matunduizi
JF-Expert Member
- Aug 20, 2018
- 7,968
- 19,368
Mwalimu mama mmoja anamacho makubwa aliitwa Iganas.
Alikuwa Mwalimu wa hesabu darasa la sita.
Alikuwa anafundisha kisha anauliza kuna mtu hajaelewa kinafiki na kwa hofu wote tunasema hapana.
Anatoa swali kupima uelewa, kila anayekosa anararuliwa fimbo sio chini ya Tatu za mgongo.
Nilikuwa nakula bakora kila iitwapo Leo. Nilichokifanya ili kuokoa uhai na ubora wa mgongo wangu nilimtafuta mkali wa darasa kwa kumuhadaa akawa ananipitishia majibu kijasusi bila Mwalimu kujua.
Hapo ndipo nilipata likizo ya viboko. Nilikuwa sijawahi kupata zaidi ya 40% hesabu. Raha ya kutopigwa fimbo ilinifanya nikomae hadi namaliza STD 7 pale shuleni matokeo Yangu ya mwisho ilikuwa ni 98% hata Mkali nikamvuka.
Wakuu woga wa fimbo ulinitoa. Na sijawahi kusoma level yoyote bila hesabu kuwepo maana ninaikupali na ninaipenda maana tumetoka nayo mbali.