1. Miaka ya 2000 mwanzoni, likizo time mshua katufata boarding school tunarudi home. Tulichelewa kuvuka boarder ya mutukula tunaitafuta bukoba... baaasi tukakutana na bonge la road block, wazee walee na SMG zao... wakapunga mkono style ya Traffic police wa awamu ya tano.. sijui mshua alitoa wapi confidence, ali reverse shangingi faster na kwa speed almost 40km/h au zaidi for about 10 minutes, akageuza huyooo tukarudi boarder tukala.. ndo ikawa pona yetu..
2. Wazee baba walikua wanammendea mshua kitambo, wakijua pesa pale ipo.. sehem ya kazi ya mshua ilikua ni polini, katika ranchi za taifa.. basi siku moja mshua kapokea mishahara ya wafanya kazi, kaenda nayo porini.. majambazi yakatonywa, yakajiandaa.. Jioni saa kumi na mbili yakatimba home na bunduki kubwa kubwa, sisi watoto hatujui A wala B. Mshua alikua katoka kaenda kupiga maji na washakji zake.. majambazi yakatukuta sisi na step mom.. yakamwambia step mom awapekele mpaka safe ilipokua, akawapeleka, sema wakashindwa kuifungua.. wakatafuta funguo wakakwama.. Mama nae hajui funguo ilipo. Wakampa kipigo cha mbwa koko lakini hakuwapa walichokitaka, kiukweli hakujua funguo ilipokuwa. Safe wakaifyatulia risasi lakini haikufunguka.. walivyoona muda unakwenda, wakabe redio, TV na jewerly wakasepa... Dingi anarudi kalewa zake, anasema funguo zilikua kwenye suruali aliyokuwa kaivaa jana yake.. suruali iko juu kwenye hook..
3. Mwaka 2016 saa nane usiku natoka zangu kula bata na wana wa TIA, nina kama mwezi nimenunua mark X.... nafika tazara taa zinawaka red, hamna magari kabisa na malori niya kuhesabu, ile nasubiria zimulike green, akatokea mtu out of nowhere anataka nishushe kioo, ana bonge la panga.. nikajaa wenge, pombe zikaniishia.. jamaa mwingine akatokea upande wa kushoto akaanza kugonga kioo kwa kitako cha bastola... mweeee, nikakanyaga mafuta gari inaondoka kwa speed matata... bahati nzuri nilikua sijaweka P(parking).. kuna semi trailer lilikua linavuka kwenda airport nililikosa kosa kuligonga.. nikanyoosha mijamaa nikaiacha haiamini kama nimeiponyoka... nilipofika buguruni sikujali kama kuna watu na magari wanavuka 24hrs... huyooo mpaka getto Tabata.. !
Sent using
Jamii Forums mobile app