Tukutane hapa tuliowahi kuvamiwa na majambazi tupeane uzoefu/ushuhuda

Tukutane hapa tuliowahi kuvamiwa na majambazi tupeane uzoefu/ushuhuda

Nakumbuka kuna siku niko peke yangu kwenye gari mchana kweupeee mitaa ya kkoo opposite na kituo cha polisi msimbazi.
Ishu ilikua hivi, kulikua na kifoleni cha kizushi tu gari zinasonga mdogo mdogo, na mie nipo kwenye foleni nimefunga zangu vioo nakula acc tu, nasogea kidogo nikasikia papapaaaa! Nikastuka, naangalia kwa umakini nje naona kila mtu anatafuta njia ya kukimbilia, wakati sijakaa vizuri naendelea kuzisikia tena papapaaa!
Kutazama pande zote kweupeeeeee yaani kama sio kkoo vile, mara namuona polisi anatokea kituoni ameshika mjegejo wake nae anapiga hewani huku anakimbilia pale ilipo gari yangu.(wakati huo mimi najiuliza, nifungue mlango nitoke nduki ama nifanyeje) mara kidogo zikalia tena upande wa pili(mtaa ule ilipo stand ya daladala za mbezi) zilipolia zile zilikua mfululizo mpaka yule askari akateleza(mie nikigeuza shingo huku nawaona wazee wa kazi hawa hapo hata presha hawana, nikigeuka huku namuona askari na mjegejo wake, hebu vuta picha upo mtu kati) basi bwana yule askari alivyoinuka tu akaifanya gari yangu guard/gadi.
Akawa anapiga juu jamaa nao wakajibu halafu haoooooo wakapanda kwenye bodaboda tatu wakasepa kuelekea yalipo makao ya klabu ya yanga, hapo ndo nikaona askari wengine wanajitokeza na raia wanaanza kurudi kwenye vyombo vyao.
Mie hapo kijasho kinanitoka pamoja na kuwa acc inawaka, sitaisahau hiyo siku, halafu kilichoniponza zaidi mpaka kujikuta uwanja wa vita ni kitendo changu cha kuwasha muziki wa sauti ya juu mpaka unashindwa kusikia mambo yanayoendelea nje, na hii tabia ilishawahi kunigharimu tena, ngoja niwape japo ni nje ya mada.
Kuna siku nayo ni mida ya mchana natoka zangu mitaa ya posta nakuja morocco, ujana mwingi nimefungulia mziki kwa sauti kuuuuubwa, nafika ile petrol station ya kabla ya mataa ya saint Peter’s nikaingia kujaza mafuta.
Nimemaliza fresh kabisa natoka ili niingie main road nakuta barabara nyeupeee hakuna hata gari, bwana bwana bwana! Hata sikujua nini kinaendelea mie nikaangalia kulia naona gari ipo mbali nikaingia, ile napandisha kile kilima kuelekea mataa naona mi V8 ya kutosha imeniweka mtu kati(kama mnavyojua magari ya msafara yanavyosambaaga barabarani, mara hili litoke kushoto kwenda kulia na lile nalo vile) msafara ukapunguza spidi kabisaaaa(na mie tayari nishachanganyikiwa nayumba tu na kagari kangu, kulia si kulia kushoto si kushoto naelea tu) kioo cha moja ya yale magari kikashushwa nikaonyeshwa tu alama za kidole ile ya weeeweeee!
Aaaah! Nilishtuka gari imezima japo ni auto(nilizima bila kujielewa yani)
Mara paaap msafara ukatembea nikabaki peke yangu nimetoa macho tu, kidogo askari yule aliekua kwenye mataa akaja mbiooo na kitambi chake
Kufika pale hakuna cha kuuliza nini wala nini nilikula makofi kama matatu ya kunirudisha kwenye hali yangu.
Nikawekwa siti ya nyuma, akaiwasha gari fasta akaipeleka kwenye kibanda chao kile cha kumalizana( hapo kumbuka hajanisemesha kitu) nafika pale nakuta clue nzima nikashushwa kama jambazi( mitama ya DAR to LAGOS nilichezea ya kutosha)
Baada ya hapo ndo naulizwa ulitaka kufanya nini mi nikawaambia sikujua kama kuna msafara
Wakaniambia umevamia msafara wa mke wa rais( kilikua kipindi cha babu cheka/mkwere)
Basi baada ya ile presha kutulia nikaanza kubembeleza yaishie pale, nikaambiwa ngoja mpaka msafara ufike salama ndo tutaongea
Ilinitoka 70 na nilikaa masaa matatu pale pale.
Nilipotoka hapo hata nikisikia honi ya bajaj napunguza mwendo kuhakikisha.
Yaani sitasahau. Poleni kwa kwenda nje ya mada


