Tukutane hapa tuliowahi kuvamiwa na majambazi tupeane uzoefu/ushuhuda

Mkuu ebu piga ka picha tu Cha huo mwanya utuaminishe mwanya tu achana na sura nzima
 
Kuna mtu ataharibu sasa atasema hao ni wanaume wa dar🤣🤣🤣
 
Mimi wakatimwingine nipo form 4 nilikua nakaba na kuchukua hell kunasiku nilimkaba babaake na rafikiyangu ananijua vizuri sababu nilitokea nyuma hakuniona nikaona Bora nimalize kabisa yani niuwe nilikaba mpaka akalegea nikajua tayari nimeua kumbe kazimia
 
Pole saaaana [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwaka 2007 asubuhi tukiwa kwenye daladala kufika buguruni mama mmoja kabaini simu yake imechomolewa na kibaka na anauhakika kibaka hajashuka akauwasha moto kuwa aliyeiba simu hajashuka akamwambia dereva tafadhali twende polisi akajitokeza Kaka mmoja akamwambia yule mama simu yako ni Aina gani na ni Sh.ngapi mama kajibu Nokia elfu sabini

Kaka akazama mfukoni akatoa laki moja tusiende polisi maana anaharaka saa hiyo tumekaribia mataa Buguruni gari ya Gongolamboto hiyo.

Mama kajibu sitaki laki line yangu instead majina ya wateja wangu wa samaki sitaki laki yako nataka simu yanguu twende polisi

Huyo aliyekua anataka kutoa laki alikua siti ya mbele karibu na dereva, basi Hari ziliporuhusiwa alitoa bastola akamuelekezea dereva akamwambia hatuendi polisi endesha gari kuelekea tazara bwana red Kumbe hakuwa peke yake huku kwenye siti niliyokaa Mimi Kumbe nimekaa na mwenzie naye akatoa bastola akaiinua juu akiamuru tutulie

Ulimi Wang ulikua wa moto mdomoni mpaka ninaufeel nilitetemeka Sana dereva alinyoosha mpaka Around uwanja wa taifa wakashuka jamaa wanne na Makoti makubwa wakaenda zao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama namuona mama wa kinokia alivyokuwa mpole

Sent using Jamii Forums mobile app
 
huu ndo umuhimu wa kucheza sanaa za mapigano....unaua kibaka au kumdhuru ndani za mapigo machacheee
 
huu ndo umuhimu wa kucheza sanaa za mapigano....unaua kibaka au kumdhuru ndani za mapigo machacheee
umesema kweli.... ningekuwa zembezembe wangeniumiza na kuniibia, na yule mzee wangemuibia hela zake aliuza gari mbili. KUJIFUNZA MAPIGANO KWA KUJILINDA NI MUHIMU MNO. NINA VISA VINGI SANA HASA VIBAKA HUWA NAWAPA KIPONDO SANA.
 
Usiombe kuvamiwa na majambazi , nilikuwa Moçambique mji mmoja unaitwa Cumba,au kwamba.kisa kilianza hivi mwenye nyumba aliniambia anataka kuivunja nyumba yake ilikuwa iko kalibu na njia ya treini na alishalipwa pesa,tukakubaliana basi nitaamia banda la uwani ingawa lilikuwa halina mlango kwa makubaliano ataweke kesho yake, basis walipovunja pakajaa uwani mabati, mbao,milango madril na mazagazaga kibao,kwa makubaliano kesho asubuhi angekuja kuvibeba na gari, ilipofika usiku akili ikawa inaniambia Leo lazima wezi weje na ukitegemea ile nyumba niliyohamia haina mlango,halafu nyumba ilivunjwa kwa kutoa vitu bila kuangusha kuta,nikajisemea hapa Leo silali,ila nikazima taa za chumbani na kuacha za inje zinawaka ili iwe rahisi kuona kitu kwa inje,basi kufika kama saa nane usiku nastuka namulikwa na tochi nilichofanya ni kupiga kelele, ratraooooooo,maana yake mwizi yule jamaa alikimbia halafu akaenda kusimama kwenye geti la mlango wa mbele,kutoka kuchungulia naona kuna watu kama sita hivi,halafu mvua inanyesha kelele zangu hazifiki popote, nilichofanya nikaona hawa jamaa wataniuwa,nikachukua paspoti yangu na Dire,nikaluka ukuta nikawaachia nyumba kwenda kuomba msaada kwa majirani,ndiyo ilikuwa ponapona yangu
 
Mama siyo wote, mama tuko wachache mwingine angetimua mbio.
 
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]noma Sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inaonekana una training za kupigana au gym Sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
umesema kweli.... ningekuwa zembezembe wangeniumiza na kuniibia, na yule mzee wangemuibia hela zake aliuza gari mbili. KUJIFUNZA MAPIGANO KWA KUJILINDA NI MUHIMU MNO. NINA VISA VINGI SANA HASA VIBAKA HUWA NAWAPA KIPONDO SANA.
sure man...ndo raha ya kucheza martial arts...yani tena kama upo na demu ndo unachukuaa sifaa zootee..manake unawaosheaa vibaka mwanzo mwisho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…