Tukumbushane: Ulishawahi kuanzisha vagi au kuanzishiwa vagi Mtaani?

Daby

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2014
Posts
33,894
Reaction score
76,810
Aseeh, ukiishi mtaani kuna mambo mengi yanatokea saana kimtaa kimtaa maana utakutana na watu wanahasira, wanaokera na wanaoonea watu bila sababu. Mimi kupiga kupigwa yameshanitokea saana.

:Kuanzishiwa vagi:
Nakumbuka kipindi cha Nyuma Morogoro kulikuwa na mechi ya simba na mtimbwa baada ya mpira kuisha kulikuwa na show ya Afande nikaona sio mbaya kusubiri show. Wakati show inaendelea kuna machalii walikuwa mobb ya watu kama 10 na kitu hivi.

Gafla vuupu wakanivamia wote, asee nilikula kichapo balaa hadi leo sijakisahau. Walinipiga kustuka nina buti moja tu. Hadi leo sijajua wale jamaa walinianzishia vagi kisa nini. Kuna nyingine nilianzishiwa pale Arusha lemanyata(pinpoint) na baunsa wa club ila hili mwisho nilishida maana nilikuwa na mobb.

:kuanzisha vagi:
Zamani nilikuwa mtata saana hasa Shuleni. Kuna siku moja tupo na rafiki yangu tunatoka Tangamano tunaingia Nguvumali. Kikawaida wanafunzi kwenye haice siti zikijaa mnatakiwa kusimama ila sisi siku hiyo tukagoma.

Konda akakomaa kwamba tusiposimama tutalipa nauli kamili ila nikamwambia jamaa hapa hanyanyuki mtu wala nin. Wakati wa kushuka bwana nikatoa nauli 50 na jamaa 50 ya mwanafunzi. Konda akasimama mlangoni hakuna kushuka akatuzuia.

Nilimpiga kipepsi huyo down, dereva akashuka akazunguka na alikuwa mtu mzima kashiba balaa. Alimshika mshkaji wangu Tanganyika jerk jamaa akabaki anaeleaelea tu juu [emoji23][emoji23]. Bila kuchelewa nilichukua jiwe nikampa la mgongo akamwachia jamaa kisha hao kona tukapotea. Kesho yake tulifuatwa Na askari wa chumba geni sijui walitufahamje.

Mtaani haya mambo yapo... tujikumbushe kidogo...
 
Hahahaha
Umenikumbusha nilipoanzishiwa vagi pale Blue bird hotel Sinza, kisa walihisi niko na mume wake ndani (mwanamke alikuja na shoga zake)
Huku na huku meneja akaja, mlango ukafunguliwa, tupsi likaingia, kuangalia sio mume wao.
Wakaomba radhi, wakasepa.....
Baada ya wiki 2 nikakutana na yule dada MK bar Kinondoni (aliyekuja Sinza kumtafuta mumewe chumbani kwetu) nilimuanzishia vagi, mpaka nikalala Oysterbay maana yule bwana alinimwaga kwa kujua eti ile varangati nilipanga mimi na yule mwanamke ili kumchomoa pesa.
 
[emoji3][emoji3][emoji3]
Sasa mechi si ikaharibika?

Huyo mwanamke boya hajui mmewe hata yupoje.
 
Nilitaka kushangaa kama usingesema utotoni ulikuwa mtata.maana mwandiko wako unaonyesha bado kuna masalia ya utata.
Jirani sina utata tena ulishaisha, sasa hivi hata ukinikataa namwachia Mungu.

Vipi wewe haujawahi kudundwa maana najua kudunda hauwezi?

Vipi
 
Sitosahau siku niliyompiga dogo mmoja ngumi ya kichwa kisha nikashuhudia akidondoka chini akaanza kupaparika,...
Nilikimbia mbio home nikajifungia mlango getto, siku hiyo nilisali kwa dua zote huku taswira ya jela ikinijia, nikawa najifariji kwamba nitapelekwa jela ya watoto manake nilikuwa sijafikisha 18 yrs..
Basi bwana ile niko ndani nachungulia kupitia dirishani ghafla naona watu wanajaa home wakiwa wamembeba yule dogo kisha huku bibi mmoja akawa ananitaja mimi kwamba ameniona kwa macho yake nimempiga yule dogo,
Ila bahati nzuri kabla ya kuanza process za kunitafuta sista wa yule dogo alifika home na kuwaambia ''mdogo wangu ana maradhi ya kuanguka, nahisi yamemunza tena''
niliposikia vile kule ndani nilishusha pumzi nzito sana huku nikimshukuru Mungu manake nilidhani nimeua tayari...
Hii imesababisha mpaka leo, kabla sijathubutu kumgusa mtu(kwa kugombana) huwa nawaza kwanza je, huyu mtu ni mzima? Itakuwaje akinifia mikononi mwangu? Basi hujikuta naepusha shari tu.
 
