mankafaraja
JF-Expert Member
- Aug 15, 2015
- 218
- 271
Gari ilielekezwa kuelekea kule taa zilpo elekeza tulinyoosha Moja kwa moja safari ya gongolamboto ilibadika
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app
Kaka Galadudu,,hii ya 2007 km chai vile[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Wale vibaka wangu walikuwa wajinga sana..........2001 hiyo nimetoka zangu kupiga liquid narudi home kama saa 7 hivi ucku, nilipokuwa naishi kuna umbali kidogo kutoka barabarani, dereva taxi kanishusha nikaanza kukata vichochoro kuelekea nyumbani, ghafla nikamulikwa usoni na tochi yenye mwanga mkali sana halafu ikatoka amri kali eti:- simama hapo hapo na ujisachi mwenyewe utoe kila ulichonacho mfukoni........yani sikujiuliza mara mbili mbili, niligeuka kwa kasi na kufyatua mbio kali sana ambazo sijawahi kukimbia.
Kuona ivo na wao wakaniunganishia kuanza kunikimbiza halafu mbaya zaidi wakaanza kuniitia mwizi, mi kusikia ivo nikapunguza mwendo hatimae nikaanza kutembea kwa mwendo wa haraka, kuona natembea na wao wakaanza kutembea na hawapigi tena kelele za mwizi, nilipoona wananikaribia nikachomoka tena mbio kali......zoezi likarudia lile lile la kupigiwa kelele za mwizi, bahati nzuri natokeza barabarani na gari ya police hii hapa, nikawaelezea tukarudi hadi walipoanza kunikimbiza lakini hakuna mtu, basi wakanisindikiza hadi nyumbani.
1993 Tabora hiyo jamaa yangu mmoja kaja mjini kupokea pesa yake ya mauzo ya tumbaku, akawa na mipango mingi balaa ikiwemo kununua baiskeli mpya, kununua radio kaseti ya Lasonic na kuongeza mke wa tatu..........hakuna hata mpango mmoja uliotimia, usiku wa hyo aliibiwa pesa yote sh 100,000/= na baamedi aliyelala nae gesti (nadhani ndo alikuwa anamfanyia intavyuu kama anafaa kuongezwa kuwa mke wake wa tatu, tangu siku hyo jamaa yangu huyo alishikwa na uchizi akatoweka nyumbani hadi tulipokuja kupata taarifa za kifo chake cha kugongwa na gari.
Juzi juzi tu hapa kuelekea kipindi cha sikukuu za krisimasi na mwaka mpya kundi la vibaka wapatao kama 17 hivi walivamia kwa jirani yangu aliyekuwa kauza kagari kake kamechakaa chakaa kwa sh milioni 6, wale wapuuzi wakataka kuja kuchukua zile pesa kama vile walimuwekeza........kwa mara ya kwanza ndo nilikatumia vizuri ka manati kangu ka kizungu, nilimkongoroa goti mmoja wao na wengine wakakimbia, yule tulimmalizia pale pale kwa kushirikiana na wananchi wenye hasira kali.
2007 kuna majambazi yalivamia mtaa flani wenye maduka mengi, sasa ile tabia ya mlinzi mmoja analinda karibu maduka 40, wakamkamata mzee wa watu wakaenda nae hadi kwenye mojawapo ya maduka anayolinda wakamkazimisha aanze kuvunja, zoezi lilipokamilika wakamlazimisha aanze kusomba vitu anapakia kwenye gari la majambazi.......ile wanamalizia mara paaaaap na mwenye duka akatokeza akamuona yule mzee mlinzi wa duka lake yupo kwenye harakati kupakia vitu kwenye gari ya wale wezi, jamaa akafyatua risasi hewani, wale wezi wakawahi kwenye gari yao ili wakimbie, na yule mzee mlinzi na akaona hapo sio pa kukaa tena, akadandia kwenye gari ya wale wezi akaondoka nao...........!!!!!!!!!!!!!!!!