Sent from my iPhone using JamiiForums
[emoji23][emoji23][emoji23] Umenifurahisha eti mitama ya Dar to Lagos

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Walituvamia 2016 Sept ,majambazi zaidi ya kumi walivamia nyumba nne usiku mmoja na ya kwetu ilikuwa ya pili ,walivyunja mlango wa chumba na ule wa mbao ndani ya sec Ila walitumbukia sebuleni maana nyumba yenyewe ilikuwa ujenzi haujaisha , hata milango haikuwa stable Sana ,wakapiga paaaa moja tu ,nikashituka nikachukua panga nikalikwaruzaa ukutani nikiwa kuchumbani paraaaaaa paraaa "nikawambia mkiingia tu tutaonyeshana kazi" wakaema we tulia "tunakuja'

Aisee kishindo Chao Kuna friji lilikuwa kwenye korido walilidondosha kulee vyakula hukooo mayai hukooo yaani ,umeme wakakata wakawa ma matochi makali balaaa ,Sasa mi kuona vile nikapanda juu kwenye makenchi maana palikuwa wazi ..wakazama chumbani wakamkuta wife kakaa tu kitandani hajui afanye Nini mi nipo kwa juu tu naangalia ,maana nilivyowachimba mkwara wangenishilka wasingeniacha hai...wakamwambia wife tunataka pesa akasema Hana chochote wakamwambia lete pochi ya kazini akawapa ,akawapa simu zake zote ,pochi ilikuwa na elfu tano ,wakasema unatuchezea wakaenda chumbani kwa mtoto wakamchukua wakamleta kwa wife , mbele yake wakamwekea panga mtoto shingoni wakasema tunahesabu Hadi kumi ...
Wakaanza walivyofika tano nikawambia chukue suruali Ina pesa hapo kwenye kochi wakachukua kulikuwa na laki mle ...basi majirani wakawa wameshutuka wakapiga filimbi wakasepa ,wakaenda kuvamia nyumba zingine 2 ...toka kilindi hicho huwa sila hata Sasa hivi nasikilizia kimtindo ....na nimefuga mbwa wa kunishtua

Sent using Jamii Forums mobile app
We jamaa mchele mchele sana,,,,,hahahahaa yan unajificha unamuacha wife

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwaka Jana Dec nimetoka Mwanza 2:30 usiku na mkonga wangu pick up cruiser kufika shy nikakuta barrier hapo nipo 1st na 2nd born wangu tukazuiliwa tukajieleza tukaambiwa Kuna utekaji mbele nikasema nitapambana nao kufika ziba kwenye 6 usiku ngoma zimejaa road na polisi wanapanga kupambana nao tukio jiran kumbe nikawaambia Nina udhuru nikatoboa, kufika igunga nikazuiliwa kuwa jamaa wapo mbele nikaosha mpaka 1 asb nipo hme dom ila nilikutana ba watu wa ajabu usiku njian wengine wamebebana, wengine Wana najembe shida niliyoiogopa Ni kwamba sikuwa na spare tairi
Duh.. agwe... ujasiri wa kutembea bila spare tyre unautoa wapi. Au ilikuwa mpya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
HII YANGU ITAKUWA KALI NA HATARI ZAIDI......

