Tukumbushane; Wakumtoa Kafara haujichagulii mwenyewe isipokuwa unachaguliwa

Tukumbushane; Wakumtoa Kafara haujichagulii mwenyewe isipokuwa unachaguliwa

Hakuna na Hayajawahi kutokea tangu dunia iumbwe
Tatizo lako ni kwamba umejikita kwenye kafara za damu zaidi. Ulipashwa kuzugumzia suala hili kwa mapana kama kubadili tabia, kuishi mfumo wa maisha tofauti na maisha ya kawaida kwa pande kama mahusiano, uhuru binafsi, matumizi na muda wa kufanya kazi, n.k.

Lakin isi kweli kwamba kila aliyefanikiwa alitoa kafara za kishirikina. Huyo ni wewe tu.

Kuna mtu kwenye Bibla anaitwa King Solomon, alimtoa nani kafara?

Kuna mtu mmoja alikuwa akiitwa Ayubu, alikuwa kamtoa nani kafara?

Niny waabudu mizimu na majini, na walozi ndio mhaharibu tafsiri nzuri ya mirathi mizuri ambany Mungu aliwaahidia binadamu, kwa kutaka kumpa ututkufu shetani.

Ushindwe na upoteee kwa Jina la Yesu.
 
Tumia akili yako vizuri. Akili ndio hirizi yenye nguvu kuliko zote.

Akili Ina nguvu kuliko uchawi wowote Wala kafara lolote
Hili nitakataa kila wakati. Kuna watu hawana akili lkn wanawashinda wenye akili.

Nguvu ipo kwenye roho na moyo na sio kwenye akili.
 
Tumia akili yako vizuri. Akili ndio hirizi yenye nguvu kuliko zote.

Akili Ina nguvu kuliko uchawi wowote Wala kafara lolote
Mwanadamu ili apate akili alitoa kafara Uhai wake. Akala Tunda la Ujuzi WA Mema na mabaya.

Huwezi pata lolote kubwa pasipo kufanya replacement.

Ndio maana ili upate akili(nitaitaja elimu kama kuchochea akili) lazima utoe muda wako na pesa.

Uliza waliosoma kuipata akili wali- sacrifice nini?

Au unafikiri akili kila mtu anayo?
 
Mwanadamu ili apate akili alitoa kafara Uhai wake. Akala Tunda la Ujuzi WA Mema na mabaya.

Huwezi pata lolote kubwa pasipo kufanya replacement.

Ndio maana ili upate akili(nitaitaja elimu Kama kuchochea akili) lazima utoe muda wako na pesa.

Uliza waliosoma kuipata akili wali- sacrifice nini?

Au unafikiri akili kila mtu anayo?
Ur still a learner
 
Tatizo lako ni kwamba umejikita kwenye kafara za damu zaidi. Ulipashwa kuzugumzia suala hili kwa mapana kama kubadili tabia, kuishi mfumo wa maisha tofauti na maisha ya kawaida kwa pande kama mahusiano, uhuru binafsi, matumizi na muda wa kufanya kazi, n.k.

Lakin isi kweli kwamba kila aliyefanikiwa alitoa kafara za kishirikina. Huyo ni wewe tu.

Kuna mtu kwenye Bibla anaitwa King Solomon, alimtoa nani kafara?

Kuna mtu mmoja alikuwa akiitwa Ayubu, alikuwa kamtoa nani kafara?

Niny waabudu mizimu na majini, na walozi ndio mhaharibu tafsiri nzuri ya mirathi mizuri ambany Mungu aliwaahidia binadamu, kwa kutaka kumpa ututkufu shetani.

Ushindwe na upoteee kwa Jina la Yesu.
Nadhani umeshindwa kumuelewa mkuu kafara sio lazima za kishirikina hata za muda au pesa ni kafara huwezi mfano kupenda mafanikio ukataka na starehe lazima utoe kafara starehe ili ufanikiwe nadhani alimaanisha hivyo.
 
Tatizo lako ni kwamba umejikita kwenye kafara za damu zaidi. Ulipashwa kuzugumzia suala hili kwa mapana kama kubadili tabia, kuishi mfumo wa maisha tofauti na maisha ya kawaida kwa pande kama mahusiano, uhuru binafsi, matumizi na muda wa kufanya kazi, n.k.

Lakin isi kweli kwamba kila aliyefanikiwa alitoa kafara za kishirikina. Huyo ni wewe tu.

Kuna mtu kwenye Bibla anaitwa King Solomon, alimtoa nani kafara?

Kuna mtu mmoja alikuwa akiitwa Ayubu, alikuwa kamtoa nani kafara?

