Tukutane hapa tuliowahi kuvamiwa na majambazi tupeane uzoefu/ushuhuda

hahahahahahahaahhahahahaahaha
 
Mzee ki kwetu Tuna usemi unasema Lyoga lya Ponera.Sasa wewe mwizi anapanga na nimeliona kabisa,alaf huwezi jua walikuwa wangapi? Pia huwezi jua Kama Ni mwizi kweli au ni watu wanataka wakutoe roho kwa sababu zao. Uli pia uache umama was kuongeza maneno kuwa nilikimbia huku nalia.Mimi sijasema mahala nililia, nyie ndio waandishi Makanjaja,wazee wa kupika story
Nimecheka sana aisee....ww muoga sana unakimbia huku unalia.....ulishindwaje kumkabili mwizi mmoja!!?
 

Duh hii kali😂😂 walikugeuzia kibao cha mwizi lol, hao wezi wamenishinda tabia
 
Joga ww...kukimbia huku unapiga kelele unafukuzwa na mwizi ndio kilio chenyewe....
 
Nimesoma huu uzi mpka hapa nasisimka! Ila ngoja niandike kisa changu. Miaka ya 2002 ikiwa ni mwaka wa pili baada ya kifo cha baba yangu, tulienda kuishi kwa bibi mzaa mama kijiji kimoja huko Sumbwanga. Miaka hiyo, kulikua na watu maarufu kama chinja chinja. Nadhani hili suala lilikua linahusiana na ushirikina. Basi bibi siku moja alienda shamba, mbali kidogo na kijiji, mimi na dada yangu tukabaki nyumbani, mida kdg sister kaniambia tumfuate bibi shamba, bas haoo kufuata njia. Kuna njia za mkato, huwa watu wanapita, mara paap, mtu anatoka kwenye nyasi ndefuuu.. Duh moyo ukaniripuka, sister ndo kabisaaa, katufanyia ishara ya kidole kuwa tukae kimya. Akatushika mikono kwenda kichakani, hapo niko mdogo maana sisiter wa 94. Kufika tukakuta watu kama 6 hivi, tupo wadogo dada kawa mpole, nikajua kabisa tunakufa hapa, basi niko kama na miaka 6 tu, nikawaambia "Msituue baba yetu alishakufa mama nae hayupo tunaishi na bibi tu baba alinambia nibaki kuja kuirudisha familia yake maana anakufa tukiwa wadogo." (kweli mshua alisema hayo b4 hajafa) Sijui ilikuaje asee, walituachia wakamwambia mmoja atusindikize mpk shm moja hivi mtoni turudi nymbn. Hayo matukio yalikua yanahusishwa sana na uchunwaji ngozi mtu akikamatwa. Very shocking hope ningeshakufa. Bibi alilia sana mpk sasa niirudi bush huwa analia kwanza ndo anani hug.
 
2016 enzi hizo nasoma chuo.. tulikuwa ghetto watu watatu yaani mimi na rafki zangu wawili.. Tulikuwa tunapiga story mara ghafla usingizi ukatupitia bila kuzima taa na dirisha lipo wazi so tulikuwa tunaonekana tulivo lala na watu wanaopita nje..
Kumbe wizi wakatuchora wakuruka geti la nje na kusogelea chumba chetu na kufungua mlango taratibuuu aiseee kulikuwa kuna smart phone 3 zipo chaji na laptop 1 jamaa alikuwa anachek movie kabla hajapitiwa na usingizi..
Mi nlikuwa nimelala huku nimeupa mgongo mlango so mwizi aliingia kwa nyuma yangu..
Nikawa kama naota kuna watu wameingia chumbani nikageuka kuelekea upande wa mlangoni yaani nikawa kawa kama nimegeuka kumuangalia mwizi anavotuibia..
Yaani nilikutana na jitu jeusi tiii alafu lina miguu mikubwa kama ya tembo alafu lipo uchi wa mnyama limejipaka mafuta mengi yaani linateleza tu aiseee wizi wanatisha jamani..
Nikapiga kelele na kumrukia maana hakuwa na silaha yoyote alinipiga na laptop usoni mpaka ikapasuka wale wenzangu kukurupuka mmoja akala teke la uso na kuzimia palepale.. Mimi kile kichapo cha laptop usoni kilinifanya nianguke kitandani mpaka nikavunja chaga za kitanda.. jamaa ndo kukimbia na kuruka ukuta na kusepa mazima ila akuiba chochote ila alikuwa na wenzake nje... sitasahau kabisa
 

Nduta kule siku za soko watu kutekwa mchana ni jambo la kawaida sana Juzi juzi wanaume walienda mpaka geti la kuingia kambini na polisi walikuwa wanawaona


