Tukumbushane dawa za zamani, naanza na chloroquine

Tukumbushane dawa za zamani, naanza na chloroquine

Chloroquine dawa ya malaria
Dah...hizi dawa kabla hata hujameza (kile kiharufu tu) unapata kichefuchefu! Na baada ya siku mbili unaaza kuwashwa🙁🙁

BTW, nimekumbuka pia zamani dispensary nyingi (hasa vijijini) hawakuwa na kipimo cha malaria (walikuwa hawapimi damu kama sasa). Nakumbuka sanasana walikuwa wanapima joto tu!
 
Aisee siisahau kristapen. Nilipigwa hii sindano baada ya hapo nikaona mgu mmoja mfupi na mwingine mrefu. Nilikiwa chiba kwa muda.
Ha ha ha haaa. Wewe bwana, pole sana. Ila hizi sindano unatakiwa ukichomwa utulie, ukitembea utaona vitu vya ajabu mwilini mwako.
 
Mimi ni dawa yangu mpaka kesho. Maduka mengi ya madawa waliacha kuuza ila unapoenda clinic nje ya nchi unaambiwa aftter 50 years inabidi uwe unameza baby Aspirin kwa ajili ya moyo wako. Wameenda mbali na kusema kuwa inaweza kuzuia cancer. Nimesoma tu ila mimi siyo muganganuzi wa kuganganua.
 
Dawaquin mbadala wa chloroquin ilikuwa ina coating ya blue yenye sukari.
 
CHLORO250MG.jpg
Usinikumbushe zilikuwa zinanisabababishia kichefuchefu, alafu unalazimishwa kumeza
 
Na kuna hii pia inaitwa calamine lotion kwa tetekuwanga...hili jina sijui nani aliligundua
"tetekuwanga"...
 
nakumbuka wimbo kwenye radio ya kenya: Cafenol ni bora kuliko asprini peke yakeeeee, hutuliza maumivu kichwa mafua na fluuuu mengine nimesahau. hahahha
Hahahaha du kumbe wazee wengi,

Hawa jamaa walikuwa mbali kwa kutangaza biashara.
Nakumbuka walikuwa wanazunguka nchi nzima wanauza madawa na sinema ya bure.
Nakumbuka those old days
 
Dah...hizi dawa kabla hata hujameza (kile kiharufu tu) unapata kichefuchefu! Na baada ya siku mbili unaaza kuwashwa🙁🙁

BTW, nimekumbuka pia zamani disspensary nyingi (hasa vijijini) hawakuwa na kipimo cha malaria (walikuwa hawapimi damu kama sasa). Nakumbuka sanasana walikuwa wanapima joto tu!
Yaa unapimwa na themometa, unasubiru kuitwa na dr
jibu linatoka malaria
 
Back
Top Bottom