Tukumbushane: Ulishawahi kuanzisha vagi au kuanzishiwa vagi Mtaani?

Mimi nakumbuka wakati bado chalii wa darasa la 6A sisahau hiyo siku tumetoka kufanya mitihani ya mwisho mwaka,

Tukamaliza vizuri wakati tunapishana pishana baada ya kumaliza mitihani bahati mbaya Mimi naingia darasani Kile kidemu kikawa kinatoka nikakitegeshea mguu kikajikwaa kikaanguka sketi ikapanda kufunika uso.
Bahati mbaya chupi imetoboka wanafunzi walivyoona tundu la chupi kelele shangwe kibao kama unavyojuwa wanafunzi tulivyokuwaga,
Nikashangaa gafla napigwa makofi na videmu kama kumi ivi akiwemo na yule chupi iliyotoboka nilikula makofi mchanganyiko alafu yanauma kinoma

Nimejitahidi kufurukuta huku na kule nikabahatisha kukunja ngumi nikaitupa kama kurusha jiwe gizani bahati mbaya nikampata kidemu kimoja ngumi ya ziwa nikaona wametulia kama sekunde tatu ivi naona kile kidemu kama kinalegea , kuangalia kwa mbali naona mwalimu anakuja na viranja wawili kurudisha macho kwa kile kidemu naona kimelala chini.
Nilipata wazo na kutoka mbiyo naskia sauti ya mwalimu kwa mbali mkamateni,
Hiyo mbiyo niliyo toka nayo hapo na kundi la wanafunzi waliokuwa wananikimbiza nikaona hapa naenda kusimamia nyumbani.
Kutokana hapakuwa mbali sana kama mita 400 iv nilipofika nyumbani nikaingia chumbani wanafunzi wamefika nawasikia kwa getini Odi,Odi,Odi dingi akatoka naskia wanamsalimia mzee shimoo baba mimi apa,
Walipoulizwa kuna nini naskia tumetumwa tumkamate tumrudishe shule walikuwa wanapigana, walipoulizwa kwani yuko wapi wakasema kaingia ndani, mzee akaanza kuita kaita kama mara tatu nikatoka, ananiuliza mbona umevimba na maalama ya makofi nikamwambia ukweli
Kwa mana mzee wangu alikuwa mkali kinoma. Akaniambia nikupeleke shule mimi mwenyewe au unaenda mwenyewe, nikamwambia naenda mwenyewe, nikatoka tena pale nimekabiziwa kwa wanafunzi twende nao, wale wanafunzi wananipeleka mperampera alafu kulikuwa na Majeba mawili yanataka kuninyanyuwa juu juu yaende kupata sifa .., Itaendelea

