Tukumbushane enzi za Shule ya Msingi na Sekondari

Cytochrome p450

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2019
Posts
5,638
Reaction score
15,044
Habarini wakuu.

Hebu tukumbushane matukio ya zamani yaliyowahi kukutokea kipindi unasoma Shule ya Msingi au Sekondari.

Nakumbuka kipindi niko Primary, nilipata mapambano mengi sana ya ngumi. Na katika mapambano yote, nili-LOOSE! [emoji23][emoji23][emoji23] Kuna jamaa sitomsahau! Alinibonda sana. Halafu tulikuwa class moja na mimi ndio kiranja.
Ni mpigaji kelele maarufu lakini akija mwalimu kuchukua list ya majina ya wapiga kelele, mchizi hayupo![emoji23][emoji23]

Dah! Old is Gold kwa kweli, nikikumbuka nacheka tu![emoji23]
 
Tukio la kuanguka darasani nilipokuwa nimelala mwalimu alipoingia. Watu walicheka sana vicheko vya chinichini.

Nilikuwa nimelala nimeshika meza, nilikuwa nimekalia kiti kibovu cha mbao, halafu nyuma ya kiti nikatundika mfuko wa madaftari(ule wa Bob Marley).

Mwalimu alipoingia ilikuwa mida baada ya uji, mimi nilikuwa nimevuta mboji kutokana na hang over ya uji. Nikasikia "Good afternoon madam" (kalikuwa ka madam ka field) huku nikiwa usingizini, na mimi nikaamka kuunga tela la kusalimia huku nikiwa nimeshika meza. Huku nyuma kumbe kiti kilishaanguka kutokana na uzito wa madaftari kwa sababu kilikuwa kibovu.

Baada ya salamu tukarudi kukaa, mimi nilipitiliza hadi chini nikiwa nimeshikilia meza yangu tena hapo nilikuwa bado nipo usingizini. Baasa ya kufika chini ndio nikaona usingizi umeisha. Niliudhika sana, watu walicheka sana, vicheko vya chini chini kutokana na uwepo wa Madam ili wasiweze kupiga kelele kwenye kipindi.

Wakati huo nilikuwa kidato cha Pili!
 
Tukio la kuanguka darasani nilipokuwa nimelala mwalimu alipoingia. Watu walicheka sana vicheko vya chinichini.

Nilikuwa nimelala nimeshika meza, nilikuwq nimekalia kiti kibovu cha mbao, halafu nyuma ya kiti nikatundika mfuko wa madaftari(ule Bob Marley).

Mwalimu alipoingia ilikuwa mida baada ya uji, mimi nilikuwa nimevuta mboji kutokana na hang over ya uji. Nikasikia "Good afternoon madam" (kalikuwa ka madama ka field) huku nikiwa usingizini, na mimi nikaamka kuunga tela la kusalimia huku nikiwa nimeshika meza. Huku nyuma kumbe kiti kilishaanguka kutokana na uzito wa madaftari kwa sababu kilikuwa kibovu.

Baada ya salamu tukarudi kukaa, mimi nilipitiliza hadi chini nikiwa nimeshikilia meza yangu tena hapo nilikuwa bado nipo usingizini. Baasa ya kufika chini ndio nikaona usingizi umeisha. Niliudhika sana, watu walicheka sana, vicheko vya chini chini kutokana na uwepo wa Madam ili wasiweze kupiga kelele kwenye kipindi.

Wakati huo nilikuwa kidato cha Pili!
😂😂😂😂
 
Dah! Tukio jengine nakumbuka nikiwa Sekondari.
Kwenye mashindano ya UMISETA, sasa tupo kwenye mchujo wa wachezaji ndani ya shule ili kupata wachezaji wa kuwakilisha shule.

Basi bhana, ilikuwa siku ya Ijumaa.. Siku hiyo mademu walijaa kibao uwanjani na kulikuwa na uvumi kipindi hicho kwamba ukiwa unaubonda mpira vizuri, basi lazima upate demu mkali. Na mimi nilikuwa vizuri actually!

Bahati mbaya siku haikuwa yangu sababu nilitaka kucheza kwa lengo la kuwaonyesha watu.. Kila nikipigiwa pasi, mpira haukai mguuni! Mara umenitoka!!

Dah!! Mwisho wa siku jina langu likakatwa.

Noma sana!
 