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mm nkajua ikawa ndo mwisho wako wakunywa pombe kabisa kumbe bado
Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi nlikutana na Majambazi kama saba hivi, juzi tu hapo, ilikuwa maeneo ya Nungwi pale, nlikuwa naenda zangu kumtembelea shemeji yenu. Majambazi hawafai kabisa. Wakanikaba, wakachukua hadi mtumbwi wangu, wakaniua kabisa halafu haoo wakadumbukia zao Nungwi, chubwiii, wakapotea zao kwenye maji nawashuhudia hivi. Yaani.
Bangi mbaya sana aisee.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh sasa walipata faida gn kuiba simu ya elfu 70? Hivi yule Mama angekubali ile laki 1 inamaana wangemuachia au wangempora? 😬
Hao majambazi siyo walioiba hiyo simu ya huyo mama. Wao inaonekana walikuwa wanatoka kwenye mishe zao, na mtu akaiba simu humo garini.

Sasa kusikia kuwa gari iende mpaka kituo cha polisi na wao wana silaha wakajua ndiyo wanaenda kukamatwa, ndiyo maana unaona jambazi alikuwa willing kutoa laki moja mama akanunue simu mpya ili wasiende kituoni.
 
Nakumbuka mwaka 2011 Siku Ya Eid pili nilienda Wet 'n' Wild Beach with Family, ilivofika Jioni saa 12 rafki zangu wakaniforce Niende South Beach... Nyumbani nilikatazwa kutoka ila sikuskia na Nilikosa gari ya kunipeleka kila mtu analalamika lile nyomi la magari Kigamboni siku za Skukuu inakua ZOGO.... Basi nilitaka kukodi Taxi lakini mwenye Taxi alikataa kunipeleka kigamboni akidai kwamba kuna foleni sn labda aniache kivukoni halafu nikishuka Pantoni ntachkua Bajaji au Pkpk mpk South Beach. Nikafata ushauri wa mwenye Taxi Sikujua km kuna Mabalaaa huko Kigamboni siku za Skukuu maana siku za Skukuu sisi huwa tunaenda Beach za hukuhuku hatuvuki.

Nilivoshuka Pantoni ilikua mida ya saa 1 usiku mapema tu, watu kibao km mkutano wa siafu! Bajaji zilikua hamna kituoni zilibaki pkpk tu, ikabidi nipande pkpk nilikua nimevaa Jeans, Blauz refu na Handbag yangu kwapani magari yalikua yanatembea taratibu mno hakuna pa kukanyaja Watu wengi walikua wanatembea kwa miguu, kumbe wale wanaotembea wengi ni wezi wamejichanganya kwenye umati wa watu. Njiani nilikua naona wanaharass wanawake na kuwashika shika, mara gafla nikashtukia mwanaume mmoja anaivuta handbag yangu, sikumuachia na mm nikawa naivuta.. Vuta nikuvute hatimae nikamshinda. Ndio yule Bodaboda ananiambia ooh 'samahani Dada nilisahau kukutahadharisha km kuna wezi shika vzr mkoba wako,' nageuka nyuma yule mwizi anaikimbiza pkpk yetu tena yupo na wenzie km 3 hivi na mbaya zaidi foleni kubwa mno magari yanatembea very slowly, nilichanganyikiwa sikujua hatma yngu itakuaje, nikageuka upande wangu wa kulia kulikua kuna gari (pickup) ipo kwenye foleni pia lakini ya Kurudi mjini yaani inaelekea magogoni, (nyuma kwenye hio pickup kulikua kuna watoto wamekaa km 4 hivi wadogo) nilijishtukia tu nimesimama juu ya Bodaboda nikamwambia mwenye Pkpk asogeze karibu na ile gari nikairukia ile gari ya watu mwenye bodaboda ananidai hela yake nikamlipa kisha nikamwambia mtoto mmoja aikalie handbag yangu ili aifiche, wale wezi walivofika walizunguka ile gari wanatafuta Handbag yangu hawaioni Bahati nzuri Dereva wa hilo gari akashuka alikua mtu mzima na ana mwili kiasi akawauliza mnataka nn kwenye gari yngu? Wakakimbia, yule Mzee akaanza kunihoji maswali nikamuelezea mkasa mzima wakanionya yy na mkewe siku nyengine nisirudie tena kwenda kigamboni siku za skukuu bila gari ya Family ni hatari. Tena walinambia una bahati sn sisi tulikua tunatoka Dar es salam Zoo, tulikua hatutaki kupita hii njia, tulipanga tuzunguke njia ya Mbagala kukwepa foleni ila nashangaa sielewi kitu gn kimenipitisha huku kumbe Mungu alipanga tuje tukunusuru ww. Walinifikisha mpk nyumbani na wao wakaendelea na safari yao, Dah. Mwenyezi Mungu awazidishie kheri popote walipo.
 
hahahajahahahahahahaha
 
Siku nyingine tutakua tunaenda wote wasikudhuru

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…