kwa mana kilichotokea kingine baada kuanza kunyanyuliwa mara unazomewa kitafata kwa sasa natakiwa nilale kesho kazini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mechi Za Shule Tumeenda Vijijini Huko. Tukaanza Kutawala Wenyej Mara Jamaa Mmoja Brazamen Akawatukana Wenyeji,Wakamaindi Wakatoboa Matairi,***** Mpira Halftime Tu Kishanuka,Mwalimu Wa Michezo Akasema Jaman Tukutane Shule Kila Mtu Njia Anaijua. Niko Na Wanangu Tunakimbia Nyuma Wanakuja Jamaa Wa2 Alafu Wanatuambia Tukiwakamata Tunawafir*. Yani Sie Tuko Wa3 Wao Wa2 Alafu Wanatutishia Kutudhalilisha Kiasi Hicho,Nikamwambia Mchizi Hapa Lazma Tutetee Shule Aisee,This Is Too Much. Mbele Tukaona Vipande Ya Kuni/Vigongo/Vikotakota Tukaviokota Alafu Tukawageukia Mabwege Mnasemaje. Wao Wanajiamni Wanadhani Wenzao Wanakuja Kumbe Wenzao Wako Mbali. Tuliwatembezea Dozi Wale Majamaa Yani Wanalia Kama Watoto,Wanaomba Msamaha,Piga Sana Za Ugoko,Magotini,Mgongoni, Tunawatukanisha Shule Yao Piga Sana. Tulipoona Nyuma Kuna Wenzao Wanakuja Tukasepa. Juma3 Headmaster Mwalimu Wa Michezo Anasema Kuna Watu Safi Sana,Wamekong'ota Washamba Wa 2 Mpaka Walimu Wao Wamelalamika Na Hawataki Mechi Tena. Basi Kujitaja Kwa Mwalim Huwez Koz Its Risky,Basi Tukabakia Heroes Huku Dormitories...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakumbuka One time nipo kwenye sherehe ya binamu yangu kipaimara it was wayback nimekaa zangu kimya kama nimelazimishwa kukaa pale.. Kuna vijana wa mitaani walikua wanazengea msosi kama unavyojua mambo ya uswazi.. Tangu nimefika asubuhi kuna kabint nilikua nakaona kanazunguka pale Mara katumwe vocha na wageni waalikwa kalikua kapoleee na sio kabishi.. Muda umefika wa kula chakula watoto walikua ni wengi balaa wakapewa portion yao maskini wababe wakala watoto wakakosa.. Utafanyaje sasa Shea yao haikuepo.. Nipo zangu ndani maana Nyumba ilikua na uzio hata cjaanza kula nkakaona kale kabinti kanashangaa tu kwa nje midomo imekauka tumaini la kula limepotea.. Roho ikaniuma.. Japo walikua wengi kwa nje lakini wengi wao walionekana wanatokea familia za jirani.. Na walikua watundu na wabishi mno.. Basi nkaona isiwe tabu nikatoka nje ya geti na kukaita kale kabinti.. Ile nafika tu nkakutana na vivulana flani ivii kuniona tu vikaanza kunitania utani wa kikubwa haswa wezere language... Hua spend mtu ayaseme makalio yangu.. Nkaachana nao na kukachukua kale kabinti mpaka jikoni nikakapa msosi kwenye sahani kila mtu kwenye sherehe ananishangaa tu.. Nkarudi ukumbini nikakaa nako jirani.. Mgao wa vinywaji umepita nkakapa soda kakawa kanakula.. Badae nkaitwa ndani na Uncle eti hajaniona tangu nimefika.. Nikawa nimesepa like 5 min ile narudi nkakuta pale amekaa mgeni mwingine aliechelewa kufika na kale kabinti hakapo.. Kumbe kamefukuzwa na wamama wa pale kakaambiwa kakalie kule nje.. Kufika nje nakuta wale vijana wameshika sahani wanakula na soda wanagawana.. Nikawachukulia poah tu wamemaliza kula kama nguruwe wakatupa sahani wakakimbia na chupa.. Nikamchukua Dogo nikaja nae ndani akiwa analia nikampa msosi mwingine nikamwambia kaa hapo usitoke.. Kakamaliza kula kakarudisha sahani maskini kakashukuru kakaondoka.. Nikakaita na kukapa sh. 1000 then nkaendelea na Mishe zingne pale.. Badae kidogo naskia naitwa nje na mmoja wa vibinti pale... Wee Dada.. Hawa wakaka wamempokonya Lisa hela ulompa.. Nikatoka nje na hasira za ajabu kufika nawakuta wale vijana.. Kuniona wakanichukulia poaah.. Nikakamata wawili mmoja akakimbia nikashusha kerbu za maana na hivi nilikua nimevaa suruali kivumbi kilitoka pale.. Nilishusha mnyigo wa maana mpaka nakuja kuwaachilia kila mmoja alipita njia yake... Sherehe ikasimama ghafla kila aliehadithiwa kile kisa akabaki anacheka na kustaajabu.. Nikatafta bodaboda nikageuza zangu home.. Mpaka Leo cuzoo hua hasau like tukio...
 
Unajua kuna baadhi ya wanaume wanadhani wanawake wote ni maboya.
Mie sipendi dharau....
Yaani mie ukinichokoza jua nikitibiwa na kupona,
lazima nikutafute tuanze A.
Niliwahi pigwa stop Masai club, Waungwana bar na pale Igo Sinza....cheza vizuri, ukinibambia tu, kiboya nina wewe.
Lol, unajua nafatilia posts zako umenifanya nimkumbuke best angu mmoja hivi anaitwa Caren yaan you sound like her.... ana matukio yamemzidi uzito... safi sana mwanamke hapaswi kua boya aiseee.

Sent from my Siemens kidole juu using JamiiForum mobile app.
 
