Tatu, ni Vijana Jazz pekee ndiyo iliyotunga nyimbo kadhaa za kuwahimiza vijana nchini kujua wajibu wao wa kulinda na kujenga nchi. Walifanya hivyo katika utunzi wao wa mwaka 1978 na mwingine wa mwaka 1983. Nyimbo hizo zote mbili zilikuwa zinaihusu CCM kwa sababu kwa wakati huo ndiyo kilikuwa chama pekee cha siasa nchini mwetu wakati wa mfumo wa chama kimoja.

Vilevile, ni bendi hii pekee ndiyo iliyotunga wimbo wa kuwalaani "Magaidi" wa Msumbiji mwaka 1987.

Inasikitisha kwa bendi hii leo kuchoka namna hii bila wadau wa muziki nchini kujali. Huwezi kuamini leo kama bendi hii kwa nyakati tofauti imewahi kuwa na wanamuziki maarufu kama Hemed Maneti, Hamza Kalala, mwenyekiti wa klabu ya soka ya Simba, Hassan Dalali ambaye ni mpiga solo mahiri aliyestaafu muziki na kujihusisha na soka.

Pia Athumani Momba "Sauti ya Chuma", Max Bushoke, Jerry Nashon "Dudumizi", George Mpupua, Cosmas Chidumule, John Kitime, Aggrey Crispo Ndumbalo na Benno Villa Anthony.

Wengine ni Suleiman Mbwembwe, Shaaban Yohana "Wanted", Hassan Shaw, Eddy Sheggy, Adam Bakari"Sauti ya Zege", Mohammed Gotagota, Mohammed Shaweji, Rashid Pembe, Kida Waziri na maarufu wengi sana ambao kwa bahati mbaya sana wamesahaulika katika orodha hii. Miongoni mwa wanamuziki hao wamo waliotangulia mbele ya haki.

Kwa upande mwingine, kufikia kilele chake cha mafanikio, bendi hii, pamoja na nyimbo zilizokwishatajwa, imetoa nyimbo maarufu kwa mitindo ya Kokakoka, Heka heka, Takatuka, Pambamoto na Air Pambamoto kama "Hekaheka Anapata", "Ngoma", "Jirekebishe Bibi"," Chiku (saizi yangu)", "Matata"," Jiko limenuna", "Maisha ya Amba" "Zenaba", "Ibrahim Nashangaa", "Zena", "Penzi Halina Umaarufu", "Mzee Tupatupa (anayependa uvulana na kukataa shikamoo kwa ajili ya kufukuzia wasichana Wadogo) "Tambiko la Pambamoto", "Mary Maria", "Ilikuwa Lifti Tu"," Shemeji wa Darisalama", na "Mundinde".

Nyingine maarufu ni"Ogopa Tapeli", "Wivu", "Penzi Haligawanyiki" namba moja na namba mbili yake ya shingo feni na macho balbu, "Mama wa Kambo Ni Mama", "Azza","Mwisho wa Mwezi", "Wifi Zangu Mnaninyanyasa", "Heshima ya Mtu", " The Top Queen Of Morocco Road", "Mama Chichi", "Shoga","Mfitini", "VIP" na nyingi nyinginezo zilizoifanya bendi hii iwe kubwa na maarufu mno.

Ni ukubwa wa muziki wake ndiyo uliifanya bendi hii ikawa na wapenzi wengi ndani na nje ya nchi. Aidha, ni changamoto ya muziki wake wa Kitanzania ndiyo iliyozilazimisha bendi za kikongo za wakati wake kama Marquiz Original, OSS, Orchestre Makassy na Kyauri Voice kupiga miondoko ya Kitanzania ili zinyang'anyane mashabiki na bendi hiyo na DDC Mlimani Park, Wana Msondo Ngoma, UDA Jazz na nyinginezo.

Endapo bendi za kikongo zingepiga miondoko ya kikongo wakati huo, zisingepata mashabiki wa kutosha kwani mashabiki wa Tanzania wa wakati huo walikuwa wamechizika na miondoko ya hapa hapa kutokana na umaarufu wa wakati huo wa bendi za hapa.

Mada hii ya wanamuziki wa Kikongo wa wakati huo kupiga miondoko ya kibongo na wa sasa kupiga ya kikongo itajadiliwa kikamilifu siku zijazo kwenye safu hii tukijaaliwa uhai.

