Tukumbushane: Adhabu ambayo uliwaahi kusimuliwa au kupewa na Wajeda

Tukumbushane: Adhabu ambayo uliwaahi kusimuliwa au kupewa na Wajeda

Twilumba

Platinum Member
Joined
Dec 5, 2010
Posts
13,780
Reaction score
16,928
WajaJF, Nimekaa katika kumbuka zangu nikakumbuka tukio hili;

Nikiwa mdogo nilikuwa nawendaa sehemu moj ilipo kambi ya JWTZ kuchukua Mabaki ya chakula kwenye kambi hiyo kwa ajili ya mbwa wangu.

Siku moja sijui ndo nilikuta wale maafande ambao ndo wapy wapya walini badilikiaje aisee, wakaniamuru kula yale mabki ya chakula kama adhabu walahi niiliilia mie siku hiyo! wakja na maji lita 4 kuwa nikimaliza kula ninywe na yale maji nimalize jamani niliunywa kidogo, baada ya kuwa nimeshidwa adhabu hizo nikalazimishwa nipigwe bakola, uwii aisee zinaumaa jamaa wanapiga karibu na kiuno zinauma ile mbaya!

Kuanzia siku hiyo yule mbwa nilimgawa sikumhitaji tena!

Kiukweli jamaa wa adhabu unique sana!

TUKUMBUSHANE KWA WALE WALIOWAHI KUTAPA ADHABU ZA HAWA JAMAA KAMA MIMI!
 
Kuna moja nishasikiaga kwamba jamaa aliharibu kwa wanajeshi akapewa adhabu akaambiwa achimbe shimo linalolingana na urefu wake halafu akimaliza atoe taarifa.

Basi jamaa akapewa vifaa akachimba kwa mbwembwe masaa yakakatika akamaliza, akaona akatoe taarifa kwa wakuu waje wakague, jamaa wakatoka kuja kukagua, kufika pale wakamuambia jamaa 'Dah, safi sana kazi nzuri haya fukia..' just imagine kukomaa kote kule alijua labda watalitumia kumbe..
 
Kuna dereva mmoja wa daladala ya kutoka stand wenda mzinga (Morogoro), alivuka eneo ambalo hatakiwi kuvuka yaai kingia eneo la jeshi, basi jamaa wakamwita akashuka wakamwiliza kama analiijua kosa akasema akasema ndiyo na kukiri kosa!

Akalizwa angependelea adhabu gani akajibuu kufyeka, akaonyeshwa sehemu ya kufyeka ilikuwa ndogo kama mita 10, alipouliza fyekeo akapewa mkasi!

Jamaa na sura ngumu wakaamwambia aanze kazi, mdogo mdogo kaanza masaa 6 hata mita 3 hajamaliza!

jamaa aliacha hata hy route ya mzinga-stand
 
hawa wajeda wanaweza kukwambia upige deki barabara.
 
hawa wajeda wanaweza kukwambia upige deki barabara.

Hiyo yupo jamaa alishaambiwa!
alipewa dekio, maji kwenye ndoo na sabuni ya omo, shughuli ilikuwa pevu!
 
Kuna moja nishasikiaga kwamba jamaa aliharibu kwa wanajeshi akapewa adhabu akaambiwa achimbe shimo linalolingana na urefu wake halafu akimaliza atoe taarifa.

Basi jamaa akapewa vifaa akachimba kwa mbwembwe masaa yakakatika akamaliza, akaona akatoe taarifa kwa wakuu waje wakague, jamaa wakatoka kuja kukagua, kufika pale wakamuambia jamaa 'Dah, safi sana kazi nzuri haya fukia..' just imagine kukomaa kote kule alijua labda watalitumia kumbe..

da ..huyo jamaa bad yuk hai kwel..maan adhabu hiy du
..
 
Mi na mshikaji wangu tulikatiza katikati ya eneo la jeshi (shortcut), aliyekuwa zamu alikuwa bro wa mtaani. Alituchenjia kama hajawahi kutuona maishani mwake. Akaturusha kichura umbali kama wa mlimani city na mwenge, kidogo nimeze ulimi wangu aisee. Namchukia mpaka leo japo nishakuwa mbaba.
 
Hahahaaa ndandawamalenja eti umeze ulimi!....
 
Back
Top Bottom