mankafaraja
JF-Expert Member
- Aug 15, 2015
- 218
- 271
USIKU HAUSHONI NGUO, ILI KUEPUKA YOTE HAYO EPUKA KUTEMBEA USIKU KAMA UNATEMBEA JITAHIDI KUWA NA PESA YA KUKUSAIDIA USAFIRI KAMA NI DHARURA CHUKUA TAHADHARI NYINGINE KAMA KUWA NA SILAHA UTAKAYOWEZA KUTUMIA VZR, KAMA VP RUDI NYUMBANI MAPEMA.Usiku una mengi, kuna wanadamu wao wamejitolea usiku kama ndio muda wao wa kutafuta chochote kitu,,, binafsi nimewai kukutana na matukio machache ya kukutana na wezi usiku.
Tukio la kwanza, nakumbuka tulikua form six miaka ya nyuma tunatoka kwenye kumbi za starehe tukiwa watatu tunarudi tuliko kua tumepanga uswahilini, njiani tulikutana na wezi wametoka kuiba samani meza, vitanda, na viti walikua wengi kiasi, jamaa walitusimamisha mmoja wao akatupiga mkwara mzito sanaa, nakumbuka walitubebesha meza, rafiki angu mmoja mwenye mwili mkubwa yeye alibebeshwa kabati, tulitembea kama kilomita mbili hivi wakatuachia, yule mwenzetu aliebeba kabati aliumwa mgongo wiki nzima.
Tukio la pili, nikiwa nakatiza mitaa ya sinza, nikakutana na kundi la vibaka wako kama sita hivi, saa sita usiku, ilikua ni ile position unakata kona unakutana na watu hawa hapa, siku sita nikapita kati kati yao maana hakukua na namna nyingine ya kukimbia, nilipigwa kabali ya hatari, huyu kashika mguu huu, mwingine kashika mguu mwingine, walinichukulia simu, waleti na viatu, tukaachana kwa mengi matusi tunatukanana.
Tatu, hii ilinikuta maeneo mapya niliyokua nimehamia, mida ya saa tano usiku nimetoka kunywa mitungi mtaa wa pili, walikuja vijana wawili kwenye boda boda na mapanga yao, mmoja nilimvamia kwa speed ya hatari nilimrukia teke moja akaanguka analia ana kufa, siku laza damu nilikimbia speed ya kufa mtu.
unaweza kushare mawili matatu kama umewai kukumbwa na mswaibu haya, then watu wakajifunza chochote na kuchukua precautions siku za mbeleni.
Kwani Ak 47 sio SMG mkuu!!?Acha kujifanya ulishakutana na majambazi, hata mlio wa AK 47 au SMG huujui
Sent using Jamii Forums mobile app
Shemeji ni mjeda au mkurya?Ila jamani wanaume wanaroho ngumu!!!!!! Nilimwambia tulock tu milango tujifungie tusubiri hatma yetu kama watakuja kuvunja vioo watukute ndani. Alinijibu kwa ukali "Sifi kiboya" yaani hizo discussion fupi zilifanyika kama tunaugomvi maana mi nilishapaniki... acheni jamani uwii
Kama Ni ubungo mataa ilikuwa 2006.,gari ilikuwa Ni ya NMBMimi mwenyewe lile tukio la ujambazi Ubungo tulikua kwenye basi la nne kutoka kwenye tukio hata wale askari wanapambana tulikua tunashuhudia aiseeee lilikua kama movie aiseee
Si mchezo mkuu....ila sijaelewa gar ya gongolamboto halafu uwanja wa taifa au ulimaanisha uwanja wa ndege!!?bado una hofu nn!??Mwaka 2007 asubuhi tukiwa kwenye daladala kufika buguruni mama mmoja kabaini simu yake imechomolewa na kibaka na anauhakika kibaka hajashuka akauwasha moto kuwa aliyeiba simu hajashuka akamwambia dereva tafadhali twende polisi akajitokeza Kaka mmoja akamwambia yule mama simu yako ni Aina gani na ni Sh.ngapi mama kajibu Nokia elfu sabini
Kaka akazama mfukoni akatoa laki moja tusiende polisi maana anaharaka saa hiyo tumekaribia mataa Buguruni gari ya Gongolamboto hiyo.
Mama kajibu sitaki laki line yangu instead majina ya wateja wangu wa samaki sitaki laki yako nataka simu yanguu twende polisi
Huyo aliyekua anataka kutoa laki alikua siti ya mbele karibu na dereva, basi Hari ziliporuhusiwa alitoa bastola akamuelekezea dereva akamwambia hatuendi polisi endesha gari kuelekea tazara bwana red Kumbe hakuwa peke yake huku kwenye siti niliyokaa Mimi Kumbe nimekaa na mwenzie naye akatoa bastola akaiinua juu akiamuru tutulie
Ulimi Wang ulikua wa moto mdomoni mpaka ninaufeel nilitetemeka Sana dereva alinyoosha mpaka Around uwanja wa taifa wakashuka jamaa wanne na Makoti makubwa wakaenda zao.
