Tukumbushane dawa za zamani, naanza na chloroquine

Tetracycline, antibiotic ya zamani
 
Salimia liniment, dawa ya kupunguza maumivu ya misuli
 
Mafuta ya samaki...box linapicha ya mtu kabeba samaki mkubwa mgongoni.
 
Hahahaha du kumbe wazee wengi,

Hawa jamaa walikuwa mbali kwa kutangaza biashara.
Nakumbuka walikuwa wanazunguka nchi nzima wanauza madawa na sinema ya bure.
Nakumbuka those old days
Hutuliza haraka zaidi, imeshinda nyingine zote, cafenol ni dawa bam bam cafenol ni dawa namba one cafenol cafenol bam baMMM
 
Hutuliza haraka zaidi, imeshinda nyingine zote, cafenol ni dawa bam bam cafenol ni dawa namba one cafenol cafenol bam baMMM
[emoji2] [emoji2] walahi nimecheka sana kwa hiyo bam bam cafenol cafenol
 
Mafuta ya samaki...box linapicha ya mtu kabeba samaki mkubwa mgongoni.
Siku tukipewa shuleni tunashinda tunavichefu chefu we acha tu. Mwezi ukifika unaona hilo gari la sijui wapi ST linakuja na waganga wakati huo nipo la pili nilikuwa naombea niwe zamu ya kuja mchana lakini bahati nbaya kila wakija nipo asubuhi. 1966 wakati huo afya ilikuwa kitu cha kwanza na elimu. Bila chakula husomi inabidi ukaguliwe kama umekuja na chakula shule.
 
Umeleta picha halisi ya miaka hiyo.....magari yao yalikuwa na namba za GT..madereva watu wazima na walikuwa na sharubu..
 
Umeleta picha halisi ya miaka hiyo.....magari yao yalikuwa na namba za GT..madereva watu wazima na walikuwa na sharubu..
Kweli nilichanganya mahesabu. GT hizo zikija wee harufu inanukia kabla hujanywa hayo mafuta. Je chanjo ile ya kwenye mkono mpaka leo ni kitambulisho cha sixtees. Ilikuwa ya TB au Missiles mimi sijui wala tulikuwa hatuulizi ila kitambulisho ninacho kwenye mkono.
 
Wewe ni wa umri wangu tumshukuru Mwenyezimungu bado tuko hai.
Ile alama ninayo pia na ilikuwa ni chanjo ya NDUI..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…