Tukumbushane kauli mbalimbali za Wanamichezo

Tukumbushane kauli mbalimbali za Wanamichezo

"Asipokuwepo mchezaji mmoja ama wawili wanalia, sasa waulize upana wa kikosi chao uko wapi? Wamepanuka wapi? Nyuma? Mbele? Pembeni?"

Masau Bwire mara baada ya timu yake kuifunga Simba Sc bao moja bila majibu
 
Nilipata Mimba wakati wa kujenga jengo la Simba,kama MO anapenda mpira akaanzishe timu yake kama Bakheres. Bi Hindu.
 
ED7FEFDC-BD5F-41E4-97D6-DDFCC9319712.jpeg
 
2C2A73CF-7937-479B-9C00-DD9CE5E79F25.jpeg
ALIPATA KUNENA HAYA...

*Wakae wakijuwa hawachezi na timu kutoka ligi ya wakulima ya Bundesliga...
Wakae wakijuwa wanacheza na timu bora ya Dunia ambayo imekamilika kila idara.*

Kauli hio ilitolewa na kiungo wa zamani wa FC Barcelona kabla ya mchezo wao wa ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Mpaka filimbi ya mwisho ilipopulizwa Bayern ilikuwa imewakung’uta Barcelona jumla ya magoli 8-2.
 
Zlatan: Chelsea can’t sign me, I have more trophies than Chelsea. I should be the one to sign Chelsea....

7343471D-B07E-4F5E-BA6E-4E909561A2AC.jpeg
 
ALIPATA KUNENA HAYA...

Siku moja nilimchezea rafu Ricardo Kaka, na alivyoinuka akanikaba koo.

Kulitokea vurumai pale kisha Wenzetu wakaja kutuamulia na kisha mpira ukaendelea.

Mara baada ya mchezo kumalizika na nikiwa naingia Vyumbani nikamuona Kaka amesimama na Gattuso wananisubiri.
Niliogopa saana, nilihisi Gattuso ameurithi ugomvi ule.

Nilipopita karibu yao Gattuso aliniita, kitu ambacho kilizidi kunipa hofu.
Gattuso akaniambia Kaka anataka kukuomba radhi kwa yote yaliotokea wakati ule pale Uwanjani ila hajui kuongea Kingereza

Nikashusha pumzi kisha nikamwambia yale yalishapita na ni mambo ya uwanjani, so yalishakwisha palepale uwanjani.

Na baada ya hapo Giggs anasema Kaka alimfuata na kumkumbatia na tangu hapo wakawa marafiki wakubwa.

420C93C5-80B9-455D-AAA5-BB7D5DCCF57C.jpeg
 
ALIPATA KUNENA HAYA...

Familia yangu woote ni washabiki wa Westham.
Siku moja bana niliifunga westham goli na kwenda kujimwaga kwa washabiki wao na kuanza kushangilia.

Huku wakiwa wananizomea na kuninenea maneno ya laana, niliinua macho na kukutana uso kwa uso na Baba yangu na Mjomba wangu wakiwa na hasira huku nao wakinishushia matusi ya nguoni...

JOHN TERRY...

D1EFDC43-47BC-428E-BEFF-1078F5E647C4.jpeg
D1EFDC43-47BC-428E-BEFF-1078F5E647C4.jpeg
 
Heshima mbele wakuu...
Katika thread hii tutapata kukumbushana kauli zilizowahi kutolewa na wanamichezo Duniani kote.

Kila mtu kwa kumbukumbu yake anafulsa ya kubandika Quotes iliyowahi kumfurahisha ama kumchukiza katika medani ya Michezo...
Pia ni ruhsa kuelezea kauli hiyo ilitolewa lini ama kwa tukio lipi...


BISMILLAH...
Yule team coach wa Yanga alisema........mashabiki wake ni uneducated one, ....nyan na mi mbwa ya kubwekabweka tu. Hawajui football
 
Back
Top Bottom