Daby
JF-Expert Member
- Oct 26, 2014
- 33,894
- 76,810
Aseeh, ukiishi mtaani kuna mambo mengi yanatokea saana kimtaa kimtaa maana utakutana na watu wanahasira, wanaokera na wanaoonea watu bila sababu. Mimi kupiga kupigwa yameshanitokea saana.
:Kuanzishiwa vagi:
Nakumbuka kipindi cha Nyuma Morogoro kulikuwa na mechi ya simba na mtimbwa baada ya mpira kuisha kulikuwa na show ya Afande nikaona sio mbaya kusubiri show. Wakati show inaendelea kuna machalii walikuwa mobb ya watu kama 10 na kitu hivi.
Gafla vuupu wakanivamia wote, asee nilikula kichapo balaa hadi leo sijakisahau. Walinipiga kustuka nina buti moja tu. Hadi leo sijajua wale jamaa walinianzishia vagi kisa nini. Kuna nyingine nilianzishiwa pale Arusha lemanyata(pinpoint) na baunsa wa club ila hili mwisho nilishida maana nilikuwa na mobb.
:kuanzisha vagi:
Zamani nilikuwa mtata saana hasa Shuleni. Kuna siku moja tupo na rafiki yangu tunatoka Tangamano tunaingia Nguvumali. Kikawaida wanafunzi kwenye haice siti zikijaa mnatakiwa kusimama ila sisi siku hiyo tukagoma.
Konda akakomaa kwamba tusiposimama tutalipa nauli kamili ila nikamwambia jamaa hapa hanyanyuki mtu wala nin. Wakati wa kushuka bwana nikatoa nauli 50 na jamaa 50 ya mwanafunzi. Konda akasimama mlangoni hakuna kushuka akatuzuia.
Nilimpiga kipepsi huyo down, dereva akashuka akazunguka na alikuwa mtu mzima kashiba balaa. Alimshika mshkaji wangu Tanganyika jerk jamaa akabaki anaeleaelea tu juu [emoji23][emoji23]. Bila kuchelewa nilichukua jiwe nikampa la mgongo akamwachia jamaa kisha hao kona tukapotea. Kesho yake tulifuatwa Na askari wa chumba geni sijui walitufahamje.
Mtaani haya mambo yapo... tujikumbushe kidogo...