Tukutane hapa tuliowahi kuvamiwa na majambazi tupeane uzoefu/ushuhuda

Tukutane hapa tuliowahi kuvamiwa na majambazi tupeane uzoefu/ushuhuda

1. Miaka ya 2000 mwanzoni, likizo time mshua katufata boarding school tunarudi home. Tulichelewa kuvuka boarder ya mutukula tunaitafuta bukoba... baaasi tukakutana na bonge la road block, wazee walee na SMG zao... wakapunga mkono style ya Traffic police wa awamu ya tano.. sijui mshua alitoa wapi confidence, ali reverse shangingi faster na kwa speed almost 40km/h au zaidi for about 10 minutes, akageuza huyooo tukarudi boarder tukala.. ndo ikawa pona yetu..

2. Wazee baba walikua wanammendea mshua kitambo, wakijua pesa pale ipo.. sehem ya kazi ya mshua ilikua ni polini, katika ranchi za taifa.. basi siku moja mshua kapokea mishahara ya wafanya kazi, kaenda nayo porini.. majambazi yakatonywa, yakajiandaa.. Jioni saa kumi na mbili yakatimba home na bunduki kubwa kubwa, sisi watoto hatujui A wala B. Mshua alikua katoka kaenda kupiga maji na washakji zake.. majambazi yakatukuta sisi na step mom.. yakamwambia step mom awapekele mpaka safe ilipokua, akawapeleka, sema wakashindwa kuifungua.. wakatafuta funguo wakakwama.. Mama nae hajui funguo ilipo. Wakampa kipigo cha mbwa koko lakini hakuwapa walichokitaka, kiukweli hakujua funguo ilipokuwa. Safe wakaifyatulia risasi lakini haikufunguka.. walivyoona muda unakwenda, wakabe redio, TV na jewerly wakasepa... Dingi anarudi kalewa zake, anasema funguo zilikua kwenye suruali aliyokuwa kaivaa jana yake.. suruali iko juu kwenye hook..

3. Mwaka 2016 saa nane usiku natoka zangu kula bata na wana wa TIA, nina kama mwezi nimenunua mark X.... nafika tazara taa zinawaka red, hamna magari kabisa na malori niya kuhesabu, ile nasubiria zimulike green, akatokea mtu out of nowhere anataka nishushe kioo, ana bonge la panga.. nikajaa wenge, pombe zikaniishia.. jamaa mwingine akatokea upande wa kushoto akaanza kugonga kioo kwa kitako cha bastola... mweeee, nikakanyaga mafuta gari inaondoka kwa speed matata... bahati nzuri nilikua sijaweka P(parking).. kuna semi trailer lilikua linavuka kwenda airport nililikosa kosa kuligonga.. nikanyoosha mijamaa nikaiacha haiamini kama nimeiponyoka... nilipofika buguruni sikujali kama kuna watu na magari wanavuka 24hrs... huyooo mpaka getto Tabata.. !
Sent using Jamii Forums mobile app
Duh hatari hao sasa ndo majambazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Msalimie sana huyu mume wako mwanaume Wa shoka...

Sent using Jamii Forums mobile app
Wangekuwa wamejificha kwenye kichaka wakamjeruhi au kumuua ungesema ni mjinga kwanini hakurudi! Mimi nadhani huyo jamaa hakuchukuwa tahadhari bali aliongozwa na ujinga (siyo ushujaa) na ilikuwa bahati tu walikuwa wameondoka!
 