Ilikuwa ni moshi mwaka 2009 mwezi wa sita mahindi yamekuwa marefu, miti mirefu, migomba mingi kiasi kwamba hata taa za umeme hazimwiliki vizuri na kuna wingu zito sana na GIZA NENE. Mida ya saa mbili usiku nimetoka town nimeshuka kwenye daladala, nikaingia njia ya kuelekea home. Njia hiyo mpaka kufika home ni parefu kidogo, halafu ina giza kuu. Katikati ya njia kuna geti la kuingia nyumba ya jirani, nilipofika pale nikakuta pikipiki mbili na washkaji waliponiona wakashtuka mmoja akaninyooshea bastola akaniambia lala chini. Sasa maana ilikuwa ghafla na tumekaribiana sana na nilikuwa najiamini sana nikamrukia nikashika ile bastola kuielekeza juu zikatoka risasi kama nne kwa haraka sana....... kumbe ndani kuna majambazi mengine manne yanaforce jamaa ayape hela na yameshatoa kipigo cha maana......

Yule jamaa baada ya risasi kuisha kwenye bunduki nikampiga ngumi akadondoka chini, mwenzake akawa anakuja na sime, ile anainyanyua anikate nikawahi kumdaka mkono nikampiga ngumi ya mbavu akaachia sime, nikampiga ngumi ya pili halafu nikawahi ile sime.
NIKAWAAMBIA MKINIFUATA NAWACHINJA, sasa mimi nilidhani walikuwa wananiwinda mimi kumbe jamaa walikuwa wanawasubiri wenzao. Mara nikaona majamaa wanne wameruka ukuta kwa speed ya hatari na wale wawili wakawasha pikipiki haraka sana wanaulizana imekuwaje jamaa akawaambia kuna mwanajeshi hapa tuondoke...... Wakati huo mimi nimeingia kwenye mahindi wakamulika na tochi huku na huku hawakuniona. Wakawasha pikipiki wakaondoka kwa kasi ya ajabu.

NIKABAKI PALE NA ILE SIME HUKU BADO SIELEWI NINI KINAENDELEA NDIYO SASA NDANI YA ILE NYUMBA WAKAANZA KUPIGA YOWE NA MAJIRANI WALIOSIKIA WAKAJA......

nakumbuka kilikuwa ni kitendo kama cha dakika mbili tu.

YULE MZEE ALINIPA LAKI MBILI AKANIAMBIA KAMA SIYO MIMI WANGEMUUA NA WANGEMUIBIA HELA NYINGI SANA.....
Hiyo siku sitaisahau aisee.
Duh kama movie

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wale vibaka wangu walikuwa wajinga sana..........2001 hiyo nimetoka zangu kupiga liquid narudi home kama saa 7 hivi ucku, nilipokuwa naishi kuna umbali kidogo kutoka barabarani, dereva taxi kanishusha nikaanza kukata vichochoro kuelekea nyumbani, ghafla nikamulikwa usoni na tochi yenye mwanga mkali sana halafu ikatoka amri kali eti:- simama hapo hapo na ujisachi mwenyewe utoe kila ulichonacho mfukoni........yani sikujiuliza mara mbili mbili, niligeuka kwa kasi na kufyatua mbio kali sana ambazo sijawahi kukimbia.

Kuona ivo na wao wakaniunganishia kuanza kunikimbiza halafu mbaya zaidi wakaanza kuniitia mwizi, mi kusikia ivo nikapunguza mwendo hatimae nikaanza kutembea kwa mwendo wa haraka, kuona natembea na wao wakaanza kutembea na hawapigi tena kelele za mwizi, nilipoona wananikaribia nikachomoka tena mbio kali......zoezi likarudia lile lile la kupigiwa kelele za mwizi, bahati nzuri natokeza barabarani na gari ya police hii hapa, nikawaelezea tukarudi hadi walipoanza kunikimbiza lakini hakuna mtu, basi wakanisindikiza hadi nyumbani.