Mimi nakumbuka wakati bado chalii wa darasa la 6A sisahau hiyo siku tumetoka kufanya mitihani ya mwisho mwaka,

Tukamaliza vizuri wakati tunapishana pishana baada ya kumaliza mitihani bahati mbaya Mimi naingia darasani Kile kidemu kikawa kinatoka nikakitegeshea mguu kikajikwaa kikaanguka sketi ikapanda kufunika uso.
Bahati mbaya chupi imetoboka wanafunzi walivyoona tundu la chupi kelele shangwe kibao kama unavyojuwa wanafunzi tulivyokuwaga,
Nikashangaa gafla napigwa makofi na videmu kama kumi ivi akiwemo na yule chupi iliyotoboka nilikula makofi mchanganyiko alafu yanauma kinoma

Nimejitahidi kufurukuta huku na kule nikabahatisha kukunja ngumi nikaitupa kama kurusha jiwe gizani bahati mbaya nikampata kidemu kimoja ngumi ya ziwa nikaona wametulia kama sekunde tatu ivi naona kile kidemu kama kinalegea , kuangalia kwa mbali naona mwalimu anakuja na viranja wawili kurudisha macho kwa kile kidemu naona kimelala chini.
Nilipata wazo na kutoka mbiyo naskia sauti ya mwalimu kwa mbali mkamateni,
Hiyo mbiyo niliyo toka nayo hapo na kundi la wanafunzi waliokuwa wananikimbiza nikaona hapa naenda kusimamia nyumbani.
Kutokana hapakuwa mbali sana kama mita 400 iv nilipofika nyumbani nikaingia chumbani wanafunzi wamefika nawasikia kwa getini Odi,Odi,Odi dingi akatoka naskia wanamsalimia mzee shimoo baba mimi apa,
Walipoulizwa kuna nini naskia tumetumwa tumkamate tumrudishe shule walikuwa wanapigana, walipoulizwa kwani yuko wapi wakasema kaingia ndani, mzee akaanza kuita kaita kama mara tatu nikatoka, ananiuliza mbona umevimba na maalama ya makofi nikamwambia ukweli
Kwa mana mzee wangu alikuwa mkali kinoma. Akaniambia nikupeleke shule mimi mwenyewe au unaenda mwenyewe, nikamwambia naenda mwenyewe, nikatoka tena pale nimekabiziwa kwa wanafunzi twende nao, wale wanafunzi wananipeleka mperampera alafu kulikuwa na Majeba mawili yanataka kuninyanyuwa juu juu yaende kupata sifa .., Itaendelea

kwa mana kilichotokea kingine baada kuanza kunyanyuliwa mara unazomewa kitafata kwa sasa natakiwa nilale kesho kazini.

Sent using Jamii Forums mobile app
Lol, nasubiri muendelezo

Sent from my Siemens kidole juu using JamiiForum mobile app.
 
Mechi Za Shule Tumeenda Vijijini Huko. Tukaanza Kutawala Wenyej Mara Jamaa Mmoja Brazamen Akawatukana Wenyeji,Wakamaindi Wakatoboa Matairi,***** Mpira Halftime Tu Kishanuka,Mwalimu Wa Michezo Akasema Jaman Tukutane Shule Kila Mtu Njia Anaijua. Niko Na Wanangu Tunakimbia Nyuma Wanakuja Jamaa Wa2 Alafu Wanatuambia Tukiwakamata Tunawafir*. Yani Sie Tuko Wa3 Wao Wa2 Alafu Wanatutishia Kutudhalilisha Kiasi Hicho,Nikamwambia Mchizi Hapa Lazma Tutetee Shule Aisee,This Is Too Much. Mbele Tukaona Vipande Ya Kuni/Vigongo/Vikotakota Tukaviokota Alafu Tukawageukia Mabwege Mnasemaje. Wao Wanajiamni Wanadhani Wenzao Wanakuja Kumbe Wenzao Wako Mbali. Tuliwatembezea Dozi Wale Majamaa Yani Wanalia Kama Watoto,Wanaomba Msamaha,Piga Sana Za Ugoko,Magotini,Mgongoni, Tunawatukanisha Shule Yao Piga Sana. Tulipoona Nyuma Kuna Wenzao Wanakuja Tukasepa. Juma3 Headmaster Mwalimu Wa Michezo Anasema Kuna Watu Safi Sana,Wamekong'ota Washamba Wa 2 Mpaka Walimu Wao Wamelalamika Na Hawataki Mechi Tena. Basi Kujitaja Kwa Mwalim Huwez Koz Its Risky,Basi Tukabakia Heroes Huku Dormitories...