Nakumbuka miaka ya nyuma kidogo nikiwa shule O-level ilikua boarding.
Siku hiyo ilikua week end tukatoroka shule kwenda mitaani kuinjoy, kula vitu adimu na kutafuta mademu.
Basi bhana tulikua wanne tumeenda mitaani tumefanya kila kitu mpaka mida ya saa tatu hivi usiku( ilikua ni kijisehemu kimechangamka sana, CENTER)
Wakati tunajiandaa kuanza safari ya kurudi shule mara ghafra wazee wa kazi wakavamia pale kwenye maduka, basi bwana purukushani za hapa na pale kila mtu akatoka nduki.
Wengi tulikimbilia makaburini coz hayakua mbali halafu ndo sehemu iliyokua walau mtu unaweza kujificha.
Basi bwana tumejificha kwenye makaburi wazee wa kazi wakaendelea kukiwasha duka baada ya duka, kati ya hayo maduka kulikua na frem ya salon na kuna wateja walikua wananyolewa(baada ya kuvamia jamaa walizima taa wakawa kimyaaa) basi majambazi si yakafungua mlango wa salon,hahahahaaaa!
Alitoka mshkaji mmoja amenyolewa upande na shuka jeupe shingoni nduki ya ajabu sana kama mshale, jamaa nae akakimbilia uelekeo wa makaburini, ile kufika akatukurupua( maana alikua nduki mbaya halafu anakimbia juu ya misalaba huku shuka linapepea kwa nyuma) kuona vile group lote tuliojificha tukadhani jamaa alikua kafufuka basi tulitoka nduki kumkimbia, na yeye kuona tunakimbia akadhani nyuma kuna jambazi linamkimbiza akaongeza spidi kutufuata, jamani jamani ilikua mshike mshike wa hatari, tulikimbia kama wendawazimu,.
Huku nyuma majambazi yameshaondoka sie tunakimbizana na jamaa. Tulijikwaruza sana kwenye vichaka pamoja na kuanguka kwenye makaburi, tuliumia sana.

Sent from my iPhone using JamiiForums
[emoji23] [emoji23] [emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usiku una mengi, kuna wanadamu wao wamejitolea usiku kama ndio muda wao wa kutafuta chochote kitu,,, binafsi nimewai kukutana na matukio machache ya kukutana na wezi usiku.

Tukio la kwanza, nakumbuka tulikua form six miaka ya nyuma tunatoka kwenye kumbi za starehe tukiwa watatu tunarudi tuliko kua tumepanga uswahilini, njiani tulikutana na wezi wametoka kuiba samani meza, vitanda, na viti walikua wengi kiasi, jamaa walitusimamisha mmoja wao akatupiga mkwara mzito sanaa, nakumbuka walitubebesha meza, rafiki angu mmoja mwenye mwili mkubwa yeye alibebeshwa kabati, tulitembea kama kilomita mbili hivi wakatuachia, yule mwenzetu aliebeba kabati aliumwa mgongo wiki nzima.

Tukio la pili, nikiwa nakatiza mitaa ya sinza, nikakutana na kundi la vibaka wako kama sita hivi, saa sita usiku, ilikua ni ile position unakata kona unakutana na watu hawa hapa, siku sita nikapita kati kati yao maana hakukua na namna nyingine ya kukimbia, nilipigwa kabali ya hatari, huyu kashika mguu huu, mwingine kashika mguu mwingine, walinichukulia simu, waleti na viatu, tukaachana kwa mengi matusi tunatukanana.

Tatu, hii ilinikuta maeneo mapya niliyokua nimehamia, mida ya saa tano usiku nimetoka kunywa mitungi mtaa wa pili, walikuja vijana wawili kwenye boda boda na mapanga yao, mmoja nilimvamia kwa speed ya hatari nilimrukia teke moja akaanguka analia ana kufa, siku laza damu nilikimbia speed ya kufa mtu.

unaweza kushare mawili matatu kama umewai kukumbwa na mswaibu haya, then watu wakajifunza chochote na kuchukua precautions siku za mbeleni.
Sijawahi aisee ila mtungi sio dili ndugu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ona Sasa Mwanaume wa Dar Ameshawaza waza habari za kupata sifa kwa mademu, kuna siku utatandikwa Mpaka unye
bablai mi sio wa dar...na hakuna mbuzi aliekatisha kama kibaka mbele yangu akaishi...huo mkono wa mchna apo kwenye avatar yako imeandaliwa kitu inaitwa shuto...hyo ikiguswa sehemu sasa ivi unaendaa kuungana na kina ngweaa
 
