Tukumbushane michezo hatari ya utotoni iliyotusababishia madhara tukaishia hospitalini

Mimi niliingiza Karanga puani. Ilikuwa hivi, jioni moja mshua karudi na karanga amepumzika huku anakula kwa kurushia mdomoni mdogo mdogo. Mimi nikaona nimuige alikuwa kalala kwenye kochi nami nikafanya vile vile.
Kimasihara punje ya karanga ikaingia puani badala nibane upande mmoja nipenge nikawa naingiza kidole pua ile ile karanga ilipoingia mzee hajui hapo. Nimehangaika weeee nilipoona nimeshindwa ndo kumwambia mzee, napo ikashindikana.
Nakumbuka siku ile bimkubwa alikuwa kapika wali nyama, haukulika. Nikabebwa mpaka hospitali ya jirani wakahangaika pale wee ikashindikana ikabidi wanipeleke Muhimbili usiku huo huo muda umeenda kinyama.
Ilitolewa japo kwa maumivu, wazee walihangaika sana mpaka kesho yake mchana ndo kurudi nyumbani! Utoto tabu sana since then sikupataga tena majanga mengine!!
 
Kula sumu,unga unga wa betri za redio zile(Tiger).tulikuwa tunashindana kabisa
 
[emoji134][emoji134][emoji134]

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Nahisi mimi nilikuwa mtundu kupitiliza hadi wazee wakahisi kuna mila wamezikosea hahaha nimegongwa sana na pikipiki ...enzo hizo njia ya ubungo ni one way...mabasi ya mkoa yanakimbia hatare wazeee wakaona huyu atakufa ngoja tumpeleke kijijini kwa bibi yake dar nikawa nakuja likizo tu tena nafungiwa ndani.ila yule bibi alijua kuninyoshaaa nikanyokeka asante sana nibibiake.nakumbuka tunatoka kule kimara baruti nyumbani tunaenda kule udsm eti kuokota vimbwa vya kizungu tunapita pori kwa pori enzi hizo kule udsm coet na ile njia ya busness kulikuwa kuna bonge la pori ila watoto tunakatisha tu.tumetoka mbaliiii
 
Dah! Kweli ulipitia mengi Sana kipindi unakua,,,ila yote yalitokana na utoto tu I'll pole Sana mkuu.
 
Nimeshavunjika mkono udogoni sababu ya sarakasi zile za kwenye matofali na matairi.
lakini sikomi hata leo nikikaa naruka tu kudadeki mpaka baby wangu Hannah anapiga Yowe ntavunja nyonga na kugegedana tushindwe.
[emoji23][emoji23][emoji23] Hapa umetisha Sana mkuy
 
Mnaijua tobo bao nyinyi???nilicheza na watoto wa mbwa wao wananichukulia wa kishua kumbe wote Wana plan moja ya kunigongesha nilipigwa tobo kilazima na flani kubwa kidogo kilichofuata ....Kyaaa ni kudra tu za MwenyeziMungu lkn tangu sikubl hio hawakuambulia hata kumi dala yangu.

Sent from my itel L5007 using JamiiForums mobile app
 
Nyingine tulienda kuogelea mtoni tukachelewa kurudi na ni mwezi mtukufu inabidi nimuwahi mzee anitume tende za futari so ikabidi tuombe lift kwenye land Rover la majani ya ng'ombe....tumefika sehemu ya kushuka tuko nyuma kwenye bodi dereva kila tukimwita hatusikii wenzangu walikua manyang'au wakaruka nikabaki peke angu ile nimeshikilia mlango ule wa nyuma nami niruke sijui hata ile land Rover ilidunda kwenye nn Kuna stuka watu kibao wamenizunguka yaani nilizimia afu nimepata mchubuko shavuni... Kimbembe naendaje kueleza home kuhusu lile jeraha ? Kwamba tulidandia gari au tuliomba lift?ya kutoka wapi na tulikua tunaenda wapi? Asee jeraha na stick juu japo nilidanganya ila habari ilifika sijui ni Nani alivujisha hii confidential information...

Sent from my itel L5007 using JamiiForums mobile app
 
Home walivuna mahindi.yakaletwa bado hayajamenywa usiku tunatoa maganda tunawasha moto tunaimba Mwenge ooh Mwenge Mbio Mbio, Huku na huku likaniangukia jichoni fasta pale nkapakwa dawa ya mswaki

Mpka leo nna alama nyeusi juu ya jicho
 
Dah pole mkuu ulikuwa na majanga. Vipi kwa Sasa ukubwani hupatagi majanga?
 
Asa hapo kisa Kiko wapi Cha majanga uliyopata
 
KUPIGWA MAKONZI (kwenzi) HADI KUZIMIA


Matukio mengine ni utoto hadi ukikumbuka unajiuliza nini hii nlikuwa nafanya.
Tulikuwa tunacheza mchezo wa kuficha tetere(mbegu) ya ubuyu kwenye moja kati ya mikono๐Ÿ‘Š๐Ÿฟ๐Ÿ‘Š๐Ÿฟ alafu mwenzako anatakiwa apatishie ni mkono gani umeweka akikosea ni bonge la kwenzi linamuhusu.

Dah yule chalii nilimuotea round za mwanzoni hadi kumchana kidogo kichwani ila kibao kilipogeukia kwangu aseee jamaa kuna round alinipiga kwenzi hadi nikapoteza fahamu.Hii kitu ilipelekea damu kuvujia kwa ndani ila nashukuru waliwahi kunipeleka hospital na hakuna aliyeunguza mchongo kwa wazee



Barton popote ulipo ulitaka kunitoa uhai skuile kisa upuuzi asee๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