Sent using Jamii Forums mobile app
iaseee nimecheka sana, sio kwa kunivunja huku mbavu zangu, lol eti chezea sana za ugoko hahahaha

Sent from my Siemens kidole juu using JamiiForum mobile app.
 
Ah hayo ndo yalikuwa mambo yangu.

Nilikuwa natembea na mkia wa taa muda wote.

Kila mimi na washikaji tukienda kwenye mechi lazima nilianzishe.

Ila nilikoma pale siku moja Wamakonde waliokuwa wanakaa kama walinzi kwenye nyumba ya jirani waliponilia timing wakanipiga jiwe juu ya hicho baada ya kumvuruga kaka yao.

Kama lile jiwe lingeshuka chini kidogo ya nyusi basi leo hii ningekuwa na chongo.

Ila niliipata maana uchokozi wangu wote ulinitokea puani.
 
Lol, unajua nafatilia posts zako umenifanya nimkumbuke best angu mmoja hivi anaitwa Caren yaan you sound like her.... ana matukio yamemzidi uzito... safi sana mwanamke hapaswi kua boya aiseee.

Sent from my Siemens kidole juu using JamiiForum mobile app.
Asante mwaya
Yah, ile dhana ya mwanamke ni kiumbe dhaifu haiswiiii siku hizi.
Wanaume wanatumia huo msemo kutuonea sana.

Yaani mtiti ambao sitakuja kuusahau ni ule wa pale Masai club.
Jikaka moja la kipemba sijui chotara lile likanitokea, mie nikamchomolea, alichofanya akaenda kununua bia kaunta, akasogea karibu yangu afu akanimiminia ile bia ndani ya maziwa, nilivaa kiblouse cha nyavunyavu kina shingo pana.
Weeeee.....nilimsukuma, nikamshika kola ya shati, alikuwa amelewa hivo anaenda tu....nikamburuta kwenye zile ngazi za kutoka nje, nilimbatua....akazima, nikasepa.
Kesho yake nashangaa askari hao home....nikajua msala wa jana Masai.
Tiwa kwenye difenda, Oysterbay.
Siku hiyo nililala maana nilipelekwa jioni.
Asubuhi yake namuona yule kaka anakuja na baba ake, wanataka niwalipe maana mwanae alipoteza wallet na simu.
Nikaanzisha tena vagi polisi nikasema yeye ndio alioanza.
Askari mmoja mtu mzima akaja, akatusikiliza akasema mwenye kosa ni yule kaka.
Kama katongoza na kakataliwa, hakukuwa na haja ya kumdhalilisha kwa kumwagia bia kwenye maziwa.

Huyooooooo nikainua makalio nikasepa na sikulipa kitu.

Wiki 2 mbele nikaenda Micasa pale Ubungo huku na huku nikakutana na yule kaka,
Akanitongoza tena ila safari hii alikuwa na adabu na hakuwa amelewa.
Mie nikakaa nae, nikanywa nae na kula nae na kucheza nae mziki club mpaka alfajiri.

Akanipa namba, nikaondoka.
Tukaanza kuwasiliana na kujikuta tumeangukia kwenye mahusiano.
Tulidumu kama mwaka na nusu, then alivyoondoka kwao Pemba ndio ikawa mwisho wetu.
Hiyo ndio raha....mwanaume anakuheshimu kutokana na mazingira aliyokupatia, anajua akizingua tu....vagi.
Sio anakukuta wa geti, anajua we boya.

Huyo best wako nimempenda bure....hakuna kuonewa onewa hapa.
 
Ah hayo ndo yalikuwa mambo yangu.

Nilikuwa natembea na mkia wa taa muda wote.

Kila mimi na washikaji tukienda kwenye mechi lazima nilianzishe.

Ila nilikoma pale siku moja Wamakonde waliokuwa wanakaa kama walinzi kwenye nyumba ya jirani waliponilia timing wakanipiga jiwe juu ya hicho baada ya kumvuruga kaka yao.

Kama lile jiwe lingeshuka chini kidogo ya nyusi basi leo hii ningekuwa na chongo.

Ila niliipata maana uchokozi wangu wote ulinitokea puani.
Ebwana eeeh, wamakonde nao wanakua watata ila hao mpk wanarusha jiwe walikua na uoga flani hivi ilifaa wakuweke mtu kati upate kipondo kama ulichompa kaka yao.... lol

Sent from my Siemens kidole juu using JamiiForum mobile app.
 