Naamini kifo cha Vijana Jazz kimeandaliwa kutokana na mtazamo wa kinyakati (timing) ya hali hiyo. Bendi hii ilianza kudorora baada ya Umoja wa Vijana wa CCM, mmiliki wa bendi hiyo, kukumbwa na dhoruba kali kufuatia mchakato wa uteuzi wa mgombea urais kutoka CCM kwa uchaguzi wa mwaka 1995.

Umoja huo ulijihusisha sana na mchakato huo kwa kujibainisha wazi wazi kuwa kwenye ushabiki wa baadhi ya wagombea. Kwa bahati mbaya kwao, aliyeshinda hakuwa mmojawapo wa wagombea wa chaguo lao! Baada ya uchaguzi tu wa mwaka huo, umoja huo ukawa katika mtikisiko mkubwa ulioikumba pia bendi yake!

Wakati bendi hiyo ikianza kuchechemea, ilitunga wimbo mzuri sana wa "Kisa cha Simu ya Mkononi" ambao, akiwa Rais, Benjamin Mkapa aliueleza kwenye Mkutano wa hadhara katika sherehe moja ya siku ya wanawake duniani kwamba alikuwa haupendi kwani unawadhalilisha wanawake.

Kilichofuata ni kwa uongozi wa bendi hiyo kueleza kuwa wasingeacha kuutumia wimbo huo hadi wapate amri rasmi ya kuuzuia. Kauli hiyo ilionekana kama kumdharau Rais! Baada ya hapo ndipo bendi hii ilipoanza kuwa hoi bin taaban ikitoa nyimbo chache chache nzuri kama "Mabaamedi."

Ni busara bendi hii isiuawe kwa sababu yoyote ile.Wadau ndani na nje ya Umoja wa Vijana wa CCM wajipange kuiinua tena bendi hii. Kama wanamuziki wake waliikosea CCM au serikali, waonywe na wasamehewe.

Tena, kutokana na tabia ya wanamuziki wetu kuhamahama bendi, inawezekana walioikosea CCM na serikali,kama kweli lipo kosa lililotendwa na wanamuziki wa bendi hiyo, leo hawapo katika bendi hiyo.

Katika kuiinua tena bendi hiyo, wadau wanaweza kuandaa mikakati mingi lakini naomba nishauri mkakati mmoja. Mkakati huo ni kurudisha mipigo asilia ya Pambamoto.

Hilo litafanikiwa kwa kuwarudisha kundini magwiji wa zamani wa bendi hiyo kama Komandoo Hamza Kalala, Benno Villa na wengine walio bado katika shughuli ya muziki. Vyovyote iwavyo, Vijana Jazz isife.Ikifa nani atanufaika?



0713 297085
Barua pepe: ibramka2002@yahoo.com

 
Hapo kwenye picha nafikiri walikuwa ndio kwanza wanaanza, maana namuona Hamis Uvuruge, Jerry Nashon " Sauti Ya Dudumizi", Hamisi Kumbakisa, Mwanyiro "Internent", Bushoke, Cosmas Chidumule, King Enock, na Abeli Baltazari waliokuwa ndio kwanza wametoka Dar International "Super Bomboka" ya Mkulu Marijani Rajabu "Mwana Manyema". Siwaoni Mkulu Gurumo na Hassan "Stereo" Bitchuka, ambao walijiunga baadaye toka Msondo Ngoma, wazee wa Amana Ilala, na Sauti Ya Zege Shabaan Dede kutoka Bima Lee.

Sikinde ni moja ya bendi zilizoshiriki sana kwenye kuubadilisha muziki wetu wa bongo na kuwa wa kisasa sana, hasa kutokana na safari zao za mara kwa mara nje ya nchi ambako walikuwa wakirekodi sana miziki yao, leo hata maduka makubwa ya muziki huko majuu utazikuta CD zao, siku hizi wapo bado lakini sio kama enzi zile,

pia mashindano yao makubwa na bendi ya Msondo Ngoma, yamewapunguza sana nguvu kwa sababu Msondo siku zote ina washabiki wengi sana wa asili na wapigaji makini sana, yaani kina Mabere, Lusungu, Mkulu Zahoro Bangwe mtoto wa nyumban, na mtoto Jumbe, George Bush Mnyali na mzee masharubu Ali Rashid, ni nguzo nzito sana za bendi hiyo, lakini kifo cha hivi karibuni cha Mkulu TX Moshi William, ambaye originally alianzia bendi ya Police Jazz, kimeipunguza sana nguvu bendi hii, ingawa majuzi imefanikiwa kumpata mtoto wa TX Moshi William (RIP) ambaye naye yuko kwenye safu ya uimbaji, lakini bado wanapwaya kidogo! Lakini ninazimia nao sana maana huko ndio unakuta mtu anacheza na kivuli chake usiku kucha mpaka muziki uishe!

ahsante Mkuu Mchongoma na hizi picha, maana ni kumbu kumbu kubwa sana ya tulikotoka!

