Tukumbushane: Wimbo bora wenye jina la kike...

Tukumbushane: Wimbo bora wenye jina la kike...

Josephina na Msondo Ngoma (By the time wanaitwa NUTA aka JUWATA, aka OTTU).

Fina nakwita unisikie huko uliko,
Tangu umeondoka, umeniachia maradhi mengi sana.
Sili, silali, kwa kufikiri, natafuta Mganga wa kunitibu "maradhi?", hajapatikana ....x2

Rudi kwanza Jose, nipate nafuu, mwenzio nateseka jamaa, fanya huruma.

(Anayekumbuka maneno ya Gurumo, amalizie).
 
Aza Aza, waraka ulotuma nimepata, punguza wasi kijana,
Kuna mengi nimesikia lakini, ah! Nimedharauuuuuuu!!!

Kuna Aza ya Hemedi Maneti na Vijana Jazz,sijui ndo hii waizungumzia ama..

Aza ee umelikatili pendo langu,(Maneti) Aza Aza mbona nilikwisha kuamini,ahadi ya kwetu,ahadi ya ndoa vipi sasa Aza eeh

Mama yoyoyoyoyo sheri wangu Aza ee,Mama yoyoyoyoyo sheri wangu Aza ee,Mama yoyoyoyoyo Azamela naumia(rudia tena)

Barua yako Aza eeh ilinishangaza hasa ulipoeleza umevunja mipango ya ndoa,lakini Aza ni kipi kilichokusibu hadi Aza ugeuke na kumbe tulishapanga

Barua yako Aza eeh ilinishangaza hasa ulipoeleza umevunja mipango ya ndoa,lakini Aza ni kipi kilichokusibu hadi Aza ugeuke na kumbe tulishapanga

Ningelikwisha oa toka siku za nyuma,lakini ilibidi nisubiri ahadi,umalizie kozi,ya masomo Tabora

Ningelikwisha oa toka siku za nyuma,lakini ilibidi nisubiri ahadi,umalizie kozi,ya masomo Tabora

Aza Aza mama umenipa aibu kwa ndugu na jamaa zangu Aza ee,Aza Aza mama umenipa aibu kwa ndugu na jamaa zangu Aza ee

(Maneti)Matarajio yangu Aza ee,ni kushi pamoja vipi leo Aza ee umenigeuka

(Maneti)Aza wangu mama ee unanishangaza Aza ee,vip leo Aza ee umenigeuka

Balantanda,

Huo wimbo wa Anza huwa unanikumbusha likizo moja naenda nyumbani nikitokea Arusha. Kufika Tabora mjini nikakuta yule Mwaarabu wetu wa Sikonge kanunua basi jipyaaa la SCANIA ambalo kama sikosei lilikuwa SABENA namba 4 au 5. Basi tulipopita tu Kipalapala, dereva wetu enzi wa haya Mabasi akiitwa SHAABAN LUVANGA akalikanyaga Scania na unafahamu kule barabara za mchanga au kokoto ila hili basi lilikuwa halijali michanga au mlima. Tukiwa speed kali ghafla matraffic wakaruka kutoka msituni na kutaka kutusimamisha. Tulikuja kusimama mbali sana kutoka walipokuwa na wao hadi wakapata uvivu kutufuata. Mzee akaliwasha basi na tukaondoka. Wakati tukio hili likitokea, wimbo wa Anza ulikuwa UKITUBURUDISHA muda wote.

..........Umalizie kozi, ya masomo TABORA..... Asante kwa kupost.

Ahhh, nilisahau kuwa hapa ilikuwa ni kipindi Mzee Kalala karudi tena Vijana Jazz. Huyu jamaa alikuwa akija Vijana, hii band ilikuwa ikitisha. Na vijana walikuwa wamepata DRUMS za UMEME. Ehhh bwana, ukisiliza kwenye SPIKA nzuri, hasa wanapomaliza ile part ya kwanza kuna drums zinapigwa utafikiri ni akina METALICA au The Rollings Stones wako kazini.
 
naomba Lyrics ya Tuma -OTTU JAZZ BEND Balatanda pulizi pulizi
 
naomba Lyrics ya Tuma -OTTU JAZZ BEND Balatanda pulizi pulizi

Bibie FL1,

Naona usikilize wimbo huo mwenyewe na ukiweza utakuwa tayari na maneno ingawa nafikiri ni rahisi sana maana Marehemu TX Moshi, anaimba taratibu sana na utaweza kumsikiliza maneno yake.