1993 Tabora hiyo jamaa yangu mmoja kaja mjini kupokea pesa yake ya mauzo ya tumbaku, akawa na mipango mingi balaa ikiwemo kununua baiskeli mpya, kununua radio kaseti ya Lasonic na kuongeza mke wa tatu..........hakuna hata mpango mmoja uliotimia, usiku wa hyo aliibiwa pesa yote sh 100,000/= na baamedi aliyelala nae gesti (nadhani ndo alikuwa anamfanyia intavyuu kama anafaa kuongezwa kuwa mke wake wa tatu, tangu siku hyo jamaa yangu huyo alishikwa na uchizi akatoweka nyumbani hadi tulipokuja kupata taarifa za kifo chake cha kugongwa na gari.

Juzi juzi tu hapa kuelekea kipindi cha sikukuu za krisimasi na mwaka mpya kundi la vibaka wapatao kama 17 hivi walivamia kwa jirani yangu aliyekuwa kauza kagari kake kamechakaa chakaa kwa sh milioni 6, wale wapuuzi wakataka kuja kuchukua zile pesa kama vile walimuwekeza........kwa mara ya kwanza ndo nilikatumia vizuri ka manati kangu ka kizungu, nilimkongoroa goti mmoja wao na wengine wakakimbia, yule tulimmalizia pale pale kwa kushirikiana na wananchi wenye hasira kali.

2007 kuna majambazi yalivamia mtaa flani wenye maduka mengi, sasa ile tabia ya mlinzi mmoja analinda karibu maduka 40, wakamkamata mzee wa watu wakaenda nae hadi kwenye mojawapo ya maduka anayolinda wakamkazimisha aanze kuvunja, zoezi lilipokamilika wakamlazimisha aanze kusomba vitu anapakia kwenye gari la majambazi.......ile wanamalizia mara paaaaap na mwenye duka akatokeza akamuona yule mzee mlinzi wa duka lake yupo kwenye harakati kupakia vitu kwenye gari ya wale wezi, jamaa akafyatua risasi hewani, wale wezi wakawahi kwenye gari yao ili wakimbie, na yule mzee mlinzi na akaona hapo sio pa kukaa tena, akadandia kwenye gari ya wale wezi akaondoka nao...........!!!!!!!!!!!!!!!!


komando kinjekitile ngwale
Hahahahaaa Huyo Mzee mlinzi aliwaza vzuri sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mie mwaka 2009 mwaka mpya walikuja njemba zaidi ya 10,nakumbuka mzee ndo siku alikuwa ameuza spacio yake kwa milioni 9 hata bank alikuwa hajaipeleka wakavunja mlango but kabla walipiga risasi moja juu mi nlivyoskia tu fasta nkapanda juu ya dari nlipanda vipi mpka leo sikumbuki basi wakafanya yao mzee alikuwa analia kama mtoto,asubuhi akaitwa mpemba akafanya dua yake bhana dah wapemba siyo watu wazuri maana baada ya dua tu jirani zetu zaidi ya wa 3 waliondoka siku ile ile mpka jioni vitu vyote vilirudi na faini juu
heahima kwenu wapemba


Sent from my iPhone using JamiiForums
Dah.
Huyo mpemba namtamani sana aisee.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
The story was:Tulikuwa na kawaida ya kupiga maji kwenye baa moja ipo mji mmoja Nyanda za juu kusini. Tulipiga "mahela " Botswana ya kutosha.Ikawa ni kutumia tu. Kumbe wale wahuni wanatuchorea ramani tu. Nikajichanganya. Niliwaacha jamaa (kutaka kutoroka nikalale maana kawaida tulikuwa tunaanza kupiga maji saa 9:00hrs/asubuhi )
Kufika nje uchochoroni kumbe wale maninja uchwara walikuwa wananifuatilia. Ndiyo wakanikaba na kuchukua nokia tochi na Tsh. 180,000/=Mwaka 2003 hiyo. That was the big money by that time. Jus' imagine 😱ne castle milk stout beer was 1100/=only!It was about money and my new cellphone and above all some respect! That's all!
Nokia torch mwaka 2003 sijui kama zilikuwepo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ha ha ha
Mi nakumbuka wakati nipo Chuo,siku moja natoka kupiga bia zangu baa ya jirani tu kama meter 500 toka getho, ilikuwa majira ya saa 6 usiku, napita karibu na kapori nikasikia mtu ananiita oyo nisubiri kugeuka nyuma nikamuona yupo Kama hatua 15 toka nilipo,nikamuuliza wewe nani ghafla akaanza nikimbiza,nilikimbia mbio kama filbert bai hakunishika, alirusha mawe Sana akanikosa.Ile nafika getho get la kuingilia limefungwa kucheki nyuma anakuja basi nikaamua kukimbia huku nazunguka nyumba nikapiga kelele kuwambia washkaji huko ndani oyooo fungueni fasta nakimbizwa na mwizi jamaa kusikia ivo akasepa.mi nikaingia ndani.
 