Ebwana eeeh, wamakonde nao wanakua watata ila hao mpk wanarusha jiwe walikua na uoga flani hivi ilifaa wakuweke mtu kati upate kipondo kama ulichompa kaka yao.... lol

Sent from my Siemens kidole juu using JamiiForum mobile app.

Siyo kwamba walikuwa waoga.

Ni kwamba niliwabonda.

Niliwatandika ngumi za Kisukuma hadi wakaamua kutumia mawe.
 
Asante mwaya
Yah, ile dhana ya mwanamke ni kiumbe dhaifu haiswiiii siku hizi.
Wanaume wanatumia huo msemo kutuonea sana.

Yaani mtiti ambao sitakuja kuusahau ni ule wa pale Masai club.
Jikaka moja la kipemba sijui chotara lile likanitokea, mie nikamchomolea, alichofanya akaenda kununua bia kaunta, akasogea karibu yangu afu akanimiminia ile bia ndani ya maziwa, nilivaa kiblouse cha nyavunyavu kina shingo pana.
Weeeee.....nilimsukuma, nikamshika kola ya shati, alikuwa amelewa hivo anaenda tu....nikamburuta kwenye zile ngazi za kutoka nje, nilimbatua....akazima, nikasepa.
Kesho yake nashangaa askari hao home....nikajua msala wa jana Masai.
Tiwa kwenye difenda, Oysterbay.
Siku hiyo nililala maana nilipelekwa jioni.
Asubuhi yake namuona yule kaka anakuja na baba ake, wanataka niwalipe maana mwanae alipoteza wallet na simu.
Nikaanzisha tena vagi polisi nikasema yeye ndio alioanza.
Askari mmoja mtu mzima akaja, akatusikiliza akasema mwenye kosa ni yule kaka.
Kama katongoza na kakataliwa, hakukuwa na haja ya kumdhalilisha kwa kumwagia bia kwenye maziwa.

Huyooooooo nikainua makalio nikasepa na sikulipa kitu.

Wiki 2 mbele nikaenda Micasa pale Ubungo huku na huku nikakutana na yule kaka,
Akanitongoza tena ila safari hii alikuwa na adabu na hakuwa amelewa.
Mie nikakaa nae, nikanywa nae na kula nae na kucheza nae mziki club mpaka alfajiri.

Akanipa namba, nikaondoka.
Tukaanza kuwasiliana na kujikuta tumeangukia kwenye mahusiano.
Tulidumu kama mwaka na nusu, then alivyoondoka kwao Pemba ndio ikawa mwisho wetu.
Hiyo ndio raha....mwanaume anakuheshimu kutokana na mazingira aliyokupatia, anajua akizingua tu....vagi.
Sio anakukuta wa geti, anajua we boya.

Huyo best wako nimempenda bure....hakuna kuonewa onewa hapa.
Hahahahaha ya huyo kaka mpemba kutoka polisi hadi mapenzi hiyo kiboko aiseee lazima usiisahau....

Nakumbuka ilikua Maisha club enzi zile ipo oysterbay nipo na best angu huyo juu, baadae akashuka kati kucheza mziki mimi nikabaki kule kule juu.... ghafla kaja lilevi flan ivi eti "oyaa best ninunulie bia" lol simple like that nikauchuna akaanza tena "namuona best ako anacheza na manzi angu ili kunizimisha nunua bia bila hivyo naenda kumuharibu" hahahaha

Ghafla namuona Careen huyu hapa anauliza huyu boya anazingua nini kumbe alikua anatuangalia na kuniona nilivyokosa raha... kabla sijasimulia jamaa akala mtama chaliiii duuuh nikaona hii soo anataka kuinuka pigwa buti la mdomo mpk walinzi wanafika jamaa 'mchuzi' umemwagika, kumbe hata hao walinzi wanamjua wakaanza kumpoza na kuomuomba aende nyumbani badala ya kumuangalia yule jamaa hali yake, daah tukasepa zetu na kuhamia kiwanja kingine.

Mara chache sana uende nae sehemu za starehe na umrudi salama bila kesi hahahaha huyu kabisa mnafanana.

Sent from my Siemens kidole juu using JamiiForum mobile app.
 
