Hii thread imetulia sana, nakumbuka nyimbo za Bimalee enzi za akina Roy, Beresa, Jumbe, Marijani nk. Kuna wimbo una-verse zifuatazo nadhani unaitwa margaret
shangazi yako nae akakusihi sanaa
uje kumuona mama Margaret ukapuuza
kukaa kwako mjini faida zake umeziona
wazazi wako wawili sasa wameshakutola
Halafu kali ni ule wa mwishomwisho wa maisha ya Dudumizi unaitwa Theresa by Vijana Jazz enzi za 80s (RIP Jerry)
Najiuliza kila mara na kujuta moyoni
ni penzi gani analokupa huyoo
ukachanganyikiwa na kuisahau sura yangu
siku ya harusi
Theresa, penzi gani analokupa wewe theresa
sema nitakupatia mpezi theresa
kama gari na mi ninalo mpenzi theresa
.........................................
Bibii,hoteli gani hujalala maama,kinywaji gani hujakunywa mama,chakula gani hujakula maama,basi sema raha ipi unataka ili nielewe niiponye Roho yangu,Theresa
Najiuliza kila mara na kujuta moyoni
ni penzi gani analokupa huyoo
Ni dawa gani aliyokunywesha
Ukachanganyikiwa na kuisahau sura yangu siku ya harusi
Theresa, penzi gani analokupa huyo kijana
sema nitakupatia mpezi theresa
kama gari na mi ninalo mpenzi theresa,mamiii
Najiuliza kila mara na kujuta moyoni
ni penzi gani analokupa huyoo
Ni dawa gani aliyokunywesha
Ukachanganyikiwa na kuisahau sura yangu siku ya harusi
Mkulu De Novo,respect yaani Dudumizi alikuwa ni Hazina kwa kweli