Kidato cha pili, kuna mjinga mmoja alikua anapenda sana kubully wanafunzi wenzake hasa wa kike, wanafunzi walishtaki kwa waalimu lakini hakuna lililobadilika,

Siku hiyo nafika zangu skonga jana yake sikwenda nakumbuka ilikua jumatano, napokea habari za kutisha, yule boya ametangaza eti jana nilienda kwao tukasex ndio maana sikwenda shule, nilishikwa na hasira za kufa mtu ukizingatia habari hizo zilimfikia my crush binti Radhia, nikaona salalee CV imeshuka kwa kiwango kisichoelezeka,

Nikamfata ilikua break time, nimemkuta anapiga msosi, nikamuuliza hayo niliyosikia ya kweli au si kweli, akacheka kwa dharau kisha akajibu ndio kwani uongo jana hatujasex, sidhani kama alimalizia sentensi, alikula kichwa cha pua, damu hizi hapa, hajakaa sawa alikula ngumi za uso zisizo na idadi akalala chini, nikaondoka, kumbe bhana wapambe wake wakamwambia sio kweli fedheha ile lazima alipe kisasi tena siku hiyo hiyo, basi akanifata na fimbo kubwa, nipo usawa wa darasa langu, alivyofika ile airushe tu nikaidaka, nikamsogeza karibu yangu, akala kichwa kingine ambacho baadae hadi mimi nilivimba, nikaichukua ile fimbo nilimchapa kama mtoto, wanafunzi wanashangilia, akaja mwalimu wa nidham akatuachanisha, alichakaa uso umeloa damu,

Kufika ofisini, staff wakamcheka sana eti unapigwaje na mwanamke namna hiyo tulijua una nguvu kumbe maneno tu, baadae akaenda hospital kutibiwa, wakapiga simu wazazi wetu wakaja, me alienda anko yeye alienda baba yake, kesi ikaongelewa mzee wake akaniomba msamaha kwa niaba ya mwanae, kosa la kupigana ni kufukuzwa shule lakini sikufukuzwa nikageuka shujaa kutokana na tabia za yule dogo zilivyowachosha waalimu na wanafunzi,

Alichekwa na wanafunzi sana, baada ya wiki tatu akahama shule, sijamsikia tena since then.
 
Duh![emoji23] Itakuaje ukikutana nae?
 
Mi primary nilikuwa sina nguvu chembamba silaha yangu kubwa ilikuwa kutemea mate watu usoni na kuwamwagia mchanga then mkuku/mbio nyingi mnoo.Pia nilifaulu kwa second selection nikapikiwa pilau .
 
Hahhahaha
 
Kidato cha pili, kuna mjinga mmoja alikua anapenda sana kubully wanafunzi wenzake hasa wa kike, wanafunzi walishtaki kwa waalimu lakini hakuna lililobadilika,

Siku hiyo nafika zangu skonga jana yake sikwenda nakumbuka ilikua jumatano, napokea habari za kutisha, yule boya ametangaza eti jana nilienda kwao tukasex ndio maana sikwenda shule, nilishikwa na hasira za kufa mtu ukizingatia habari hizo zilimfikia my crush binti Radhia, nikaona salalee CV imeshuka kwa kiwango kisichoelezeka,

Nikamfata ilikua break time, nimemkuta anapiga msosi, nikamuuliza hayo niliyosikia ya kweli au si kweli, akacheka kwa dharau kisha akajibu ndio kwani uongo jana hatujasex, sidhani kama alimalizia sentensi, alikula kichwa cha pua, damu hizi hapa, hajakaa sawa alikula ngumi za uso zisizo na idadi akalala chini, nikaondoka, kumbe bhana wapambe wake wakamwambia sio kweli fedheha ile lazima alipe kisasi tena siku hiyo hiyo, basi akanifata na fimbo kubwa, nipo usawa wa darasa langu, alivyofika ile airushe tu nikaidaka, nikamsogeza karibu yangu, akala kichwa kingine ambacho baadae hadi mimi nilivimba, nikaichukua ile fimbo nilimchapa kama mtoto, wanafunzi wanashangilia, akaja mwalimu wa nidham akatuachanisha, alichakaa uso umeloa damu,

Kufika ofisini, staff wakamcheka sana eti unapigwaje na mwanamke namna hiyo tulijua una nguvu kumbe maneno tu, baadae akaenda hospital kutibiwa, wakapiga simu wazazi wetu wakaja, me alienda anko yeye alienda baba yake, kesi ikaongelewa mzee wake akaniomba msamaha kwa niaba ya mwanae, kosa la kupigana ni kufukuzwa shule lakini sikufukuzwa nikageuka shujaa kutokana na tabia za yule dogo zilivyowachosha waalimu na wanafunzi,

Alichekwa na wanafunzi sana, baada ya wiki tatu akahama shule, sijamsikia tena since then.
Hebu nitumie namba yako kule PM

nina_mazungumzo na wewe.
 
Back
Top Bottom