Tukumbushane: Ulishawahi kuanzisha vagi au kuanzishiwa vagi Mtaani?

Tukumbushane: Ulishawahi kuanzisha vagi au kuanzishiwa vagi Mtaani?

Sijawahi chokoza mtu ila vagi naliweza sana ,,waliowahi kunianzia wanajua !! Kutoa vagi moja tuu ilo nliisoma namba nlipata kichapo cha mbwa mwizi
 
Unajua kuna baadhi ya wanaume wanadhani wanawake wote ni maboya.
Mie sipendi dharau....
Yaani mie ukinichokoza jua nikitibiwa na kupona,
lazima nikutafute tuanze A.
Niliwahi pigwa stop Masai club, Waungwana bar na pale Igo Sinza....cheza vizuri, ukinibambia tu, kiboya nina wewe.
Hufai kwa matumiz ya binadamu!! Kumbe kuna madem ukibambia umenunua kesi?😛😛
 
Mavalangati nikiyoanzisha hayahesabiki, mimi nilikuwa mzee wa sime, nilikuwa na sime mbili, mija ndefu balaa nyingine fupi.
Mimi na jamaa zangu nikiwa kinara nilimpiga jamaa bapa ya sime kila alieona japo ni usiku alipiga ukunga, walijua jamaa kafa, haikuishia hapo, jamaa wa mtaa tukiwafungia kutokupita kitaa kwetu mwaka mzima, kama vile hakukuwa na serikali.
Ujana ujinga, uhuni ujunga, ubabe ujinga, nikiwahi kulala polisi mara moja tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mavalangati nikiyoanzisha hayahesabiki, mimi nilikuwa mzee wa sime, nilikuwa na sime mbili, mija ndefu balaa nyingine fupi.
Mimi na jamaa zangu nikiwa kinara nilimpiga jamaa bapa ya sime kila alieona japo ni usiku alipiga ukunga, walijua jamaa kafa, haikuishia hapo, jamaa wa mtaa tukiwafungia kutokupita kitaa kwetu mwaka mzima, kama vile hakukuwa na serikali.
Ujana ujinga, uhuni ujunga, ubabe ujinga, nikiwahi kulala polisi mara moja tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mara moja hii au!
 
Sijawahi chokoza mtu ila vagi naliweza sana ,,waliowahi kunianzia wanajua !! Kutoa vagi moja tuu ilo nliisoma namba nlipata kichapo cha mbwa mwizi
Kama mbabe vileee.. nije nikuanzishie vagi?
 
I see hakuna kitu ninachoogopa kama ugomvi iwe kupigana au maneno siwezi.
 
Hahaha.. hapo kama umenizidi ndiyo natumia viwembe
Tatizo asili jirani.
Mi Angu jiwe au kulia kama mtu simuwezi.na hii nilikuwa nalia kwa hasira ,kwanini huyu simuwezi.

Ila hiyo zana yako hiyo...sikuwahigi kuifikiria kabisa jirani.
 
Mimi nakumbuka wakati bado chalii wa darasa la 6A sisahau hiyo siku tumetoka kufanya mitihani ya mwisho mwaka,

Tukamaliza vizuri wakati tunapishana pishana baada ya kumaliza mitihani bahati mbaya Mimi naingia darasani Kile kidemu kikawa kinatoka nikakitegeshea mguu kikajikwaa kikaanguka sketi ikapanda kufunika uso.
Bahati mbaya chupi imetoboka wanafunzi walivyoona tundu la chupi kelele shangwe kibao kama unavyojuwa wanafunzi tulivyokuwaga,
Nikashangaa gafla napigwa makofi na videmu kama kumi ivi akiwemo na yule chupi iliyotoboka nilikula makofi mchanganyiko alafu yanauma kinoma

Nimejitahidi kufurukuta huku na kule nikabahatisha kukunja ngumi nikaitupa kama kurusha jiwe gizani bahati mbaya nikampata kidemu kimoja ngumi ya ziwa nikaona wametulia kama sekunde tatu ivi naona kile kidemu kama kinalegea , kuangalia kwa mbali naona mwalimu anakuja na viranja wawili kurudisha macho kwa kile kidemu naona kimelala chini.
Nilipata wazo na kutoka mbiyo naskia sauti ya mwalimu kwa mbali mkamateni,
Hiyo mbiyo niliyo toka nayo hapo na kundi la wanafunzi waliokuwa wananikimbiza nikaona hapa naenda kusimamia nyumbani.
Kutokana hapakuwa mbali sana kama mita 400 iv nilipofika nyumbani nikaingia chumbani wanafunzi wamefika nawasikia kwa getini Odi,Odi,Odi dingi akatoka naskia wanamsalimia mzee shimoo baba mimi apa,
Walipoulizwa kuna nini naskia tumetumwa tumkamate tumrudishe shule walikuwa wanapigana, walipoulizwa kwani yuko wapi wakasema kaingia ndani, mzee akaanza kuita kaita kama mara tatu nikatoka, ananiuliza mbona umevimba na maalama ya makofi nikamwambia ukweli
Kwa mana mzee wangu alikuwa mkali kinoma. Akaniambia nikupeleke shule mimi mwenyewe au unaenda mwenyewe, nikamwambia naenda mwenyewe, nikatoka tena pale nimekabiziwa kwa wanafunzi twende nao, wale wanafunzi wananipeleka mperampera alafu kulikuwa na Majeba mawili yanataka kuninyanyuwa juu juu yaende kupata sifa .., Itaendelea