Sent using Jamii Forums mobile app
DuuhKwa adhabu za hatari :
-walianza kwa kuto.mba moto usiku kucha. Yaani tuliwasha moto mkali wa kuni kubwakubwa. Wakavua nguo na kuanza kupitisha dushe zao kwenye moto polepole kama wanachoma panya.
-baada ya kuhakikisha wameijiivisha wenyewe na kuungua vooozee lote tuliwapa maji ya kunywa ya vuguvugu watulize uchungu
-tulichonga majiti kama mambo za kupimia kiwanja na kuwadidimiza mmojammoja utosini ikiwa ni mkono wa buriani. It was so sweet to see those skunks begging and thriving for our mercy!
Mbona Mimi naona katumia akili za daraja LA juu kusoma mazingira na kugundua hilo ni eneo ambalo tukio limeshafanyika??Nadhani akili yako ya kulala chini ya gari wakati ujambazi ulishafanyika ndio bure kabisa!!
Huyo jamaa yuko poa sana,ni jasiri,mtulivu na ana akili
Sent using Jamii Forums mobile app
Hivyo yule mzee alibahatisha hakuibiwa tenaEeeeeh bwana hili kundi unalifahamu mkuu??? Liliwahi kuvamia lodge ya home miaka ileeeee naishi home ila cha ajabu yanatembea na mapanga sijui majambia tu hayana bunduki...kumi yanajipanga nje kuangalia usalama na kumi mengine yanazama ndani... Siku hiyo mnyama nimejilaza usiku wa manane kumbe yalishamchorea ramani mshua mmoja alikuja kulala pale lodge na alikua na mpunga wa maana kwenye briefcase yake. Majamaa kuvunja mlango yule manager wa lodge akaanza kupiga kelele za msaada jamaa yakamuwahi alichezea kichapo huku kabanwa mdomo, muda huo nilishafika dirisha kubwa maana dirisha moja la hiyo lodge limeelekea home ila kutokana na kuwepo kwa liukuta lirefu na geti yasingeweza kuingia ndani... Sijui ule ujasiri niliutoa wapi nachokumbuka yaliingia kila chumba na jamaa limoja linaonekana ndio tembo lao lina booooonge la mwili ndio lilikua linajivuta linauvamia mlango unajiachia wenyewe. Wakaingia chumba kimoja wakakuta binti mkali amelala na kichupi tu nikasikia yanasema "Hatujaja kuangalia pichu wala chiu ya mtu hapa tunataka helaaaa tuuuu" basi mnyama si nikaropoka "Wewe hapo nimeona sura yako, na wewe hapo yaani inshort niliwataja kama wanne hivi wakawa wanatafuta sauti inatoka wapi maana mimi nje nawaona ndani maana nje giza ila ndani hawaoni nje sababu ya mwanga ndani. Jamaa kuona vile wakaongea "hoya mfanyieni kazi kuna dogo nje huku ametuchora, weeee kusikia vile acha nipige yowe la hatari nje "Jamani weziiiiiiiiiiiiiii" uzuri jirani yetu ni mwanajeshi mwenye nyota zake tatu akachomoka na bunduki yake usiku ikapigwa hewani "Paaaaaaah" majamaa yakaambiana "Kimenuka wana tusepe" yakakimbia mpaka kesho hata nikikutana nao siwakumbuki maana kwa ule uoga hata sikukariri sura zao kwa umakini ila wamewatesa saaaana wafanyabiashara wa maeneo ya kimara na mbezi miaka ile
apoo ukitaka kwanza wajae upepo unakaa sanchingdachi stance...au nekohachidachi...yani wanakua kama wanaangalia moviee....aaaaa ayo mambo yana raha yakeKawe ukwamani,
Nilikua nipo Jambo Lee na mwanangu mmoja tumekula ugimbi wa kutosha pale, tukahamia La Roca tukala mundende hadi mida ya saa 8 usiku. Yule jamaa yangu alikua anaishi kawe kulekule halafu Yuko tipsy balaa nkaona sio kesi ngoja nimsindikize magetoni kwake (mitaa ya nyuma ya myfair,ccm) mimi nirudi niendelee na cnn. Jamaa nkamfikisha salama lakini kwa taabu saana maana kuna chochoro sio za nchi hii.