Hahahaha
Umenikumbusha nilipoanzishiwa vagi pale Blue bird hotel Sinza, kisa walihisi niko na mume wake ndani (mwanamke alikuja na shoga zake)
Huku na huku meneja akaja, mlango ukafunguliwa, tupsi likaingia, kuangalia sio mume wao.
Wakaomba radhi, wakasepa.....
Baada ya wiki 2 nikakutana na yule dada MK bar Kinondoni (aliyekuja Sinza kumtafuta mumewe chumbani kwetu) nilimuanzishia vagi, mpaka nikalala Oysterbay maana yule bwana alinimwaga kwa kujua eti ile varangati nilipanga mimi na yule mwanamke ili kumchomoa pesa.
Shost upo
 
Sitosahau siku niliyompiga dogo mmoja ngumi ya kichwa kisha nikashuhudia akidondoka chini akaanza kupaparika,...
Nilikimbia mbio home nikajifungia mlango getto, siku hiyo nilisali kwa dua zote huku taswira ya jela ikinijia, nikawa najifariji kwamba nitapelekwa jela ya watoto manake nilikuwa sijafikisha 18 yrs..
Basi bwana ile niko ndani nachungulia kupitia dirishani ghafla naona watu wanajaa home wakiwa wamembeba yule dogo kisha huku bibi mmoja akawa ananitaja mimi kwamba ameniona kwa macho yake nimempiga yule dogo,
Ila bahati nzuri kabla ya kuanza process za kunitafuta sista wa yule dogo alifika home na kuwaambia ''mdogo wangu ana maradhi ya kuanguka, nahisi yamemunza tena''
niliposikia vile kule ndani nilishusha pumzi nzito sana huku nikimshukuru Mungu manake nilidhani nimeua tayari...
Hii imesababisha mpaka leo, kabla sijathubutu kumgusa mtu(kwa kugombana) huwa nawaza kwanza je, huyu mtu ni mzima? Itakuwaje akinifia mikononi mwangu? Basi hujikuta naepusha shari tu.

Haha utakuja kupewa kesi za kuua.

Haya mambo ya kuzima wanayo wanawake ndiyo maana nikiona nakasirika kama nagombana na mwanamke naondoka taratibu.

Watu wengine washajifia wanasubiri upepo wa kupita nao tu
 
Jirani sina utata tena ulishaisha, sasa hivi hata ukinikataa namwachia Mungu.

Vipi wewe haujawahi kudundwa maana najua kudunda hauwezi?

Vipi
Jirani yangu we acha tu..mimi nilikuwa mkorofi jmn uwiii sitaki kukumbuka kabisa.
Mengine sitaki kufunguka sana ila kwa ufupi ukiniletea maniaje kukuzingu sion shida kabisaaa..na pia nilikuwa nikipata nguvu zaidi kutoka kwa marafiki zangu ambao wengi sana walikuwa wanaume.

Ila kun siku hii siwezi isahau kabisa.nilivaa koti la binamu yangu wa kike kumbe ndani bhana kuna barua ya mwanaume wake alikuwa anataka kumpa mtu ampelekee kwa bahati mbaya nikachukua lile koti bila kujua chochote.bhana eeee...................

Nimemaliza zangu kucheza mpira wa miguu na wavulana huko narudi kuingia darasani kumbe sasa akati navaa lile koti nikadondosha ile barua bhana akaiokota mdada(sijuiyuko wapi huyu dada maana ninahistoria nae sana) hapo sina hili wala lile nikaingia zangu darasani sasa ngoma wakati wa kurudi nyumbani.......

Mwili wote unanisisimka nikajiambiakuna kitu hakiko sawa.aiseeh!!!ile nakata kona ya shule nishike barabara ya kwenda nyumban kundi la wanafunzi kama miambili hivi wananisindikiza nyumbn na wimbo wao "tumeijua siri ya barua"X 100 hivi.

Aiseeh siwez sahau kabisa hii kitu.
Basi nikafika zangu home mama na baba wakashangaa kafanya nini kwani??yule dada kaitoa barua kaiksbidhi kwa wazazi nikasema uwiiii najiteteaje mimi jmn maana baba angu alikuwa anapiga kipigo cha mbwa mwizi.

Baba alipomaliza kuisoma akawaambia umati ulionisindikiza,"nyie nendeni huyu niachieni""mamaaaa kusikia hivyo nikasema eheee nafwa leo. Maajabu ya Musa nikaambiwa nenda kabadilishe nguo huko na "siku nyingine uwe makini"jamn sikuamini.

Nikaanza kujitetea lkni mama hiyo barua si yangu na siijui..mama akasema ni ya fulani (akamtaja jina huyo binamu yangu)sikuamini nikamwambia mama hebu nione.

Kuisoma mwisho wa barua kuna lile kopa lililotobolewa na mshale chini yake kuna jina la huyo binam yangu.

Hapo ndo ikawa pona yangu jirani
...........................................................................
Hii ilifanyika ili kunikomoa manake nilikuwa sishikiki kwa ukorofi aiseeh.
 