1. 2007(TARIME VIJIJINI) niko kidato cha kwanza majira ya saa10 usiku nikiwa na bro tunaenda shule ghafla kwenye kona tunakutana na wezi wa mifugo kama 7 wakiwa na bunduki tukaambatana nao, ikafika mahali wao wakaenda kivyao nasi kivyetu. MUNGU saidia hawakutudhuru wala kutuhoji.

2. 2011-2013 (MKOA Z). Nimekaa na majambazi nyumba jirani, mara nyingi nikitoka usiku kwenda uani nilikuwa nikiwakuta wanagawana bidhaa walizopora kama TV, PC, masufuria, bufa, simu, vocha za jumla, malobota ya nguo, viatu nk. Nawapita nazama uani kisha narudi kulala. Hawakuwa na noma na watu wa kitaa, tena tulikuwa tunapiga nao stori tu kama kawaida na ukiwa na shida wanakusaidia. Watamletea noma yule tu atayetaka kuwachomesha. Vibaka walijaribu kuvunjia watu maduka na nyumba, wakawafata wakawapa onyo wasitake kuwaharibia sehemu za maficho yao na walitii. Za mwizi ni 40, ktk majukumu yao ya usiku walikutana na mheshimiwa(jina na cheo kapuni) wakamuua bila kujua walomuua ana cheo gani. Wote walikamatwa, kwa sasa wananyea ndoo.
 
Kidogo nami niligwaya huo uamuzi wake, Ndio maana tulibishana kwa muda. Kesho yake nilimuhoji kivipi alipata guts za kushuka eneo kama lile. Alijibu kuwa alifanya udadisi wa haraka akapata majibu yafuatayo... moja, aliniambia kabisa aliamini kabisa wale majambazi hawakua na silaha za moto Ndio maana wameteka kwa haraka sana na wakakimbia, (maana waliteka gari 3 tu) akanambia ukitaka kujua majambazi wana silaha za moto wanaweza kuteka hata gari kumi kwa muda huo huo na hawaondoki eneo la tukio haraka haraka, pili kama wanasilaha za moto huwa wakiteka point A huwa wanarudi nyuma kuteka point B ndio maana kurudi nyuma haikuwa option yake. Na majambazi wanaoteka barabarani huwa wakiteka mbele na wakaweka kizuizi kwa nyuma yule atakae watii bila kurudi reverse watamnyang'anya vitu tu na usipokua mbishi hate hawakupigi, Ila ole wako urudi nyuma gari ikushinde wakikudaka ni kifo ama kipigo cha mbwa koko maana yeyote atakayefanikiwa kurudi nyuma ndio huwa snitch maana lazima akapige siku polisi ama awashtue madereva wenzie, Lakini akanambia pia kama aliamini kama hawana silaha za moto akishuka hawawezi kujitokeza maana watadhani yeye ana mguu wa kuku Ndio maana amejiamini kushuka, akaongeza kuwa nao huwa wanaogopa kufa pia hivo ukiwatisha wanatishika. Cha mwisho ni mtu anayeziamini sana Instinct zake.
Kajuaje yote hayo kama sio nayeye aliwahi kuwa jambazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom