Tukumbuke Zamani: Historia ya Taifa letu katika picha

Tukumbuke Zamani: Historia ya Taifa letu katika picha

jasusi,umenikumbusha hii mutu ray abdul,hivi huyu alikuwa undercover cop au janja yake. i remember alikuwa friends na mtoto mmoja wa nyerere,hivyo ikulu alikuwa anaingia kama kwake,alaafu jamaa could talk,he had more then hundred names

Ray Abdul (rip) was a real city boy. Hata hilo jina alijipachika. Tulikuwa pamoja Agha Khan ( Tambaza) and he got to know Andrew Nyerere. Hakuwa cha undercover au nini. I last saw him in Moshi at Freeman Mbowe's wedding. Hata gharama ya kurudi Dar alikuwa ameishiwa ikabidi tumchangie and that was the last time I saw him. I did not know he had died mpaka nilipoona hapa JF.
 
Namuona hapa Choggy Sly (RIP) akiwa kazini enzi hizo huko Silversands:

Nadhani alikuwa akivinjari zaidi mitaa ya Rungwe Oceanic, siyo Rungwe Beach, au vipi mkuu FMES. Hivi Rungwe Oceanic iliishia wapi?

Mkuu Kichuguu,

Kwa kweli leo umeniacha hoi sana, maana huyu ni mwenyewe kabisa Chogo Salum au "Choggy Sly", na mkuu Son Of Alaska you are right upande wa kulia ni mkulu Ahmed "Shalamar", ambaye mara kwa mara walikuwa wakishindana sana na Mkulu Tass na Nico Scaba Scuba, kwenye mashindano ya Robot na zile ngoma mbili kali sana then yaani "You Can't Hide Your Love" by David Joseph, na ile ngoma niyngine ya "Beee Pop Don't Stop" by Man Parish,

Hapo kwenye picha ninaamini ilikuwa ni kujitayarisha na kuanza kwa mashindano ya Robot na Breakdance, na hapo ni Shalamar akijiandikisha na pembeni ni mmoja wa majaji wa hayo mashidano, mkuu Rungwe Oceanic ilikuwa ya Mzee Mwakitwange, (RIP) habari za hoteli yake baada ya kifo chake sinazo sana, lakini nitazipata by kesho.

kwenye picha ya choggy sly kulia kwake nadhani ni abdul shalamar,bingwa wa kucheza ROBOT,jamani ni ajabu na kweli but how come no one has mentioned ADDY SALLY,i believe he was allready in the game before all them Dejays

Mkuu ni kweli, lakini wengi tulikuwa wadogo wakati akiwa anachipukia, lakini kabla hajafikia kileleni akahamia Lusaka, Zambia, ambako kama nilivyosema huko nyuma niliwahi kumkuta miaka ya mwishoni mwa 70s, akiwa the best DJ in town kwenye ukumbi wa Studio 22, downtown Lusaka, ghorofa ya 22.

Lakini ni kweli kwamba alikuwa ni one of the best DJ nchini.
 
Katambuga

Kuna wakati hivi vilikuwa viatu vya kawaida kabisa kwa Watanzania. siku hiz watu huvaa kwa madoido tu


2440d1221580699-tukumbuke-zamani-historia-ya-taifa-letu-katika-picha-katambuga.jpg

Ilikuwa ukivivaa halafu jua likakuwakia mchana inakuwa ni kasheshe.
 
Ray Abdul (rip) was a real city boy. Hata hilo jina alijipachika. Tulikuwa pamoja Agha Khan ( Tambaza) and he got to know Andrew Nyerere. Hakuwa cha undercover au nini. I last saw him in Moshi at Freeman Mbowe's wedding. Hata gharama ya kurudi Dar alikuwa ameishiwa ikabidi tumchangie and that was the last time I saw him. I did not know he had died mpaka nilipoona hapa JF.