Ingia hii SITE: http://www.rusumo.com/entertainment/media.php

Kwenye ile sehemu ya kuchezea mziki, bonyeza sehemu ya kwanza ya DANCE na hapo, shuka chini hadi sehemu zilipo nyimbo za OTTU Jazz band na utaukuta wimbo huu. Mie hapa nasikiliza sasa hivi.

Ukishindwa, niambie nikuelekeze zaidi.... enjoy.

Mwenye site hii, kama ukisoma hapa nasema ASANTE KWA MIZIKI mizuri.
 
kumbe kuna wapenzi wa dansi humu.. nilidhani kizazi cha bongo flava ndio kimeshatu waipu auti!? Then there is hope for some old folks! Maana wengine tumezoea minesoneso ya taratibu.. mambo ya kufokeana masikioni hatuwezi..

Wakuu, hivi hii mambo ya bongo flava, ni vibao gani vinaweza kukufanya in 20 yrs time ukakumbuka enzi hizi.....zaidi ya MPOTO na MJOMBA wake?.....Very sad for my kids n grandpals......sijui watasimulia nini!!!!

Vile vibao vya zamani, vikipigwa na wambieni unajisikia amani moyoni, uzalendo unaibuka, mshikamano, huruma, malavida ya kubembeleza etc etc........! aaaaah
 
Hapana Balantanda! Hiyo Aza ni ya DDC Mlimani Park!
Halafu kuna hii hapa:
Nakupenda sana kweli, si kwa uzuri tu ulionao hata tabia zako kwa kweli ni za kuridhisha,
Hadija Ewe Hadija, wa moyo, Asante sana nasema kwa tabia zako!

Chorus:
Tabia zako dada ni za kuridhisha, nikikukosa nitampata mwingine, nakuomba dada kaa utulie........
 
bibie fl1,

naona usikilize wimbo huo mwenyewe na ukiweza utakuwa tayari na maneno ingawa nafikiri ni rahisi sana maana marehemu tx moshi, anaimba taratibu sana na utaweza kumsikiliza maneno yake.

Ingia hii site: http://www.rusumo.com/entertainment/media.php

kwenye ile sehemu ya kuchezea mziki, bonyeza sehemu ya kwanza ya dance na hapo, shuka chini hadi sehemu zilipo nyimbo za ottu jazz band na utaukuta wimbo huu. Mie hapa nasikiliza sasa hivi.

Ukishindwa, niambie nikuelekeze zaidi.... Enjoy.

Mwenye site hii, kama ukisoma hapa nasema asante kwa miziki mizuri.

thanx sikonge hapa nilipo naburudika kwa raha zangu
 
Wakuu, hivi hii mambo ya bongo flava, ni vibao gani vinaweza kukufanya in 20 yrs time ukakumbuka enzi hizi.....zaidi ya MPOTO na MJOMBA wake?.....Very sad for my kids n grandpals......sijui watasimulia nini!!!!

Vile vibao vya zamani, vikipigwa na wambieni unajisikia amani moyoni, uzalendo unaibuka, mshikamano, huruma, malavida ya kubembeleza etc etc........! aaaaah

Mkuu wa docebit, huwezi amini... hata wazee wetu nao walikua wakiambiwa na wazazi wao kwamba miziki ya enzi zao haikuwa mizuri na haina kumbukumbu.. its a corcle of life

we subiri chemsha bongo, pi pii, kamanda, binti, salima (papii), mtu na pesa (twanga), angurumapo simba (twanga), neema (diamond), safari sio kifo (akudo) nk

Ni mambo ya muda tu utasikia enzi zetu bwana alikuwapo aki kiba, marlow, jay, benz, nk... wengalia rap ulaya wanamsifia KRSOne, Rev Run, NWA etc

Its all a matter of time... i love one song ilikuwa inaimba hivi

[Mbwembwe]
bwana ehh, ohh bwana eehh
hali hii mpaka lini jamanieee
ukiamka na shida ya jana jerry eh
na ya leo inaongezeka

Msongo
Nyamaza ohhoo nyamaza
ndio dunia mama bebii sikia

etc........... HIII ILIKUWA MSONGO YA 92 MAZEE
 
Bibie FL1,

Naona usikilize wimbo huo mwenyewe na ukiweza utakuwa tayari na maneno ingawa nafikiri ni rahisi sana maana Marehemu TX Moshi, anaimba taratibu sana na utaweza kumsikiliza maneno yake.

