Tukumbushane vipindi vya ITV, CTN, na DTV 1994

Tukumbushane vipindi vya ITV, CTN, na DTV 1994

Wana jamvi leo nimeona japo turevew miaka hii ya nyuma vipindi vya television enzi zile 1994 kuibukia miaka ya 2000. Binafsi nakumbuka mbali sana hasa vipindi vya television ITV mfano Egoli place of Gold, 21 jump Street, Time trax, movie ya V, Rino Renz, vichekesho Kama Fresh Prince of bell air, family matters, Living Single ya Queen Latifa, Tausi ya mjuba, Vitimbi(masakuu, Ojwang' Othrong'ong'o) Vioja Mahakamani, Mambo hayo ya kina Waridi, Sumbi, bocha na Aisha. Pia kulikuwa na Tamthiliya kama The young and the restless, Sun seat beach, na Acapulco bay.

Aidha nakumbuka tulikuwa tunaangalia UEFA kupitia CFI(Canal France International). Matangazo nakumbuka kama Revola, komoa, lotion ya Jambo, hebu vingine mnisaidie CTN na DTV. Je kipindi kile watangazaji unawakumbuka? Wa ITV, CTN, na DTV. Mimi kwa itv namkumbuka Suzan Mongi nilimpenda sana sana. Karibuni tuflash back jamani.
Tausi
 
Umenikumbusha enzi hizo CNN wanatuletea live ya World War I kutoka katika viwanja tofauti tofauti accros Europe. Kuna mtangazaji momoja nimemsahau, mwaweza kunikumbusha.

Mniombee.
World War I live?????
Hhhahahaaa we jamaa kweli unaikumbuka ITV wengine tunaigiza tu.
 
Nani anakumbuka matamasha ya CORA africa toka bondeni aisee yalikua yananoga.

Nakumbuka kwa Mara ya kwanza Tanzania tuliwakilishwa na msanii flani wa kike matata na kibao chake cha "ngoma inogilee ngoma imekolea ngoma ya pwani tatata mdundikooo"

Nimemsahau ila alikuaga US na alishaokoka na kuacha secular.
 
Wana jamvi leo nimeona japo turevew miaka hii ya nyuma vipindi vya television enzi zile 1994 kuibukia miaka ya 2000. Binafsi nakumbuka mbali sana hasa vipindi vya television ITV mfano Egoli place of Gold, 21 jump Street, Time trax, movie ya V, Rino Renz, vichekesho Kama Fresh Prince of bell air, family matters, Living Single ya Queen Latifa, Tausi ya mjuba, Vitimbi(masakuu, Ojwang' Othrong'ong'o) Vioja Mahakamani, Mambo hayo ya kina Waridi, Sumbi, bocha na Aisha. Pia kulikuwa na Tamthiliya kama The young and the restless, Sun seat beach, na Acapulco bay.

Aidha nakumbuka tulikuwa tunaangalia UEFA kupitia CFI(Canal France International). Matangazo nakumbuka kama Revola, komoa, lotion ya Jambo, hebu vingine mnisaidie CTN na DTV. Je kipindi kile watangazaji unawakumbuka? Wa ITV, CTN, na DTV. Mimi kwa itv namkumbuka Suzan Mongi nilimpenda sana sana. Karibuni tuflash back jamani.
You are good man! Memory kali kabisa and refreshing, asante sana
 
Kuna tamthilia ilikuwa inaitwa SUNSET BEACH balaaa saaana mpaka shule kwetu enzi hizo Forodhani ya kina Munira,Hemed Kavu,Hamisi Makaveli ilikuwa moto.....tukapatunga sehemu karibu na geti etiii SUNSET BEACH
 
images

Letii RIP
 
Me Nakumbuka CTN na Movie zao za TNT zingine hazina Color lakini unakomaa unatizama hivyo hivyo Deck ya Video haichelewi kuchafuka pesa za kukodisha mikanda cheche ilipandishwa bora ununue chips... maana unaweza kodisha mkanda umeme umekatika na wakodishaji wanautaka na hujautizama bulshait
 
Nakumbuka world Cup 94 me na brother tunacheki mpira nilikua kidato cha 3
 
Neighbor, everybody need good neighbor........ Halafu kulikuwa na mziki wa kibongo unasumbua enzi hizo sijui nani kapiga. Kukurukakala zako wewe zitakuponza acha we acha we, kukurukakala zako wewe zitakuponza brother sister.
Ayayayaaa! Mkuu umenikumbusha hiyo tamthiliya kama sijakosea ilikuwa weekdays saa moja usiku.
 
Back
Top Bottom