Siyo kwamba walikuwa waoga.

Ni kwamba niliwabonda.

Niliwatandika ngumi za Kisukuma hadi wakaamua kutumia mawe.
hahahaha kama ngumi za kisukuma lazima wakae... mna ngumi nzito sana nyie, lol

Sent from my Siemens kidole juu using JamiiForum mobile app.
 
Hahahahaha ya huyo kaka mpemba kutoka polisi hadi mapenzi hiyo kiboko aiseee lazima usiisahau....

Nakumbuka ilikua Maisha club enzi zile ipo oysterbay nipo na best angu huyo juu, baadae akashuka kati kucheza mziki mimi nikabaki kule kule juu.... ghafla kaja lilevi flan ivi eti "oyaa best ninunulie bia" lol simple like that nikauchuna akaanza tena "namuona best ako anacheza na manzi angu ili kunizimisha nunua bia bila hivyo naenda kumuharibu" hahahaha

Ghafla namuona Careen huyu hapa anauliza huyu boya anazingua nini kumbe alikua anatuangalia na kuniona nilivyokosa raha... kabla sijasimulia jamaa akala mtama chaliiii duuuh nikaona hii soo anataka kuinuka pigwa buti la mdomo mpk walinzi wanafika jamaa 'mchuzi' umemwagika, kumbe hata hao walinzi wanamjua wakaanza kumpoza na kuomuomba aende nyumbani badala ya kumuangalia yule jamaa hali yake, daah tukasepa zetu na kuhamia kiwanja kingine.

Mara chache sana uende nae sehemu za starehe na umrudi salama bila kesi hahahaha huyu kabisa mnafanana.

Sent from my Siemens kidole juu using JamiiForum mobile app.
Mara nyinhi wanaume wa Club wanatuchukulia poa sisi.
Dawa yao ni kupimana nao ubavu tu.
hamna namna
 
!
!
Kuna mshikaji aliwahi kunitapeli na demu wake aisee mida ya saa moja moja, mitaa ya chuo cha radhi. Daaaah alinianzishia timbwili hilo siwezi kusahau.
 
Haha utakuja kupewa kesi za kuua.

Haya mambo ya kuzima wanayo wanawake ndiyo maana nikiona nakasirika kama nagombana na mwanamke naondoka taratibu.

Watu wengine washajifia wanasubiri upepo wa kupita nao tu
Ahahha naogopa sana kwenda jela,
sio kwasababu ya mateso ya kule ila Nina mambo mengi sana ya kufanya uraiani mzee,
Ndomana hata kumiliki bastola nilikataa manake akili zangu nazijua mwenyewe
 
!
!
Kuna mshikaji aliwahi kunitapeli na demu wake aisee mida ya saa moja moja, mitaa ya chuo cha radhi. Daaaah alinianzishia timbwili hilo siwezi kusahau.
Kakutapeli halafu kakuanzishia timbwili hahahha lol

Sent from my Siemens kidole juu using JamiiForum mobile app.
 
Aaaah umenikumbusha kitambo kidg nakumbuka kipindi Niko skonga o_level nipo 4m4 tulipata tour ya kushiriki michezo na shule iliyo kua mbali kidogo na hapo kwaiyo ikatulazimu tukodi gari kwa sababu ilikua ni mbali sawa na kutoka g.mboto hadi bagamoyo.kiukweli kimichezo shule yetu inajitahidi hata swala la ugomvi tulikua tunalimudu vizuri lkn siku ile tulikwenda wachache kutokana na gari lilikua moja.vag lilianza baada ya refa kufanya upendeleo wa penalt wahuni wakaona jau si wakaingia uwanjani bila kujali uchache wao walimpa vitasa refa vya kufa mtu sasa wanafunzi wa hiyo shule tuliowafata nao wakaingia uwanjani mi nikua napenda ugomvi lkn siku hiyo nilisanda kuna wahuni walikua wanalusha mawe never seen b4.tulivalia sare ya kijani wao nyekundu ko ilikua rahisi kututambua hivyo mawe yalitufikia ipasavyo nilivyoona shuhuli imeambatana na mvua nikavua suruali nikabaki na bukta ili nisitambulike uzuri gari tulilokuja nalo halikupaki shuleni lilikua mbali kidg na shule.tulivofika shuleni kwetu captain akaandika barua ya friend match tukawatumia ili waje tulipize lakini hawakuja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom