Kuna moja nishasikiaga kwamba jamaa aliharibu kwa wanajeshi akapewa adhabu akaambiwa achimbe shimo linalolingana na urefu wake halafu akimaliza atoe taarifa.
Basi jamaa akapewa vifaa akachimba kwa mbwembwe masaa yakakatika akamaliza, akaona akatoe taarifa kwa wakuu waje wakague, jamaa wakatoka kuja kukagua, kufika pale wakamuambia jamaa 'Dah, safi sana kazi nzuri haya fukia..' just imagine kukomaa kote kule alijua labda watalitumia kumbe..
Mi na mshikaji wangu tulikatiza katikati ya eneo la jeshi (shortcut), aliyekuwa zamu alikuwa bro wa mtaani. Alituchenjia kama hajawahi kutuona maishani mwake. Akaturusha kichura umbali kama wa mlimani city na mwenge, kidogo nimeze ulimi wangu aisee. Namchukia mpaka leo japo nishakuwa mbaba.