Tukumbushane vipindi vya ITV, CTN, na DTV 1994

Tukumbushane vipindi vya ITV, CTN, na DTV 1994

Huwa nakumbuka kale ka mdundo ka lile tangazo la fanta ambao walikua ndio wadhamini wa kipindi na pia namkumbuka Sunday Shomary na Suzan Mungi walikua wanapendeza sana
Yeah one of the best memories ever, tumekumbuka Mali Sana mkuu
 
Wana jamvi leo nimeona japo turevew miaka hii ya nyuma vipindi vya television enzi zile 1994 kuibukia miaka ya 2000. Binafsi nakumbuka mbali sana hasa vipindi vya television ITV mfano Egoli place of Gold, 21 jump Street, Time trax, movie ya V, Rino Renz, vichekesho Kama Fresh Prince of bell air, family matters, Living Single ya Queen Latifa, Tausi ya mjuba, Vitimbi(masakuu, Ojwang' Othrong'ong'o) Vioja Mahakamani, Mambo hayo ya kina Waridi, Sumbi, bocha na Aisha. Pia kulikuwa na Tamthiliya kama The young and the restless, Sun seat beach, na Acapulco bay.

Aidha nakumbuka tulikuwa tunaangalia UEFA kupitia CFI(Canal France International). Matangazo nakumbuka kama Revola, komoa, lotion ya Jambo, hebu vingine mnisaidie CTN na DTV. Je kipindi kile watangazaji unawakumbuka? Wa ITV, CTN, na DTV. Mimi kwa itv namkumbuka Suzan Mongi nilimpenda sana sana. Karibuni tuflash back jamani.
Dah! Nimetoa machozi ya furaha na huzuni..
CTN na DTV By then...
ITV nilipenda football mundial kila alhamis SAA 1 usiku.

Nilihisi niyakuja ku wa a mchezaji maarufu duniani.
 
Mambo Hayo
Tausi
Mizengwe ya Zembwela na Max
Egoli
Taarifa ya habari ya ITV ikisomwa na Rukia Mtingwa
UEFA CL tulikuwa tunaangalia ITV kupitia Canal + nafikiri
Kulikuwa na Family Matters unakutana na Steve na kijisauti chake
Kulikuwa na muvi 1 walikuwa wanaionesha sana ITV nimeisahau jina,kuna Jaji/Hakimu alikuwa anaenda kukamata wahalifu usiku halafu anawapa taarifa Polisi waje kuchukua wahalifu,kesho yake mhalifu akipelekwa Mahakamani anakutana na jamaa ndio kakalia kiti cha hukumu.
Vituko vya akina mzee ojwang na mwala,sasa mtu akiwa mfupi tulikuwa tunamwita mwala
 
Tamasha la Michezo,,ITV kila jpili Saa Nane mchana,,tamthilia ya Passions Bibi Thabita na mjukuu wake wachawi hatari
 
Kifuatacho ITV, yule dada muhindi ndo alikuwa anasema kifuatacho ITV na kutoa muhtasari kidogo kama ni tamthilia, nakumbuka tamthilia ya Acapulco, na moja ilikuwa kali sana nimesahau jina ila ina neno beach!

Sio ya mzee Asernegas ilikuw ainaitw la revancha sijui na ile ya kina babrita. Sikumbuki jina lake.. pia ya kuna yule solidad Au ya wafilipino wale kina Yina makaspaa. Nahs inaitw pangak sayo
 
Back
Top Bottom