Unajua bongo then usingeweza kujua nani ni nani, Mkulu Ray (RIP) ambaye nilimuona mara ya mwisho kwenye mazishi ya Mkwawi, kule Mvumi, Dodoma hakuwa mjinga kama sometimes alivyokuwa aki-act, halafu kwa mtu mwenye shida kama alivyokuwa aki-act he was too clean, halafu hata siku moja sikusikia akiwa Rumande wala Jela, as opposed na washikaji zake kina Joseph Kuo (RIP),

Mimi undercover wengi nilikuwa ninawashitukia kwenye kubadili "mtimti" kama tulivyokuwa tunaziiita US dollars, wao siku zote walikuwa na US Dollars wanatafuta kuzibadili kwa mwendo wa kuruka, badala ya benki na walikuwa wakitafuta watu waminifu wa kuwabadilishia, Ray Abdu siwezi kukubali wala kukataa kama hakuwa undercover lakini alikuwa strange kidogo, ila a nice guy na very comical.

Mungu Amuweke Pahali Pema Peponi.
 
Ilikuwa ukivivaa halafu jua likakuwakia mchana inakuwa ni kasheshe.

Sio tu kwamba ilikuwa kidogo; vilikuwa na kila aina ya dizaini....Kuna ambavyo vilikuwa vizito na vingine ndo vilikuwa vyepesiiii we wacha tu. Ukiyakata malapa yako mazuri kutoka kenya; basi unatafutiwa sandals hizo; nina imani bado yapo tu pale kuelekea kariakoo shimoni....
 
Nakubaliana na wewe kabisa. 'Nginde' bado ni sehemu ya UwT. Ninapovinjari hapo Dar hupenda kwenda pale DDC Kariakoo (Old Traford) Ukiwa pale unachoweza kuona ni ustaarabu wa hali ya juu uliopo. Huwezi kukutana na mambo ya kutembea na 'mukaka' na kucheza shati likiwa mfuko wa nyuma wa suruali. Hapo utawakuta kina mama wengi ambao wamekuja bila hata mapatna wao. Ikitokea vurugu muziki huzimwa haraka sana na wababe hujitokeza na kutuliza ghasia hizo.

Ni kweli unajua wao walikuwa tofauti sana, kwanza walikuwa na nidhamu ya ajabu, very stable kulinganisha na bendi zingine zote nchini, na walikuwa wanaweza kumchukua mwanamuziki yoyote waliyemtaka, halafu wakiwa Mlimani Park kulikuwa hakuna fujo hata siku moja, na "wakorofi" wengi against serikali walikuwa wakikamatiwa either kule Mlimani au DDC.

Lakini ninaamini kuwa walikuwa the best, ni wao pekee waliokuwa wanaweza kuwapa Marquis a run for their money, kwa sababu enzi zile Kamanyola ilikuwa moto wa kuotea mbali sana, unakumbuka enzi zile wakati wa kuelekea kwenye Maulidi, Mkulu Generali Nguza Viking "Chibwiye" anatokea gazei la Uhuru/Mzalendo amevaa kanzu na baraghashia na Mkulu Kikumbi Mwanza Mpango "King" Kiki? Duh! yaani White House ilikuwa tu ni masanga, yaani kwenye kuagiza bia ilikuwa barmaid anaambiwa apime urefu wa muagizaji wa zile bia, kama masanduku sita afya, kama urefu ni masanduku kumi afya tu

Hazitakuja kurudi tena zile enzi, za section moja ndani ya White House kwa ajili ya Mabahria tu waliorudi Fresh, miwani ya Rayben kwa wingi sana usiku wa manane, huku manguruwe left hand yamepaki nje, Marquiz wanamaliza saa kumi, mnahamia Sikinde uwt hawamalizi mpaka daybee! aaaghhhrrrr! Halafu madenish wapakuaji wa meli wako arround kibao, baada ya mwezi mmoja tu nchi kavu baharia ameishiwa anaanza kuuza kwanza Rayben, mara nguruwe la baharia linakuwa sanya sanya, kiudogo limeuzwa kwa Mpemba limekuwa texi bubu, ooohh mara baharia kaondoka bila kuaga, akija kurudi humuoni tena kwenye mastarehe this time anajenga nyumba, na karudi na machine ya kutengeneza juice na anafuga kuku sasa!

Haki ya Mungu, bongo saafi!
 
fm kuna siku nilienda site jirani pale ..nikaamua nipite nione kama RUNGWE OCEANIC.kama..bado ipo hot...mwaka huu mwanzoni....ukienda utasikitika sana ..hasa baada ya mzee mwakitwange kufariki...siku hizi RUNGWE OCEANIC HAS BEEN REDUCED TO RUINS..just go and seee...utafikiri umefika kaole bagamoyo...nothing..nothing....sijui vijana wake hawana interest na hiyo biashara.....maana pale ni hot cake...wanaweza kupata strategic partner ..!
 
Unajua nitafuatilia kujua what happened maana ninakumbuka Robert alikuwa anaonekana kuwa kichwa sana, na zile siku za mwishoni ni yeye aliyekuwa anai-run ile hotel, si unajua sisi ni wale wakulu ambao siku zote tulikuwa hatupendi kulipa kiingilio getini,

by this weekend nitakuwa na habari kamili maana one of my wife's bro anaoa mtoto mmoja wa Mwakitwange (RIP), nitamuulizia zaidi kilichojiri, maana last time niliskia walikuwa na ishus za mirathi, kama familia ya Kasambala, na Batengas. Maana maneno yako Mkulu PM ni kweli pale ni mahali babu kubwa sana kwa biashara najua hawawezi kukosa muwekezaji, si unajua matajiri wa bongo siku zote wanakuwaga madeni matupu, kama unakumbuka Kanyamala (RIP) na Dodoma, na jinsi mtoto wake alivyoishia kuchekesha baada ya wahindi kuja na kuchukua mali yote wakidai walikuwa wanamdai marehemu!.
 
Mwakjj,
Somethings will never change. Ninaporudi nyumbani siku za kwanza huwa naona shida sana kuoga maji ya baridi. Lakini after a few days naenjoy sana tu. Pia umetambua kuwa nyama iliyopikwa kwenye jiko la mkaa ni tamu kuliko iliyopikiwa kwenye jiko la umeme?
Jasusi,kama vile uko huku nyumbani,nimetoka kupata maakuli ya jioni na baada ya kumuuliza mamaa mbona kitoweo leo safi hivi? unajua kajibuje? `baba naniihi umeme ulikatika nimepikia mkaa` kwi kwi natamani nakesho mama chanja akiandaa maakuli ya jioni ukatike tena nile uhondo kama leo,karibu Jasusi ila kwa masharti, usihamie.
 
Unajua nitafuatilia kujua what happened maana ninakumbuka Robert alikuwa anaonekana kuwa kichwa sana, na zile siku za mwishoni ni yeye aliyekuwa anai-run ile hotel, si unajua sisi ni wale wakulu ambao siku zote tulikuwa hatupendi kulipa kiingilio getini,

by this weekend nitakuwa na habari kamili maana one of my wife's bro anaoa mtoto mmoja wa Mwakitwange (RIP), nitamuulizia zaidi kilichojiri, maana last time niliskia walikuwa na ishus za mirathi, kama familia ya Kasambala, na Batengas. Maana maneno yako Mkulu PM ni kweli pale ni mahalai babu kubwa sana kwa biashara najua hawawezi kukosa muwekezaji, si unajua matajiti wa bongo siku zote wanakuwaga madeni matupu, si unakumbuka Kanyamala (RIP) na Dodoma, na jinsi mtoto wake alivyoishia kuchekesha baada ya wahindi kuja na kuchukua mali yote wakidai walikuwa wanamdai marehemu!.

mkuu hiyo ndio tofauti ya matajiri wa kihindi au kizungu na matajiri wa kiswahili....waswahili utajiri wao akiondoka mao unaisha ..yaani ukioneshwa watoto wa matajiri wa zamani asilimia kubwa leo ni pooor...

ndio maana watu kama rostam anakuwa na jeuri ya kusema kuwa utajiri wake upo accumulated tangu kwa babu yake wa mwaka 1880....yaani business empire with more than 100 years..that is common kwa wenzetu..look at hatim karimjees..et al..wao siku zote wako juu..unlike people like mengi who is slowly sinking....
 
