Tukumbushane vipindi vya ITV, CTN, na DTV 1994

Hakika. Mwaka huo 1994 ndio nimeamza kuangalia World Cup iliyofanyika Marekani. Ndio mwaka dingi amenunua TV home. Halafu ligi kama Barclays (EPL), Bundesliga na Serie A ilikuwa tunaangalia bure tu. Hakuna malipo yoyote, hapa kuwa na ving'amuzi. Mchawi antenna tu ya ndani na nje.
 
Africa journal nilikua nakipenda
Makala nzuri sana zile. Umenikumbusha mbali. Kila Jumapili usiku. Muandaaji wa kipindi amefariki ktk ajali ktk harakati za kutafuta habari, alikuwa anaitwa Mohammed Amin. Ndio maana kipindi hakikuonekana tena.
 
Susan Mungi alikua KISU sana those years, sasa hvi kawa bonge, shepu imekua ya kiutu uzima sana; ulaya sio kuzuri kiviiile.
Kipindi hiko anaitwa Suzana Lukindo. Alikuwa anatangaza taarifa ya habari yeye na Fauziat Abood. Kabla ya kuja akina Julius Nyaisanga kutangaza
 
Kulikuwa na tamthilia inaitwa V viumbe vilikuja duniani

nilikuwa naogopa lakini skosi kuangalia ktk ITV
 
Mimi nakumbuka world cup94 Italy ITV walirusha matangazo ya mpira kiufasaa na kulikuwa na tangazo la salama condoms nlikuw nalipenda sana..
Na Lile tangazo la bia ya TUSKER. Ukiona tangazo la TUSKER, REVOLA na SALAMA CONDOM ujue uchambuzi na mechi unakaribia kuanzia. Enzi hizo (world cup 1994) wachambuzi ni Charles Hillary na Mickdad Mahmoud
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…