Basi wakati narudi, npo kwenye chocho moja mara ghafla naona kwa mbele kundi la mtu kama 7 linakuja wengine Wana nondo, wengine visu, wengine mawe. Mmoja wapo akarusha jiwe nikakwepa, bahati nzuri hua natembea sana nunchuks zangu kiunoni muda wote. Basi nkazichomoa, nkakaa kibadachi stance nikiwasubiri wasogee...........
Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa ufupi:Walinikaba na kupora simu na fedha watu kama sita hivi. Niliwatambua wawili. Mungu nisamehe. Niliwakuta Ubungo terminal 2003.Mmoja alikufa palepale. Yule mmoja alitoroka tukampata Makambako 2005.Alichezea visu vya tumbo akatutajia waliobaki. Mwaka uliofuata walikuja wao na wazazi wao kuomba msamaha na kurudisha walichopora. It was too late! Sijui kilichoendelea ila I feel so good hawapo duniani. Nilewe kwa hela zangu,halafu unikabe na kuniachia alama za maisha? Something bad gonna happen! [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Angepigwa shaba ya tako sasa si ndio uboya wenyewe huo...
Unafika sehemu unasikia harufu ya damu mbichi,harufu ya risasi alafu unashuka kwenye gari kwenda kutoa gogo barabarani kisa huwezi kufa kiboya wakati huo huna uhakika kama wazee wa kazi wameshaondoka au laah..
Bora angepiga uturn arudi alikotoka kuliko kujidai shababi kwenye kutoa gogo
Kwa ufupi:Walinikaba na kupora simu na fedha watu kama sita hivi. Niliwatambua wawili. Mungu nisamehe. Niliwakuta Ubungo terminal 2003.Mmoja alikufa palepale. Yule mmoja alitoroka tukampata Makambako 2005.Alichezea visu vya tumbo akatutajia waliobaki. Mwaka uliofuata walikuja wao na wazazi wao kuomba msamaha na kurudisha walichopora. It was too late! Sijui kilichoendelea ila I feel so good hawapo duniani. Nilewe kwa hela zangu,halafu unikabe na kuniachia alama za maisha? Something bad gonna happen! [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
una bahati ulipona na upo kusimulia hekaya. wenzio wanatupiwa baharini.Nakumbuka mwaka Fulani pale salenda brg nilikutana na vibaka mida ya saa mbili 2 dah walinisaula virongaronga vyangu na vinauli na mabapa nimeyaambulia
Wallah u made my day[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]eti ww hapo nakujua na ww na ww[emoji3][emoji3]Eeeeeh bwana hili kundi unalifahamu mkuu??? Liliwahi kuvamia lodge ya home miaka ileeeee naishi home ila cha ajabu yanatembea na mapanga sijui majambia tu hayana bunduki...kumi yanajipanga nje kuangalia usalama na kumi mengine yanazama ndani... Siku hiyo mnyama nimejilaza usiku wa manane kumbe yalishamchorea ramani mshua mmoja alikuja kulala pale lodge na alikua na mpunga wa maana kwenye briefcase yake. Majamaa kuvunja mlango yule manager wa lodge akaanza kupiga kelele za msaada jamaa yakamuwahi alichezea kichapo huku kabanwa mdomo, muda huo nilishafika dirisha kubwa maana dirisha moja la hiyo lodge limeelekea home ila kutokana na kuwepo kwa liukuta lirefu na geti yasingeweza kuingia ndani... Sijui ule ujasiri niliutoa wapi nachokumbuka yaliingia kila chumba na jamaa limoja linaonekana ndio tembo lao lina booooonge la mwili ndio lilikua linajivuta linauvamia mlango unajiachia wenyewe. Wakaingia chumba kimoja wakakuta binti mkali amelala na kichupi tu nikasikia yanasema "Hatujaja kuangalia pichu wala chiu ya mtu hapa tunataka helaaaa tuuuu" basi mnyama si nikaropoka "Wewe hapo nimeona sura yako, na wewe hapo yaani inshort niliwataja kama wanne hivi wakawa wanatafuta sauti inatoka wapi maana mimi nje nawaona ndani maana nje giza ila ndani hawaoni nje sababu ya mwanga ndani. Jamaa kuona vile wakaongea "hoya mfanyieni kazi kuna dogo nje huku ametuchora, weeee kusikia vile acha nipige yowe la hatari nje "Jamani weziiiiiiiiiiiiiii" uzuri jirani yetu ni mwanajeshi mwenye nyota zake tatu akachomoka na bunduki yake usiku ikapigwa hewani "Paaaaaaah" majamaa yakaambiana "Kimenuka wana tusepe" yakakimbia mpaka kesho hata nikikutana nao siwakumbuki maana kwa ule uoga hata sikukariri sura zao kwa umakini ila wamewatesa saaaana wafanyabiashara wa maeneo ya kimara na mbezi miaka ile