Nimesoma huu uzi mpka hapa nasisimka! Ila ngoja niandike kisa changu. Miaka ya 2002 ikiwa ni mwaka wa pili baada ya kifo cha baba yangu, tulienda kuishi kwa bibi mzaa mama kijiji kimoja huko Sumbwanga. Miaka hiyo, kulikua na watu maarufu kama chinja chinja. Nadhani hili suala lilikua linahusiana na ushirikina. Basi bibi siku moja alienda shamba, mbali kidogo na kijiji, mimi na dada yangu tukabaki nyumbani, mida kdg sister kaniambia tumfuate bibi shamba, bas haoo kufuata njia. Kuna njia za mkato, huwa watu wanapita, mara paap, mtu anatoka kwenye nyasi ndefuuu.. Duh moyo ukaniripuka, sister ndo kabisaaa, katufanyia ishara ya kidole kuwa tukae kimya. Akatushika mikono kwenda kichakani, hapo niko mdogo maana sisiter wa 94. Kufika tukakuta watu kama 6 hivi, tupo wadogo dada kawa mpole, nikajua kabisa tunakufa hapa, basi niko kama na miaka 6 tu, nikawaambia "Msituue baba yetu alishakufa mama nae hayupo tunaishi na bibi tu baba alinambia nibaki kuja kuirudisha familia yake maana anakufa tukiwa wadogo." (kweli mshua alisema hayo b4 hajafa) Sijui ilikuaje asee, walituachia wakamwambia mmoja atusindikize mpk shm moja hivi mtoni turudi nymbn. Hayo matukio yalikua yanahusishwa sana na uchunwaji ngozi mtu akikamatwa. Very shocking hope ningeshakufa. Bibi alilia sana mpk sasa niirudi bush huwa analia kwanza ndo anani hug.