Tukumbushane kauli mbalimbali za Wanamichezo

ALIPATA KUNENA HAYA...

Nikimuangalia Vinicious Jr anavyo cheza Mpira nakumbuka kipindi changu nacheza huku nikiwa nimelewa...

Kauli hio ameisema Mtume na Nabii wa mwisho wa Soka Ronaldo de Assis Moreirra al maarufu kama Ronaldinho Gaucho alipoulizwa juu ya uwezo wa Kinda wa Real Madrid Vinicious Jr.

 
ALIPATA KUNENA HAYA...

Huu upuuzi ndio unapelekea Dunia iamini kuwa tuzo ya mwisho ya mwanasoka bora wa Dunia ilikuwa ni ile ya Ricardo Kaka pindi alipoiongoza klabu ya AC Milan kutwaa mataji makubwa matatu ya Dunia huku akionesha kiwango cha hali ya juu ambacho hata wapinzani walisadiki.

Kauli hio ilitolewa na mchambuzi wa Duru za Michezo Duniani ambae pia ni msemaji wa AC Milan Afrika Mashariki mwamba Gang Chomba...
 
Kama mpira unadunda basi udunde baharini - by Gang Chomba.

Hili lilikuwa game tafu kati ya AC Milan sikumbuki na timu gani kwenye UEFA Championship, na kweli AC Milan waliibuka kidedea.
 
Kama mpira unadunda basi udunde baharini - by Gang Chomba.

Hili lilikuwa game tafu kati ya AC Milan sikumbuki na timu gani kwenye UEFA Championship, na kweli AC Milan waliibuka kidedea.
😂🤣😂🤣 dhidi ya Manchester United katika Dimba la Sansiro ambapo United walichutama na kupigwa 3-0
 
kama mpira ungekuwa na Mdomo basi kila dakika ungeomba upelekwe kwa Ronaldinho Gaucho ili akauchezee na wenyewe ufurahi...

Silvio Berlusconi mmiliki wa AC Milan
Nimesoma na kufurahi sana jinsi alivyomtendea haki nabii wa soka.Nitaitunza kwa ajili ya vizazi na vizazi vije viisome
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…