Ingia hii SITE: http://www.rusumo.com/entertainment/media.php

Kwenye ile sehemu ya kuchezea mziki, bonyeza sehemu ya kwanza ya DANCE na hapo, shuka chini hadi sehemu zilipo nyimbo za OTTU Jazz band na utaukuta wimbo huu. Mie hapa nasikiliza sasa hivi.

Ukishindwa, niambie nikuelekeze zaidi.... enjoy.

Mwenye site hii, kama ukisoma hapa nasema ASANTE KWA MIZIKI mizuri.

Nkwingwa,nilikuwa siijui hii Site ni nzuri sana,najiburudikia tu hapa..Wabeja sana
 
Jamani mbona mmepooza nyimbo zimeisha ?
Najua zamani kulikuwa na nyimbo nzuri nzuri na tamu sio hiki kizazi tunachokimbizana na bongo fleva
 
Hakuna wimbo wa Vero(nica)? I swear nimewahi kuusikia sehemu
Mariamu nao hakuna?
 
kuna huu wa TABU sijui ni nani kauimba....ni wewe kipenzi nikupendae, kwa jina unaitwa Tabu, mwenye sura nzuri ya kupendeza, tabia na heshima yako ni ya kuridhisha, japokuwa maana ya jina lako ni matatizo kwangu mimi lina maana ya furaha na faraja,,,,,
 
Aza...

Mama yoyoyo....sheli wangu Aza eeeh
Azamela naumia...
Barua yako Aza eeeeh
Ilinishangaza Aza uliponieleza mipango ya ndoa
 
Nkwingwa,nilikuwa siijui hii Site ni nzuri sana,najiburudikia tu hapa..Wabeja sana

Balantanda,
Inabidi niseme asante kwa FL1. Hata mimi nilikuwa siifahamu ila wakati nataka kuufahamu huu wimbo wa TUMA (nilikuwa nimeusahau) ndiyo google ikanipeleka hapo.

Ila please, nenda chini sehemu ya herufi P, utakuta wimbo wa POLISI JAZZ - Mwaka wa watoto. Huu wimbo unanirudisha mbali sana. Ilikuja kuchukua muda mrefu kufahamu kuwa kumbe mwimbaji alikuwa ni TX Moshi (RIP). Huu wimbo nimeutafuta kwa miaka mingi na ni leo hii (sasa hivi) nausikiliza.

wabeja kulimba mwanawane

Ha haaaa, FL1. Tunasema "Wabeja KULUMBA mwanawane."

Inabidi niseme asante kwa ombi lako la wimbo wa Tuma, kwani ndiyo limenifisha hapa. Asante pia zimwendee MSAFIRI RUSUMO kwa hii website safi kabisaa.
 
naomba Lyrics ya Tuma -OTTU JAZZ BEND Balatanda pulizi pulizi

Nimesimama kwenye kona ya Uhuru na Msimbazi,natizama wanaopita wanaorudi mama ee,huenda nikaiona sura yake Tuma

Nimesimama nikiwaza ahadi yetu tuliyopanga,tukutane Darisalama Tuma mamaa nia na madhumuni wazazi wakuone

Nimesimama nikiwaza ahadi yetu tuliyopanga,tukutane Darisalama Tuma mamaa nia na madhumuni wazazi wakuone

Nikarudi maskani Roho yangu inauma shoga yake kanijia na kunieleza Tuma e Tuma ee kishaolewa

Nikapatwa na mshituko moyo wangu kwenda mbio,sikutegemea Tuma kama angevunja ahadi yetu,ama kweli penye udhia penyeza rupia

Usinione nimekonda ewe Tuma hakuna lingine mama ila ni wewe Tuma(rudia tena)

(TX)Usiku wote nalala nikikuwaza na kuita jina lako oooh Tuma,naomba mama kama unanisikia mama unijulishe mama japo kwa barua

(TX)Matatizo umpenda anayependwa na wengi huenda ukanywa sumu au ukajinyonga,kwa kuwa Moshi bado ni kijana kubembeleza mama kawaida yangu

Usinione nimekonda ewe Tuma hakuna lingine mama ila ni wewe Tuma(rudia
tena)

Back
Top Bottom