Tukumbushane ukoloni uliowahi fanyiwa na wazee wako

Nkemia

Senior Member
Joined
Jul 1, 2016
Posts
153
Reaction score
148
Mimi kwakweli sitasahau ukoloni wa Mzee wa kununua stendi ya Tv na kuwa anaisukuma kuipeleka chumbani mara baada ya kumaliza kuangalia taarfa....ki ukweli ule kwangu nilikuona naona ni ukoloni ile mbaya

Ebu tukumbushane ukoloni wa hawa wazee wetu wa zaman
 
kumwagilia kilamti wa mchungwa ndoo kubwa ya maji, nakumbuka mzee alikua hapendi kunikuta nimekaatu, yani akija akikukuta umechil unapunga yeye anakupangia kazi haijalishi umetoka kufanya nn, so ikiwa nikisikia mzee anarudi inabidi kujipa kazi yyte ikiwezekana unarudia ileuliotoka kuifanya [HASHTAG]#nakupenda[/HASHTAG] dingi
 
Mzee wangu alikuwa na tabia ya kuzima TV kwa remote, halafu anamalizia na ile button ya kwenye TV na kuingia na remote chumbani hivyo TV haiwaki mpaka utumie remote kuiwasha.
Kwa utundu wangu nikabuni mbinu. Nilikuwa naminya ile "button" ya kwenye TV, then na-"press" na ku-"hold" button za kuongeza sauti na kubadilishia channel kwa pamoja na TV inawaka bila kutumia remote.
Nikimaliza kuangalia naweka auto switch off, namalizia na button ya TV halafu huyooo nakwenda zangu.
Ila Kuna siku alirudi kazini, akaigusa TV akakuta ya moto dah kipigo alichonipa sitaki kukikumbuka.
 
Da Mzee wako nae alikuwa nouma had anagusa Tv [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] du alitisha........umenikumbush mbali sana aisee
 
Mzee alikuwa na pikipiki na alikuwa hapendi mtu aiguse 110 yake,... Siku moja akasafiri kwa kushindwa kujizuia nikajikuta nimeitoa na kuondoka nayo kwenda kupiga misele kwa mademu. Duh! Kumbe mzee alikuwa anaweka Alama pale alipopaki na ukisogeza tu atajua. Aliporudi akauliza nani katoa pikipiki, watu kimya... Kikatembea kipigo cha jumla watu wakachoka wakanitaja... Duh! Nakumbuka siku hiyo nililala nje. Amezeeka sasa hivi nikimkumbusha anacheka tu. Pikipiki ipo ila kwa sasa nina kagari.....live long senior.
 
Daah nakumbuka kipindi tukiwa wadogo mzee wetu alikua na tabia ya kutuchapa kila anunuapo bidhaa mpya na kuileta nyumbani.Mfano Nakumbuka siku moja alinunua chupa ya chai kabla hata haijaanza matumizi akatutia bakora huku akitusihi na kutukanya kuwa tukiichezea inaweza kupasuka,Basi ikawa kila akinunua kitu chochote akikileta nyumbani lazima tuchapwe!![emoji22] [emoji22] [emoji22] [emoji22]
 
One day tulikuwacheza Chandimu Nyuma ya Soko la kisutu badala ya kwenda Madrasa jion sasa Baba ubaya karudi kwny misele yake ile kumuona tu kwa kuwa wenzetu wanajua Mzee wetu ni mgomvi sana kwa watoto wake tukalala chini style ya kuzimia ili asitutambue, alipoona tukio hilo akasogea na Baiskel yake atoe Msaada bila ya kujua ni mimi na Mdogo wangu, alipotukuta ni sisi tena ilikuwa ni kujificha style basi alifunga Mashati yetu kwny Baiskel yake kwny kiti cha nyuma akawa anaendesha sisi tuna kimbia mpaka home kikaja kupiga cha walimu wa Mbeya sec
 
Nilianza kusoma gazet nikiwa mdogo sana (vidudu) basi dingi kwa kutaka ujiko akija mgeni tu unaitwa kumsomea gazet n enzi hzo hatuna TV, yan ukisikia hodi tu unajiandaa
Bi mkubwa ugomvi ulikua ni kufungia kuku yan ikifika join mhakikishe kila kuku kaingia ndo muingie ndan, kuna siku karud harusin night kali akaenda kuhesabu kuku akakuta mmoja hayupo: tukaamshwa nyumba nzima kwenda kumtafuta, hatukulala dat day
 
Ilikuwa marufuku kuvaa viatu visivyo na material ya ngozi, hakuna kuendesha pikipiki wala gari kwakuwa vyombo vya moto ni hatari
 
Ha ha ha da hcho kipigo nadhan kilikuwa c mchezo
 
Pole sana huo sasa duuu ni zaid ya ukoloni
 
Ha ha ha ha et kipigo cha mwl wa mbeya
 
Duuu
 
hahahhaa ah uhuuhh jaman hii kali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…