kwa mana kilichotokea kingine baada kuanza kunyanyuliwa mara unazomewa kitafata kwa sasa natakiwa nilale kesho kazini.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu malizia tu

sent from my BlackBerry keyone using JamiiForums mobile app
 
[emoji3][emoji3] hao watu hawafai mkuu.
Kwa wale wanaojua racing za motor cycle kuna siku jamaa zangu fulani walitutoroka wa kaenda hadi TMA na 250. Sasa wakajichanganya wakaingilia mule ndani kwa njia za panya.

Wakakamatwa pikipiki zikatolewa upepo halafu kila mmoja akaambiwa abebe yake walibaki kuzivuta tu. Toka saa 7 mchana wakaja kuachiwa saa 4 usiku
6c975da3d6860490640c88c71cf486bb.jpg

mondoli hahaaaaaaa
 
Nakumbuka One time nipo kwenye sherehe ya binamu yangu kipaimara it was wayback nimekaa zangu kimya kama nimelazimishwa kukaa pale.. Kuna vijana wa mitaani walikua wanazengea msosi kama unavyojua mambo ya uswazi.. Tangu nimefika asubuhi kuna kabint nilikua nakaona kanazunguka pale Mara katumwe vocha na wageni waalikwa kalikua kapoleee na sio kabishi.. Muda umefika wa kula chakula watoto walikua ni wengi balaa wakapewa portion yao maskini wababe wakala watoto wakakosa.. Utafanyaje sasa Shea yao haikuepo.. Nipo zangu ndani maana Nyumba ilikua na uzio hata cjaanza kula nkakaona kale kabinti kanashangaa tu kwa nje midomo imekauka tumaini la kula limepotea.. Roho ikaniuma.. Japo walikua wengi kwa nje lakini wengi wao walionekana wanatokea familia za jirani.. Na walikua watundu na wabishi mno.. Basi nkaona isiwe tabu nikatoka nje ya geti na kukaita kale kabinti.. Ile nafika tu nkakutana na vivulana flani ivii kuniona tu vikaanza kunitania utani wa kikubwa haswa wezere language... Hua spend mtu ayaseme makalio yangu.. Nkaachana nao na kukachukua kale kabinti mpaka jikoni nikakapa msosi kwenye sahani kila mtu kwenye sherehe ananishangaa tu.. Nkarudi ukumbini nikakaa nako jirani.. Mgao wa vinywaji umepita nkakapa soda kakawa kanakula.. Badae nkaitwa ndani na Uncle eti hajaniona tangu nimefika.. Nikawa nimesepa like 5 min ile narudi nkakuta pale amekaa mgeni mwingine aliechelewa kufika na kale kabinti hakapo.. Kumbe kamefukuzwa na wamama wa pale kakaambiwa kakalie kule nje.. Kufika nje nakuta wale vijana wameshika sahani wanakula na soda wanagawana.. Nikawachukulia poah tu wamemaliza kula kama nguruwe wakatupa sahani wakakimbia na chupa.. Nikamchukua Dogo nikaja nae ndani akiwa analia nikampa msosi mwingine nikamwambia kaa hapo usitoke.. Kakamaliza kula kakarudisha sahani maskini kakashukuru kakaondoka.. Nikakaita na kukapa sh. 1000 then nkaendelea na Mishe zingne pale.. Badae kidogo naskia naitwa nje na mmoja wa vibinti pale... Wee Dada.. Hawa wakaka wamempokonya Lisa hela ulompa.. Nikatoka nje na hasira za ajabu kufika nawakuta wale vijana.. Kuniona wakanichukulia poaah.. Nikakamata wawili mmoja akakimbia nikashusha kerbu za maana na hivi nilikua nimevaa suruali kivumbi kilitoka pale.. Nilishusha mnyigo wa maana mpaka nakuja kuwaachilia kila mmoja alipita njia yake... Sherehe ikasimama ghafla kila aliehadithiwa kile kisa akabaki anacheka na kustaajabu.. Nikatafta bodaboda nikageuza zangu home.. Mpaka Leo cuzoo hua hasau like tukio...
dah!!...we chiqa uligeuka mtaekwondoo vile...
 
hayo mambo niliyaogopa wakati jamaa mmoja aliangushiwa dondi la kitaifa akaanguka chini akawa anapumua kwa taabu..baada ya dakika chache jamaa akapepesa macho na kuaga..usiwaone watu wanatembea mitaani wakijichachua na kujifanya wababe ukatamani kuchimbiana mbichi na wao..watu afya mgogoro utampuliza adunde chini kama gunia la viazi kumbe ndio mwisho wake
 
Back
Top Bottom