1.
Joseph Batholomeo Mulenga amekwishatangulia kwenye njia ya haki. Mwanamuziki huyu mwenye asili ya Zambia baada ya kutoka Sikinde alikwenda Bima Lee. Kama unakumbuka kule Bima Lee walijulikana kama 'The Top Three' Mulenga (Solo), Gama (Rythm) na Mwanyiro (Bass). Bima Lee waliporomosha vibao kama Tugemaso, Neema (Nimesimama kwenye mnara wa Bismin. Barabara kubwa iendayo bandari ya salama, machozi yanimwagika....) na Makulata. Bima ya wakati huo ilikuwa imekamilika kweli kweli kwani safu ya waimbaji iliongozwa na Dede, Marehemu Jerry Nashon (Dudumizi), Roy Basshekanako (yu hai?) na Marehemu Othman Momba.

Mkuu sawa sawa, nafikri wimbo wa "Makulata" ulikuwa ndio kilele cha Dede Bima Lee, na style yake ya "Magneti Tingisha", halafu unaikumbuka ile ngoma ya Roy kabla kina Dede hawajavamia, yaani "Sheri Sharifa ninakuja Eeh"

2
. Baada ya kutoka Bima Lee, Mulenga alijiunga na Bendi ya MK Group. Kule alikuwa na kina Mbombo wa Mbomboka, Kasongo Mpinda Clayton na Marehemu Kalala Mbwembwe na kina Sid Morris (Barkeys?) Mafumu Bilal Bobenga. Wimbo maarufu pale kama unakumbuka ni 'Kibela Acha Chuki' Sina hakika ila nadhani huko ndiko umauti ulipomkuta. Kalala Mbembwe naye alifia Iringa na kuzikwa huko huko baada ya kuvunjika bendi ya Tancut alianzisha bendi yake (sikumbuki jina) ila moja ya nyimbo zake ni 'Lutandila' Kalala atakumbukwa pia kwa wimbo wake maarufu wa Fanta (Fanta unambie kama ninayo makosa mama... kumbuka tulivyopatana na wewe fanta... umesahau mema niliyokutendea mama .... Fanta wangu...)

1. Mulenga siku hizi yupo wapi?

2. Mbombo wa Mbombo Kamunembu, ninamkumbuka sana enzi za Kiki na Marquis Kamanyola, under Mkulu Chinyama Chiyanzi (RIP) na ile Kombi yao yenye picha ya shamba na machungwa, ninakumbuka kibao chake kimoja cha "Chakula chakula kwa Bombee" aliimba akishirikiana na Mbuya Makonga "Adios" (RIP), Kanku Kelly, Lutulu Kiniki ( ambaye baadye alijiunga na Mangelepaa ya Nairobi), Nkurlu Wabangoi, King Kiki, na Chinyama mwenyewe,

- Baaadaye alitoka na kwenda kuanzisha Safari Sound, akiwa kule alitunga wimbo mmoja maarufu sana uitwao "Marie Josee Imegee" au "Mama tuchunge Watoto" katika mtindo aliounzisha yeye wa "604", lakini kabla hajaurekodi owner wa Safari Resort aliyekuwa mmiliki wa OSS, Hugo Kisima akamkata bogi na kumuajiri Kiki, ambaye aliishia kuurekodi kama wake na kupata sifa sana,

- Sijui na yeye siku hizi yuko wapi?

3. Kassongo Mpinda, huyu naye another gwiji aliyetokea Marquis, unakumbuka jinsi alivyoweza kuliziba pengo la Kiki alipotoka Marquis na kuingia OSS, kabla hajaanzisha bendi yake ya Double O,

- Huyu ndiye aliyeimba "Seya" original na ile "Nataka kucheka sina mbavu" kwa mtindo wa "Ogelea Piga Mbizi", baada ya Tshimanga Assosa, kuingia Marquis akitokea Makassy, Kassongo aliamua kujiunga na MK Group ambako nako aliwika sana na vibao kama "Nishike mkono", "Kibela Acha Wivu" na "Tegemea Unachoshika Mkononi",

- Baaada ya wamiliki wa bendi hii kuachana njia panda, Capt. Komba aliwaanzishia bendi maalum ya wa-Zaire wote waliokuwa wakiwika zamani, kama Ndala Kasheba "Supreme", Kiki, Nguza Viking, Kassongo Mpinda, kwa pamoja walikuwa wakipiga kwenye ukumbi wa Obey Police Mess, na Sinza, niliwaona mara ya mwisho pale kabla Nguza hajafungwa na wanawe,

- Sasa sijui Kassongo yupo wapi, maana yeye na Mzee Mwema Mudjanga au "Mzee Chekenchaa" Waliiamusha sana Marquis baada yua Kiki kutoka na nyimbo kama "Maiga" (mwanamama ambaye akishirikiana na Super Wandema alikuwa mcheza shoo), "Maria Nyerere", nafikiri unaukumbuka wimbo wa "Nabwela Lyiko la Zambia" na "Jeni" zilizoimbwa na mwandada Tabia Mwanjelwa, aliyetokea bendi moja ndogo pale Margott!