Mukulu,

Shabaan Dede alihamia Sikinde akitokea Juwata Msondo ngoma ambapo hadithi ni kuwa alinyang'anywa unifomu wakiwa wanapiga mziki.

Alipohamia Sikinde, kibao chake cha kwanza kilikuwa Talaka Rejea akisimulia kisa cha kukimbia msondo. Mwishoni mwa wimbo, Bichuka anaimba majina ya wana sikinde waliotoka Msondo na kuunda sikinde, Abel, Mulenga,Mwanyiro, Gurumo, Bitchuka, Mwarami na wengine.

Msondo chini ya Mabela, Mnenge Ramadhani, Lusungu wakajibu Talaka Rejea na ule wimbo wa "umekubali kuuza nyumba na kununua kiwanja-Radhi ya Wazazi imekupata" kuhusu Dede kuuza kiwanja na kuamia kwa wakwe zake.

Stori moja niliyowahisikia ni ya Gurumo akiwa Sikinde, walikuwa DDC Magomeni, katikati ya wimbo, washabiki wa Msondo walikuwa wameingia wakamtupia "Molotov" la mavi yakiwa ndani ya pakti ya maziwa!

Ushindani kati ya Msondo na Sikinde ulikuwa ni mkubwa sawa na ule wa Kamanyola na Masantula ngoma ya mpwita!
 
Hii aliisema Mtikila wakati anajitahidi kujitafutia "soko" la kisiasa. Sidhani kama ina ukweli wowote.Wazanaki hawana dalili yoyote kuhusiana na makabila yaliyoko Burundi.

WildCard,

Kuna Empire kubwa sana East and Central Africa, inaitwa Bahima kama sikukosea ambayo ni shina ya makabila kadhaa yaliyoko Rwanda, Congo, Burundi, Tanzania, Uganda mpaka Kenya.

Katika ugomvi wa sasa kati ya Museveni na Kagame, chimbuko lake ni hilo la wao wawili kutoka shina moja na ndio maana Museveni anautaka sana ukuu wa EAC!

Sasa kabila la Nyerere Zanaki, inasemekana ni Bahima Empire.
 
WildCard,

Kuna Empire kubwa sana East and Central Africa, inaitwa Bahima kama sikukosea ambayo ni shina ya makabila kadhaa yaliyoko Rwanda, Congo, Burundi, Tanzania, Uganda mpaka Kenya.

Katika ugomvi wa sasa kati ya Museveni na Kagame, chimbuko lake ni hilo la wao wawili kutoka shina moja na ndio maana Museveni anautaka sana ukuu wa EAC!

Sasa kabila la Nyerere Zanaki, inasemekana ni Bahima Empire.

Bahima na Bahinda ni koo zinazozunguka maeneo yote ya Uganda, Rwanda, Burundi, Ukanda wa Ziwa wa Victoria, Tabora na Kigoma kwa Tanzania na sehemu kubwa ya nchi ya Congo.
 
pale mbowe disco,kulikuwa na dj mmoja i think gerald,wanasema alikuwa hajui kusoma,eti yeye akiipapasa sahani ya santuri na vidole vyake,ameshajua nyimbo gani.hii mutu ilikuwa inapanga ngoma hatari. wakuu,eti nini asili ya jina la hospitali ya muhimbili ?

