Gru
JF-Expert Member
- Nov 14, 2017
- 492
- 1,055
Mimi niliingiza Karanga puani. Ilikuwa hivi, jioni moja mshua karudi na karanga amepumzika huku anakula kwa kurushia mdomoni mdogo mdogo. Mimi nikaona nimuige alikuwa kalala kwenye kochi nami nikafanya vile vile.
Kimasihara punje ya karanga ikaingia puani badala nibane upande mmoja nipenge nikawa naingiza kidole pua ile ile karanga ilipoingia mzee hajui hapo. Nimehangaika weeee nilipoona nimeshindwa ndo kumwambia mzee, napo ikashindikana.
Nakumbuka siku ile bimkubwa alikuwa kapika wali nyama, haukulika. Nikabebwa mpaka hospitali ya jirani wakahangaika pale wee ikashindikana ikabidi wanipeleke Muhimbili usiku huo huo muda umeenda kinyama.
Ilitolewa japo kwa maumivu, wazee walihangaika sana mpaka kesho yake mchana ndo kurudi nyumbani! Utoto tabu sana since then sikupataga tena majanga mengine!!