Nakumbuka miaka ya nyuma kidogo nikiwa shule O-level ilikua boarding.
Siku hiyo ilikua week end tukatoroka shule kwenda mitaani kuinjoy, kula vitu adimu na kutafuta mademu.
Basi bhana tulikua wanne tumeenda mitaani tumefanya kila kitu mpaka mida ya saa tatu hivi usiku( ilikua ni kijisehemu kimechangamka sana, CENTER)
Wakati tunajiandaa kuanza safari ya kurudi shule mara ghafra wazee wa kazi wakavamia pale kwenye maduka, basi bwana purukushani za hapa na pale kila mtu akatoka nduki.
Wengi tulikimbilia makaburini coz hayakua mbali halafu ndo sehemu iliyokua walau mtu unaweza kujificha.
Basi bwana tumejificha kwenye makaburi wazee wa kazi wakaendelea kukiwasha duka baada ya duka, kati ya hayo maduka kulikua na frem ya salon na kuna wateja walikua wananyolewa(baada ya kuvamia jamaa walizima taa wakawa kimyaaa) basi majambazi si yakafungua mlango wa salon,hahahahaaaa!
Alitoka mshkaji mmoja amenyolewa upande na shuka jeupe shingoni nduki ya ajabu sana kama mshale, jamaa nae akakimbilia uelekeo wa makaburini, ile kufika akatukurupua( maana alikua nduki mbaya halafu anakimbia juu ya misalaba huku shuka linapepea kwa nyuma) kuona vile group lote tuliojificha tukadhani jamaa alikua kafufuka basi tulitoka nduki kumkimbia, na yeye kuona tunakimbia akadhani nyuma kuna jambazi linamkimbiza akaongeza spidi kutufuata, jamani jamani ilikua mshike mshike wa hatari, tulikimbia kama wendawazimu,.
Huku nyuma majambazi yameshaondoka sie tunakimbizana na jamaa. Tulijikwaruza sana kwenye vichaka pamoja na kuanguka kwenye makaburi, tuliumia sana.

Sent from my iPhone using JamiiForums
mkuuu umenivunja mbavu atarii na hii gahawaaa
 
mkuuu umenivunja mbavu atarii na hii gahawaaa

Utaamini ni ghahawa mpaka yakukute, nakwambia ilikua mtafutano wa haja siku hiyo sitasahau maisha yangu, halafu mwenzangu alikua anakimbia huku anasali kichaga kwa nguvu mpaka nikawa nataka kucheka ila nikigeuka nyuma tu naona kundi la wananzengo wako mbio hatari

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kuna jamaa yangu napiga nae kazi sehemu mmoja, mwaka juzi wakampeleka ndugu yao KMcMc cjui ndio inavyoitwa hiyo hospital kutoka huku dar, basi buana wakachukua gari yao ndogo na ilikuwa na watu kama4 pamoja na mgonjwa ambaye alikuwa mama wa umri umesogea.
Safari ikaanza jioni kutoka dar na kuelekea Moshi, walipanga kule wafike harafu asubuhi wageuze warudi dar. Sasa wakiwa porini kuelekea Moshi, mbele yao kukawa kunakuja gari, ile gari ilikuwa inapiga taa Kwa fujo sana, lengo lilikuwa kuwataadhalisha jamaa huko mbele.

Lakini jamaa hawakutilia mkazo na kudharau zile warning za taa, sasa walipofika jirani jamaa alisikia sauti kwa mbali kutoka kwenye ile gari ikisema kwamba""MNAKWENDA KUFA""lakini gari unapofunga vioo ni ngumu kusikia kwa ufasaha sauti kutoka nje kwa hiyo jamaa hakujali, baaada ya dakika kma3, hamad gogo kubwa lipo barabarani.

Yule dereva alijitahid sana kurudisha gari kwa nyuma na kutafuta jinsi ya kugeza, baaada ya kuona hawa wanatuchezea ilipigwa risasi yule jamaa yetu alikaa mbele anakwambia imempitia sikioni, basi wakapotezana gari ikaingia mtaroni ndipo jamaa walipofika, unaambiwa ile milango walifungua kwa shoka flani hivi vidogo vidogo kama mtu anapasua kigogo cha mnazi.

Stori ndefu sana, ila anakwambia hataki kusikia kusafiri usiku kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
Aaaaaaa malizia bwana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Exactly angeuawa kirahisi Sana afu angeonekana bonge la mpumbavu

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyo jamaa kuna watu wamesema eti alikuwa shujaa lakini mimi nasema alikuwa mjinga sana. Tena huenda alikuwa anaongozwa na ulevi otherwise huwezi kufanya jambo la kijinga kama kuteremka na kujaribu kutoa gogo huku hujui ni nini kinachoendelea!
 
Hahahahahah mkajua msukuleeee

Back
Top Bottom