1.
Joseph Batholomeo Mulenga amekwishatangulia kwenye njia ya haki. Mwanamuziki huyu mwenye asili ya Zambia baada ya kutoka Sikinde alikwenda Bima Lee. Kama unakumbuka kule Bima Lee walijulikana kama 'The Top Three' Mulenga (Solo), Gama (Rythm) na Mwanyiro (Bass). Bima Lee waliporomosha vibao kama Tugemaso, Neema (Nimesimama kwenye mnara wa Bismin. Barabara kubwa iendayo bandari ya salama, machozi yanimwagika....) na Makulata. Bima ya wakati huo ilikuwa imekamilika kweli kweli kwani safu ya waimbaji iliongozwa na Dede, Marehemu Jerry Nashon (Dudumizi), Roy Basshekanako (yu hai?) na Marehemu Othman Momba.
Mkuu sawa sawa, nafikri wimbo wa "Makulata" ulikuwa ndio kilele cha
Dede Bima Lee, na style yake ya "Magneti Tingisha", halafu unaikumbuka ile ngoma ya
Roy kabla kina
Dede hawajavamia, yaani "Sheri Sharifa ninakuja Eeh"
2
. Baada ya kutoka Bima Lee, Mulenga alijiunga na Bendi ya MK Group. Kule alikuwa na kina Mbombo wa Mbomboka, Kasongo Mpinda Clayton na Marehemu Kalala Mbwembwe na kina Sid Morris (Barkeys?) Mafumu Bilal Bobenga. Wimbo maarufu pale kama unakumbuka ni 'Kibela Acha Chuki' Sina hakika ila nadhani huko ndiko umauti ulipomkuta. Kalala Mbembwe naye alifia Iringa na kuzikwa huko huko baada ya kuvunjika bendi ya Tancut alianzisha bendi yake (sikumbuki jina) ila moja ya nyimbo zake ni 'Lutandila' Kalala atakumbukwa pia kwa wimbo wake maarufu wa Fanta (Fanta unambie kama ninayo makosa mama... kumbuka tulivyopatana na wewe fanta... umesahau mema niliyokutendea mama .... Fanta wangu...)
1.
Mulenga siku hizi yupo wapi?
2.
Mbombo wa Mbombo Kamunembu, ninamkumbuka sana enzi za Kiki na Marquis Kamanyola, under Mkulu Chinyama Chiyanzi (RIP) na ile Kombi yao yenye picha ya shamba na machungwa, ninakumbuka kibao chake kimoja cha "Chakula chakula kwa Bombee" aliimba akishirikiana na
Mbuya Makonga "Adios" (RIP), Kanku Kelly,
Lutulu Kiniki ( ambaye baadye alijiunga na Mangelepaa ya Nairobi),
Nkurlu Wabangoi,
King Kiki, na
Chinyama mwenyewe,
- Baaadaye alitoka na kwenda kuanzisha Safari Sound, akiwa kule alitunga wimbo mmoja maarufu sana uitwao "Marie Josee Imegee" au "Mama tuchunge Watoto" katika mtindo aliounzisha yeye wa "604", lakini kabla hajaurekodi owner wa Safari Resort aliyekuwa mmiliki wa OSS, Hugo Kisima akamkata bogi na kumuajiri
Kiki, ambaye aliishia kuurekodi kama wake na kupata sifa sana,
- Sijui na yeye siku hizi yuko wapi?
3.
Kassongo Mpinda, huyu naye another gwiji aliyetokea Marquis, unakumbuka jinsi alivyoweza kuliziba pengo la Kiki alipotoka Marquis na kuingia OSS, kabla hajaanzisha bendi yake ya Double O,
- Huyu ndiye aliyeimba "Seya" original na ile "Nataka kucheka sina mbavu" kwa mtindo wa "Ogelea Piga Mbizi", baada ya
Tshimanga Assosa, kuingia Marquis akitokea Makassy,
Kassongo aliamua kujiunga na MK Group ambako nako aliwika sana na vibao kama "Nishike mkono", "Kibela Acha Wivu" na "Tegemea Unachoshika Mkononi",
- Baaada ya wamiliki wa bendi hii kuachana njia panda, Capt. Komba aliwaanzishia bendi maalum ya wa-Zaire wote waliokuwa wakiwika zamani, kama
Ndala Kasheba "Supreme", Kiki, Nguza Viking, Kassongo Mpinda, kwa pamoja walikuwa wakipiga kwenye ukumbi wa Obey Police Mess, na Sinza, niliwaona mara ya mwisho pale kabla
Nguza hajafungwa na wanawe,
- Sasa sijui Kassongo yupo wapi, maana yeye na
Mzee Mwema Mudjanga au "Mzee Chekenchaa" Waliiamusha sana Marquis baada yua Kiki kutoka na nyimbo kama "Maiga" (mwanamama ambaye akishirikiana na Super Wandema alikuwa mcheza shoo), "Maria Nyerere", nafikiri unaukumbuka wimbo wa "Nabwela Lyiko la Zambia" na "Jeni" zilizoimbwa na mwandada
Tabia Mwanjelwa, aliyetokea bendi moja ndogo pale Margott!
Huyu
Tabia Mwanjelwa naye sijui yupo wapi wazee wa Mbeya tupeni habari, halafu wazee wa Kariakoo
Mkulu Ford wa sokoni Karikaoo aliyeimbwa na Safari Sounds ya kina
Gurumo na
Bitchuka, yupo wapi siku hizi?