komando kinjekitile ngwale
Walimsalula kila kitu maana mchoro wote ulishachorwa kila kitu na walikua wanajua huyo mzee analala chumba namba ngapi so hakuna ambaye alipona labda yule dada wa chumba cha mwisho aliyekutwa na pichu tu ndio alipona kama alikua na mali
Hahahahaha hyo noma aiseeeTandika temeke nimekabwa sana miaka ya 2009 mpaka wakasema mwacheni huyu wa jana
U risk yo family for nothing
sure man...ndo raha ya kucheza martial arts...yani tena kama upo na demu ndo unachukuaa sifaa zootee..manake unawaosheaa vibaka mwanzo mwisho
Axee juz kati tu tumetok na mwana kupga masanga city cetre igoma,mishale ya ngoma nane tunarud mageton,tukakuna na vicheche ka kumi iv,ss mwnzangu yy kashiba kidogo ana li mwli,kaanz kutisha kuwa wote napasua vichwa,jamaa wakasita kidogo,cha kuja kustahajabisha akataka kuokota jiwe huku keshawaambia atapasua vichwa kwa risasi,tulikimbizwa,nashukuru Mungu miguu yangu haijawah nisalitiWandugu njooni uku mtilike tufurahishe nafsi.
Me sina tukio lolote, huwa sitembei usiku sana.
Sent using Jamii Forums mobile app
hii imenichekesha sana yaani kibaka ana confidence ya kufa mtu ei "oyo nisubiri"Mi nakumbuka wakati nipo Chuo,siku moja natoka kupiga bia zangu baa ya jirani tu kama meter 500 toka getho, ilikuwa majira ya saa 6 usiku, napita karibu na kapori nikasikia mtu ananiita oyo nisubiri kugeuka nyuma nikamuona yupo Kama hatua 15 toka nilipo,nikamuuliza wewe nani ghafla akaanza nikimbiza,nilikimbia mbio kama filbert bai hakunishika, alirusha mawe Sana akanikosa.Ile nafika getho get la kuingilia limefungwa kucheki nyuma anakuja basi nikaamua kukimbia huku nazunguka nyumba nikapiga kelele kuwambia washkaji huko ndani oyooo fungueni fasta nakimbizwa na mwizi jamaa kusikia ivo akasepa.mi nikaingia ndani.
Hahahahahaaa! Endelea kufuatilia commentsNi kwamba ulikuwa na kukodi chako cha kulipa visasi au nini? Maana wengine hujui yaliyowapata.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kweli kabisa mkuu mimi enzi za ukuaji nilikua napiga sana zoezi la capoeira almaarufu paranawe ila ilikuwa for a self defense tu sasa kaka yangu mkubwa akawa anachanganya na makareti sijui judo akajiona mtamu balaa, siku hiyo katoka kazini usiku anatembea mdogo mdogo mara watu hawa hapa wamemuweka mtu kati wana panga zimenolewa jamaa si akajikuta shababi kupambana na hao wahuni, kilichomkuta tulipigiwa simu na wasamaria wema tukamuangalie ndugu yetu yupo mahututi hospitali, tangu siku hiyo jamaa anakuambia akikutana na watu wakamtaiti kama hana ujanja ananyanyua mikono juu tu wachukue wanavyovitaka wasepeusiku kwenye watu wengi hauwezi kuyakumbuka haya, ukibisha utapigwa sanaa.
Mwaka 2005 mida ya saa tisa usiku natoka kwenye promotion ya safari lager miaka iyo,bia za mafungu,mtu tano hizi hapa,wakaanza mtama,nikala teke,nilikuwa najiweza nikarusha ngumi nakumpasua mmoja,wakaokota mawe ,speed nikatoka maana mawe sio,njombe hiyo.Usiku una mengi, kuna wanadamu wao wamejitolea usiku kama ndio muda wao wa kutafuta chochote kitu,,, binafsi nimewai kukutana na matukio machache ya kukutana na wezi usiku.
Tukio la kwanza, nakumbuka tulikua form six miaka ya nyuma tunatoka kwenye kumbi za starehe tukiwa watatu tunarudi tuliko kua tumepanga uswahilini, njiani tulikutana na wezi wametoka kuiba samani meza, vitanda, na viti walikua wengi kiasi, jamaa walitusimamisha mmoja wao akatupiga mkwara mzito sanaa, nakumbuka walitubebesha meza, rafiki angu mmoja mwenye mwili mkubwa yeye alibebeshwa kabati, tulitembea kama kilomita mbili hivi wakatuachia, yule mwenzetu aliebeba kabati aliumwa mgongo wiki nzima.
Tukio la pili, nikiwa nakatiza mitaa ya sinza, nikakutana na kundi la vibaka wako kama sita hivi, saa sita usiku, ilikua ni ile position unakata kona unakutana na watu hawa hapa, siku sita nikapita kati kati yao maana hakukua na namna nyingine ya kukimbia, nilipigwa kabali ya hatari, huyu kashika mguu huu, mwingine kashika mguu mwingine, walinichukulia simu, waleti na viatu, tukaachana kwa mengi matusi tunatukanana.