Daaah umenikumbusha nilianzishiwa vagi na jamaa mmoja hivi alinikuta na manzi yake....
Manzi nilikua namjua akanicall anakuja home nikamwambia poa, tuka kaa kama siku 4 hivi kumbe aliharibu kwa jamaa yake akakimbilia kwangu bila kunambia....
Tupo sehemu tunakula, njemba kafika kamdaka, nikahoji vipi bob mbona hivyo si ndio akaanza kuropoka kwa nguvu eti "jamaaani huyu mke wangu kanitoroka kaja kuolewa na huyu dada" hahahaha watu wakamwambia mshikaji hata kama umedata si kihivyo bhana hawa wataoanaje??

Vagi ilikua kubwa sana madreva tax wakaja kunitetea dada yao wanajua sinaga makuu, wakamshushia kichapo heavy na manzi mwenyewe akamkataa basi maumivu juu ya maumivu....

Kuanzisha vagi mara nyingi sana nikiona mnyama anateswa, mtoto anapigwa au mwanamke anaonewa hua siwezi kuvumilia kabisa kabisa. lol

Sent from my Siemens kidole juu using JamiiForum mobile app.
 
[emoji3][emoji3]
Jirani, kwa hiyo ukamharibia binamu yako tongozo lake...

BTW, ungeliendeleza na huyo mkaka maana umati ulishajua unadate naye
 
Tukumbushane mkuu
Nakumbuka miaka imwepita kidogo tulienda na teams yetu kupiga mechi ya kirafiki jeshini ila tulipofika wakasema hawajapata barua yeyote kuwa tunaenda kucheza na wao mechi bali walisemwa wamevamiwa ila kilichotokea ni kurukishwa vichura tu"""hafu ikarushwa shilingi juu kama tukipatia tunacheza mechi ila tukikosa tunakula kipigo hafu hamna mechi kuchezwa.....

Dàaaah nshakua mhenga
 
Daaah umenikumbusha nilianzishiwa vagi na jamaa mmoja hivi alinikuta na manzi yake....
Manzi nilikua namjua akanicall anakuja home nikamwambia poa, tuka kaa kama siku 4 hivi kumbe aliharibu kwa jamaa yake akakimbilia kwangu bila kunambia....
Tupo sehemu tunakula, njemba kafika kamdaka, nikahoji vipi bob mbona hivyo si ndio akaanza kuropoka kwa nguvu eti "jamaaani huyu mke wangu kanitoroka kaja kuolewa na huyu dada" hahahaha watu wakamwambia mshikaji hata kama umedata si kihivyo bhana hawa wataoanaje??

Vagi ilikua kubwa sana madreva tax wakaja kunitetea dada yao wanajua sinaga makuu, wakamshushia kichapo heavy na manzi mwenyewe akamkataa basi maumivu juu ya maumivu....

Kuanzisha vagi mara nyingi sana nikiona mnyama anateswa, mtoto anapigwa au mwanamke anaonewa hua siwezi kuvumilia kabisa kabisa. lol

Sent from my Siemens kidole juu using JamiiForum mobile app.
Shule kuna jamaa alikuwa inasadikika anawatigo watu usiku wakilala. Sasa fununu zilizagaa kwa kila mtu ila wa kuthibitisha hakwepo.

Siku moja jamaa akajichanganya akamtigo dogo wa form one dogo akasikia wakati jamaa anamalizia. Dogo alipiga kelele raia wakajaa wakaanza kumpiga jamaa. Daah jamaa alichezea balaa nusu afe. Toka siku hiyo kumgusa mtu kwenye umati siwezi
 
Nakumbuka miaka imwepita kidogo tulienda na teams yetu kupiga mechi ya kirafiki jeshini ila tulipofika wakasema hawajapata barua yeyote kuwa tunaenda kucheza na wao mechi bali walisemwa wamevamiwa ila kilichotokea ni kurukishwa vichura tu"""hafu ikarushwa shilingi juu kama tukipatia tunacheza mechi ila tukikosa tunakula kipigo hafu hamna mechi kuchezwa.....

Dàaaah nshakua mhenga
[emoji3][emoji3] hao watu hawafai mkuu.
Kwa wale wanaojua racing za motor cycle kuna siku jamaa zangu fulani walitutoroka wa kaenda hadi TMA na 250. Sasa wakajichanganya wakaingilia mule ndani kwa njia za panya.

Wakakamatwa pikipiki zikatolewa upepo halafu kila mmoja akaambiwa abebe yake walibaki kuzivuta tu. Toka saa 7 mchana wakaja kuachiwa saa 4 usiku
6c975da3d6860490640c88c71cf486bb.jpg
 
Mechi ilikufa, pesa sikupewa na kuachwa nikaachwa.
Ndio maaana nilitambaa nae tu pale MK.

Mwanamke hajui hata nyendo za mmewe...huyo boya tu.
[emoji3][emoji3] pole aseeeh
 
Back
Top Bottom