Niny waabudu mizimu na majini, na walozi ndio mhaharibu tafsiri nzuri ya mirathi mizuri ambany Mungu aliwaahidia binadamu, kwa kutaka kumpa ututkufu shetani.

Ushindwe na upoteee kwa Jina la Yesu.
Ukisoma vizuri Uzi wangu nafikiri utaelewa vizuri namaanisha Jambo gani.

Nimeelezea mambo Kama Starehe, nimetaja sehemu Afya, nimetaja mahali elimu kubwa n.k.

Hao kina Solomon huenda huwajui vizuri na Ka unataka nikujuze basi nitafanya kazi hiyo.

Solomon kisheria hakupaswa kuwa mfalme kulingana na kanuni za kifalme za wakati ule, aliyepasqa kuwa mfalme ni Kaka yake Kwa Mama mwingine kwani yeye ndiye alikuwa mkubwa, Solomon aliamuru Kaka yake auawe kusudi asije akamsumbua hapo mbele.
Unafikiri hiyo ni nini?

Huyo Ayubu ili athibitike ni mkamilfu ulifikiri akipewa ukamikifu bure Kwa kuletewa mezani Kama mkate,
Hujui ni Mali kiasi gani alizofilisika huyo Ayubu?
Hujui ni maumivu kiasi gani alipita watoto wake wote Saba walipokufa vifo vya ajabu?
Hujui ni kiasi gani aliteseka alivyoumwa manusura age?
Au ulidhani hiyo kafara/sadaka inayotajwa hapa ni nini?

Wewe ndiye umejikita kwenye ushirikina na huenda ni mshirikina Kama sio mchawi. Mada yangu imeeleza pande zote mbili, upande wa Mungu na upande wa Shetani, lakini Kwa vile wewe ni mchawi umeona upande WA Shetani upande wa Mungu hujaona.

Uliambiwa ukiwa na Yesu ndio hutatoa kafara🤣🤣🤣 kuna watu wajinga Sana.
Huyo Yesu mwenyewe alijitoa kafara sembuse ninyi mnaomuamini?
Yeye alitaka kukomboa Wanadamu, ulifikiri angekomboa kienyeji na kirahisi ili apewe sifa za kipuuzi pasipo kujitoa kafara,

Lakini naomba nisikulaumu sijui unaelimu gani na pia sijui namna akili yako inavyofanya kazi.
 
“Maisha ya kawaida ndiyo yaliyokusudiwa yawe ya furaha”…. say no more!

A word is enough for the wise.[emoji276]
 
Naomba ufahamu hapa..tunahitaji kutoa sadaka ya kafara au kutoa sadaka ya vitu kama kujituma zaidi ili kufanikiwa???
Jitume Zaidi ili ufanikiwe. Mtoa Mada hajui hata kafara maana yake nini
 
Jitume Zaidi ili ufanikiwe. Mtoa Mada hajui hata kafara maana yake nini
Wewe ndio nafikiri unajua kiwango cha chini Sana katika masuala haya.

Wewe Kwa akili yako unafikiri unafanikiwa Kwa sababu ya kujituma kwako?
🤣🤣🤣
 
Huku kukatishana tamaa sasa! Kwanza tushike lipi sasa maana kila siku tunaambiwa tujitume kisawasawa ili tufanikiwe kutoboa maisha haya

Leo kamanda taikuni tena unatuambia maisha ya kawaida ndo yenye furaha. Hebu tufafanulie kwa mifano kuntu kuhusu hiyo kawaida unayoiongelea hapa maana kwa tafsiri yako (kuhusu kafara) inaonesha hakuna anayeishi hayo maisha ya kawaida, labda mamental retarded tu!
 
KAFARA HAUJICHAGULII MWENYEWE; UNACHAGULIWA.

Na, Robert Heriel

Naomba tukumbushane kidogo,

Ili mtu yeyote afanikiwe lazima kafara lihusike, upande wowote ule iwe Kwa upande wa Mungu au upande wa Shetani,
Na Kwa wale wasioamini masuala ya Shetani na Mungu basi, tunaweza iweka iwe upo upande mwema au upande wa Uovu.

Kafara lazima litolewe ili ufanikiwe.

Kwa bahati mbaya Kama sio nzuri kafara haujichagulii, Bali unachaguliwa na huyo unayemuomba Msaada au mafanikio.

Kuna watu waliwahi kwenda Kwa waganga WA kienyeji wakiwa wamejipanga kabisa kuwatoa watoto wao Kafara, lakini walipofika Kwa waganga wakaambiwa tofauti na walichokuwa wamefikiria,

Siku zote kile unachokipenda kuliko vyote ndio hupendekezwa kitolewe kafara.

