Tukumbushane Wachezaji wanaopiga wenzao Miba na Team zao

Tukumbushane Wachezaji wanaopiga wenzao Miba na Team zao

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2014
Posts
7,926
Reaction score
17,030
Kwa Tanzania imekuwa kama utamaduni. Ushirikina umeshika chat sana katika mpira wetu. Mbaya zaidi ni wachezaji wa Team mmoja kufikia hatua nao wanarogana wakigombea namba.

Team moja kubwa hapa Dar ina mchezaji huyo nasikia ukiletwa namba yake hutodumu. Anakupiga misumali. Unapata jeraha hata ukiwa kitandani. Yaani unageuka kitandani usiku kiuno au goti linavunjika. Miezi 6 unapata matibabu.

Mwingine mkichuana kwenye namba ukipangwa wewe goli hulioni sehemu sahihi. Pale unapoliona goli ukashoot kumbe umelenga mpira kwenye kibendera cha kona. Watu hawakuelewi kabisa. Unaanza pigwa bench

Kuna kipa anasema siku akipangwa yeye huwa anaona mipira mitatu yote inakuja golini so anafanya kuotea tu halisi ni upi. Akikosea anadaka panzi ule halisi unaingia golini.
 
Hii timu ni Yanga haina ubishi.....kuna mchezaji hapa mtaani kwetu anachezea hiyo timu anatusimuliaga matukio ya huyo mchawi wao. Anadai kuna baadhi ya wachezaji walishamwendea kwa babu ili akiwagusa tu ajiue mwenyewe.
 
Huyu jamaa ni dhahiri kuwa ni mchawi haswa, alipokuwa Simba ilikuwa hivyo hivyo.....watu walimlalamikia sana na hakukuwa na mchezaji Simba alimpenda.
Sana. Huyu ni mshirikina, mchawi sana. Alikuwa anawaroga wenzie wasiwe kwenye kiwango. Pia akiamua siku hiyo asifungwe hafungwi. Lakini pia akiamua kuchukua mshiko afungwe anauza match.
 
Mi nikiona mtu anakosea kiswahili anakuwa anathibitisha kichwani ni empty kabisa.

Ikishakua❌
Ikishakuwa✅
Inakua❌
Inakuwa✅
Umeamua kuhamisha magoli? bado haisaidii kitu,
Habari huletwa kwa fact na sio kwa kusikia,punguza umbea na habari zako zakusikia.
 
Mmemsahau JUMA ABDUL wenzake walilalama kwamba ukicheza namba yake Uwanjani lazima Uvunjike tu. Kijana wetu BOXER anaendeleaje lakini wadau
 
Umeamua kuhamisha magoli? bado haisaidii kitu,
Habari huletwa kwa fact na sio kwa kusikia,punguza umbea na habari zako zakusikia.
Usilazimishe kutafuta wanaume kwa nguvu. Mimi situmiee aina yako. Maana naona ni muda sana unasisitiza kuwa karibu nami. Hizo tabia Tz tunapingana nazo sana.
 
Mmemsahau JUMA ABDUL wenzake walilalama kwamba ukicheza namba yake Uwanjani lazima Uvunjike tuuu. Kijana wetu BOXER anaendeleaje lkn wadau
Siku hizi yupo wapi? Juma Abdul? Kuna mchezaji wa team flani kiatu chake kiliibwa kikaenda kutwa Zanzibar kwa mganga.
 
Usilazimishe kutafuta wanaume kwa nguvu. Mimi situmiee aina yako. Maana naona ni muda sana unasisitiza kuwa karibu nami. Hizo tabia Tz tunapingana nazo sana.
Naona umeshindwa kujibu hoja na umeingia kwenye uimbaji wa taarabu! unakimbilia kuanzisha thd huku ukijua kabisa kua ni empty set! Halafu siku zote mtu huwaza afanyalo akidhani kua na wengine hufanya kama yeye,kumbe unatafuta wanaume eeh! naona umeamua kua muwazi indirect.
 
Sana. Huyu ni mshirikina, mchawi sana. Alikuwa anawaroga wenzie wasiwe kwenye kiwango. Pia akiamua siku hiyo asifungwe hafungwi. Lakini pia akiamua kuchukua mshiko afungwe anauza match.
Kweli kabisa, cha kushangaza watu wanamjuwa kuwa ni mchawi wanamwangalia tu kumlia timing
 
Back
Top Bottom