Huyu Tabia Mwanjelwa naye sijui yupo wapi wazee wa Mbeya tupeni habari, halafu wazee wa Kariakoo Mkulu Ford wa sokoni Karikaoo aliyeimbwa na Safari Sounds ya kina Gurumo na Bitchuka, yupo wapi siku hizi?
 
Joseph Batholomeo Mulenga amekwishatangulia kwenye njia ya haki. Mwanamuziki huyu mwenye asili ya Zambia baada ya kutoka Sikinde alikwenda Bima Lee. Kama unakumbuka kule Bima Lee walijulikana kama 'The Top Three' Mulenga (Solo), Gama (Rythm) na Mwanyiro (Bass). Bima Lee waliporomosha vibao kama Tugemaso, Neema (Nimesimama kwenye mnara wa Bismin. Barabara kubwa iendayo bandari ya salama, machozi yanimwagika....) na Makulata. Bima ya wakati huo ilikuwa imekamilika kweli kweli kwani safu ya waimbaji iliongozwa na Dede, Marehemu Jerry Nashon (Dudumizi), Roy Basshekanako (yu hai?) na Marehemu Othman Momba.

Baada ya kutoka Bima Lee, Mulenga alijiunga na Bendi ya MK Group. Kule alikuwa na kina Mbombo wa Mbomboka, Kasongo Mpinda Clayton na Marehemu Kalala Mbwembwe na kina Sid Morris (Barkeys?) Mafumu Bilal Bobenga. Wimbo maarufu pale kama unakumbuka ni 'Kibela Acha Chuki' Sina hakika ila nadhani huko ndiko umauti ulipomkuta. Kalala Mbembwe naye alifia Iringa na kuzikwa huko huko baada ya kuvunjika bendi ya Tancut alianzisha bendi yake (sikumbuki jina) ila moja ya nyimbo zake ni 'Lutandila' Kalala atakumbukwa pia kwa wimbo wake maarufu wa Fanta (Fanta unambie kama ninayo makosa mama... kumbuka tulivyopatana na wewe fanta... umesahau mema niliyokutendea mama .... Fanta wangu...)

Tuko pamoja.

Mzee hapo nimekukubali khaaaswa
kunamtu mmoja kama ninakumbuka vizuri jina lakeanaitwa ROY Bashekanako huyu alikuwa wapi?pia kuna bendi moja ambayo sijaiyona hapa baoni inaitwa MULE MUVA au ni mtindo huo
Naile bendi iliyo piga ile wimbo wa milima ya kwetu nibendi gani ile wkuu
ninfikiria ni kida waziri lakini sikumbuki bendi gani
 
Mwakjj,
Somethings will never change. Ninaporudi nyumbani siku za kwanza huwa naona shida sana kuoga maji ya baridi. Lakini after a few days naenjoy sana tu. Pia umetambua kuwa nyama iliyopikwa kwenye jiko la mkaa ni tamu kuliko iliyopikiwa kwenye jiko la umeme?

Mimi mpaka leo kitoweo changu hupikwa kwa kutumia jiko la mkaa. Halafu maji yangu ya kukoga huwa hayachemshwi labda wakati wa winter tu.
 
FMES,

Umemtaja Roy, ongeza Belesa Kakere, Bima walikuwa na sauti murua sana hata kabla ya Dede.

Bima Lee walikuwa ni bendi yenye nguvu. Anzia; Sophi, Penzi la Simanzi (utunzi wa Dede), Penzi la huba (katika mahaba, kama unawako, usijiingize katika huba la mwenzio....)

Mnakumbuka Club Rahaleo Show? Muziki Asilia, na kile kipindi cha kusikia nyimbo mpya za Bendi (forgot the name)?
 
Back
Top Bottom