Naam, Gerald alikuwa hajui kusoma. Ukienda kumuomba akuweke wimbo fulani na unamtajia yitle ya wimbo huo anakwambia huo hatuna, lakini dakika chache unausikia 🙂. Inasemekana alikuwa anaweka nyota za debe nzito katika kila album, lakini alikuwa anajua kupanga debe moja baada ya nyingine unaweza kujikuta uko kwenye stage saa nzima unacheza debe tu. Mbowe ilikuwa kiboko. DJ KaliiKalii (RIP) alikuwa ni dj mzuri sana maana yeye alikuwa anayaweza mayai pia hivyo siku akiamua kurap na kuweka debe nzito ilikuwa ni balaa tupu. Kulikuwa na squad pale Mbowe ya kukata na shoka na kulikuwa hakuna disco zuri kama Mbowe na ukienda sehemu nyingine tofauti ilikuwa ni kubwa sana kama usiku na mchana.
 
Mzee Fd ES,
Umesahau akina Ibrahim Kiswabi, Ahmed Amasha, Ibrahim Marekano, Daudi Salum aka Kaburu, Mwalusako, Abdalah Mtemi, Said George n.k.,toka timu ya Kamiseta Tabora, hawa ilikuwa chachu kubwa saana fainali ya Umiseta Iringa, nafikiri ilikuwa 76, Tabora ilipokutana na Dar ambayo ilikuwa na safu uliyoitaja hapo. Wakati huo Tabora ilikuwa ilikuwa inavifaa kwelikwli

Jamaa wengi hawa tulikuwa nao pale Tabora wakati nikiwa mwanafunzi wa TS. Skwadi kubwa la wanakandanda hao walikuwa wanafunzi wa Kazima Sekondari. Hiyo ni kabla ya Mbunge Mheshimiwa Charles Kajege Muguta hajaingia pale; na kwa bahati mbaya Mbunge Muguta hakuvuma sana kama walomtangulia ingawa alikuwa potential sana kwenye kabumbu, na nadhani imechangia sana kumfikisha bungeni. Kaburu (Daud Salum wa Kilosa) aliondoka TS akiwa Form 5.
 
Msimsahau na marehemu Jabari la Muziki. Nyimbo zake nyingi zilikonga nyoyo za Watanzania wengi sana kama huu hapa.

Wazazi wazazi nachoka na maneno yenu ya kila siku nyie.
Naona bure mnasumbuka mnayoyataka sintowatimizia
mnanilazimisha kuolewa, na mimi ningali mdogo
Ni miaka 12 tu mume nitamuweza wapi

Samahani samahani, samahani Baba na mama
sintoweza kuolewa na miaka 12 sasa
Mnanipa mume mapema mapema, masomo je?
fikiria Baba, dunia ya leo kukosa kisomo ni taabu

~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*

Oh! Georgina, siku uliyoondoka, uliniacha nalia na machozi
Umeenda kuishi kmbali nami, Georgina wa mama
Sipati usingizi nikikumbuka tulivyoishi mimi nawe Georgina aaa
Oh Georgina

Umeondoka Georgina, umeniachia masikitiko
Georgina Georgina Oooooo
Lini utarudi, uniondoe wasi wasi
Georgina wa mama

LOL! Zamani kulikuwa na muziki safi sana Tanzania hauna matusi, hauna maneno machafu machafu kama hizi nyimbo siku hizi za akina bongo flava na upupu gani sijui.
 
field marshall,dj kalikali ni marehemu,baadaye akaibuka mdogo wake katika fani ya reggae kwa jina kalikawe naye vilevile ni marehemu.
jamani humu ukumbini inabidi tuseparate the man from the boys.NAULIZA je kuna member yoyote humu kacheza disco sansui lililokuwa seaview.

Nilishakusanya sana pesa nikiwa dogo 1974-76 pale Seaview Hotel!

Msimsahau DJ Mzee wa Mji Eddy Saly!
 
Ngoja niwarudishe kwenye mpira wa miaka ya sabini tena, kwani wakati huo tulikuwa na kandanada la hali ya juu sana haijapata kutokea. Inawezakana baadhi ya picha zimeshawekwa hapa ila nadhani hakuna tatizo kama nitazirudia, kwani wahenga walitufundisha kuwa jambao jema linastahili kurudiwa tena na tena.

Simba
attachment.php

African Sports

attachment.php

Coastal
attachment.php


Cosmo

attachment.php


Sijaelewa jina hili la Cosmo lilikuwa lina maana gani


Mseto ya Morogoro

attachment.php




Pan African

attachment.php


Yanga Wakitokea Ziarani

attachment.php



Golikipa Semainda akifanya vitu vyake

attachment.php

Picha zote zimetoka Idara ya Maelezo.
 