Kama unapenda watoto wako zaidi basi ukienda Kwa mganga au Kwa Mungu basi hicho ndicho utakachoambiwa ukitoe, utoe Yule mtoto umpendaye.

Kama unampenda Mkeo au mumeo, na hapa nazungumzia upendo uliopitiliza sio ule upendo wa juu juu. Basi ukienda Kwa waganga au Kwa Mungu kuomba msaada basi jua kafara litamhusu Mkeo/mumeo.

Kuna watu huenda Kwa waganga, wakifika wanaambiwa hapa hakuna makafara ya kumwaga damu, lakini hupewa masharti kwenye sehemu nyeti mno, mfano mtu Kama anapenda kunywa pombe ataambiwa asinywe pombe mpaka anaingia kaburini, au kama anapenda wanawake basi ataambiwa asichepuke awe na Mke mmoja tuu, yaani lazima utoe kafara kile ukipendacho kuliko.

Ni kawaida mtu akahangaika sana kwa njia halali na siku anakaribia kufanikiwa unakuta Mama/Baba yake anakufa au mke au mume wake anakufa. Mtu huyo hulia Sana, huona Mali alizozipata hazina thamani Kama aliyekufa.

Ukiomba mazuri iwe Kwa Mungu au Kwa Shetani basi jua umeamua kumtoa au kutoa kafara moja ya vitu ulivyonavyo unavyovipenda Sana.

Hakuna Duniani aliyefanikiwa pasipo kutoa Kafara. Kafara ndilo humfanya mtu awe na roho ngumu Sana.

Ni hatari kutafuta mafanikio Kwa ajili ya mtu mwingine au ya starehe Fulani, kwani hicho hicho umachohangaikia ndicho unachokifanyia replacement na mafanikio uyatafutayo.

Wengi waliotafuta pesa ili wanywe na wastarehe waliishia kuambiwa wasitumie tena vilevi na waliokaidi Walikufa.

Wengi waliotafuta mafanikio ili Wale vizuri waliishia kupata magonjwa ya uzito uliopitiliza, unene, shinikizo la damu, sukari n.k wakaambiwa wapunguze au waache kabisa Kula vyakula hivyo.

Apendaye Sana huumia Sana.
Maisha yanahitaji kiasi.
Ukihitaji ziada utapaswa ufanye ziada, lazima utoe kafara.

Lengo la maisha ni kuishi kawaida, Kupata matokeo yakawaida.

Hata waliotaka kufaulu kwa kiwango cha juu walitoa kafara muda na nguvu zao Kwa kusoma usiku kucha, walitoboa ozone ili tuu wapate daraja la Kwanza,

Maisha ya kawaida ndiyo yaliyokusudiwa yawe yafuraha.

Ukihitaji mafanikio makubwa jua IPO tayari kutoa Kafara moja ya mambo uliyonayo uyapendayo, je ni Mama au Baba yako sijui, je mi Mkeo au mumeo sijui, je mi mtoto Mimi sijui, au je mi Afya yako?

Penda kiasi, mafanikio kiasi.

Ni Yule Mtibeli

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Kafara ni imani na mawazo ya kivivu. Hakuna kitu kama hicho. Ukichakarika unafanikiwa bila hayo makafara yako. Kafara nadhani ni kwa mafala na wenye uwezo uchwara
 
Kafara ni imani na mawazo ya kivivu. Hakuna kitu kama hicho. Ukichakarika unafanikiwa bila hayo makafara yako. Kafara nadhani ni kwa mafala na wenye uwezo uchwara
Kwa nini unatusi? Umeelewa kafara aliyozungumzia mtoa mada? Una umri gani kwanza wewe mzee? 50+ or?
 
Unanikumbusha mbali kupendwa huku nusu nitolewe kafala
 
Tatizo lako ni kwamba umejikita kwenye kafara za damu zaidi. Ulipashwa kuzugumzia suala hili kwa mapana kama kubadili tabia, kuishi mfumo wa maisha tofauti na maisha ya kawaida kwa pande kama mahusiano, uhuru binafsi, matumizi na muda wa kufanya kazi, n.k.

Lakin isi kweli kwamba kila aliyefanikiwa alitoa kafara za kishirikina. Huyo ni wewe tu.

Kuna mtu kwenye Bibla anaitwa King Solomon, alimtoa nani kafara?

Kuna mtu mmoja alikuwa akiitwa Ayubu, alikuwa kamtoa nani kafara?

Niny waabudu mizimu na majini, na walozi ndio mhaharibu tafsiri nzuri ya mirathi mizuri ambany Mungu aliwaahidia binadamu, kwa kutaka kumpa ututkufu shetani.

Ushindwe na upoteee kwa Jina la Yesu.

Soma comment No. 18

#YNWA
 
Back
Top Bottom