Tatu, hii ilinikuta maeneo mapya niliyokua nimehamia, mida ya saa tano usiku nimetoka kunywa mitungi mtaa wa pili, walikuja vijana wawili kwenye boda boda na mapanga yao, mmoja nilimvamia kwa speed ya hatari nilimrukia teke moja akaanguka analia ana kufa, siku laza damu nilikimbia speed ya kufa mtu.
unaweza kushare mawili matatu kama umewai kukumbwa na mswaibu haya, then watu wakajifunza chochote na kuchukua precautions siku za mbeleni.
Very, interesting... sipati picha ingekuwa msafara wa mzeebaba huyu wa sasa[emoji16][emoji16][emoji23]
Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16], vipi hao wazee wa kazi kariakoo walikamatwa
Sent using Jamii Forums mobile app
Ikawaje???Kawe ukwamani,
Nilikua nipo Jambo Lee na mwanangu mmoja tumekula ugimbi wa kutosha pale, tukahamia La Roca tukala mundende hadi mida ya saa 8 usiku. Yule jamaa yangu alikua anaishi kawe kulekule halafu Yuko tipsy balaa nkaona sio kesi ngoja nimsindikize magetoni kwake (mitaa ya nyuma ya myfair,ccm) mimi nirudi niendelee na cnn. Jamaa nkamfikisha salama lakini kwa taabu saana maana kuna chochoro sio za nchi hii.
Basi wakati narudi, npo kwenye chocho moja mara ghafla naona kwa mbele kundi la mtu kama 7 linakuja wengine Wana nondo, wengine visu, wengine mawe. Mmoja wapo akarusha jiwe nikakwepa, bahati nzuri hua natembea sana nunchuks zangu kiunoni muda wote. Basi nkazichomoa, nkakaa kibadachi stance nikiwasubiri wasogee...........
Sent using Jamii Forums mobile app
Akapewa kichapo na hela akatoaDu mnamo Mwaka 2007 jijini Dar kulikuwa na Ujambazi Sana
Siku mmoja tupo na washikaji mtaani tunapiga stori kwenye uwanja wa Mpira ambao upande wake mmoja una Gema/Mmomonyoko wa udongo wenye kina sio chino ya Futi 12-15
Sasa bhana wakati stori zikinoga tukasikia Mlio wa SMG zikamiminwa kama tatu hizi za Mfululizo juu kisha ikasikika sauti mmoja Kaa chini Kumbe bwana Bar iliyomita chache sana na uwanja ilikuwa imevamiwa
Yaliyojiri sasa
Sisi tuliokuwa tumekaa uwanjani tukapata na mfazaiko mkubwa maana Risasi zilipigwa kama mita 7 kutoka sisi tulipokuwa tumekaa ghafla tukakimbilia kwenye Gema lenye futi sio chini ya 12 tukajirusha kwaajili ya kunusuru Maisha yetu
tulivyofika chini halo ya kuwa tumeseleleka sana kwenye hayo maporomoko ngozi zetu zikawa zimechubuka chubuka kufika chini tukambia mbio ilipofika kesho yake kila mtu alishindwa kutembea kutokana na maumivu na michubuko na vidonda tulivyovipata!!!
Shughuli ilikuwa pale Bar sasa jamaa mmoja katika Yale majambazi akawa anapita na kiroba /salfeti akikusanya Fedha, Simu, pochi na vitu vingine vya thamani
Sasa bwana wakafika ktk meza ya mama mmoja wa Kichaga yeye na bwana wake wakagoma kutoa hela na simu jamaa wakaamua kuanza kumkata Vidole bwana wake kimoja baada chengine akakatwa vidole viwili fasta akatoa wallet na simu
mama wakichaga naye akapigwa na mapanga kichwani wakamuumiza sana akawa anavuja damu nyingi sana tukawa tumepata funzo kuwa wazee wakazi wakikutait kubali tu kuwapa kama ni pesa au simu
Aisee sito sahau
Sent using Jamii Forums mobile app
Alikuwa ana silahaKuna bwege mmoja alitaka kunitaitisha mitaa ya mazizini ukonga, ila nilimdhibiti vizuri.
Zamani nikiwa chalii, niliwahi kushuhudia dingi mkubwa (R.I.P) akipambana na majambazi wanne na akawa-outshine though walimjeruhi sana kwa kumkatakata mapanga.
Sent using Jamii Forums mobile app