Attachments

  • simba.jpg
    simba.jpg
    28.1 KB · Views: 547
  • cosmo.jpg
    cosmo.jpg
    46.2 KB · Views: 538
  • mseto.jpg
    mseto.jpg
    24.1 KB · Views: 532
  • pan.jpg
    pan.jpg
    26.7 KB · Views: 588
  • yanga.jpg
    yanga.jpg
    43.7 KB · Views: 564
  • semainda.jpg
    semainda.jpg
    43.7 KB · Views: 517
Msimsahau na marehemu Jabari la Muziki. Nyimbo zake nyingi zilikonga nyoyo za Watanzania wengi sana kama huu hapa.

Wazazi wazazi nachoka na maneno yenu ya kila siku nyie.
Naona bure mnasumbuka mnayoyataka sintowatimizia
mnanilazimisha kuolewa, na mimi ningali mdogo
Ni miaka 12 tu mume nitamuweza wapi

Samahani samahani, samahani Baba na mama
sintoweza kuolewa na miaka 12 sasa
Mnanipa mume mapema mapema, masomo je?
fikiria Baba, dunia ya leo kukosa kisomo ni taabu

~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*

Oh! Georgina, siku uliyoondoka, uliniacha nalia na machozi
Umeenda kuishi kmbali nami, Georgina wa mama
Sipati usingizi nikikumbuka tulivyoishi mimi nawe Georgina aaa
Oh Georgina

Umeondoka Georgina, umeniachia masikitiko
Georgina Georgina Oooooo
Lini utarudi, uniondoe wasi wasi
Georgina wa mama

LOL! Zamani kulikuwa na muziki safi sana Tanzania hauna matusi, hauna maneno machafu machafu kama hizi nyimbo siku hizi za akina bongo flava na upupu gani sijui.

Nyimbo karibu zote hizi ninazo; nilinunua kanda zake pale RTD mwaka 2002 nikazi-digitize na kuzifanyia audio editing sana. Ila muda wa kuzisikiliza huwa unakuwa ni wa mkwara sana hasa kulingana na wingi wa nyimbo zenyewe kwa vile nilichukua collection yote ya kuanzia miaka ya sitini. Nyingi huwa nazikumbuka kwa kolasi tu.
 
Burudani na muzik wa Dansi;

View attachment 2321
Mbaraka Mwinshehe Mwaruka, nani kama yeye East Africa...? R.I.P

View attachment 2322
Hemed Maneti, "Chiriku"...R.I.P! Huyu enzi hizo alikuwa anaongoza troop la Wana pambamoto moto kweli kweli!... Maskini Vijana Jazz, TOT wakaja kuwapiku kwenye ulaji wa uhamasishaji! CCM bwana, arrgghh!


View attachment 2323
...wana Sikinde Ngoma ya ukae enzi hizo na Leyland lao, palikuwa 'hapatoshi' hawa jamaa na wana Masantula Ngoma ya Mpwita chini ya Guitar lenye nyuzi dazeni la Ndala Kasheba na King Kikii..

Mchongoma

Wakati wa Masantula, OSS ilikuwa chini ya uongozi wa Kingi Kiki aliyekuwa akitamba na wale akina dada wa kichaga, nadhani mmoja alikuwa akiitwa Frida ingawa sina uhakika. King Kiki aliwatoa jasho sana OMACO (Orchestra Marquiz Company) ya mahasidi wake akina Chinyama Chiyaza hadi wakaamua kumrudisha kundini tena. Wakati huo Ndala Keshaba alikuwa bado ana hanja hanja mtaani tu. Baada ya Huggo Kissima kushindwa kumkeep King Kiki ndipo akamleta Freddie Ndala Keshaba ambaye aliingia na kombora lake la nyuzi dazaniu na kuibua mitindo mbalimbali mmojawapo ukiwa ule wa Chunusi ambao alikuwa akiwajibu Marquiz (ambako alikokuwa King Kiki wakati huo) kuwa kama wao ni Ogelea Piga Mbizi basi yeye ni chunusi na wasithubutu kuchezea majini tena. Nyimbo zake zilikuwa heavy sana kuliko za hao Marquiz. Hebu chukua nafasi usikilize wimbo kama Marashi ya Pemba au Kesi ya Kanga ndipo ujue kuwa Freddie(RIP) kweli alikuwa Supreme
 
Back
Top Bottom