Miaka miwili iliyopita tulivamiwa na wezi nyumbani usiku wa saa saba, sina uhakika waliingiaje maana ilikua nyumba ina fence na geti milango yetr ina grill za nondo ngumu, vioo vya madirisha tuliacha wazi ili kupata hewa
Nadhani walikua wanatuchora muda maana waliingia wakati Mr hayupo amesafiri so nilikua all alone na watoto and i was 9 months pregnant
Nikiwa usingizini nikahisi kama nazibwa mdomo nakosa pumzi, nikahisi labda nipo ndotoni lakini nilipofungua macho nakutana na sime tatu, mbili zimeelekezwa kwa boys wangu wawili na moja imenielekea, huyu alieniwekea sime akaniambia tulia kimya ukipiga kelele tunachinja watoto(mr akisafiri huwa nalala na watoto hawa wadogo mmoja alikua na miaka minne na mwingine 6)
Huyu wa miaka sita yeye akaanza kupambana nao akawa anawarushia mara mateke mara vingumi vyake anawaambia muache mama yangu maana alikua amenishika shingo kama anataka kunikaba
Nikiangalia hali yangu na tumbo la miezi tisa, nina watoto watatu ndani tena wa kike yupo chumba kingine, I was terribly worried nikajisemea nainachohitaji ni usalama wa watoto wangu kwanza
Ikabidi nimwambie mtoto atulie, wakati namtuliza mtoto mwizi mmoja akaniamrisha ninyanyuke nifungue safe maana ilikua imefungwa kwa password, walikua wamevaa mask na waliwasha taa zote za nyumba nzima, ndani walikua watatu, sijui nje walikua wangapi
Nikawa mpole nikamfungulia, palikua na document tu hapakua na hela,
Kwa hesabu za harakaharaka ni kwamba ndani waliingia muda mrefu sana na walikua wameshahamisha baadhi ya vitu sema sijui walituwekea dawa hatukusikia, maana pale chumbani palikua pamepekuliwa kila kitu kilikua hovyo mpaka simu yangu walikua wameishika mkononi na baadhi ya vitu walikua wameshachukua,
Yule kiongozi wao akanimuru nimvulie pete zangu za ndoa,nikafanya hivyo, akahitaji passowrd za mpesa na airtel money, nikampatia na akahamisha pesa hapohapo, nilikua na app ya sim banking wakahitaji passowrd pia,nikawapatia na wakahamisha pesa, walipoona nipo calm na ninawapa ushirikiano wakaweka silaha chini wakavua na mask wakawa very confortable kusearch, walisearch kila mahali, vyumba vyote na walichukua kila walichotaka, walikua na Noa imepaki nje
kifupi walispend zaidi ya dakika 30 pale ndani, mmoja akabaki wakati wengine wanapeleka vitu kwenye noah nje na walikua wanatokea geti kubwa bila woga
Walipomaliza, wakaniambia ole wako upige kelele, bado tuna kazi kwa majirani zako,ukipiga kelele tutarudi na tutakubaka mpaka huyo mtoto tumboni atoke, Nilikaa kimya nikachungulia dirishani mpaka nilipohakikisha wametoka, nikatoka nikafunga milango na geti maana waliiacha wazi, then after tukaka na watoto sebleni, walikua wanaogopa,nilikua naogopa pia nikashindwa kujizuia nikawa nalia tu, i had nothing to tell the kids, sikua na neno la kuwatia moyo au kuwafariji, i was helpless,sikua na simu wamechukua zote,tv hamna, laptop hamna, hata tablets za watoto,sikua na kitu chochote cha kuniwezesha kufanya mawasiliano, na mtaa tuliokua tunaishi ulikua kimya nyumba zipo mbalimbali na hata ukipiga kelele sio rahisi kwa jirani wasikie. For the first time i cried like a baby mbele za watoto, ikabidi wao wageuke wafariji wangu, huyu wa kiume aliekua anapigana na wezi akawa ananiambia mama usilie, kesho baba akija atawakamata wote na tutawapiga mpaka warudishe tablets zetu tucheze game
Watoto walisinzia kwenye miguu yangu ila mimi sikulala mpaka mida ya saa 11 nikasikia mngurumo wa bajaji ya jirani inapita(huwa anarudi saa 11 kila siku. Nikatoka nje ya geti mbiio nikamsimamisha, nikamwambia tumevamiwa usiku, ndio ikabidi aanze kuwapigia majirani wengine,na mimi nikaomba simu nikatoa taarifa kwa Mr, ndugu jamaa na marafiki, cha kushangaza kumbe wale wezi walifunga mtaa, walivamia nyumba sita kwa usiku huo,ten nyumba zingine wamingia zilikua na fence ya umeme
Nashukuru Polisi walifanya kazi yao kikamilifu, walikamatwa woote,tulikwenda kuwatambua na sikukosa mahakamani hata siku moja mpaka siku ya hukumu, watoto wangu walikua sehemu ya ushahidi, nakumbuka siku watoto wanatoa watu walipata hisia kali sana na uchungu, yule mwendesha mashtaka alishidwa kujizuia alipata hisia za uchungu na hasira sema miiko ya kazi ilimbana akakaa kimya
Mwisho wa siku hukumu ilitoka na Walipigwa mvua thelathini kwa kwesi ya Arm robery
Tuliuza ile nyumba na hatujawahi kurudi ule mtaa tena,baadhi ya vitu vilipatikana tukaambiwa tukavitambue pale oysterbay ila hatukwenda maana tuliona vitayupatia kumbukumbu mbaya, wakala aliehamishiwa pes akutoka kwenye simu yangu alikamatwa na alishtakiwa pia
Go down walilokua wanahifadhi vitu lilivamiwa na polisi na mmiliki alikamatwa
Hii kumbukumbu haijafutika mpaka leo, na kwa watoto ilikuwa worse,ilibidi tuwatafutie mwana saikolojia wa kuwasaidia, maana ilifika wakati hata mtu akigonga geti wanakimbia kujificha wanahisi ni mwizi